Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 9–15. Mafundisho na Maagano 88: “Ijengeni … Nyumba ya Mungu”


“Agosti 9-15. Mafundisho na Maagano 88: ‘Ijengeni … Nyumba ya Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 9-15. Mafundisho na Maagano 88,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
chumba chenye viti na mabenchi

Agosti 9–15

Mafundisho na Maagano 88

“Ijengeni … Nyumba ya Mungu”

Rais Russell M. Nelson alisema, “ninaahidi kwamba unapofanya kazi kwa bidii kurekebisha nyumba yako kuwa kitovu cha kujifunza injili, … ushawishi wa adui katika maisha yako na katika nyumba yako utapungua” (“Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 113).

Andika Misukumo Yako

Kila mara, Bwana hutupa mtazamo mdogo wa “ukuu na uweza” Wake usio na mipaka (Mafundisho na Maagano 88:47) kupitia kutoa ufunuo kwa manabii Wake. Mafundisho na Maagano 88 ni ufunuo sawa na huo—unaohusu nuru na utukufu na falme ambazo zinaweza kufanya mahangaiko ya dunia kuonekana yasiyo na maana kwa kulinganisha. Hata kama hatuwezi kufumbata yote ambayo Bwana anatufunza, tunaweza angalau kuhisi kwamba kuna zaidi kwenye umilele kuliko kile tunachoweza kufikiri sasa. Bila shaka, Bwana hakuzungumza juu ya maajabu haya makuu ili kututisha au kutufanya tuhisi duni. Kwa kweli, Yeye aliahidi, “siku itakuja mtakayomjua Mungu” (mstari wa 49; italiki imeongezwa). Pengine ilikuwa ni kwa ukubwa huo kwamba Bwana aliwasihi Watakatifu Wake huko Kirtland kuunda Shule ya Manabii. “Jiandaeni wenyewe,” Yeye alisema. “Tayarisheni kila kitu kinachohitajika; na ijengeni … nyumba ya Mungu” (mstari wa 119). Kwani ni katika nyumba takatifu ya Mungu—na katika nyumba zetu—kwamba Yeye anaweza, kuliko mahala pengine popote, kuinua uoni wetu juu ya ulimwengu huu, “kuufichua uso wake [kwetu],” na kutuandaa “kustahimili katika utukufu wa selestia” (mistari 68, 22).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 88

Mwokozi anatupatia tumaini na amani.

Siku kadhaa baada ya onyo kwamba vita “vitamwagika juu ya mataifa yote” (Mafundisho na Maagano 87:2), Bwana alitoa ufunuo kwamba Joseph Smith aliliita “‘jani la mzeituni’ … lililochumwa kutoka kwenye Mti wa Peponi, ujumbe wa Bwana wa amani kwetu sisi” (Mafundisho na Maagano 88, kichwa cha habari cha sehemu). Ni kwa jinsi gani ufunuo huu ni sawa na jani la mzeituni, ishara ya kale ya amani? (Ona pia Mwanzo 8:11). Ni kweli zipi katika sehemu hii zinakusaidia kuhisi tumaini na amani kwa Kristo?

Mafundisho na Maagano 88:6–67

Nuru na sheria huja kutoka kwa Yesu Kristo.

Maneno nuru na sheria yamerudiwa mara nyingi katika sehemu ya 88. Maneno haya yametumiwa katika maandiko mengine kumwelezea Yesu Kristo na injili Yake (kwa mfano, ona Isaya 60:19; Yohana 1:1–9; 3 Nefi 15:9). Wekea alama au andika mistari ambapo unapata maneno haya katika Mafundisho na Maagano 88:6–67, na andika kile unachojifunza kuhusu Mwokozi, nuru, na sheria. Mistari hii inaweza kukuvuvia kufanya mabadiliko katika maisha yako ili upokee kwa uaminifu zaidi nuru na kuishi “sheria ya Kristo” (mstari wa 21).

Ona pia Sharon Eubank, “Kristo: Nuru Ing’aayo Gizani,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 73–76.

Picha
familia ikijifunza maandiko

Maandiko yana sheria ya Kristo.

Mafundisho na Maagano 88:62–126

Tayarisheni kila kitu kinachohitajika.

Katika baadhi ya njia, tunaishi katika nyakati ambazo Bwana alizielezea wakati “vitu vyote vitakuwa katika vurugu; na hakika, watu watavunjika mioyo” (Mafundisho na Maagano 88:91). Unaposoma mistari 62–126, fikiria jinsi ushauri wa Bwana unavyoweza kukusaidia kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi. Haya ni baadhi ya maswali ya kuzingatia:

Mistari 62–76:Unapotafakari mistari hii, unapata msukumo kufanya nini ili “kusogea karibu” na Mungu? (mstari wa 63). Fikiria nini amri ya Bwana ya “jitakaseni” inachoweza kumaanisha kwako (mstari wa 68).

Mistari 77–80, 118–26.Kwa nini inaweza kuwa “muhimu kwako kufahamu” mada zote za kimwili na kiroho? (mstari wa 78). Ni kwa jinsi gani unafuata ushauri wa “kutafuta kujifunza”? (mstari wa 118). Je! unafikiri inamaanisha nini kujifunza “kwa kusoma na pia kwa imani”?

Mistari 81–116:Fikiria kuandika unabii kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi katika mistari hii. Kwa nini unafikiri Bwana angekutaka wewe ujue kuhusu mambo haya?

Mistari 117–26.Fikiria kusoma mistari hii ukiwa na hekalu mawazoni; ni nini unapata hapa ambacho kingeweza kukusaidia kujiandaa kuingia kwenye nyumba ya Bwana?

Ona pia D. Todd Christofferson, “Kujiandaa kwa Kurudi kwa Bwana,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 81–84; David A. Bednar, “Tafuta Kujifunza kwa Imani,” Ensign, Sept. 2007, 61–68; Watakatifu, 1:164–66; “Shule na Endaumenti,” Ufunuo katika Muktadha, 174–82.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 88:14–33, 95–101.Je, tunajifunza nini kuhusu Ufufuo kutoka kwenye mistari hii? Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinashawishi chaguzi tunazofanya?

Mafundisho na Maagano 88:33.Ungeweza kuanza mjadala kwenye mstari huu kwa kuwaomba wanafamilia kuzungumzia zawadi ambazo wamepewa—zote zile walizopokea kwa furaha na zingine ambazo hawakupokea kwa furaha. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumwonesha Bwana kwamba tunafurahia katika zawadi ya utukufu wa selestia ambao Yeye anatupatia? Ni kwa jinsi gani tunamfurahia “yeye aliyetoa zawadi”?

Mafundisho na Maagano 88:63, 68.Mistari hii ina baadhi ya maneno ya matendo ambayo yanaweza kukuvuvia kufikiria njia za ubunifu za kufundisha ujumbe katika mistari kwa watoto wako. Kwa mfano, mnaweza kucheza mchezo wa kujificha ili kujadili kifungu cha maneno “nitafuteni kwa bidii nanyi mtanipata” (mstari wa 63; italiki imeongezwa).

Mafundisho na Maagano 88:81.Kama familia, tambueni baadhi ya alama za kuonya ndani na kuzunguka nyumba yenu, kama vile lebo za kuonya kwenye madawa au alama za barabarani kwa madereva. Ni kwa jinsi gani maonyo haya yanatusaidia? Ni nini Baba wa Mbinguni anatutaka “tuwaonye jirani [zetu]” kukihusu?

Mafundisho na Maagano 88:119.Ili kuipa msukumo familia yako kuifanya nyumba yenu sawa na maelezo katika mstari wa 119, jaribu kitu kama hiki: Andika vifungu vya maneno kutoka kwenye mstari huu kwenye vipande vya karatasi, na vitumie kufunika picha ya hekalu. Someni Mafundisho na Maagano 88:119 pamoja, na waruhusu wanafamilia kuondoa kila kipande cha karatasi wakati wanaposikia kifungu kinachohusika kwenye mstari. Ni nini tunaweza kufanya kuzifanya nyumba zetu “nyumba ya Mungu”? (mstari wa 119).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Nearer, My God, to Thee,” Nyimbo za Kanisa, na. 100.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wape watoto nafasi ya kuonesha ubunifu wao. Wakati unapowaalika watoto wako kubuni kitu kinachohusiana na kanuni ya injili, unawasaidia si tu kuelewa vyema kanuni hiyo, bali pia unawapa kitu halisi cha kukumbuka juu ya kile walichojifunza (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Picha
Yesu na wanafunzi

Yesu Kristo anatupatia amani. Amani Ninawapeni, na Walter Rane

Chapisha