Imani Si Bahati Nasibu, bali ni Chaguo
Imani katika Yesu Kristo ni kipawa kutoka mbinguni ambacho kinakuja pale tunapochagua kuamini na tunapokitafuta na kukishikilia.
Mwokozi aliiona nguvu au udhaifu katika imani ya wale waliomzunguka. Kwa mtu, Alisema kwa idhini, “Imani yako ni kubwa.”1 Alisema tena kwa mwingine “Enyi wenye imani haba.”2 Aliwauliza wengine, “Imani yenu iko wapi?”3 Na Yesu alimtofautisha mwingine na, “[Katika Israeli yote] sijampata mwenye imani kubwa.”4
Najiuliza mwenyewe, “Je, Mwokozi anaiona imani yangu vipi?” Na jioni hii ninawauliza ninyi, Je Mwokozi anaiona imani yenu vipi?”
Imani katika Bwana Yesu Kristo siyo kitu ambacho ni kioja, kinachoelea hewani. Imani haituangukii kwa bahati, wala kukaa nasi kama urithi. Ni kama vile maandiko yanavyosema, ”kitu..., ushahidi wa vitu ambavyo havionekani.”5 Imani hutoa nuru ya kiroho, na nuru hiyo ni utambuzi.6 Imani katika Yesu Kristo ni kipawa kutoka mbinguni ambacho huja pale tunapochagua kuamini7 na tunapoitafuta na kuishikilia. Imani yako huenda inakua au inafifia. Imani ni kanuni ya nguvu, muhimu si tu kwa maisha haya, bali katika kuendelea kwetu mbele ya pazia.8 Kwa neema ya Kristo, siku moja tutaokolewa kupitia imani ya jina Lake.9 Matarajio ya baadaye ya imani yetu si bahati nasibu, bali ni chaguo.
Imani ya Kijana Mbrazili
Mwezi uliopita huko Brazil, nilikutana na Aroldo Cavalcante. Alibatizwa akiwa na umri wa miaka 21, muumini wa kwanza wa Kanisa katika familia yake. Imani yake iliwaka sana, na mara moja alianza kujiandaa kuhudumu misheni. Cha kusikitisha, mama ya Aroldo aligundulika kuwa na saratani. Miezi mitatu baadaye, ni siku chache kabla hajafariki, aliongea na Aroldo juu ya wasiwasi wake mkubwa. Hapakuwa na ndugu wa kusaidia. Aroldo atatakiwa kuchukua majukumu ya kuwalea dada zake wadogo wawili na kaka mdogo wake. Alitoa ahadi hii kwa mama yake aliyekuwa anakata roho.
Mchana alifanyakazi benki, na usiku alihudhuria chuo kikuu. Aliendelea kushika maagano yake ya ubatizo, lakini matumaini yake ya kuhudumu misheni yalitoweka. Misheni yake ilikuwa ni kuitunza familia yake.
Miezi kadhaa baadaye akiwa anaandaa maongezi ya sakramenti, Aroldo alisoma maneno ambayo Samweli aliyaongea kwa Mfalme Sauli: “Kutii, alisoma, “ni bora kuliko sadaka.”10 Aroldo alipokea hisia ambayo haiwezekani kwamba alitakiwa kutii maneno ya nabii ya kuhudumu misheni. Pasipohofu na vikwazo vilivyopo mbele yake, alisonga mbele kwa imani kubwa.
Aroldo alimwokoa kila Mbrazili cruzeiro alivyoweza. Akiwa na miaka 23, alipokea wito wake wa misheni. Alimwambia kaka mdogo wake kiasi cha pesa cha kutoa toka kwenye akaunti yake kwa ajili ya familia. Aroldo bado hakuwa na pesa ya kutosha ya kulipia gharama za misheni yake pamoja na pesa za matumizi kwa ajili ya kaka mdogo wake na dada zake, lakini kwa imani aliingia MTC. Wiki moja baadaye alipokea baraka ya kwanza kati ya nyingi. Benki ambayo ilimwajiri Mzee Cavalcante bila ya kutarajia waliongeza pesa yake mara dufu ya aliyopaswa kulipwa baada ya kuacha kazi. Miujiza hii, pamoja na mingine, ilitoa kipato kilichotakiwa kwa ajili ya misheni yake na familia yake wakati yeye hayupo.
Miaka ishirini baadaye, Ndugu Cavalcante anatumikia kama rais wa Kigingi cha Recife Brazil Boa Viagem. Akiangalia nyuma, aliongelea juu ya siku zile, “Nilipojaribu kuishi kwa wema, nilihisi upendo na mwongozo wa Mwokozi. Imani yangu ilikua, ikiniruhusu mimi kushinda changamoto nyingi.”11 Imani ya Aroldo hakuipata kwa bahati nasibu, bali kwa chaguo.
Kuna Wakristo wengi wa kike na kiume wenye imani kubwa katika Bwana Yesu Kristo, na tunawastahi na kuwaheshimu.
Hawapo Tena kwenye Uwanda Huru
Lakini ndugu, tumepewa kitu cha ziada, ukuhani wa Mungu, nguvu za Mungu zimerejeshwa duniani kupitia malaika watakatifu. Hili linakufanya uwe tofauti. Hausimami tena kwenye uwanda huru. Imani yako itakua siyo kwa bahati nasibu, bali kwa chaguo.
Jinsi tunavyoishi maisha yetu huongezea au hufifiza imani yetu. Maombi, utiifu, ukweli, usafi wa mawazo na matendo, na kutokuwa na ubinafsi huzidisha imani. Bila hivi, imani hufifia. Kwa nini Mwokozi alisema kwa Petro, “nimekuombea wewe ili imani yako isitindike”?12 Kwa sababu kuna adui ambaye anataka kuiangamiza imani yetu! Usichoke katika kuilinda imani yako.
Maswali ya Uaminifu
Kuongelea maswali ya ukweli ni sehemu muhimu ya kujenga imani, na tunatumia vyote akili na mawazo yetu. Bwana alisema, “Mimi nitakujulisha wewe akilini mwako na katika moyo wako.”13 Siyo majibu yote yatakuja mara moja, lakini maswali mengi yanaweza kujibiwa kwa kujifunza kwa nia halisi na kutafuta majibu kutoka kwa Mungu. Kutumia akili zetu bila moyo hakutaleta majibu ya kiroho. “Mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.”14 Na ili kutusaidia, Yesu alituahidi “Mfariji mwingine” alimwita Yeye ”hata Roho wa kweli.”15
Imani kamwe haidai majibu ya kila swali bali hutafuta uhakikisho na ujasiri wa kusonga mbele, wakati mwingine kukiri, “Sijui kila kitu, lakini ninajua ya kutosha kusonga mbele katika njia ya ufuasi.”16
Kujitumbukiza wenyewe katika shaka ya kila mara, kunachangiwa na majibu kutoka kwa wasio na imani na wasio wema, kunadhoofisha imani ya mtu katika Yesu Kristo na Urejesho.17 ”Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi.”18“
Kwa mfano, maswali kuhusu Nabii Joseph Smith siyo mageni. Yamekuwa yakivurumishwa na wakosoaji wake tangu kazi hii ianze. Kwa wale wenye imani ambao, wanaotazama kupitia kioo cha rangi cha karne ya 21, kwa uaminifu walihoji matukio au kauli za Nabii Joseph karibu miaka 200 iliyopita, ninatoa ushauri wa kirafiki: Kwa sasa, acheni tumpe Kaka Joseph mapumziko! Katika siku za usoni, utakuwa na habari mara 100 zaidi ya yale yanayopatikana katika injini za kusaka intaneti, na itatoka kwa Baba yetu aliye Mbinguni anayejua yote.19 Fikiria ujumla wa maisha yake – alizaliwa maskini na hakupata elimu ya kutosha, Joseph alitafsiri Kitabu cha Mormoni chini ya siku 90.20 Makumi ya Maelfu ya wanaume na wanawake wenye uaminifu na kujituma wanaushukuru urejesho. Akiwa na umri wa miaka 38 Joseph alitia muhuri ushahidi wake kwa damu yake. Ninashuhudia kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu. Yaweke haya akilini mwako, na songa mbele!
Vipawa Ambavyo Vinapanua Imani Yetu
Biblia na Kitabu cha Mormoni, vinatupa uhakika mwema kwamba Yesu Kristo, ni Mwana wa Mungu. Mkononi mwangu nina nakala ya kwanza ya Kitabu cha Mormoni kwa Kifaransa, kilichochapishwa na John Taylor alipoanza kazi ya utumishi huko Ufaransa mwaka 1852. Baadhi au vyote Kitabu cha Mormoni sasa kipo katika lugha 110 ulimwenguni kote. Kinaleta ushahidi wa kiroho na wenye kuguswa na ukweli wa Urejesho. Ni lini ilikuwa siku ya mwisho ambayo ulisoma Kitabu cha Mormoni toka mwanzo hadi mwisho? Kisome tena. Kitaongeza imani yako.21
Kipawa kingine kutoka kwa Mungu kinachopanua imani yetu ni mwongozo wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Leo tumewaidhinisha washiriki watatu wa Kumi na Wawili wapya, na ninawakaribisha Mzee Rasband, Mzee Stevenson, na Mzee Renlund katika umoja mtakatifu wa Akidi ya Kumi na Wawili. Paulo alisema:
“Naye alitoa wengine kuwa mitume, … manabii; …
“Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu … :
“Hata na sisi sote tutakapoufikia …umoja wa … imani … kumfahamu sana Mwana wa Mungu … :
“… ili tusiwe tena … tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, [wa wale ambao] tukizifuata njia za udanganyifu.”22
Mwongozo wa Urais wa Kwanza na wa Kumi na Wawili unasaidia kuilinda imani yetu.
Japokuwa mwanzo wako wa moto wa imani unaweza kuwa mdogo, chaguzi njema huleta kujiamini katika Mungu, na imani yako inakua. Matatizo ya duniani yanavuma dhidi yako, na nguvu za uovu zinakuja gizani zikitegemea kuizima imani yako. Tunapoendelea kufanya chaguzi njema, kumwamini Mungu na kumfuata Mwanawe, Bwana huongeza mwanga wa ufahamu wetu na imani yetu itatulia na haitayumbishwa. Rais Gordon B. Hinckley alifundisha: “Usiogope … Siku za usoni ni angavu kama wa imani yako.”23
Porter, Zane, and Max Openshaw
Imani ya wavulana wa Kanisa hili ni ya ajabu!
Mwezi June 12 wa mwaka huu, nilipokea barua pepe ikiniambia kwamba askofu toka kata ya Utah, mke wake, na watoto wao wawili waliuawa katika ajali ya ndege. Askofu Mark Openshaw alikuwa anaendesha ndege toka kwenye uwanja mdogo, wakati ghafla ilipoanguka toka angani na kugonga aridhini. Askofu Openshaw, mke wake, Amy, na watoto wao Tanner na Ellie waliuawa katika ajali hii. Kwa miujiza mtoto wao mdogo wa miaka mitano, Max, alitupwa nje ya ndege na kiti chake, akiwa amenusurika kwa kuvunjika mifupa.
Nilifahamishwa kwamba mwana wao Mzee Porter Openshaw alikuwa akitumikia katika Misheni ya Marshall Islands Majuro na kwamba mwana wao wa miaka 17, Zane, alikuwa kwenye shule ya mpango kijamii wa kutembeleana huko Ujerumani.
Nilimpigia simu Mzee Poenshaw wakati wa Krismasi. Japokuwa alivunjika moyo kwa vifo visivyo tarajiwa vya mama, baba, kaka, na dada yake, Wasiwasi wa Mzee Openshaw mara moja uligeukia kwa wadogo zake wawili.
Hatimaye ilikuwa Mzee Openshaw na kaka yake Zane walioamua kwamba wengine wangeweza kusaidia nyumbani na kwamba Porter abaki misheni. Walijua hicho ndicho ambacho wazazi wao wangependa.
Nilipokuwa nikiongea na Mzee Openshaw, nilihisi uchungu wake lakini pia moto wa imani yake usioweza kuzimwa, “Ninajiamini, “aliniambia, “na nilijua wazi bila shaka kwamba nitaiona tena familia yangu. … Nguvu katika majaribu yetu daima yanapatikana katika … Bwana wetu, Yesu Kristo, … Mkono wa Mungu Mwenyezi umekuwa dhahiri katika kunisaidia [mimi] na ndugu zangu katika [hii] changamoto ngumu.”24
Nilikutana na Zane kwa mara ya kwanza kwenye msiba. Nikiwa nayatazama majeneza manne yakiwa mbele yetu kanisani, nilishangazwa kwa imani ya kijana huyu wa miaka 17 akiongea katika umati. “Leo,” alisema, “tumekusanyika kwa mioyo yenye unyenyekevu na nafsi zilizochoka, kuyakumbuka maisha ya mama yangu, baba, Tanner, na Ellie. … Tumeongea pamoja, tumelia pamoja, kukumbuka pamoja, na kuhisi mkono wa Bwana pamoja. …
“Siku niliyosikia habari za ajali, nilikuta barua katika mkoba wangu ikitoka kwa mama yangu. Katika barua aliandika: “Zane, kumbuka wewe ni nani na umetoka wapi. Tutakuombea na tunakukosa.’ Zane akaendelea: “Pasingekuwa na maneno ya mwisho yaliyofaa toka kwa mama yangu. Ninajua kwamba yeye, pamoja na Tanner, Ellie, na baba yangu … wanaomba kwa ajili ya [kaka yangu na] mimi. Ninajua kwamba … wanaomba kwamba nijue mimi ni nani … kwa sababu mimi, kama ninyi, ni mwana wa Mungu, na amenileta mimi hapa. Ninashuhudia … bila kujali upweke tunaosikia, Mungu hatatuacha.”25
Wapendwa rafiki zangu, imani yenu haikuanza baada ya kuzaliwa, na haitakoma baada ya kifo. Imani ni chaguo. Imarisheni imani yenu na muishi kwa kustahili maneno ya Mwokozi: “Imani yako ni kubwa.” Unapofanya hivyo, ninakuahidi kwamba imani yako, kupitia neema ya Yesu Kristo, siku moja, itakuwezesha kusimama na wale uwapendao, wasafi na bila waa katika uwepo wa Mungu, katika jina la Yesu Krsito, amina.