Tazama, Mama Yako
Hakuna upendo hapa duniani unaokaribia kukisia upendo safi wa Yesu Kristo kuliko upendo usio na uchoyo wa mama mwenye kujitolea kwa mtoto wake.
Acheni niungane nanyi nyote kumkaribisha Mzee Ronald A. Rasband, Mzee Gary E. Stevenson, na Mzee Dale G. Renlund pamoja na wake zao katika ushirika mzuri sana wanaoweza kufikiria.
Akitoa unabii wa Upatanisho wa Mwokozi, Isaya aliandika, ”Ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni wetu.”1 Ono la ajabu la siku za mwisho lilisisitizia kwamba ”[Yesu] alikuja ulimwenguni ... kuchukua dhambi za ulimwengu.”2 Yote maandiko ya kale na ya kisasa yanashuhudia kwamba ”aliwakomboa mwenyewe na akawainua, akawachukua siku zote za kale.”3 Wimbo unaoenziwa unatusihi ”tusilikize sauti ya Mkombozi mkuu!”4
Inua, chukua, beba, komboa. Haya ni maneno ya kimasiya ya nguvu sana, yakutia moyo. Yanaleta msaada na tumaini ya safari njema kutoka pale tupo hadi pale tunahitaji kuwa—lakini hatuwezi kufika bila msaada. Maneno haya rahisi pia yanaashiria mzigo, masumbuko na uchovu—maneno ambayo yanayofaa zaidi kuelezea huduma Yake ambaye, kwa gharama isiyoweza kusemeka, anatuinua tunapoanguka, anatubeba kwenda mbele nguvu zinapokwisha, anatupeleka nyumbani salama wakati usalama unaonekana upo mbali nasi. ”Na Baba yangu alinituma,” Yeye alisema, ”ili nipate kuinuliwa juu kwenye msalaba; ... kwamba kama nilivyoinuliwa juu ... hata hivyo watu wainuliwe juu ... kusimama ... yangu.”5
Lakini unaweza kusikia katika lugha hii uwanda mwingine wa jitihada za binadamu ambazo kwazo pia tunatumia maneno kama vile chukua na chukuliwa,beba na inua,tenda kazi na komboa.? Kama vile Yesu alivyomwambia Yohana hasa wakati wa kile kitendo cha Upatanisho, ndivyo Yeye anavyosema kwetu sote,” Tazama, mama yako!”6
Leo mimi natangaza kutoka kwenye jukwaa hili kile ambacho kimesemwa hapo zamani: hakuna upendo hapa duniani unaokaribia kukisia upendo safi wa Yesu Kristo kuliko upendo usio na choyo wa mama mwenye kujitolea kwa mtoto wake. Isaya alipokuwa, ananena kimasiya, alitaka kuonyesha upendo wa Yehova, alionyesha taswira ya kujitolea kwa mama. Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye?” yeye aliuliza. Ni upuuzi jinsi gani, yeye anadokeza, ingawa si upuuzi kama kufikiria Kristo atatusahau sisi.7
Aina hii ya upendo wa dhati ”huvumilia, na ni karimu, ... haitafuti mambo yake, ... lakini ... huvumilia vitu vyote, huamini vitu vyote, hutumaini vitu vyote, hustahamili vitu vyote.”8 Cha kutia moyo sana, uaminifu kama huu ”kamwe haifutuki”9 ”Kwani milima itaondoka, na vilima vitaondelewa,” Yehova alisema, ”bali wema wangu hautaondoka kwako.”10 Vivyo hivyo wasema mama zetu.
Unaona, siyo tu kwamba wanatuzaa, bali pia wanaendelea kutuvumilia sisi. Siyo tu kutubeba kabla kuzaliwa bali kubeba kwa maisha yote ambako kunaufanya umama kuwa kazi zito sana. Bila shaka kuna hali fulani chache za kuvunja moyo, lakini mama wengi wanajua kwa hisia na silika kwamba hili ni jukumu takatifu la hali ya juu. Uzito wa utambuzi huu haswa juu ya mabega ya mama kijana unaweza kuwa jambo zito sana.
Mama kijana wa ajabu hivi majuzi aliniandikia: Je! Ni kwa jinsi gani kwamba mwanadamu anaweza kupenda mtoto kwa kina sana kwamba uwe tayari kuisalimisha sehemu kubwa ya uhuru wako kwa ajili yake? Je! Ni kwa jinsi gani upendo wa binadamu unaweza kuwa na nguvu hivi kwamba kwa hiari unaweza kujiweka chini ya majukumu, hatari, wasiwasi, na majonzi na kurudia tena na tena hayo hayo? Ni upendo wa aina gani unaoweza kukufanya wewe uhisi, mara unapopata mtoto, maisha yako kamwe, si yako mwenyewe tena? Upendo wa mama ni lazima uwe ni mtakatifu. Hakuna sababu nyingine kwayo. Kile kina mama wanafanya ni sehemu muhimu ya kazi ya Kristo. Kujua hilo kunafaa kutosha kutuambia uzito wa upendo kama huo utakuwa na mapana ya kuanzia kwa lile lisilowezekana hata kufikia njozi, tena na tena, mpaka kwa usalama na wokovu wa yule mtoto wa mwisho duniani ndipo pia tunaweza kusema hivi pamoja na Yesu, ’[Baba!] Mimi nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.’11”
Kwa ufasaha wa barua hiyo ukipiga mwangwi katika akili zetu, acha mimi nishiriki matukio matatu yanayoakisi ushawishi wa kimalikia wa kina mama ulioshuhudiwa katika huduma majuma machache tu yaliyopita:
Hadithi yangu ya kwanza ni ya tahadhari, kutukumbusha kwamba si kila jitihada ya kina mama ina mwisho wa kitabu cha hadithi, angalau sio mara moja. Kumbusho hilo linatokana na mazungumzo yangu na rafiki mpendwa wa miaka 50 ambaye alikuwa anafariki mbali na Kanisa hili alijua katika moyo wake kuwa ni la kweli. Haijalishi jinsi nilivyompenda, nilivyojaribu kumfariji, sikuonekana kumletea amani. Hatimaye alinitizama machoni, ”Jeff,” alisema “kwa vyovyote itakavyokuwa uchungu kusimama mbele ya Mungu, mimi siwezi kufikiria vile nitasimama mbele ya mama yangu. Injili na watoto wake vinamaanisha kila kitu kwake. Mimi najua nimevunja moyo wake, na hili linavunja wangu.
Nina hakika kabisa kwamba baada ya kufa kwake, mama yake alimpokea rafiki yangu kwa mikono wazi; hivyo ndivyo wazazi hufanya. Lakini sehemu ya tahadhari ya hadithi hii ni kwamba watoto wanaweza kuvunja moyo ya mama zao. Hapa pia, tunaona mlinganisho mwingine na Mungu. Hamna haja ya kutukumbusha kwamba Yesu alikufa kwa kuvunjika moyo, moyo uliochoka kutokana na kubeba dhambi za ulimwengu. Hivyo katika wakati wowote wa majaribu, na tuweze “kutazama mama [yetu]” vile vile Mwokozi wetu na tusiwaletee huzuni ya kutenda dhambi.
Pili, mimi nitaongea kuhusu kijana ambaye aliingia katika uwanja wa misheni akiwa mstahiki lakini kwa uchaguzi wake mwenyewe alirudi nyumbani mapema kwa mvuto wa jinsia moja na msononeko fulani alioupata kwa ajili hiyo. Alikuwa bado ni mstahiki, lakini imani yake ilikuwa katika kilele cha hatari, mzigo wake wa mhemko ukawa mzito sana, na maumivu yake ya kiroho yakazidi sana na sana. Alikuwa kila upande anaumwa, amekanganyikiwa, amekasirika, na mpweke.
Rais wa misheni wake, rais wa kigingi wake na askofu wake walitumia masaa yasiyohesabika wakipekua na wakilia na kumbariki walipokuwa wanamshikilia, lakini sehemu kubwa ya donda lake ilikuwa ya kibinafsi hata kwamba aliificha sehemu hii mbali na wao. Baba mpendwa katika hadithi hii alimwaga nafsi yake yote kumsaidia mwana, lakini kwa ajili ya hali ya ajira yake iliyokuwa na shughuli nyingi sana ilimaanisha usiku mrefu wa nafsi hii uliwakabili tu mvulana huyu na mama yake. Mchana na usiku, kwanza kwa majuma, kisha kwa miezi ambayo iligeuka kuwa miaka, walitafuta uponyaji kwa pamoja. Kupitia vipindi vya machungu (hasa yake lakini wakati fulani ya mama yake) na hofu isiyo na kikomo (hasa kwa mama yake lakini wakati fulani kwake), mama alishuhudia—kuna lile neno zuri, lenye uzito—kwa mwanawe ushuhuda wake wa nguvu za Mungu, wa Kanisa Lake lakini hasa upendo Wake kwa mtoto huyu. Kwa hali hiyo hiyo alishuhudia juu ya upendo usiobadilika, usiokufa kwake yeye pia. Kuleta hiyo mihimili miwili muhimu pamoja ya uwepo wake hasa—injili ya Yesu Kristo na familia yake—mama alimwaga nafsi yake katika maombi bila kikomo. Alifunga na akalia, akalia na akafunga, kisha akasiliza na akasikiliza mwana huyo akimwambia kila mara jinsi moyo ulikuwa unavunjika. Basi akambeba—tena—ila wakati siyo tu kwa miezi tisa. Wakati huu alifikiria kwamba uchungu wa uzazi kupitia mandhari yaliyoparuzwa ya huzuni wake ingekuwa milele.
Lakini kwa neema ya Mungu, kwa kung’ang’ania kwake, msaada wa viongozi wengi wa Kanisa, marafiki, wana familia, na tabibu, huyu mama mwenye kuomba sana amemwona mwanawe akija nyumbani hata nchi ya ahadi. Cha kuhuzunisha tunatambua kwamba baraka kama hiyo haiji, wala haijakuja, kwa wazazi wote ambao wanaumwa na moyo kwa ajili ya hali aina tofauti za watoto wao, Na acheni niseme, huu mvuto wa jinsia wa mwana huyu haukubalika kimiujiza—hakuna yeyote alitarajia itafanyika. Lakini kidogo kidogo, moyo wake ulibadilika.
Akaanza kurudi kanisani. Alichagua kupokea sakramenti kwa hiari na ustahiki. Akapata sifu ya hekaluni na akakubali wito wa kuhudumu kama mwalimu wa seminari ya asubuhi, ambapo alifanikiwa kiajabu. Na sasa, baada ya miaka mitano yeye kwa maombi yake mwenyewe na msaada wa Kanisa, alirudi katika uwanja wa misheni kumaliza huduma yake kwa Bwana. Mimi nimelia kwa ajili ya ujasiri, uadilifu, na sharti la kijana huyu la kutatua mambo na kushika imani yake. Yeye anajua kwa ana deni kubwa kwa wengi, lakini anajua ana deni kwa watu wawili wa kimasiya katika maisha yake, wawili ambao walimzaa, na walimbeba, na wakawa uchungu wa uzazi na kumkomboa yeye—Mwokozi wake, Bwana Yesu Kristo, na mama yake mwenye kujitolea, mkombozi, mtakatifu sana kabisa.
Mwisho, hii ni kutokana na kuwekwa wakfu upya kwa Hekalu la Mexico City majuma matatu yaliyopita. Ilikuwa huko tulimwona rafiki yetu mpendwa Lisa Tuttle Pieper amesimama katika ibada ya kuweka wakfu yenye maongozi. Lakini alisimama kwa shida kwa sababu kwa mkono wake mmoja aliushikilia mkono Dora, bintiye mpendwa lakini mwenye changamoto sana, hali pamoja na wengine alijaribu kuufanya mkono wa kulia wa Dora uliofifia wa binti mrembo wa Mungu aweze kupunga kwa kitambaa cheupe na kwa kilio kilichoeleweka naye tu alisema, ”Hosana, hosana, hosana kwa Mungu na kwa Mwanakondoo.”12
Kwa kina mama wetu wote kila mahali, kale, sasa, ama siku zijazo, mimi nasema. “Asanteni kwa kuzaa, kufunza nafsi, kuumba hulka, na kwa kuonyesha upendo halisi wa Kristo.” Kwa Mama Hawa, kwa Sera, Rabeka, na kwa Raheli, kwa Mariamu wa Nazareti, na kwa Mama aliye Mbinguni, nasema, “Asanteni kwa kazi yenu muhimu katika kutimiza madhumuni ya milele. Kwa kina mama wote mlio katika kila hali, ikijumuisha wale ambao mnaong’ang’ana, mimi nasema, “Muwe na amani. Muamini katika Mungu na mjiamini wenyewe. Mnafanya vyema kuliko mnavyofikiria. Kwa kweli, ninyi ni waokozi katika Mlima Sayuni,13 na kama Bwana mnayemfuata, upendo wenu ’kamwe haupungui neno.’14” Mimi singeweza kutoa wasifu mkuu kwa yeyote. Katika jina la Yesu Kristo, amina.