Desemba 28–Januari 3. Mafundisho na Maagano 1: ‘Sikilizeni Enyi Watu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
Desemba 28–Januari 3. Mafundisho na Maagano 1,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021
Desemba 28–Januari 3
Mafundisho na Maagano 1
Sikilizeni, Enyi watu
Fikiria juu ya Mafundisho na Maagano 1 kama utangulizi binafsi wa Bwana kwa kitabu hiki cha funuo zake za siku za mwisho. Yeye anataka wewe ujue nini kuhusu Mafundisho na Maagano? Tafakari swali hili, na andika msukumo wowote ambao unakuja unaposoma sehemu ya 1.
Andika Misukumo Yako
Mnamo Novemba 1831, Kanisa la Yesu Kristo la urejesho lilikuwa ndio kwanza lina mwaka mmoja na nusu. Ingawa lilikuwa linakua, lilikuwa bado kundi lisiloonekana la waumini wanaoishi katika mpaka sehemu ya watu wachache, wakiongozwa na nabii mwenye umri wa kati ya miaka ya ishirini. Bali Mungu aliwafikiria waumini hawa kuwa watumishi Wake, na Alitaka funuo alizowapa kuhubiriwa kwa ulimwengu.
Mafundisho na Maagano sehemu ya 1 ni utangulizi wa Bwana kwa mkusanyiko wa funuo hizi, na kwa uwazi inaonesha kwamba japokuwa uumini wa Kanisa ulikuwa mdogo, hapakuwa na chochote kidogo kuhusu ujumbe ambao Mungu alitaka Watakatifu Wake washiriki. Ni “sauti ya onyo” kwa ajili ya “wakazi wote wa dunia,” ikiwafundisha kutubu na kuanzisha “agano la milele” la Mungu (Mistari 4, 8, 22). Watumishi wanaobeba ujumbe huu ni “wadhaifu na wa kawaida,” lakini watumishi wanyenyekevu ndiyo wale Mungu anaowahitaji—wakati ule na sasa—kulileta Kanisa “kutoka kusikoonekana na kutoka gizani” (Mistari ya 23, 30).
Kwa ziada kuhusu historia ya Mafundisho na Maagano 1, ona Watakatifu, 1:140–43.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
Bwana ananialika “kuchunguza amri hizi.”
Dibaji inatambulisha kitabu. Inaainisha dhamira na makusudi ya kitabu na kusaidia wasomaji kujiandaa kusoma. Unaposoma sehemu ya 1—“dibaji” ya Bwana kwenye Mafundisho na Maagano (mstari wa 6)—tafuta dhamira na makusudi Bwana aliyotoa kwa ajili ya funuo zake. Unajifunza nini kutokana na sehemu ya 1 ambacho kitakusaidia kufaidika zaidi kutokana na kujifunza kwako Mafundisho na Maagano? Kwa mfano, unaweza kutafakari nini inamaanisha “kusikia sauti ya Bwana” katika funuo hizi (mstari wa 14) au “kuchunguza amri hizi” (mstari wa 37).
Ona pia utangulizi kwa Mafundisho na Maagano.
Mafundisho na Maagano 1:1–6, 23–24, 37–39.
Mungu anazungumza kupitia watumishi Wake, na maneno Yake yatatimizwa.
Sehemu ya 1 inaanza na kumalizika kwa tangazo la Mungu kwamba Anazungumza kupitia watumishi Wake waliochaguliwa (ona mistari 4–6, 23–24, 38). Andika kile unachojifunza kutokana na ufunuo huu kuhusu Bwana na sauti Yake. Unajifunza nini kuhusu watumishi wa Bwana? Lini umesikia sauti ya Bwana katika sauti ya watumishi Wake? (Ona mstari wa 38).
Mafundisho na Maagano 1:3, 24–28, 31–33.
Kama mimi ni mnyenyekevu, kurudiwa na Bwana kunaweza kunielekeza kwenye kutubu.
Tambua kwamba katika mstari wa 3 na mistari 24–28, Bwana alisema kwamba dhambi za watu na makosa vitajulikana. Kwa upande mmoja huu ni uzoefu wenye uchungu, huzuni, na kwa upande mwingine ni uzoefu wenye kuelekeza. Kwa nini hali hizi ni tofauti sana? Fikiria jinsi unavyoonesha hisia wakati unapotambua juu ya dhambi zako na udhaifu. Ni sifa zipi unazopata katika mistari 24–28 ambazo zinaweza kukusaidia kujibu katika njia sahihi? Ni nini mistari hii, pamoja na mistari 31–33, inakufundisha kuhusu jinsi Bwana anavyochukulia udhaifu wako na dhambi zako?
Ona pia Mithali 3:11–12; Etheri 12:27; Moroni 6:8.
Mafundisho na Maagano 1:12–30:35–36
Bwana alirejesha injili Yake kunisaidia mimi kukabiliana na changamoto za siku za mwisho.
Ingawa sehemu ya 1 inaonya juu ya siku za dhiki zinazokuja, pia ina ujumbe wa kutia moyo: “Mimi Bwana, nikijua majanga yajayo juu ya wakazi wa dunia, nimemwita mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na kusema naye kutoka mbinguni” (mstari wa 17).
Kumbuka majanga ambayo Bwana alionya kuyahusu (ona, kwa mfano, mistari 13–16, 35). Ni majanga yapi mengine unayaona katika ulimwengu wa leo—au katika maisha yako mwenyewe ? Mistari 17–30 inaelezea kile Bwana alichokifanya kwa ajili yako katika matazamio ya majanga haya. Fikiria kutengeneza orodha ya kile unachokipata.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani
-
Mafundisho na Maagano 1:1–6, 37–39.Kuanzisha majadiliano kuhusu maonyo kutoka kwa Bwana, ungeweza kuzungumza kuhusu maonyo tunayopokea kutoka kwa wengine kuhusu hatari tusizoweza kuziona—kama vile sakafu ya kuteleza, dhoruba kali, au gari linalokuja. Je, mifano hii hutufundisha nini kuhusu maonyo ya Bwana? Kulingana na Mafundisho na Maagano 1:1–6, 37–39, ni kwa jinsi gani Bwana anatuonya? Je, Yeye ametuonya kuhusu nini hivi karibuni? Pengine ungeweza kuangalia au kusoma sehemu za jumbe za mkutano mkuu wa hivi karibuni na kutafuta mifano ya sauti ya Mungu ya “onyo.”
-
Mafundisho na Maagano 1:16.Inamaanisha nini “kuendeleza haki za [Bwana]”? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa na uhakika tunafanya hivyo, na hatutembei “katika njia [yetu] wenyewe”?
-
Mafundisho na Maagano 1:30.Inamaanisha nini kusema kwamba kanisa ni la “kweli na hai”? Ili kufanya familia yako ifikirie kuhusu swali hili, labda ungewaonesha picha za vitu vilivyo hai na vitu visivyo hai. Ungeweza pia kujadili kile mnachoweza kufanya kama familia kusaidia “kuleta [Kanisa] kutoka kusikoonekana na kutoka gizani.”
-
Mafundisho na Maagano 1:37.Fikiria kupanga kama familia jinsi “mtakavyochunguza amri hizi” katika Mafundisho na Maagano mwaka huu. Ni kwa jinsi gani utafanya kusoma maandiko kuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya familia? Ni mawazo gani ya kujifunza yanaweza kukusaidia kujifunza kutoka kwenye maandiko? (Ona “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Maandiko kwa Familia Yako” mwanzoni mwa nyenzo hii.)
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, 110–11 hususani mstari wa mwisho.