Chagua Nuru
Ni sharti tuchague kufuata ushauri wa kinabii, tutambue na kutenda kulingana na msukumo wa kiroho, na kuwa watiifu kwa amri za Mungu, na kutafuta ufunuo binafsi.
Siyo kitambo sana, mke wangu na mimi tuliamua kwamba tunapaswa kupata uzoefu kamili wa eneo lililo karibu na nyumba yetu katika magharibi kasikazini mwa Montana. Tulipanga kwenda na baiskeli zetu hadi Hiawatha Trail, mtambo wa reli ambao uligeuzwa ambao huvuka Rocky Mountains kati ya Montana na Idaho. Tulitarajia siku ya burudani pamoja na marafiki zetu, tukifurahia urembo asili wa eneo hilo.
Tulijua safari yetu kwenye mkondo mzuri wa maili 15 (kilometa 24) ingejumuisha madaraja yanayovuka makorongo ya kina kikuu na penyo ndefu zinaopitia milima ya mpwaruzo. Kwa hiyo tulijiandaa kwa taa zilizofungwa kwenye helmeti zetu na baiskeli.
Wale ambao walikuwa wameshaenda mapema walituonya kwamba penyo zilikuwa na giza na kwamba tulihitaji taa kali sana. Tulipokusanyika mbele ya lango kuu la Taft Tunnel, mlinzi alielezea baadhi ya hatari za mkondo huo, ikujumuisha mashimo ya kina kwenye ulingo, kuta za kukwaruza, na giza totoro. Kwa hamaki, tukasonga mbele katika upenyo. Baada ya kuendesha baiskeli kwa muda dakika chache tu, giza lililotabiriwa lilitumeza. Taa nilizokuja nazo zikawa ni bure, na punde giza likatuzidi. Ghafula nikaanza kuigiwa na kiwewe, kuchanganywa, na kikanganyika.
Niliona aibu kukiri kiwewe changu kwa marafiki na wanafamilia wangu. Ingawa nilikuwa mwendesha baiskeli mwenye uzoefu, sasa nikawa ninajihisi kama kamwe shiaendesha baiskeli. Nilijaribu kuwa wima mkanganyiko wangu ulipoongezeka. Mwishowe, baada ya kusema shida zangu kwa watu waliokuwa karibu nami, niliweza kuukaribia mwangaza wenye nguvu sana wa rafiki yangu. Kwa kweli, kila mmoja katika kundi alianza kujenga duara karibu naye. Kwa kukaa karibu naye na kutegemea kwa muda mwangaza wake na mwangaza wa kundi lote, tulisonga mbele katika giza ndani ya upenyo ule.
Baada ya kile kilichoonekana kama masaa mengi, niliona mwangaza mdogo. Mara moja, nikaanza kuhisi uhakikisho wa kwamba mambo yote yatakuwa shwari. Niliendelea kusonga mbele, nikitegemea tu mwangaza wa marafiki na mwangaza uliokuwa unazidi kuangaza. Kujiamini kwangu polepole kukarudi mwangaza ulipozidi kuongezeka kwa ukubwa na ukali. Kipindi kabla ya kufika mwisho wa upenyo, sikuhitaji tena msaada wa marafiki zangu. Kiwewe chote kilitoweka nilipokuwa nikisokota matanga upesi kuelekea kwenye mwangaza. Nilihisi shwari na uhakikisho hata kabla ya kufikia asubuhi iliyokuwa na joto na ukuu.
Tunaishi katika ulimwengu ambao tutapata uzoefu ambao hutia changamoto imani yetu. Tunaweza kujisikia kujiamini kwamba tuko tayari kukabiliana na changamoto hizo—na kugundua matayarisho yetu hayakuwa ya kutosha. Na kama vile rafiki yangu alikuwa amenionya kuhusu giza, tunaonywa hivyo leo. Sauti za kitume zinatuhimiza tujitayarishe wenyewe kwa mianga yenye nguvu kubwa, nguvu za kiroho.
Vivyo hivyo, tunaweza kuhisi kupata aibu, tusijikie vizuri, ama kukanganyika kiroho tunapokumbana na changamoto kwa imani yetu. Kwa kawaida, uzito na muda wa hisia hizi utategemea tunavyojibu. Kama hatufanyi lolote, shaka, kiburi, na hatimaye ukengeufu unaweza kutuondosha kutoka kwenye mwangaza.
Nilijifunza masomo fulani muhimu kutokana uzoefu wangu katika upenyo. Nitashiriki machache pamoja nanyi
Kwanza, bila kujali giza la shaka lilivyo kali, tunachagua ni kwa kipindi gani na ni kwa kiwango gani tutairuhusu itushawishi sisi. Ni lazima tukumbuke jinsi Baba wa Mbinguni na Mwanawe wanavyotupenda. Hawatatutekeleza, wala hawataruhusu tushindwe kama tutafuta msaada Wao. Kumbuka tukio lililomkuta Petro katika mawimbi makali katika Bahari ya Galilaya. Petro alipoona giza lenye baridi likimzunguka, alitambua shida yake mara moja na akachagua wakati huo huo kuomba msaada. Hakushuku nguvu za Mwokozi za kumuokoa; kwa urahisi aliita na kwa sauti, ”Bwana, niokoe.”1
Katika maisha yetu, mkono wa Mwokozi ulionyoshwa unaweza kuchukua umbo jingine zaidi ya msaada kutoka kwa rafiki wa kuaminika, kiongozi ama mtu mwenye upendo. Wakati tunahangaika gizani, hakuna makosa kutegemea kwa muda mwangaza wa wale wanaotupenda na wenye nia nzuri juu yetu.
Tunapofikiria kwa makini, kwa nini tuwasilikilize wasioonekana, sauti za kejeli za wale walio katika yale majumba makubwa na mapana ya nyakati zetu na kupuuza maombi ya wale wanaotupenda kweli. Kuna wengi wasiojua kuwa wanapendelea kubomoa badala ya kuinua na kubeza badala ya kuinua. Maneno yao ya kejeli yanaweza kujichimbia ndani ya maisha yetu, mara nyingi mpasuko wa nukta wa mikanganyiko ya kielektroniki iliyotengenezwa kwa makini na makusudi ya kuangamiza imani yetu. Je! Ni jambo la busara kuiachia hali yetu njema ya milele katika mikono ya wageni? Je! Ni jambo la busara kudai kuelimishwa na wale ambao hawana mwangaza wa kutupa ama wale ambao wanaweza kuwa na njama yao ni fiche kutoka kwetu? Hawa ni watu fiche, kama wakiwasilishwa kwa ukweli, kamwe hatutawapatia hata dakika moja, lakini kwa sababu wanatumia vibaya vyombo vya kijamii, wakijificha wasijulikane kwa ukaguzi, wanapata umaarufu usiofaa.
Uchaguzi wetu wa kuwasikiliza wale ambao wanakejeli vitu vitakatifu utatupeleka mbali na mwangaza wa Mwokozi wa kuokoa na unaoleta uzima. Yohana aliandika: ”Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”2 Kumbukeni, wale wanaotupenda kweli wanaweza kutusaidia kujenga imani yetu.
Kama vile tu nilivyoona aibu katika upenyo ule, sisi pia tunaweza kuona aibu kuomba msaada tunapokuwa na shaka. Labda sisi ndiyo wale ambao wengine wanatutazamia wapate nguvu, na sasa tunahitaji msaada. Tunapotambua kwamba mwangaza na faraja ambayo Mwokozi anatunyooshea ni ya thamani sana hatupaswi kuipoteza kwa sababu ya kiburi, basi viongozi wa Kanisa wenye maongozi, wazazi na marafiki wa kuaminika wanaweza kusaidia. Wamesimama tayari kutusaidia katika kupata hakikisho la kiroho ambalo litatuimarisha dhidi ya changamoto za imani.
Pili, ni sharti tuamini katika Bwana ili kukuza nguvu za kiroho ndani yetu. Hatuwezi kutegemea mwangaza wa wengine milele. Mimi nilijua kwamba giza katika upenyo halitadumu kama nitaendelea kusokota matanga kandoni mwa rafiki yangu na nikiwa karibu na usalama wa kundi. Lakini matarajio yangu yaliniwezesha kuendelea mbele peke yangu mara nilipoweza kuona mwangaza. Bwana hutufundisha, ”Sogeeni karibu nami na mimi nitasogea karibu na nyinyi; nitafuteni kwa bidii nanyi mtanipata; ombeni, nanyi mtapewa; bisheni, nanyi mtafunguliwa.”3 Ni sharti tutende, tukitarajia kwamba Bwana atatimiza ahadi Yake kutuinua kutoka gizani kama tutasogea karibu Naye. Adui, hata hivyo, atajaribu kutushawishi kwamba kamwe hatujahisi ushawishi wa Roho na kwamba itakuwa rahisi sana tu tukijaribu kusitisha.
Rais Dieter F. Uchtdorf anatushauri ”tilieni shaka mashaka yenu kabla kutilia shaka imani yenu.”4 Katika kata yangu ya nyumbani, mvulana mmoja hivi majuzi alisema, ”Kuna mambo ambayo nilihisi kwamba hayawezi kuelezeka katika lugha ingine ile bali ni vya Mungu. Huu ni uaminifu wa kiroho.
Tunapokabiliwa maswali, ama ushawishi wa kuwa na shaka, tunapaswa kukumbuka baraka za kiroho na hisia ambazo zilipenya mioyoni mwetu na maisha yetu hapo awali na kuweka imani yetu katika Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe Yesu Kristo. Ninakumbushwa ushauri uliotolewa katika wimbo unaofahamika: ”Usimtilie shaka Bwana wala wema wake [kwani] tumeshamthibitisha katika siku zilizopita.”5 Kupuuza na kudharau uzoefu wa kiroho wa awali kutatupeleka mbali na Mungu.
Utafutaji wetu wa mwangaza utaboreshwa na hiari yetu ya kuitambua itakapoangaza katika maisha yetu. Maandiko ya kisasa yanaelezea mwangaza na kuwapatia ahadi wale wanaoipokea: ”Kile kilicho cha Mungu ni nuru; na yule ambaye huipokea nuru, na kukaa ndani ya Mungu, hupokea nuru zaidi; na nuru hiyo huzidi kung’ara hata mchana mkamilifu.”6 Jinsi tulivyokuwa tunasokota matanga kuelekea kwenye mwangaza, tulijikaza zaidi, ndiyo uangavu wa ushawishi wake huzidi katika maisha yetu. Kama vile mwangaza mwisho wa upenyo ule, ushawishi Wake unaweza kutuletea kujiamini, kufanya maazimio, faraja, na—cha muhimu sana—nguvu za kujua kwamba Yeye yu hai.
Tatu, hakuna kiza kilicho totoro, chenye usumbufu, ama kilicho kikali ambacho hakiwezi kushindwa na mwangaza. Mzee Neil L. Andersen majuzi alifundisha: ”Kadiri uovu unavyoongezeka duniani, ndivyo nguvu za kiroho zinavyoongezeka kwa wale wema. Kadiri dunia inavyoporomoka katika usalama, ndivyo Bwana hutayarisha njia kwa wale wanaomtafuta Yeye, akiwapatia hakikisho kuu, uthibitisho mkuu, na imani kuu katika mwelekeo wa kiroho tunaokwenda. Kipawa cha Roho Mtakatifu huwa mwangaza angavu katika kizakiza cha machweo.”7
Kaka zangu na dada zangu, hatujaachwa peke yetu kushawishiwa na kila wazo na badiliko katika mtazamo wa ulimwengu, lakini tunazo nguvu za kuchagua kuamini badala ya kuwa na shaka. Ili kupata nguvu tulizoahidiwa za kufidia za kiroho, ni sharti tuchague kufuata ushauri wa kinabii, tutambue na kutenda kulingana na msukumo wa kiroho, na kuwa watiifu kwa amri za Mungu na tutafute ufunuo wa binafsi. Ni sharti tuchague. Na tuchague nuru ya Mwokozi. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.