Kustahili Baraka Zetu Zilizoahidiwa
Ona la baraka za Baba yetu za ajabu zilizoahidiwa lazima ziwe kitovu cha fokasi mbele ya macho yetu kila siku.
Je! Hammpendi huyu dada katika video? Tanajua kwamba wengi wenu ambao hamjapata nafasi ya kuzaa watoto wenu wenyewe ambao mmetumia maisha yenu kuwapenda, kuwalea, kuwafundisha na kuwabariki watoto. Na eh, ni kwa jinsi gani Baba yetu wa Mbinguni pamoja nasi, dada zenu, tunawapenda kwa ajili ya hivyo.
Je! Sisi wote, ikijumuisha ninyi dada wadogo wapendwa katika Msingi na Wasichana, tumepata nafasi ya kumshika mtoto mchanga katika mikono yetu na kumfanya yeye atazame katika macho yetu? Je! Tumesikia hisia tukufu na takatifu zinazomzingira huyu roho wa selestia, majuzi kabisa ametumwa kutoka kwa Baba yetu aliye Mbinguni hata kwenye mwili mdogo halisi, ulioumbwa upya? Mimi mara kwa mara nimepata hisia tamu sana, ororo sana, na za kiroho sana.
Miili yetu ni vipawa vitakatifu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni. Ni mahekalu binafsi. Tunapoyaweka kuwa safi na halisi, tunaweza kuwa wastahiki kumsaidia Baba yetu wa Mbinguni kuumba miili kwa watoto Wake wa kiroho.
Rais Boyd K Packer katika hutoba yake ya mwisho ya mkutano mkuu, ambayo ninyi mnaweza kuikumbuka kama ”kuki na busu,” alishuhudia kwamba ”amri ya kuzaana na kujaza dunia ... ni muhimu ... na ni chanzo cha furaha ya mwanadamu. Kupitia kwa utekelezaji wa haki wa nguvu hii [uumbaji], tunaweza kuja karibu na Baba yetu wa Mbinguni na kupata ujalivu wa shangwe, na hata uungu. Nguvu za uumbaji siyo sehemu ya ziada ya mpango; ndiyo mpango wenyewe.
Aliendelea:
”Upendo wa kweli huhitaji kujizuia hadi baada ya ndoa kushiriki huba hii ambayo hufungua hizo nguvu takatifu ... [kwa] kuepukana na hali ambazo tamaa za kimwili zinaweza kuibuka. ...
”... Furaha yetu katika maisha ya duniani na kuinuliwa hutegemea jinsi tunavyojibu hizi tamaa zisizozima, na kali.”1
Dada zangu wapendwa, vijana wote na wale ambao si vijana, mimi nimepata kuhisi wasiwasi mwingi nilipokuwa nikiandaa hotuba hii. Kama Alma Kijana alivyosema, ”Natamani kutoka sehemu za ndani kabisa za moyo wangu ... kwamba msikilize ... mliite jina lake takatifu, na kukesha na kusali daima, kwamba msijaribiwe zaidi ya yale ambayo mnaweza kuvumilia, ... kwamba muinuliwe katika siku ya mwisho.”2
Baadaye, Mormoni pia alishuhudia kwamba katika siku za Alma, Korihori, mpinga Kristo, ”aliwahubiria, ... , akipotosha mbali mioyo ya ... wanawake wengi.”3
Dada, Shetani ameinua bango la aina ya Korihori katika siku zetu kwa ufanisi unaoongezeka. Ni nini baadhi ya vyombo vyake? Vitabu wa mapenzi vyenye kusisimua shauku, vipindi vya televisheni vya mapenzi, wanawake walioolewa wakianza tena uhusiano na wapenzi wao wa zamani kwenye mtandao wa kijamii, ponografia. Sisi sharti tuwe makini sana, dada wapendwa! Hatuwezi kucheza na mishale mikali ya Shetani na tukose kuchomeka. Mimi sijui chochote ambacho kitatuhitimisha kwa uenzi wa kila mara wa Roho Mtakatifu kama vile maadili.
Wengi katika ulimwengu wa leo wanatafuta kuridhishwa ghafula na elimu mara moja kwenye Intaneti. Kinyume chake, tungebarikiwa sana kama tungefanya imani na subira na kwenda kwa Baba yetu wa Mbinguni, chanzo cha ukweli wote. Kuna majibu mengi na uhakikisho unaoweza kuja kupitia kupekua na kujifunza maandiko kwa maombi ya dhati na kusihi, lakini hamna ahadi kama hizo kwenye Intaneti. Nabii Yakobo anashuhudia: ”Kwani Roho huzungumza ukweli wala sio uwongo. Kwa hivyo, huzungumza kuhusu vile vitu vilivyo, na vile vitu vitavyokuwa.”4
Wakati tunajihusisha na kutazama, kusoma, ama kufanya chochote ambacho ni duni kuliko viwango vya Baba, kinatudhalilisha, Bila kujali umri, kama tutatazama, tutasoma, tutasikiliza, ama kuchagua kufanya kitu ambacho hakiambatani na viwango vya Bwana katika Kwa Nguvu ya Vijana basi kitupilie mbali, kirarue, na funga mlango mara moja.
Hakuna yeyote kati yetu ambaye ni kamili, lakini tunapotenda dhambi, Rais Packer ametukumbusha: ’Tazama, yule ambaye ametubu dhambi zake, huyu anasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena’
”Ahadi ni: ’Tazama, yule ambaye ametubu dhambi zake, huyu anasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena’ (M&M 58:42). …
”... Upatanisho, ambao unaweza kumkomboa kila mmoja wetu, hauna makovu. Hiyo inamaanisha kwamba bila kujali kile tumefanya ama pale tumekuwa ama jinsi jambo limetokea, kwa kutubu kikweli, Yeye ameahidi kwamba Yeye atapatanisha. Na wakati Yeye alipatanisha, hayo yalisuluhishwa. Kuna wengi wetu ambao hugaagaa hapa na pale … kwa hisia za hatia, bila kujua kweli jinsi ya kuepuka. Unaepuka kwa kukubali Upatanisho wa Kristo, na yote yale ambayo yamekuwa machungu yanaweza kuwa mazuri na upendo na milele.”5
Licha ya toba, kuna misaada ama vyombo gani vilivyotolewa kutusaidia kuwa wasafi na waadilifu? Msingi na Wasichana wote wanajua na kuimba wimbo ”Scripture Power (Nguvu za Maandiko).”6 Je! Tunaweza kuupanua kuwa ”Sala za Nguvu,” Nguvu za Hekalu,” Nguvu za Maagano,” na ”Nguvu za Maadili”?
Pia kuna baraka kuu na ahadi za ulinzi zinazihusiana na uvaaji unaofaa wa nguo zetu za hekaluni. Mimi nimekuja kuhisi kwamba mimi kiistairi nimevalia majoho ya kifalme nilipewa na Baba yangu wa Mbinguni. Tunapojitahidi kuvaa vazi linalofaa, Mimi nashuhudia kwamba Baba yetu anatambua kama ishara kubwa ya upendo wetu na ucha Mungu Kwake. Ni ishara ya maagano ambayo tumefanya Naye, na Yeye ameahidi, ”Mimi, Bwana, ninafungwa wakati ninyi mnapofanya ninayosema; lakini msipofanya ninayosema, ninyi hamna ahadi. ”7
Hivi majuzi niliongea na rafiki wa zamani ambaye alikuwa amepata talaka mbili kwa sababu ya uteja na kutokuwa mwaminifu kwa waume wake. Yeye na watoto wake watatu wameteseka pakubwa. Alisihi, ”Mimi nimejaribu sana kuishi kwa haki. Kwa nini nimepatwa na majaribu mengi hivi? Ni nini nilichokosea? Ni nini Baba wa Mbinguni anataka mimi nifanye? Mimi ninasali na kusoma maandiko yangu, ninawasaidia watoto wangu, kwenda hekaluni kila mara.”
Nilipokuwa nikimsikiza huyu dada, nilihisi kupiga kelele, ”Unafanya vyema! Unafanya vyema yale yote ambayo Baba wa Mbinguni anataka na anatumaini utafanya!”
Vyema, wengi wamesema kwamba ahadi za Baba zilizoahidiwa ziko ”mbali sana kabisa,” hasa wakati maisha yetu yanafurika kwa changamoto. Lakini Alma alimfunza mwanawe kwamba ”maisha haya ndiyo wakati wa watu kujitayarisha kukutana na Mungu.”8 Si wakati wa kupokea zetu baraka zote. Rais Packer alielezea kwamba ’”Na wao waliishi kwa furaha milele’ kamwe uwa haijaandikwa kwenye onyesho la pili. Mstari huu ni wa onyesho la tatu wakati fumbo lishafunuliwa na kila kitu kuwa shwari.”9 Hata hivyo, ono la baraka za Baba yetu za ajabu zilizoahidiwa ni sharti ziwe kitovu cha fokasi mbele ya macho yetu kila siku—pamoja na ufahamu ”wa wingi wa wororo wa rehema yake”10 sisi tunaupata kila siku.
Kina dada, mimi sijui kwa nini tuna majaribio mengi ambayo tunayo, lakini hii hisia yangu binafsi, dada, kwamba zawadi ni kubwa sana, vivyo hivyo milele na milele, vivyo hivyo furaha na zaidi uelewa wetu kwamba katika ile siku ya zawadi, sisi tunaweza kuhisi kusema kwa Baba yetu mwenye rehema na upendo, ”Haya ndiyo yote ambayo yalikuwa yanahitajika?” Mimi naamini kwamba kama sisi kila siku tunaweza kukumbuka na kutambua kina cha upendo ambao Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe wanao kwa ajili yetu, tungekuwa radhi kufanya chochote Wao wanatuomba ili kurudi tena katika uwepo Wao, tuzungukwe na upendo Wao milele. Ingejalisha nini, dada zangu, kile kitakachotupata hapa kama, mwishowe, haya majaribio ndiyo mambo hasa ambayo yatatuhitimisha kwa uzima wa milele na kuinuliwa katika ufalme wa Mungu pamoja na Baba yetu na Mwokozi wetu.
Mimi nashuhudia kwamba miili yetu ni vipawa vitakatifu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni na kwamba tunapoiweka miili yetu kuwa halisi na safi kupitia dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi wetu, na kuweka ono la zawadi za Baba yetu zilizoahidiwa kila siku mbele yetu, sisi siku moja tutapokea ”vyote ambavyo Baba [yetu] anavyo.”11 Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.