Kumkumbuka Yule Tunayemwamini
Tumaini letu la kuishi tena pamoja na Baba linategemea Upatanisho wa Yesu Kristo
Nilipokuwa na umri wa miaka tisa, bibi yangu mzazi mwenye mvi, wa futi nne-inchi kumi na moja (150-sentimita), alikuja kukaa wiki chache na sisi nyumbani kwetu. Siku moja mchana alipokuwa pale, kaka zangu wawili pamoja nami tuliamua kuchimba shimo kwenye uwanja pande ya barabara kutoka nyumbani kwetu. Sijui ni kwa nini tulifanya hivyo. Wakati mwingine wavulana hutaka tu kuchimba mashimo. Tulikuwa wachafu kidogo, lakini sio kitu ambacho kingetuletea shida sana. Vijana wengine katika kitongoji waliona jinsi ilivyosisimua kuchimba shimo na wakaanza kusaidia. Kisha sisi sote tukachafuka pamoja. Ardhi ilikuwa ngumu, hivyo tukavutana mpira wa maji na kuweka maji kidogo ndani ya shimo ili kulainisha udongo. Tulipatwa na tope tulipokuwa tukichimba, lakini shimo liliweza kuwa refu zaidi.
Mtu katika kikundi chetu aliamua kwamba tugeuze shimo letu kuwa bwawa la kuogelea, hivyo tukaijaza kwa maji. Kwa vile nilikuwa mdogo na nilitaka kukubalika, nilishawishiwa kuruka ndani na kujaribu. Sasa nilikuwa mchafu kwa kweli. Sikuwa nimepanga kuchafuka na matope, lakini hapo ndipo mimi niliishia.
Ilipoanza kuwa baridi, nilivuka barabara, nikitaka kutembea hadi nyumba kwetu. Bibi yangu alinikuta katika mlango wa mbele na alikataa kunifungulia mlango. Aliniambia kuwa ikiwa ataniruhusu ndani, nitaingiza matope ndani ya nyumba ambayo alikuwa amesafisha. Hivyo nilifanya kile ambacho yeyote mwenye umri wa miaka tisa angefanya kulingana na hali ilivyokuwa na kukimbia mlango wa nyuma, lakini yeye alikuwa mwepesi kuliko nilivyofikiri. Niliingiwa na hamaki, nikagonga miguu yangu, na kudai kuingia ndani ya nyumba, lakini mlango ulibakia umefungwa.
Nilikuwa nimelowa maji, matope, baridi, na katika mawazo ya utoto wangu nilifikiri kuwa nitakufa katika bustani langu mwenyewe. Hatimaye, nilimuuliza kile ambacho ningefanya ili kuingia ndani ya nyumba. Kabla sijajua, nilijikuta nimesimama katika bustani ilhali bibi yangu akiniosha kwa mpira wa maji. Baada ya kile kilichoonekana kama milele, bibi yangu alinitangaza kuwa msafi na kuniruhusu niingie nyumbani. Ndani ya nyumba kulikuwa na joto na nikaweza kuvaa nguo kavu na safi.
Kwa mifano hii halisi ya maisha akilini, tafadhali fikiria maneno yafuatayo ya Yesu Kristo: “Na hakuna kitu kichafu kinachoweza kuingia kwenye ufalme wake; kwa hivyo hakuna chochote ambacho huingia kwenye pumziko lake isipokuwa wale ambao wameosha nguo zao ndani ya damu yangu kwa sababu ya imani yao, na kutubu kwa dhambi zao zote, na uaminifu wao hadi mwisho.”1
Kusimama nje ya nyumba yetu na kuoshwa na maji na bibi yangu ilikuwa vibaya na haikufurahisha. Kunyimwa nafasi ya kurudi na kuwa pamoja na Baba yetu wa Mbinguni kwa sababu tulichagua kubakia katika au kuchafuliwa na shimo la matope la dhambi inaweza kusikitisha milele. Hatupaswi kujidanganya wenyewe kuhusu kinachohitajika ili kurudi na kubakia katika uwepo wa Baba yetu aliye Mbinguni. Lazima tuwe wasafi.
Kabla ya kuja hapa duniani, tulishiriki kama wana na mabinti wa kiroho wa Mungu katika baraza kuu.2 Kila mmoja wetu alikuwa makini, na hakuna hata mmoja wetu aliyelala usingizi. Katika baraza hilo, Baba yetu wa Mbinguni aliwasilisha mpango. Kwa sababu mpango ulihifadhi haki yetu ya kujiamulia na ulihitaji kwamba tujifunze kutokana na uzoefu wetu na si tu kutoka Kwake, Yeye alijua kwamba tutatenda dhambi. Pia alijua kwamba dhambi ingetufanya kuwa wachafu na kutoweza kurudi katika uwepo Wake kwa sababu mahali anapoishi ni safi hata zaidi kuliko nyumba iliosafishwa na bibi yangu.
Kwa sababu Baba yetu wa Mbinguni anatupenda na ana kusudi Lake “kuleta kutokufa na uzima[wetu] wa milele,”3 Mpango wake ulijumuisha jukumu la Mwokozi; mtu ambaye angeweza kutusaidia kuwa safi bila kujali jinsi tumekuwa wachafu. Wakati Baba yetu wa Mbinguni alipotangaza haja ya Mwokozi, naamini kila mmoja wetu aligeuka na kumtazama Yesu Kristo, mzaliwa wa Kwanza katika Roho, mmoja ambaye aliyeendelea kadri ya kuwa kama Baba.4 Naamini kila mmoja wetu alijua itabidi iwe ni Yeye, kwamba hakuna hata mmoja wetu angeweza kuifanya, bali kwamba Yeye angeweza na kwamba atafanya hivyo.
Katika bustani ya Gethsemane na msalabani Golgotha, Yesu Kristo aliteseka mwili na roho, akatetemeka kwa sababu ya uchungu, alimwaga damu katika kila kinyweleo, akamlilia Baba Yake kuiondoa kikombe cha machungu kutoka Kwake,5 na hata hivyo bado Yeye alikinywa.6 Kwa nini alifanya hivyo? Kwa maneno Yake, Alitaka kumtukuza Baba Yake na kukamilisha “maandalizi yake kwa wanadamu.”7 Alitaka kuweka ahadi Yake na kuwezesha kurudi kwetu nyumbani. Ni nini Yeye anatuuliza tufanye kama jibu? Anatusihi kwa urahisi tukiri dhambi zetu na kutubu ili tusiweze kuteseka jinsi Alivyoteseka.8 Anatualika kuwa wasafi ili tusiweze kuachwa nje ya nyumba ya Baba yetu wa Mbinguni.
Ingawa kuepuka dhambi ndio mtindo upendwao katika maisha, kulingana na thamani ya Upatanisho wa Yesu Kristo, haijalishi ni dhambi gani tumefanya au ni kina gani tumeingia katika lile tope . Haijalishi ikiwa umeaibika au kuona haya kwa ajili ya dhambi, kama vile Nabii Nefi alivyosema, “zinatunasa kwa urahisi.”9 Haijalishi kwamba sisi tuliuza haki yetu ya uzaliwa wa kwanza kwa chakula cha dengu.10
Cha muhimu ni kwamba Yesu Kristo, ni Mwana wa Mungu, aliteseka “maumivu na masumbuko na majaribio ya kila aina” ili “ ajue kulingana na mwili jinsi ya kuwasaidia watu wake kulingana na unyonge wao.”11 Cha muhimu ni kwamba alikuwa tayari kujinyenyekeza,12 kuja hapa duniani na kujishusha “chini yao wote”13 na kuteseka “mikangamo makali kuliko mtu yeyote”14 Cha muhimu ni kwamba Kristo anatetea kesi yetu mbele ya Baba, ”akisema: “Baba, tazama mateso na kifo chake Yeye ambaye hakutenda dhambi, ambaye ulipendezwa Naye … Kwa hiyo, Baba, wasamehe hawa ndugu zangu ambao wanaamini juu ya neno langu, ili waweze kuja kwangu na kupata uzima usio na mwisho.”15 Hicho ndicho cha maana na ndicho kinachopaswa kutupatia sote matumaini mapya na dhamira ya kujaribu mara moja zaidi, kwa sababu hajatusahau.16
Nashuhudia kwamba Mwokozi kamwe hatatuacha tunapomtafuta kwa unyenyekevu ili kutubu; kamwe hatatuona kama kusudi lililopotea; Kamwe hatasema, “Ee hapana, si wewe tena”; kamwe hatatukataa kwa sababu ya kushindwa kuelewa jinsi ilivyo vigumu kuepuka dhambi. Anayaelewa yote kikamilifu, ikiwemo pamoja na hali ya huzuni, aibu, na kuchanganyikiwa ambayo ni matokeo yasiyoepukika ya dhambi.
Toba ni halisi na inafanya kazi. Sio uzoefu wakutunga au bidhaa “ya akili wazimu.”17 Ina uwezo wa kuinua mizigo na kuibadilisha na matumaini. Inaweza kusababisha mabadiliko makuu ya moyo itakayotuletea kuwa “hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima.”18 Kutubu kwa haja sio rahisi. Mambo yenye umuhimu wa milele ni nadra kuwa hivyo. Lakini matokeo yake ni ya thamani. Kama vile Rais Boyd K. Packer alivyoshuhudia katika hotuba yake ya mwisho kwa wale Sabini wa Kanisa: Wazo ni hii: Upatanisho hauachi nyayo, hauachi alama. Kile unarekebisha kinarekebika. ... Upatanisho hauachi nyayo, hauachi alama. Huponya tu, na kile umeponya hubakia kimepona.”19
Vivyo hivyo matumaini yetu ya kuishi tena na Baba hutegemea Upatanisho wa Yesu Kristo, juu ya utayari wa Yule kiumbe mmoja asiyekuwa na dhambi kujichukulia juu Yake, tofauti kabisa na matakwa ya haki, uzito wote wa dhambi za wanadamu wote, zikiwemo zile dhambi ambazo wana wengine na mabinti wa Mungu huamua kuteseka wenyewe bila sababu kwa ajili yake.
Kama washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho, tunatambua uwezo mkuu unatokana na Upatanisho wa Mwokozi kuliko watu wengine wengi kwa sababu tunajua kwamba tukifanya maagano, kutubu kila mara, na kuvumilia hadi mwisho, Atatufanya warithi pamoja na Yeye20 na kama Yeye tutapokea yote ambayo Baba anayo.21 Hilo ni fundisho muhimu sana, na bado ni kweli. Upatanisho wa Yesu Kristo hufanya mwaliko wa Mwokozi kuwa “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”22 inawezekana kikamilifu badala ya kutofikiwa kwa shida.
Maandiko yanafundisha kwamba kila mtu lazima “wahukumiwe kulinganana hukumu takatifu ya Mungu.”23 Katika siku hiyo hakutakuwa na nafasi ya kujificha miongoni mwa kundi kubwa au kulaumu wengine kama kisingizio kwa uchafu wetu. Shukrani, maandiko pia yanafundisha kwamba Yesu Kristo, Yeye ambaye aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu, ambaye ni wakili wetu kwa Baba, ambaye anatuita marafiki Zake, ambaye anatupenda hadi mwisho, Yeye hatimaye atakuwa ndiye mwamuzi wetu. Moja ya baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo zinazopuuzwa kila wakati ni kuwa “Baba ... amempa Mwana hukumu yote.”24
Ndugu na dada, ukihisi kuvunjika moyo au unashangaa ikiwa utawahi kutoka nje ya shimo la kiroho ambao umechimba, tafadhali kumbuka ni nani anayesimama “kati [yetu] na haki,” “aliyejawa na huruma kwa watoto wa watu,” na aliyejichukulia juu Yake maovu yetu na makosa na “kutosheleza madai ya haki.”25 Kwa maneno mengine, jinsi Nefi alivyofanya katika wakati wake wa mashaka, kukumbuka tu kwa “Yule [wewe] unayemwamini,”26 hata Yesu Kristo, na kisha utubu na uone tena “mng’aro mkamilifu wa tumaini.”27 Katika jina la Yesu Kristo, amina.