2010–2019
Waliobarikiwa na Wenye Heri ni Wale Wanaoshika Amri za Mungu
Oktoba 2015


10:19

Waliobarikiwa na Wenye Heri ni Wale Wanaoshika Amri za Mungu

Vikwazo vilivyowekwa na Bwana vinatujengea bandari salama dhidi ya maovu na maongozi haribifu.

Wakati fulani uliopita, nikiwa natembelea Australia, nilisafiri hata kwenye Horseshoe Bay maridadi, inayo maarufu kwa mchezo wa kuteleza mawimbini. Nilipokuwa nikitembea ufukweni, nilivutiwa sana na uadhimu wa ukubwa wa mawimbi yakipasuka kwa kishindo nje tu ya ghuba na mawimbi madogo madogo yakija karibu na ufukwe.

Nilipoendelea na matembezi yangu, nilikutana na kundi la watelezaji mawimbini Wamarekani. Walikuwa wazi wameudhika kuhusu kitu fulani, wakiongea kwa sauti na wakifanya ishara kuelekea bahari. Wakati nilipowauliza shida ilikuwa ni nini, walionyesha tu nje ya ghuba ambapo mawimbi makubwa yalikuwa yanavunjika.

”Tazama kule,” mmoja wao aliniambia kwa hasira. ”Jee unaweza kuona kizuizi?’’ Nikitazama kwa makini sasa, niliweza kwa hakika kuona kizuizi kikinyooka kupita mdomo wa ghuba, pale ambapo mavimbi makubwa ya kutamanisha yalikuwa yakivunjika. Kizuizi kilionekana kama kimetengezwa na kimia kizito na kuhimiliwa na maboya juu ya maji. Kulingana na watelezaji wa mawimbi, kilishuka hadi chini ya sakafu ya bahari.

Mtelezalaji mawimbi Wamarekani aliendelea: ”Tumekuja hapa kwenye safari maisha yetu yote kuteleza juu ya mawimbi haya makubwa. Tunaweza kuteleza kwenye mawimbi madogo katika ghuba lenyewe, lakini kizuizi kinasabisha tusiweze kuteleza kwenye mawimbi makubwa. Hatujui kwa nini kizuizi kipo pale. Yote tunayojua ni kwamba kimeharibu safari yetu kabisa.”

Wakati Watelezaji mawimbi Wamarekani walipozidi kusisimka sana, usikivu wangu ulivutwa kwenye mtelezaji mawimbi aliye karibu—mtu mzee na wazi alikuwa mwenyeji. Alionekana kuendelea kukerwa alipokuwa anasikiliza malalamishi yaliyokuwa yanaongezeka kuhusu kizuizi.

Mwishowe, aliamka na kwenda pale kundi lilipokuwa. Bila kusema lolote, alitoa darubini yake kutoka mkobani na kumpa mmoja wa watelezaji mawimbini, akionyesha kuelekea kwenye kizuizi. Kila mmoja wa watelezaji mawimbini alitazama kwa darubini. Wakati zamu yangu ilipofika, kwa msaada wa kiookuzi, niliweza kuona kitu fulani ambacho nilikuwa sijakiona mapema: pezi ya mgongoni—papa wakubwa wakila karibu na mwamba upande mwingine wa kizuizi.

Kundi upesi lilitulia. Mtelezaji mawimbini mzee akatwaa tena darubini yake na kugeuka kwenda zake. Alipokuwa akifanya hivyo, alisema maneno kamwe sitayasahau: ”Msilaumu sana kile kizuizi,” alisema, “Ndiyo kitu cha pekee ambacho kinawazuia msiliwe.”

Tukisimama  kwenye ufukwe ule mzuri, mtazamo wetu ghafula ulikuwa umebadilika. Kizuizi ambacho kilionekana imara na kikwazo—ambacho kilionekana kama kuzuia burudani na msisimko wa kuteleza hasa kwenye mawimbi makubwa—kimekuwa kitu tofauti sana. Kwa uelewa wetu mpya wa hatari ambayo ilikuwa inavizia hapo chini, kizuizi sasa kilitoa ulinzi, usalama, na amani.

Wakati ninyi na mimi tunatembea mapito ya maisha na kufuata ndoto zetu, amri na viwango vya Mungu—kama kile kizuizi—wakati fulani vinaweza kuwa vigumu kueleweka. Vinaweza kuonekana kuwa vigumu na visiopindika, vinaziba barabara ambayo inaokena ya kufurahisha na kusisimua na ambayo inafuatwa na wengi. Kama vile Mtume Paulo alivyoelezea, ”Tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo,”1 kwa mtazamo finyu kama huu, kwamba hatuwezi kila mara kufahamu hatari kubwa iliyojificha chini.

Lakini Yeye ambaye ”huelewa vitu vyote”2 hujua kabisa pale hatari hizo zilipo. Yeye hutupa mwelekeo mtakatifu, kupitia amri zake na mwongozo wa upendo, ili kwamba tuweze kuepuka hatari hizi—ili kwamba tuweze kupanga mwelekeo katika maisha yetu ambao unalindwa kutokana na wawindaji wa kiroho na mataya yaliyoachama ya dhambi.3

Sisi tunaonyesha upendo wetu kwa Mungu—na imani yetu katika Yeye—kwa kufanya vyema tuwezavyo kila siku kufuata njia ambayo Yeye ametupangia sisi na kwa kushika amri ambazo Yeye ametupa. Sisi hasa tunaonyesha kwamba imani na upendo katika hali ambapo hatuwezi kuelewa kikamilifu sababu za amri za Mungu ama njia halisi Yeye anatuambia tufuate. Ni uamuzi wa rahisi kufuata mkondo ndani ya kizuizi mara tunapojua kuwa wawindaji wenye meno makali wanaosongana nje yake. Ni vigumu sana kuwa katika njia ndani ya kizuizi wakati yale yote tunayoyaona ni mawimbi ya kusisimua na kutamanisha ule upande mwingine. Na bado, katika nyakati hizo—nyakati ambapo tunachagua kufanya imani, kuweka imani yetu katika Mungu, na kuonyesha upendo wetu Kwake—kwamba tunakua na kupata mengi.

Katika Agano Jipya, Anania hakuweza kuelewa amri ya Bwana kumtafuta na kumbariki Saul—mtu ambaye hasa alikuwa na leseni ya kuwatia gerezani waumini wa Kristo. Bado, kwa sababu alitii amri ya Mungu, Anania alihusika katika kuzaliwa kiroho kwa Mtume Paulo.4

Tunapoamini katika Bwana tutumie imani yetu, tukitii amri Zake, na kufuata njia ambayo Yeye ametupangia, tunakuwa zaidi ya yule mtu ambaye Bwana anatutaka tuwe. Ni huku ”kuwa”—huu uongofu wa moyo—ambao ni muhimu sana. Mzee Dallin  H. Oaks ametufunza: “Haitoshi kwa mtu yeyote tu kupitia utendaji wa kila siku. Amri, ibada, na maagano ya injili siyo orodha ya amana inayohitajika kufanya katika akaunti fulani ya mbinguni. Injili ya Yesu Kristo ni mpango ambao hutuonyesha jinsi ya kuwa kile Baba yetu wa Mbinguni anatamani sisi tuwe.”5

Utiifu wa kweli, kwa hivyo, ni kujitoa wenyewe Kwake kabisa na kumruhusu Yeye kujenga njia yetu kote katika maji yaliyotulia na maji yaliyochafuka, tukielewa kwamba Yeye anaweza kututendea zaidi kuliko tunavyoweza kujifanyia wenyewe.

Tunapojiweka wenyewe chini ya mapenzi Yake, tunaongezeka katika amani na furaha. Mfalme Benyamini alifundisha kwamba wale ambao wanashika amri za Mungu “wamebarikiwa na wana furaha ... katika vitu vyote, kimwili na kiroho”6 Mungu anataka sisi tuwe na furaha. Anataka sisi tuwe na amani. Anataka sisi tufanikiwe. Anataka sisi tuwe salama na tulindwe kutokana na vishawishi vya ulimwengu vinavyotuzunguka.

Kwa njia ingine, Bwana anaamuru msianzishe mzingile mengine wa kuchosha chini ya maji ya vizuizi ambayo ni lazima tujifunze kwa kinyongo kuvumilia katika maisha haya ili kwamba tuweze kuinuliwa katika maisha yajayo. Badala yake, vizuizi vilivyowekwa na Bwana vinatutengenezea sisi bandari salama mbali na vishawishi viovu na angamizi ambavyo vinginevyo vinatuburuza hetuburuza chini hata kwenye vina vya kukata tamaa. Amri za Bwana zinatolewa kutokana na upendo na kutujali; zimedhamiriwa kwa furaha yetu katika maisha haya7 kama vile tu zimedhamiriwa kwa furaha yetu na kuinuliwa kwetu katika maisha yajayo. Zinatia alama njia ambayo tunatakiwa kutenda—na muhimu zaidi—zinaangaza kile tunapaswa kuwa.

Kama katika vitu vyote vizuri na vya kweli, Yesu Kristo anasimama kama mfano bora. Kitendo kikuu cha utiifu katika milele yote kilitokea wakati Mwana alijisalimisha Mwenyewe kwa mapenzi ya Baba. Akiomba kwa unyenyekevu mwingi sana kwamba kikombe kiweze kuondolewa—ili Yeye aweze kusafiri njia ingine badala hii ambayo ilikuwa imetiwa alama kwa ajili Yake—Kristo alijisalimisha Mwenyewe kwenye mapito ambayo Baba Yake alitaka Yeye ayapitie. Ilikuwa ni njia ambayo ilimwongoza kupitia Gethsemane na Golgotha, ambapo Yeye alivumilia machungu na mateso yasiyoweza kufikirika, na ambapo Yeye alikuwa amewachwa peke yake wakati Roho wa Bwana alipojiondoa. Lakini njia hiyo hiyo ilishia kaburi tupu katika ile siku ya tatu, kwa kilele za ”Amefufuka!”8 zikivuma katika masikio na mioyo ya wale ambao walimpenda Yeye. Ilijumuisha furaha na faraja isiyoweza kufikirika ambayo kitovu chake ilikuwa ni Upatanisho Wake kwa watoto wote wa Mungu katika milele yote. Kwa kuruhusu mapenzi Yake yamezwe na yale ya Baba, Kristo alitupa fursa ya amani ya milele, furaha ya milele, na uzima wa milele.

Mimi nashuhudia kwamba sisi tu watoto wa Mungu mwenye upendo. Mimi nashuhudia kwamba Yeye anataka sisi tuwe na furaha na tuwe salama na tubarikiwe. Kwa ajili hiyo, Yeye alitutengenezea njia iongozayo hadi Kwake na Yeye aliweka vizuizi ambavyo vitatulinda tukiambaa njiani. Tunapofanya vyema tuwezavyo kufuata njia hiyo, tunapata usalama wa kweli, furaha, na amani. Na tunapojiweka chini ya mapenzi Yake, tunakuwa kile Yeye anataka tuwe. Katika jina la Yesu Kristo, amina.