2010–2019
Moyo Wangu Huyatafakari Siku Zote
Oktoba 2015


10:10

Moyo Wangu Huyatafakari Siku Zote

Mimi kwa uaminifu naomba ninyi mtachagua kuyatafakri maneno ya Mungu kwa mapana na kina.

Kikazi, mimi ni mwekezaji. Kiimani, mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.1 Katika kuendesha biashara, mimi nilitumia kanuni bora za kifedha. Ninapoishi kwa imani, ninajitahidi kufuata kanuni za kiroho ambazo zitanisaidia kuwa zaidi kama Mwokozi.

Mialiko Huleta Baraka

Kati ya baraka nyingi binafsi nilizozipokea katika maisha haya zimekuja kama matokeo ya mtu fulani akinialika kufanya jambo gumu. Katika roho hiyo, ningependa kumwalika kila mmoja wenu mialiko miwili. Wa kwanza una matokeo ya kifedha. Kwa mwaliko wa pili, matokeo yake ni ya kiroho. Mialiko yote, kama ikikubaliwa, itahitaji juhudi za nidhamu ya muda mrefu ili kupata mavuno.

Mwaliko wa Kwanza

Mwaliko wa kwanza ni rahisi: Ninawaalika muweke akiba ya pesa kila wiki. Kiasi unachoweka sio muhimu sana; hiyo ni juu yako. Unapokuza tabia ya kuweka akiba, utanufaika kibinafsi. Na wewe pia unaweza kupata fursa za kuwasaidia wengine kifedha kama matokeo ya bidii yako. Fikiria matokeo chanya ya kuweka akiba kila wiki kwa miezi 6. mwaka, miaka 10, ama zaidi. Juhudi ndogo za kila wakati kwa muda mrefu zinaweza kuzaa matokeo makubwa.2

Mwaliko wa Pili

Mwaliko wangu wa pili ni tofauti kabisa na ule wa kwanza na ni muhimu zaidi kuliko wa kwanza. Na ndiyo huu: Mimi nawaalika ”mtafakariri”3 mstari mmoja wa maandiko kila wiki. Neno tafakariri halipatikani katika kamusi, bali linapatikana katika sehemu moja ya moyo wangu. Basi tafakariri inamaanisha nini? Ningependa kusema ni muunganisho wa asiliamia 80 ya tafakari na asiliamia 20 ya kukariri.

Kuna hatua mbili rahisi:

Kwanza, chagua mstari wa maandiko kila wiki na uuweke mahali ambapo utauona kila siku.

Pili, soma ama fikiria mstari huu mara kadhaa kila siku na utafakari maana ya maneno yake na vishazi muhimu katika wiki yote.

Fikiria matokeo ya kuinua ya kufanya hivyo kila wiki kwa miezi 6, mwaka, miaka 10, ama zaidi.

Unapofanya juhudi hii, utahisi amani kuu ya akilini na ongezeko la kiroho. Wewe utaweza pia kuwafunza na kuwainua wale uwapendao kwa njia za maana sana.

Kazama Ukitumia Neli

Kama ukichagua kutafakariri kila wiki, unaweza kuhisi kama mtu aliyependelea kuzama majini kwa neli hapo zamani lakini sana ameamua kujaribu kuzama majini kwa vifaa vya hewa. Kwa uamuzi huo, uelewa wa kindani wa kanuni za injili utakuwa wako na mtazamo mpya wa kiroho utabariki maisha yako.

Kuzama Ukitumia Vifaa vya Hewa

Unapofikiria juu ya mstari uliochaguliwa kila wiki, maneno, na vishazi vitaandikwa kwenye moyo wako.4 Maneno na vishazi pia vitaandikwa kwenye akili yako. Kwa maneno mengine, kukariri kutafanyika kwa urahisi na uasili. Lakini lengo la msingi la kutafakariri ni kukupa mahali palipoinuliwa kwa mawazo yako kwenda—mahali ambapo panakuweka karibu na Roho wa Bwana.

Mwokozi alisema, “Yahifadhini katika akili zenu daima maneno ya uzima5 Kutafakariri ni njia rahisi na ya kuelimisha ya kufanya hivyo tu.

Naamini Nefi alikuwa mtafakariri. Alisema, ”Kwani moyo wangu unafurahia maandiko, na moyo wangu huyatafakari [siku zote], na kuyaandika kwa elimu na faida ya watoto wangu.”6 Alikuwa anawajali watoto wake alipokuwa anatafakari na kuandika maandiko. Je! Familia yako inaweza kufaidi vipi unapoendelea siku zote kujitahidi kuijaza akili na maneno ya Mungu?

Mstari wangu

Hivi majuzi nilitafakariri Alma 5:16. Inasema, ”Ninawaambia, mnaweza kuwaza kwamba mnasikia sauti ya Bwana, siku ile, ikiwaambia: Njooni kwangu mliobarikiwa, kwani tazameni, kazi zenu zimekuwa kazi za haki usoni mwa dunia?”

Mwishoni mwa wiki, haya ndiyo yaliandikwa katika akili yangu: Fikiria kusikia sauti ya Bwana ikisema, ”Njooni kwangu mliobarikiwa, kwani tazameni, kazi zenu zimekuwa kazi za haki” usoni mwa dunia.”(Alma 5:16).

Kama unavyoweza kuona, mimi sikukariri mstari wote neno kwa neno. Hata hivyo, nilitafakari tena na tena vipengele muhimu vya mstari huu na pale vinapatikana. Lakini sehemu bora ya mchakato huu ilikuwa kupata mahali pa juu sana pa mawazo yangu kwenda. Wiki yote nilitazama picha ya Mwokozi akisema maneno ya kunitia moyo mimi. Hiyo taswira iligusa moyo wangu na kuwa maongozi kwangu ya kutaka kufanya ”kazi ya haki.” Hicho ndicho kinaweza kutokea wakati sisi ”tunapomtazama [Kristo] katika kila wazo.”7

Lazima Tujibu Mapigo

Unaweza kuuliza, ”Kwa tufanye hivyo?” Mimi nitajibu kwamba tunaishi katika nyakati za kuzagaa kwa uovu unaozidi kila siku. Hatuwezi kukubali hali kama ilivyo tu na kulishwa maneno machafu na picha ovu zilizopo karibu kila mahali tunapogeuka na tusifanye chochote katika mjibizo. Lazima Tujibu Mapigo. Wakati akili zetu zimejazwa na mawazo na picha za kuinua, wakati sisi ”daima tunamkumbuka yeye,”8 hamna nafasi iliyobaki kwa uchafu na taka.

Katika Kitabu cha Mormoni, Yesu Kristo anawaalika watu wote ”kutafakari juu ya vitu ambayo [Yeye] amesema.”9 Chukulia kutafakariri kama nyongeza katika kujifunza maandiko kibinafsi na kama familia, lakini kamwe usiache iwe mbadala. Kutafakariri ni kitu kama tembe ya vitamini ya ichukuayo muda zaidi katika lishe yako ya sasa ya kiroho.

Ni Vigumu Sana

Unaweza kusema, ”Kutafakariri inaonekana kuwa vigumu sana kwangu.” Usife moyo. Kitu kigumu kinaweza kuwa kizuri. Kristo anatualika sisi tunafanye vitu vingi vigumu kwa sababu Yeye anajua tutabarikiwa kama matokeo ya juhudi zetu.10

Maandiko kwenye Simu

Jirani yetu kijana alipata njia rahisi ya kutafakariri. Yeye huyaweka maandiko yake ya wiki kwenye skrini ya simu yake. Wazo lingine unaloweza kujaribu ni kushiriki mstari wako na ndugu zako, mtoto wako, ama rafiki yako. Mke wangu, Julie, pamoja nami tunasaidiana. Sisi tunachagua mistari yetu kila Jumapili. Yeye huiweka yake kwenye jokofu letu. Mimi huiweka yangu katika gari langu. Kisha tunashiriki mawazo yetu kuhusu mistari yetu wiki yote. Pia tunapenda kujadili mistari yetu pamoja na watoto wetu. Tunapofanya hivyo, inaonekana vizuri sana kwao kushiriki mawazo yao pamoja nasi kuhusu neno la Mungu

Dada Durrant akibandika maandiko kwenye jokofu
Ndugu Durrant akibandika maandiko kwenye gari

Julie pamoja nami ni sehemu ya kundi la mtandaoni ambapo wanafamilia, marafiki, na wamisionari wanaweza kushiriki maandiko kila wiki na mara kwa mara kujumuisha wazo husika ama ushuhuda. Kuwa sehemu ya kundi huifanya rahisi kushikilia jambo hili. Binti yangu wa shule ya upili na kundi la marafiki zake wanatumia vyombo ya habari na ujumbe mfupi kushiriki maandiko mmoja na mwingine.

Msichana anashiriki maandiko kwenye mtandao wa kijamii

Tafadhali msisite kujumuisha watu wa imani zingine katika makundi yenu. Wao pia wanatafuta njia za kuinua mawazo yao na kuhisi kuwa karibu na Mungu.

Manufaa Yake ni Nini?

Dada Durrant akijifunza maandiko

Kwa hivyo, manufaa yake ni nini? Julie pamoja nami tumekuwa tukitafakariri mstari kila wiki kwa zaidi ya miaka mitatu sasa. Mwanzoni, tuliweka lengo la miaka 20. Hivi majuzi aliniambia: ”Wakati ulinialika kutafakariri maandiko kila wiki kwa miaka 20 nilishangaa kama ninaweza kufanya hivyo kwa mwezi mmoja. “Mimi sina hizo shaka tena. Mimi siamini imekuwa furaha jinsi kuweka maandiko kwenye jokofu kila wiki na tu kwa kuyatafakariri kila wakati ninapoyaona, huinua roho yangu.”

Baada ya kutafakariri kwa miezi sita, dada kutoka Texas, Marekani, alisema: ”Ushuhuda wangu umeimarishwa,  ... na mimi nimehisi kuwa karibu na Baba yangu wa Mbinguni. ... Mimi napenda jinsi neno la Mungu linanibadilisha kuwa bora.”

Rafiki tineja aliandika: ”Mimi hasa nimefurahia kuweza [kutafakariri] kwa sababu kumenisaidia kuzingatia mambo ambayo ni muhimu sana.”

Mmoja wa wamisionari wetu alishiriki haya: ”Mimi nimekuwa nikitafakariri mstari kila wiki tangu June 2014, na napendelea hivyo. ... Maandiko haya yamekuwa kama marafiki zangu kwamba ninaweza kuyategemea nyakati za haja.”

Kwangu mimi, nimehisi Roho zaidi sana katika maisha yangu ninapotafakariri kila wiki. Upendo wangu wa maandiko umeongezeka kama matokeo ya kujitahidi ”kuuacha wema yapambe mawazo [yangu] bila kukoma.11

Fikiria mwaliko huu na baraka kuu zilizoshikirishwa na Nefi: ”Kwa hivyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherekea neno la Kristo, na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele.12 Katika roho ya ”kusherekea neno la Kristo,” kutafakariri ni kama kumega kwa meno chakula kitamu na kisha kukitafuna pole pole, ili ukifurahie kikamikifu.

Mwanamke alika saladi

Mstari Wako ni Upi?

Je! Utatafakariri mstari wa maandiko kila wiki kwa sehemu ya mwezi hu uliyobakia? mwaka huu uliyobakia? Je! Na hata zaidi labda? Julie pamoja nami tuliwaalika wamisionari wetu shupavu wa Texas Dallas watafakariri pamoja nasi kwa miaka 20. Tutavuka mstari wa kumaliza pamoja katika muda mfupi wa miaka 17. Kisha tutaweka lengo jipya la kuinua mawazo yetu na kutuleta karibu na Kristo.

Unaweza kututafuta kwa kuuliza, ”Mstari Wako ni Upi?” Lakini unapofanya hivyo, kuwa tayari kushiriki maandiko yako pia. Kila mmoja wetu atainuliwa kama matokeo ya ubadilishanaji wetu.

Unaweza kufikiria jinsi maisha yako na ya familia yako yanaweza kubadilika kama utaandika mstari mpya wa maandiko katika moyo wako na akili yako kila wiki kwa miezi michache ama miaka michache ijayo ama hata zaidi?

Yesu Kristo Ndiye Mfano Wetu

Yesu Kristo lazima alikuza upendo wa maandiko akiwa mdogo sana. Yeye lazima alikuwa akisoma na kutafakari maandiko akiwa mtoto mdogo ili kuwa na mazungumzo ya maana na wasomi wenye hekima katika hekalu alipokuwa na umri wa miaka 12.13 Yeye alianza huduma Yake akiwa umri wa miaka 30,14 na Yeye alirejea maandiko akiwa mdogo na kila mara kote katika huduma Yake.15 Je! Tunaweza kusema bila kukosea kwamba Yesu alitumia karibu miaka 20 kujifunza na kuyatafakari maandiko kama sehemu ya maandalizi ya huduma Yake. Je! Kuna kitu unachohitaji kukifanya leo cha kukuandaa mwenyewe kiroho kwa nafasi za kufundisha siku zijazo na kubariki familia yako na marafiki?

Fanya Imani Yako na Ufanye Hivyo.

Katika rejeo, mimi natumaini utaamua kuweka akiba pesa kila wiki. Fanya imani yako, fanya nidhamu mwenyewe, na ufanya hivyo. Mimi pia kwa imani naomba wewe utachagua kutafakari maneno ya Mungu kwa mapana na kina kila wiki. Fanya imani yako, fanya nidhamu mwenyewe, na ufanye hivyo.

Tofauti na mwaliko wangu wa kwanza wa kuweka akiba pesa manufaa yote ta mwaliko wangu wa pili wa kuokoa nafsi mwaliko utakuwa wako milele na milele—mbali na nondo na kutu la ulimwengu huu.16

Mzee D Todd Christofferson alitoa huu ushauri wa wazi na ahadi: ”Jifunze maandiko kwa makini, makusudi. Tafakari na uombe juu yake. Maandiko ni ufunuo, na yataleta ufunuo wa zaida.”17

Hitimisho

Mimi nawaahidi hautajuta kuandika mstari wa maandiko kwenye akili na moyo wako kila wiki. Utapata hisia za madhumuni ya kiroho, ulinzi, na nguvu za kila mara.

Kumbuka maneno ya Yesu Kristo wakati alisema, ”Mfanye vitu ambavyo mmeniona nikifanya.”18 Na sisi tuyatumie kikamilifu maneno Yake katika maisha yetu, Mimi naomba hivyo katika jina la Yesu Kristo, amina.