Mafundisho na Maagano 2021
Januari 11–17. Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65: “Mioyo ya Watoto Itawageukia Baba Zao”


“Januari 11–17 Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65: “Mioyo ya Watoto Itawageukia Baba Zao,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021 (2020)

“Januari 11–17 Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Moroni Anamtokea Joseph Smith

Aliniita kwa Jina, na Michael Malm

Januari 11–17

Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65

“Mioyo ya Watoto Itawageukia Baba Zao”

Anza maandalizi yako kwa kusoma Mafundisho na Maagano 2 na Joseph Smith—Historia ya 1:27–65. Mawazo katika muhtasari huu yanaweza kukusaidia kufundisha kweli katika vifungu hivi.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ungeweza kuanza darasa kwa kuwaomba watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu matembezi ya malaika Moroni kwa Joseph Smith.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Joseph Smith—Historia ya 1:27–54

Baba wa Mbinguni alimwita Joseph Smith kumsaidia kufanya kazi Yake.

Shukrani ya watoto kwa ajili ya Nabii Joseph Smith inaweza kuongezeka pale wanapojifunza kuhusu kazi ambayo Mungu alimwita kufanya.

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha ya Moroni akimtembelea Joseph Smith (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 91). Waombe watoto kuonesha mambo wanayogundua katika picha. Fanyia muhtasari tukio la matembezi ya Moroni kwa Joseph. Kadiri inavyohitajika, rejea kwenye Joseph Smith—Historia ya 1:27–54 na “Sura ya 3: Malaika Moroni na Mabamba ya Dhahabu” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 13–17). Waalike watoto wajifanye kuwa Joseph Smith katika hatua mbalimbali kwenye hadithi kwa kukunja mikono yao kana kwamba wanasali, wakijifanya kupanda Mlima Kumora, na kadhalika.

  • Soma Joseph Smith—Historia ya 1:33 kwa sauti, na waombe watoto wasimame wakati wanaposikia kirai “Mungu alikuwa na kazi ya kufanywa nami.” Ni nini Mungu alimtaka Joseph afanye? Ni nini Yeye anatuomba sisi tufanye? Waache watoto wachore picha za vitu Mungu anavyowataka wafanye, kama vile kusali, kutumikia, au kusoma maandiko.

Mafundisho na Maagano 2

Eliya alimpa Joseph Smith funguo za kuunganisha familia pamoja.

Kujifunza kuhusu nguvu ya kuunganisha iliyorejeshwa kupitia Joseph Smith kungeweza kuwasaidia watoto kuwa na shukrani kwa baraka za familia za milele.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kusema jina “Eliya” mara kadhaa. Waombe wasikilize jina hili pale unaposoma Mafundisho na Maagano 2:1. Elezea kwamba haya ni maneno ya Moroni kwa Joseph Smith, na yanafundisha kwamba Eliya angekuja kurejesha mamlaka ya ukuhani. Eliya baadaye alimtokea Joseph ndani ya Hekalu la Kirtland na kumpa Nabii nguvu ya kuunganisha familia pamoja.

  • Waombe watoto wakuambie jambo wanalopenda kuhusu familia zao. Onesha picha ya familia pembeni ya hekalu—familia yako mwenyewe, ikiwezekana (au ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 120). Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anataka familia zetu ziwe pamoja milele, na hii ndiyo sababu moja ya Yeye kutupatia mahekalu.

  • Imbeni pamoja “Familia Zinaweza Kuwa Pamoja Milele” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188). Ni nini wimbo huu unasema tunaweza kufanya ili kuwa pamoja na familia zetu milele?

Mafundisho na Maagano 2

Kujifunza kuhusu mababu zangu kunaweza kunipa shangwe.

Hata watoto wadogo wanaweza kufurahia kuhusu na kuhisi shangwe ya historia ya familia.

Shughuli za Yakini

  • Mwalike mzazi wa mmoja wa watoto kuja darasani na kushiriki hadithi kuhusu babu (na onesha picha kama ipo). Zungumza kuhusu shangwe unayohisi wakati unapojifunza kuhusu historia ya familia yako.

  • Mpe kila mtoto karatasi yenye umbo la moyo. Wasaidie kuandika majina yao na “ninaahidi kuwakumbuka mababu zangu” juu yake. Soma Mafundisho na Maagano 2:2, na uelezee kwamba Eliya alikuja kugeuza mioyo yetu iwaelekee mababu zetu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Joseph Smith—Historia ya 1:28–29

Ninaweza kusali ili kusamehewa.

Watoto unaowafundisha wanaweza wakati mwingine kuhisi “hatia kwa udhaifu [wao] na kutokuwa wakamilifu” (Joseph Smith—Historia ya 1:29) kama Joseph Smith alivyohisi. Wasaidie wajifunze kwamba wanaweza kumgeukia Baba wa Mbinguni kwa ajili ya msamaha.

Shughuli za Yakini

  • Soma pamoja na watoto Joseph Smith—Historia ya 1:29. Je, ni kwa jinsi gani Joseph Smith alihisi kuhusu makosa yake? Ni nini alifanya kuhusu makosa hayo? Nini tunaweza kujifunza kutokana na mfano wa Joseph ambacho kinaweza kutusaidia wakati tunapofanya makosa? Waulize watoto jinsi inavyowafanya wahisi kujua kwamba Joseph aliitwa na Mungu japokuwa hakuwa mkamilifu.

  • Kwa nini ni muhimu kufikiria kuhusu “hali ya msimamo wetu mbele za [Mungu]”? (Joseph Smith—Historia ya 1:29). Waambie watoto kile unachofanya wakati unapojiuliza kuhusu hali ya msimamo wako kwa Mungu.

Joseph Smith—Historia ya 1:30–54

Joseph Smith aliitwa na Mungu kufanya kazi muhimu.

Kusoma ujumbe wa Moroni kwa Joseph Smith kunaweza kuwasaidia watoto kuimarisha shuhuda zao kuhusu wito mtakatifu wa Joseph.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuigiza au kuchora picha za matukio kutoka Joseph Smith—Historia ya 1:30–54, kama vile Moroni akimtokea Joseph (mistari 30–47), Joseph akizungumza na baba yake (mistari 48–50), na Joseph akipata mabamba (mistari 51–54). Nini tunajifunza kutokana na tukio hili kuhusu kazi Joseph aliyoitwa kufanya?

  • Soma pamoja na watoto Joseph Smith—Historia ya 1:33–35, na waombe wasikilize kile Moroni alichotaka Joseph ajue kuhusu kazi Joseph aliyoitwa kufanya. Ni kwa jinsi gani tumebarikiwa kwa sababu Joseph Smith alitimiza kazi yake kama mtafsiri wa Kitabu cha Mormoni? Waalike watoto kusoma Kitabu cha Mormoni kila mara.

Mafundisho na Maagano 2

Baba wa Mbinguni anataka familia ziunganishwe hekaluni.

Moroni alimwambia Joseph Smith kwamba Eliya angekuja “kufunua … Ukuhani” (mstari wa 1). Hii humaanisha nguvu ya kuunganisha ambayo huwezesha familia kuunganishwa milele na kutuwezesha sisi kupokea ibada kwa ajili ya mababu zetu hekaluni.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto wasome unabii katika Mafundisho na Maagano 2:1. Waombe watafute nani Bwana angemtuma katika siku za mwisho na kile ambacho mtu huyu angefunua. Onesha picha ya Eliya ndani ya Hekalu la Kirtland (ona Kitabu cha sanaa ya Injili, na. 95), na zungumza kuhusu jinsi unabii huu ulivyotimia miaka 13 baada ya matembezi ya Moroni (ona Mafundisho na Maagano 110:13–15).

  • Elezea kwamba Eliya alirejesha funguo za ukuhani ambazo zinaruhusu familia kuunganishwa pamoja milele. Onesha vitu ambavyo vingeweza kuwasaidia watoto kuelewa kile inachomaanisha kuunganisha kitu, kama vile kopo la chakula au mfuko wa plastiki wa kuhifadhia wenye kifungio cha zipu. Ni kwa jinsi gani vitu hivi vinatusaidia kuelewa kile inachonaanisha kwa familia kuunganishwa?

  • Onesha picha ya hekalu, na wasaidie watoto kutaja baadhi ya mambo tunayofanya hekaluni. Elezea kwamba ubatizo wa wafu, ndoa ya milele, na kuunganisha familia hekaluni vyote vinawezekana kwa sababu ya funguo za ukuhani alizorejesha Eliya.

  • Mwalike msichana au mvulana katika kata kushiriki uzoefu ambapo alipata jina la babu na alibatizwa kwa ajili ya babu yule hekaluni.

    Hekalu la Palmyra New York

    Familia zinaunganishwa hekaluni kwa nguvu iliyorejeshwa kupitia Eliya.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuwaomba wazazi wao kuwasimulia hadithi kuhusu mmoja wa mababu zao au kuwasaidia kuandaa chakula pendwa cha babu na kukila kwa pamoja.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko. Ili kuwasaidia watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko, fokasi katika mstari mmoja wa maandiko au hata kirai muhimu tu. Unaweza kuwaalika watoto kusimama au kuinua mikono wakati wanaposikia neno hilo au kirai hicho. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21.)