Mafundisho na Maagano 2021
Desemba 28–Januari 3. Mafundisho na Maagano 1: “Sikilizeni, Enyi Watu”


“Desemba 28–Januari 3. Mafundisho na Maagano 1: “Sikilizeni, Enyi Watu”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Desemba 28–Januari 3. Mafundisho na Maagano 1,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

familia ikisoma maandiko

Desemba 28–Januari 3

Mafundisho na Maagano 1

“Sikilizeni, Enyi Watu”

Hatua yako ya kwanza katika kujitayarisha kufundisha inapaswa kuwa kujifunza kwa sala Mafundisho na Maagano 1. Unapofanya hivyo, sikiliza misukumo kuhusu mahitaji ya watoto, na tafuta kanuni ambazo zitakuwa na maana kwao. Misukumo hii itakusaidia wewe kupanga shughuli za maana ili kufundisha kanuni hizi.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Nyanyua juu Mafundisho na Maagano, na waombe watoto kushiriki jambo lolote wanalojua kuhusu kitabu hiki. Nani alikiandika kitabu hiki? Je, kina nini? Kwa nini ni cha muhimu? Kwa msaada, ungeweza kurejelea “Sura ya 23: Mafundisho na Maagano” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 90–92). Shiriki upendo wako wa Mafundisho na Maagano na hamu yako ya kujifunza kutoka katika kitabu hicho mwaka huu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 1:4

Kupitia manabii Wake, Bwana anatuonya juu ya hatari ya kiroho.

Bwana alitangaza kwamba sauti Yake ni “sauti ya onyo.” Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto kusikiliza na kutii maonyo Yeye anayotoa?

Shughuli za Yakini

  • Waache watoto washike picha za alama za kuonya—kama vile hatari za foleni, hali mbaya ya hewa, au sumu—na zungumza kuhusu jinsi gani zinavyotuonya juu ya hatari. Au simulia hadithi kuhusu wakati ambapo ulitii onyo. Linganisha maonyo haya na maonyo Bwana anayotoa kwetu kupitia manabii Wake. Shuhudia kwamba Yeye hutuonya kwa sababu Anatupenda na anataka sisi tuwe salama (ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii).

  • Wasomee watoto kutoka Mafundisho na Maagano 1:4: “Na sauti ya onyo itakuwa kwa watu wote.” Shiriki jambo ambalo nabii amefundisha hivi karibuni ambalo linaweza kutuweka salama. Onesha picha husika, kama itawezekana. Zungumza kuhusu jinsi unavyofuata ushauri wa nabii.

Mafundisho na Maagano 1:17, 29.

Joseph Smith ni nabii wa Mungu.

Pale wewe na watoto mnapoanza kujifunza Mafundisho na Maagano, wasaidie kujenga shuhuda zao za wito mtakatifu wa Joseph Smith.

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha ya Nabii Joseph Smith (ona Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia; ona pia Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 87). Waombe watoto wasimame kando ya picha na kushiriki kile wanachofahamu kuhusu Joseph Smith.

  • Waache watoto washikilie picha ya Mwokozi na picha ya Joseph Smith. Zungumza nao kuhusu kile Mwokozi alichotupatia kupitia Joseph Smith, kama vile amri (ona mstari wa 17) na Kitabu cha Mormoni (ona mstari wa 29). Waambie watoto kwamba katika Mafundisho na Maagano watajifunza kuhusu amri Bwana alizotoa kwa Kanisa kupitia Joseph Smith.

  • Shiriki hisia zako kuhusu Joseph Smith, na shuhudia kwamba Mungu alisema “nimemwita mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na kusema naye kutoka mbinguni” (mstari wa 17).

Mafundisho na Maagano 1:38

Maneno ya nabii ni maneno ya Mungu.

Watoto unaowafundisha yaweza kuwa wamewahi kumsikia Rais wa Kanisa akizungumza, lakini wanaweza wasitambue kwamba maneno yake yanatoka kwa Mungu. Wasaidie kutambua maneno ya nabii kama maneno ya Mungu.

Shughuli za Yakini

  • Chezeni mchezo rahisi kwa kutoa maelekezo kwa mtoto mmoja na kumuuliza kurudia maelekezo kwa watoto wengine. Wasaidie kuona kwamba maelekezo ya mtoto ni sawa na kufuata maelekezo yako na kwamba kumfuata nabii ni sawa na kumfuata Bwana. Wasomee mstari wa mwisho wa Mafundisho na Maagano 1:38: “Iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa.”

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu manabii, kama vile ubeti wa mwisho wa “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11). Shiriki ushuhuda wako kwamba nabii huzungumza neno la Mungu.

  • Shiriki picha, kipindi kilichorekodiwa, au video fupi ya nabii anayeishi. Toa ushuhuda wako kwamba nabii hutuambia kile Mungu anataka sisi tujue. Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu nabii.

    kikao cha mkutano mkuu

    Nabii anatufunza kile Mungu anataka sisi tujue.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 1:15–17, 29–30

Bwana alifahamu changamoto ambazo tungepitia, hivyo Yeye alirejesha injili kupitia kwa Joseph Smith.

Unaweza kuwasaidia watoto kujiandaa kwa ajili ya changamoto za baadaye kwa kuwafundisha jinsi Urejesho wa injili unavyotoa ulinzi wa kiroho.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kufikiria baadhi ya matatizo ya ulimwenguni leo. Rejea Mafundisho na Maagano 1:15–16 pamoja nao, na wasaidie kutambua baadhi ya matatizo ambayo Bwana alitoa unabii kwamba yangetokea. Waalike kugundua katika mstari wa 17 na 29–30 kile Bwana alichofanya kutusaidia kukabiliana na changamoto za wakati wetu.

  • Waombe watoto wafikirie kwamba wanajiandaa kwa safari. Ni nini wangefungasha? Ni kwa jinsi gani ingewasaidia kujua kwamba mvua ingenyesha wakati wa safari yao au kwamba gari yao ingepasuka tairi? Someni pamoja mstari wa 17, na jadili kile Bwana alichojua kingetokea kwetu na jinsi Yeye alivyoandaa kwa hilo. (Kama ni muhimu, elezea kwamba “majanga” ni madhara au kitu cha kuogofya.) Ni kwa jinsi gani amri za Mungu hutusaidia kukabiliana na changamoto za wakati wetu?

Mafundisho na Maagano 1:30

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni kanisa la Bwana la “kweli na lililo hai.”

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuwa na shukrani kwa baraka kuu za kuwa waumini wa “kanisa pekee la kweli na lililo hai”?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuorodhesha baadhi ya vitu ambavyo ni hai na baadhi ya vitu ambavyo si hai (ikiwezekana, leta picha au mifano). Kuna tofauti gani kati ya kitu hai na kitu kisicho hai? Someni pamoja mstari wa 30. Inamaanisha nini kwamba Kanisa ni la “kweli”? kwamba liko “hai”?

  • Onesha picha, kama vile mchoro wa picha ya Mwokozi, na waombe watoto wauelezee huku taa za chumba zikiwa zimezimwa. Tumia shughuli hii kuwasaidia watoto kuona kwamba kwa watu wengi, Kanisa la kweli la Mwokozi liko katika “kutoonekana” na “gizani.” Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu Kanisa?

Mafundisho na Maagano 1:37–38.

Neno la Bwana linadumu milele.

Unaweza kuwasaidia watoto kujenga imani yao katika Yesu Kristo kwa kuwafundisha kwamba neno Lake ni hakika na la kutegemewa.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kulinganisha vitu ambavyo ni vya muda, kama vile povu au kipande kidogo cha theluji, na vitu ambavyo vinaonekana vya kudumu, kama mlima au jua. Waombe watafute katika mstari wa 37–38 kitu ambacho Bwana alisema ni cha kudumu. Kwa nini ni baraka kujua kwamba neno la Mungu “halitapita kamwe”?

  • Wasaidie watoto kuelewa kwamba “sauti ya watumishi wangu” hujumuisha sauti za mitume na manabii wetu. Wasaidie watoto kutafuta “unabii na ahadi” katika hotuba ya mkutano mkuu wa hivi karibuni iliyotolewa na mmoja wa watumishi wa Bwana. Toa ushuhuda wako kwamba maneno haya yamevuviwa na Bwana na “yote yatatimizwa.”

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Fanya marejeo pamoja na watoto kile walichojifunza leo, na waalike kuchagua kitu kimoja ambacho wanahisi kila mmoja anapaswa kukijua. Wahimize kukishiriki na rafiki au mwanafamilia.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto hujifunza kwa njia nyingi. “Watoto wote hawafanani, na kila mtoto anakua kwa haraka. Juhudi zako katika kuwafundisha watoto zitakuwa za ufanisi zaidi unapotumia mbinu mbali mbali za kufundishia,” ikijumuisha hadithi, visaidizi vya kuona, na muziki (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).