2010–2019
Haupo Peke Yako katika Kazi hii
Oktoba 2015


15:48

Haupo Peke Yako katika Kazi hii

Unapotoka kwenye huduma moja ya ukuhani hadi nyingine, wewe utamwona Bwana yupo katika kazi hii pamoja nawe.

Ndugu, tunashukuru kwamba Bwana amewaaita Mzee Ronald A. Rasband, Mzee Gary E. Stevenson, na Mzee Dale G. Renlund  kama Mitume wa Bwana Yesu Kristo. Mioyo yetu, maombi yetu, na imani yetu iwahimili.

Tunajua uwezo wao mkubwa. Na bado watahitaji hakikisho katika miito yao, kama vile sisi tunavyohitaji, kwamba Bwana yu pamoja na wao katika kazi Yake. Shemasi mpya kabisa anahitaji amini hiyo, kama kuhani mkuu wenye uzoefu ambaye anapokea wito mpya.

Kujiamini huku kunakua mnapokuja kuona kwamba Yeye amewaita kupitia watumishi Wake. Uhamasisho wangu ni kukusaidia kujua kwamba wakati unapofanya sehemu yako, Bwana huongeza nguvu Zake kwenye juhudi zako.

Wito wowote tunaopokea katika ufalme wa Bwana huhitaji zaidi kuliko hukumu yetu ya mwanadamu na uwezo wetu binafsi. Miito hii inahitaji msaada kutoka kwa Bwana, ambao utakuja. Hata shemasi mpya atajifunza kwamba ni kweli, na ataendelea kujifunza kwa miaka mingi.

Mmoja ya wajukuu wangu yupo hapa usiku wa leo katika mkutano wake wa kwanza wa ukuhani. Alitawazwa shemasi siku sita zilizopita. Anaweza kutarajia kwamba kazi yake ya kwanza ya wajibu wa ukuhani itakuwa ni kupitisha sakramenti Jumapili ijayo. Maombi yangu ni kwamba ataona muda huo kama ulivyo halisi.

Yeye anaweza kufikiri kazi yake kwa Bwana ni kupitisha trei za sakramenti kwa kila mtu katika mkutano wa sakramenti. Lakini madhumuni ya Bwana siyo tu kuwa watu wapokee mkate na maji. Ni kuwawezesha kushika maagano yao ambayo yatawapeleka wao mbele katika njia ya uzima wa milele. Na kwa hilo kutendeka, Bwana sharti hatoe uzoefu wa kiroho kwa yule mtu ambaye shemasi anampa trei.

Nimeona hilo likitokea katika kituo cha kutunza wazee wakati shemasi alipoinama mbele kupitisha trei kwa bibi mwenye mvi. Aliangalia mkate kama vile ulikuwa una thamani kubwa. Kamwe sijasahau tabasamu lake aliposhiriki na kisha akanyoosha mkono wake kupapasa kichwa cha shemasi, akisema kwa sauti, “Ee, asante sana!”

Shemasi yule alikuwa kwa kawaida akifanya huduma yake ya ukuhani. Na hali, Bwana alizidisha juhudi za tendo la shemasi. Ilikuwa wazi kwamba dada ambaye alikumbuka Mwokozi alipokuwa akionyesha shukrani za dhati kwa huduma ya shemasi. Alikuwa amethibitishiwa kwa kumhudumia sakramenti kwake kwamba angekuwa na Roho kuwa pamoja naye. Hakuwa peke yake siku ile kituo cha kutunza. Wala shemasi hakuwa peke yake katika huduma hii.

Mwalimu kijana katika Ukuhani wa Haruni hawezi kuhisi, anapokwenda kufundisha familia, kwamba ni mwenza pamoja na Bwana katika kazi Yake. Mimi bado nakumbuka ushuhuda rahisi wa mwenza kijana wa mafundisho ya nyumbani ambaye alikuja kwenye nyumba yetu. Roho alithibitisha maneno yake kwangu na familia yangu. Anaweza asikumbuke siku hiyo, lakini nakumbuka.

Bwana atatukuza juhudi za mvulana tena wakati yeye anaitwa kuwa kuhani. Ubatizo wa kwanza anaoufanya unaweza kuwa wa kijana asiyemjua. Anaweza kuwa na wasiwasi kuhusu kama atasema maneno sahihi na kufanya ibada sawasawa.

Lakini Bwana, ambaye yeye ni mtumishi Wake, atatukuza wito wake. Mtu aliyembatiza amechagua kuelekea njia ya uzima wa milele. Bwana atafanya sehemu Yake kubwa. Aliifanya kwangu mwanzo wakati mvulana niliyembatiza, machozi yakitiririka usoni mwake, alisema sikioni mwangu, “Mimi ni msafi. Mimi ni msafi.”

Unapohama kutoka huduma ya ukuhani moja kwenda kwa mwingine, utamwona Bwana yuko kazini pamoja nawe. Nilijifunza hili kutoka na kukutana na rais wa akidi ya wazee katika mkutano mkuu wa kigingi miaka mingi iliyopita. Katika mkutano mkuu kulikuwa na zaidi ya majina 40 ya wanaume yalioletwa ambao walikuwa wapokee Ukuhani wa Melkizedeki.

Rais wa kigingi aliniegemea na kuninon’gonezea, “Wanaume hao wote wazee watarajiwa waliokuwa si awashiriki kikamilifu.” Kwa mshangao, nilimuuliza rais ni mpanglio gani ulitumika kuwaokoa wanaume hawa.

Alimwashiria kijana huko ya nyuma ya  kanisa. Alisema, “Yule pale. Karibu wote wa wanaume hawa wamerudishwa kwa sababu ya yule rais wa akidi ya wazee.” Alikuwa amekaa safu ya nyuma, amevaa kikawaida, miguu yake ameinyoosha pamoja na buti zake zilizo bondeka zimekunjana mbele yake.

Nilimwomba rais wa kigingi kutambulisha kwake baada ya mkutano. Tulipokutana, nilimwambia kijana nilishangazwa kwa kile alichokifanya na nilimwuliza jinsi gani alivyokifanya. Alipandisha mabega yake. Kwa dhahiri hakufikiria anafaa sifa zozote.

Kisha alisema kwa upole, “Namjua kila jamaa asiyeshiriki kikamilifu katika mji huu. Karibu wote wana magari aina ya pikapu. Nina gari pia. Ninaoshewa pikapu yangu kule wanakooshewa zao. Hatimaye, wanakuwa marafiki zangu.

“Kisha ninangoja mpaka kitu fulani kinaharibika katika maisha yao. Siku zote hutokea. Wananieleza kuhusu hivyo. Nasikiliza na siwakosoi. Kisha wanaposema, “Kuna kitu fulani kisichokuwa sawa katika maisha yangu. Lazima kuwe na kitu bora kuliko hivi,’ ninawaambia nini kilichopotea na wapi wanaweza kukipata. Wakati mwingine wananiamini, na wanapofanya hivyo nawachukuwa pamoja nami.”

Unaweza kuona kwa nini alikuwa hana majivuno. Ilikuwa kwa sababu alijua alikuwa amefanya sehemu yake ndogo na Bwana alikuwa anafanya iliyobaki. Ilikuwa ni Bwana aliyegusa mioyo ya wanaume hawa katika matatizo yao. Alikuwa ni Bwana ambaye alikuwa amewapa hisia kwamba ni lazima kuwe na kitu bora kwao na matumaini kwamba wanaweza kukiona.

Kijana, ambaye—kama nyinyi—alikuwa mtumishi wa Bwana, kwa urahisi aliamini kwamba kama alifanya sehemu yake ndogo, Bwana angewasaidia wale wanaume kufuata njia ya nyumbani na kwenye furaha Yeye pekee angeweza kuwapa. Mtu huyu pia alijua Bwana amemwita kama rais wa akidi ya wazee kwa sababu angefanya sehemu yake.

Kutakuwa na nyakati katika huduma zenu wakati hamtakuwa na mafanikio ya ajabu na yanayoonekana kama ya yule rais kijana wa akidi ya wazee. Huu ni muda ambao mtahitaji kuwa wenye kujiamini ili Bwana, akijua mtafanya sehemu yenu katika kazi, aliyowaita kupitia watumishi wake wenye mamlaka. Kuwa imani katika wito kutoka kwa watumishi wa Bwana ilikuwa ni muhimu sana katika huduma ya umisionari ya baba ya babu yangu Henry Erying.

Alibatizwa mnamo Machi 11,1855, St Louis, Missouri. Erastus Snow alimtawaza kwenye ofisi ya kuhani muda mfupi baadaye.  Rais wa Kigingi cha St. Louis, John H. Hart alimwita kuhudumia misheni kwa Taifa la Cherokee mnamo Oktoba 6.1 Alitawazwa mzee mnamo Oktoba 11. Aliondoka kwa farasi kwenda misheni ya Cherokee mnamo Oktoba 24. Alikuwa na umri wa miaka 20 na mwongofu wa miezi sita tu.

Kama mwenye ukuhani yoyote alikuwa na sababu ya kujihisi hajahitimu ama hajajitayarisha vyema, alikuwa Henry Eyring. Sababu ya pekee ambayo angeweza kuwa nayo ya ujasiri wa kwenda ilikuwa kwa ajili alijua katika moyo wake kwamba Mungu amemwita kupitia watumishi Wake wenye mamlaka. Ilikuwa chanzo cha ujasiri wake. Hiyo lazima iwe chanzo cha ujasiri wetu wa kuvumilia, wito wetu wowote ule katika ukuhani.

Baada ya Mzee Henry Eyring kuhudumia kwa miaka mitatu migumu na kufuatia  kifo cha Rais wa misheni, Henry Eyring alipendekezwa na kuthibitishwa kama rais wa misheni kwenye  mkutano uliofanyika Oktoba  6,1858. Alishangazwa na kushtushwa kama shemasi mpya angeshtushwa. Aliandika, “Ilikuwa kabisa kisichotegemewa kwangu mimi kuitwa kwenye ofisi ile yenye majukumu makubwa lakini kama ilivyokuwa mapenzi ya ndugu nilikubali kwa furaha, na kuhisi wakati huohuo udhaifu wangu mkubwa na ukosefu wa uzoefu.”2

Na sasa—Rais Eyring alisafiri kwenda katika Mataifa ya Cherokee, Creek, na Choctaw katika mwaka 1859. Kupitia juhudi  zake, Bwana aliongeza, kama Henry alivyoandika, “idadi katika kanisa.” Alianzisha matawi mawili lakini aliandika kwamba “wachache sana wako hai katika kazi hii.”3

Mwaka mmoja baadaye, alikabiliwa na uhalisi mgumu kwamba viongozi wa kisiasa miongoni mwa watu aliyokuwa akihudumia hawakuruhusu wamisionari wa Watakatifu wa Siku za Mwisho kufanya kazi yao. Alipokuwa akitafakari atafanya nini, alikumbuka maelekezo kutoka kwa rais wake wa misheni aliyepita yakisema kwamba anapaswa kurefusha misheni yake mpaka mwaka 1859.4

Katika Oktoba ya mwaka huo, Henry aliandika kwa Rais Brigham Young kwa maelekezo, lakini hakupokea majibu kwa swali lake. Henry aliandika, “Kutoweza kusikia chochote kutoka kwa Rais wa Kanisa, nilimwita Bwana katika maombi, nikimwomba anionyeshe mawazo na mapenzi Yake kulingana na kubaki kwangu zaidi au kurudi Sayuni.”

Aliendelea: “Ndoto inayofuata nilipewa kama jibu kwa maombi yangu. Niliota nimeshafika katika Jiji la [Salt Lake na mara moja nikaenda kwenye ofisi ya [Rais Brigham] Young, ambako nilimkuta. Nilimwambia: ‘[Rais] Young, nimeacha misheni yangu nimekuja kwa hiari yangu mwenyewe lakini kama kuna makosa katika hili, niko radhi kurudi na kumaliza misheni yangu.’ [Katika ndoto nabii] alijibu: ‘Umekaa kwa muda mrefu wa kutosha, ni sawa.”

Henry aliandika katika shajara yake, “Baada ya kuwa na ndoto ambazo zilikuwa kiuhalisia zimetimizwa nilikuwa na imani ya kuamini, kwamba hii pia ingekuwa na kwa hiyo nikaanza mara moja kujitayarisha kwa kuanza.”

Aliwasili katika Jiji la Salt lake Agosti 29,1860, akiwa ametembea sehemu kubwa ya safari. Siku iliyofuata, aliingia ofisi ya Rais Brigham Young.5

Henry alielezea tukio kwa maneno haya: “[Mimi] nilimtembelea [Rais]Young, ambaye alinipokea [mimi] kwa upole sana. Nilimwambia, ‘[Rais] Young nimekuja bila kuitwa, kama nimefanya makosa, niko radhi kurudi kumalizia misheni yangu. ’[Brigham Young] alijibu: ‘Ni sawa, sisi tumekuwa tunakutafuta.”

Henry alielezea furaha yake, akisema, “Hivyo ndoto yangu kiuhalisia ilitimizwa.”6

Furaha yake ilikuja kutoka uthibitisho kwamba Bwana alikuwa akifanya kazi pamoja naye na kumtunza. Alijifunza kile ambacho ni cha kweli kwetu sote—kwamba watumishi wa Bwana wanapata maongozi kujua mapenzi ya Bwana. Na Henry Eyring amethibitisha, kile ninachojua vilevile, kwamba nabii, kama rais wa ukuhani, anatiwa maongozi na Mungu kuwalinda na kuwatunza watumishi wa Bwana na kuwaita.

Bila kujali wito wako wowote ule katika ukuhani, unaweza wakati mwingine kuhisi Baba wa Mbinguni alikuwa hana habari kukuhusu wewe. Unaweza kuomba kujua mapenzi yake, na kwa nia ya dhati kufanya chochote Yeye anachokuomba kufanya kwa usawa, utapokea jibu.

Baba wa Mbinguni atakuruhusu ujisikie kwamba anakujua, kwamba anadhamini huduma yako, na kwamba unakuwa unastahili maamkuzi unayotaka sana kuyasikia: “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuwe juu ya mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako.”7

Ni ombi yangu kwamba kila mwenye ukuhani atanyoosha mkono wake kwa imani kuokoa kila nafsi ambayo ana wajibu nayo. Mungu ataongeza uwezo Wake kwenye juhudi za mtumishi Wake. Mioyo ya watu itaguswa kufanya chaguzi ambazo zitazileta kwenye mapito ya injili kuelekea kwenye furaha na mbali kutoka huzuni.

Ni ombi langu vilevile kwamba kila mwenye ukuhani atahisi upendo na utunzaji wa makini wa Baba wa Mbunguni, wa Mwokozi, na wa nabii wa Mungu katika wito wake katika ukuhani.

Natoa ushahidi wangu maalumu kwamba tuko katika huduma ya Bwana Yesu Kristo aliyefufuka. Nashuhudia kwamba ametuita wewe na mimi katika huduma Yake akijua uwezo wetu na msaada wa mahitaji yetu. Atabariki juhudi zetu zaidi ya mategemeo yetu ya upendo mkuu, tunapotoa yetu yote katika huduma Yake. Nashuhudia kwamba nabii wa Mungu, ambaye ni rais wa ukuhani wote duniani, anapatiwa maongozi na Mungu.

Natoa shukrani zangu kwa mifano ya wenye ukuhani waaminifu kila mahali. Baba wa Mbinguni na Mwokozi wanashukuru kwamba ninyi mnafanya sehemu yenu. Wanawajua, Wanawalinda, na Wanawapenda. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ons “Minutes of the Conference,” St. Louis Luminary, Oct. 13, 1855, 187.

  2. Henry Eyring letter to Brigham Young, Oct. 7, 1858, Brigham Young Office Files, Church History Library, Salt Lake City.

  3. Henry Eyring report to Church Historian’s Office, Aug. 1860, Missionary Reports, Church History Library, Salt Lake City.

  4. Ona Henry Eyring letter to Brigham Young, Oct. 9, 1859, Brigham Young Office Files, Church History Library, Salt Lake City.

  5. President’s Office Journals, Aug. 31, 1860, vol. D, 137, Brigham Young Office Files, Church History Library, Salt Lake City,

  6. Henry Eyring reminiscences, 1896, typescript, 27–28, Church History Library, Salt Lake City.

  7. Mathayo 25:23.