Neno la Kupendeza la Mungu
Neno la kupendeza la Mungu linatuonyesha haja wa toba ya kila mara katika maisha yetu ili tuweze kushika ushawishi wa Roho Mtakatifu.
Wengi wetu ambao tunakutana ili kushiriki katika mkutano huu tumekuja “kusikia neno la kupendeza la Mungu, ndio, neno ambalo linaponya nafsi iliyojeruhiwa” (Yakobo 2:8). Neno hilo linaweza kupatikana katika maandiko na katika ujumbe kutoka kwa viongozi wetu, na kutuletea matumaini na faraja katika giza la mateso.
Kupitia kwa uzoefu wetu katika maisha, tunajifunza kuwa shangwe katika dunia hii si kamili, lakini katika Yesu Kristo furaha yetu ni kamili (ona M & M 101:36). Yeye atatupa nguvu ili tusiweze kuteseka kwa namna yoyote ya mateso isipokuwa imezwe kwenye shangwe Yake (ona Alma 31:38).
Mioyo yetu inaweza kujazwa na machungu tunapoona mpendwa akiteseka na maumivu ya ugonjwa wa mbaya.
Kifo cha mtu tunayempenda kinaweza kuacha sehemu tupu katika nafsi zetu.
Wakati baadhi ya watoto wetu wanapopotea kutoka kwa njia ya injili, tunaweza kujihisi wenye hatia na kuwa na wasiwasi juu ya hatima yao ya milele.
Matumaini ya kufunga ndoa ya selestia na kuanzisha familia katika maisha haya yanaweza kuanza kufifia kadri muda unavyosonga
Unyanyasaji kutoka kwa wale ambao wanatakiwa kutupenda kunaweza kuacha makovu machungu katika nafsi zetu.
Uzinzi wa mwanandoa unaweza kuharibu uhusiano tuliotumainia utakuwa wa milele.
Haya na mateso mengine mengi yanayohusiana na hali hii ya majaribu wakati mwingine hutufanya tujiulize swali moja lile ambalo Nabii Joseph Smith aliuliza: “Ee Mungu, uko wapi?” (M&M 121:1).
Katika nyakati hizo ngumu katika maisha yetu, neno la kupendeza la Mungu ambalo huponya nafsi iliyojeruhiwa huleta ujumbe ufuatao wa faraja kwa moyo wetu na akili yetu:
“Amani iwe katika nafsi yako; taabu yako na mateso yako yatakuwa kwa muda mfupi;
“Na halafu, kama utastahimili vyema, Mungu atakuinua juu” (M&M 121: 7–8).
Neno la kupendeza la Mungu hutujaza na matumaini, kujua kwamba wale walio waaminifu katika dhiki, watapata malipo makubwa zaidi katika ufalme wa mbinguni na kwamba “kwani baada ya taabu kubwa huja baraka” (ona M&M 58:3–4).
Neno la kupendeza la Mungu, kama ilivyonenwa kwa njia ya manabii, linatupa uhakikisho kwamba kuunganishwa kwetu milele, kukiendelezwa na uaminifu wetu kwa ahadi za kiungu ambazo tulipewa kwa huduma yetu bora kwa ajili ya ukweli, kutatubariki na vizazi vyetu (ona Orson F. Whitney, in Conference Report, Apr. 1929, 110).
Pia kunatupa uhakikisho kwamba, baada ya sisi kuishi maisha ya uaminifu, hatutapoteza baraka yoyote kwa kutokufanya mambo fulani kama kamwe hatukupewa nafasi ya kuyafanya. Kama tumeishi kwa uaminifu mpaka wakati wa kifo chetu, “tutapata baraka zote, kuinuliwa na utukufu ambao kila mwanamume au mwanamke [ambaye amepata nafasi] hiyo atapata.” (Ona The Teachings of Lorenzo Snow, ed. Clyde J. Williams [1984], 138.)
Sasa, ni muhimu kuelewa kwamba baadhi ya mateso na dhiki inaweza kuingia katika maisha yetu kama kwa kweli tutashindwa kutubu dhambi zetu. Rais Marion G. Romney alifundisha: “Mengi ya mateso na dhiki zinazopitiwa na watu wa dunia hii ni matokeo ya dhambi isiotubiwa na isiokomeshwa. … Kama vile mateso na huzuni hufuata dhambi, hivyo furaha na shangwe hufuata msamaha wa dhambi” (in Conference Report, Apr. 1959, 11).
Kwa nini ukosefu wa toba husababisha mateso na maumivu?
Moja wapo wa majibu yanayowezekana ni kwamba “adhabu iliwekwa na sheria ya haki kutolewa, ambayo ilileta majuto ya dhamiri” (Alma 42:16, 18; ona pia mstari wa 16). Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba sisi ndio hujilaani wenyewe na kwamba ni mateso ya kukata tamaa katika akili zetu ambayo huyafanya kuwa makali kama ziwa la moto na kibiriti (ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 224).
Tukijaribu kutuliza dhamiri yetu kwa kujaribu “kujisamehe wenyewe hata kwa njia ndogo kwa sababu ya dhambi zetu” (Alma 42:30 au kwa kujaribu kuzificha, kitu pekee ambacho tutatimiza ni kumkosea Roho (ona M & M 121: 37) na kuchelewesha toba yetu. Aina hii ya nafuu, kando na kuwa ya muda mfupi, hatimaye italeta maumivu zaidi na huzuni katika maisha yetu na itapunguza uwezekano wetu wa kupokea ondoleo la dhambi.
Kwa mateso ya aina hii, neno la kupendeza la Mungu pia huleta faraja na tumaini; linatuambia kwamba kuna nafuu kutokana na maumivu yanayosababishwa na athari za dhambi. Nafuu hii inatokana na toleo la Upatanisho wa Yesu Kristo na inafanyika tunapofanya imani Kwake, kutubu, na kuwa watiifu kwa amri Zake.
Ni muhimu kwamba tutambue kwamba kama vile ondoleo la dhambi, toba ni mchakato na si kitu kinachotokea kwa wakati moja. Inahitaji uthabiti katika kila moja ya hatua yake.
Kwa mfano, tunaposhiriki sakramenti, tunamwonyesha Bwana kwamba tutamkumbuka daima na kushika amri Zake. Huo ni usemi wa dhamira yetu ya dhati.
Wakati tunapoanza kumkumbuka na kushika amri Zake kila siku—na sio tu siku ya Sabato—ndipo ondoleo la dhambi zetu huanza kufanyika na ahadi Yake ya kuwa na Roho Wake pamoja nasi huanza kutendeka.
Bila utii wa kweli ambao ni lazima uongozane na dhamira yetu, athari za ondoleo zinaweza kutoweka kwa muda mfupi na uenzi wa Roho huanza kujiondoa. Tutakuwa kwenye hatari ya kumheshimu kwa midomo yetu ilihali tukiondoa mioyo yetu toka Kwake (ona (ona 2 Nefi 27:25).
Mbali na kutufariji, neno la kupendeza la Mungu linatuonya kwamba mchakato huu wa kupokea ondoleo la dhambi zetu unaweza kuingiliwa wakati tunajihusisha “katika majivuno ya ulimwengu,” na unaweza kuendelezwa tena kwa njia ya imani ikiwa tutatubu kwa dhati na kujinyenyekeza (ona M&M 20:5–6).
Ni majivuno gani yanayoweza kuingilia kati katika mchakato wa kupokea ondoleo la dhambi zetu na ambayo yanayohusishwa na kuweka siku ya Sabato kuwa takatifu?
Baadhi ya mifano ni pamoja na kuchelewa kufika kwa mkutano wa sakramenti bila sababu halali; kuwasili, kabla ya kujichunguza wenyewe, kula mkate na kunywa kutoka kwa kikombe isivyostahili (angalia na 1 Wakorintho 11:28); kuwasili kabla ya kukiri dhambi zetu na kabla ya kuomba Mungu msamaha kwa ajili yazo.
Mifano mingine: kukosa staha kwa kubadilishana ujumbe kutoka kwa vifaa vyetu vya kielektroniki, na kuacha mkutano mara tu baada ya kushiriki sakramenti, na kushiriki katika shughuli nyumbani kwetu ambazo hazifai kwa siku hiyo takatifu.
Ni nini kinachoweza kuwa moja ya sababu ya kwa nini, sisi hatujui haya yote, mara nyingi tunashindwa kuweka siku ya Sabato takatifu?
Katika kitabu cha Isaya, tunaweza kupata jibu kwamba, ingawa inahusiana na Sabato, pia inahusu amri nyingine ambazo ni lazima tutii. “Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu;” (Isaya 58:13).
Maneno muhimu ni “geuka … kutoka kwa anasa yako,” au kwa maneno mengine, kufanya mapenzi ya Mungu. Mara nyingi, mapenzi yetu—yakijengwa na tamaa, hamu, na tamaa ya mtu wa kawaida—haziambatani na mapenzi ya Mungu. Nabii Brigham Young alifundisha kwamba “wakati mapenzi, tamaa, na hisia za mtu ni tiifu kwa Mungu na matakwa Yake, mtu huyo amesafishwa. Ni kwa mapenzi yangu kumezwa katika mapenzi ya Mungu, ambayo itanielekeza katika mema yote, na hatimaye kunipa uzima wa milele” (Deseret News, atika Sept. 7, 1854, 1).
Neno la kupendeza la Mungu linatualika kutumia uwezo wa Upatanisho ili kuutumia kwetu sisi na kuweza kupatanishwa na mapenzi Yake—na si kwa mapenzi ya shetani na mwili—hivyo sisi, kwa neema Yake, tunaweza kuokolewa (ona 2 Nefi 10: 24–25).
Neno la kupendeza la Mungu ambalo tunashiriki leo linatuonyesha umuhimu wa toba ya kila mara katika maisha yetu ili tuweze kuweka ushawishi wa Roho Mtakatifu kwa muda mrefu iwezekanavyo.
Kuwa na uenzi wa Roho kutatufanya kuwa watu bora. Kutanong’oneza amani na furaha kwa nafsi zetu; itaondoa uovu, chuki, wivu, ugomvi, na uovu wote kutoka mioyoni mwetu; na nia yetu yote itakuwa ni kutenda mema, kuleta haki, na kujenga ufalme wa Mungu (onaTeachings: Joseph Smith, 98).
Pamoja na ushawishi wa Roho Mtakatifu, hatutaudhika, wala hatutawaudhi wengine; tutajihisi wenye furaha zaidi, na akili zetu zitakuwa safi zaidi. Upendo wetu kwa wengine utaongezeka. Tutakuwa na nia zaidi ya kusamehe na kueneza furaha kwa wale walio karibu nasi.
Tutashukuru kuona jinsi wengine wanavyoendelea, na tutatafuta mazuri kwa wengine.
Ni ombi langu kwamba tutaona furaha inayotokana na kujitahidi kuishi katika haki na kwamba tutaweza kuweka uenzi wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu kwa njia ya toba ya kweli na daima. Tutakuwa watu bora, na familia zetu zitabarikiwa. Juu ya kanuni hizi nashuhudia katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.