Mafundisho na Maagano 2021
Januari 18–24. Mafundisho na Maagano 3–5: “Kazi Yangu Itasonga Mbele”


“Januari 18–24. Mafundisho na Maagano 3–5: “Kazi Yangu Itasonga Mbele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Januari 18-24. Alma 3–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Watu wakifanya kazi shambani

Wakati wa Mavuno huko Ufaransa, na James Taylor Harwood

Januari 18–24

Mafundisho na Maagano 3–5

“Kazi Yangu Itasonga Mbele”

Unapojifunza Mafundisho na Maagano 3–5, unaweza kupokea misukumo kuhusu kile watoto unaowafundisha wanahitaji kuelewa. Shughuli katika muhtasari huu zinaweza pia kukupa mawazo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onesha picha ya Joseph Smith kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na wasaidie watoto kushiriki kile wanachokijua kuhusu hadithi inayoelezwa. Wasaidie kukumbuka hadithi ya Martin Harris kupoteza kurasa za mwanzo za Kitabu cha Mormoni (ona “Sura ya 4: Martin Harris na Kurasa Zilizopotea,” Mafundisho na Maagano, 18–21; au Watakatifu, 1:51–56).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 3:7–10

Ninaweza kuchagua mema wakati wengine wanapojaribu kunifanya nitende mabaya.

Wasaidie watoto wajifunze kile Joseph Smith alichojifunza: ikiwa watamwamini Baba wa Mbinguni, Yeye atakuwa “pamoja [nao] katika wakati wote wa matatizo” (Mafundisho na Maagano 3:8).

Shughuli za Yakini

  • Fanyia marejeo hadithi ya Martin Harris na kurasa za muswada zilizopotea (ona Hadithi za Mafundisho na Maagano, 18–21, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Shiriki pamoja na watoto baadhi ya hali muhimu wakati wanapoweza kujaribiwa kufanya jambo wanalojua si jema. Ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni hutusaidia kuchagua mema? (ona Mafundisho na Maagano 3:8).

    Picha
    Martin Harris

    Martin Harris, na Lewis A. Ramsey

  • Soma maneno haya kutoka Mafundisho na Maagano 3:8: “Yeye angelikunyooshea mkono wake na kukutegemeza.” Waalike watoto kusimama na kunyoosha mikono yao pale unaposoma tena kirai. Shiriki pamoja nao baadhi ya njia ambazo Bwana anaweza kunyoosha mkono Wake kuwasaidia wakati wengine wanapojaribu kuwafanya wafanye mambo mabaya. Waache wafanye zamu kunyoosha mikono yao pale wanapoelezea njia zingine ambazo Bwana hunyoosha mkono Wake kutusaidia.

Mafundisho na Maagano 4

Bwana ananihitaji mimi kuifanya kazi Yake.

Watoto wanaweza “kuingia katika utumishi wa Mungu” (Mafundisho na Maagano 4:2) katika njia nyingi, na wanaweza kujitayarisha sasa kwa fursa za ziada katika siku za baadaye.

Shughuli za Yakini

  • Soma Mafundisho na Maagano 4:1 kwa watoto. Leta baadhi ya picha ambazo zinaelezea kazi ya “ajabu” ya siku za mwisho ya Mungu (kama vile picha za wamisionari, mahekalu, na Kitabu cha Mormoni). Waache watoto wafanye zamu kuchagua picha na kuizungumzia. Shiriki kwa nini kazi ya Bwana ni ya ajabu kwako.

  • Wasaidie watoto wafikirie juu ya matendo au kuchora picha zikielezea kirai “mtumikie kwa moyo wenu wote, uwezo, akili na nguvu zenu zote” (Mafundisho na Maagano 4:2). Shiriki mfano wa mtu unayemfahamu anayemtumikia Mungu katika njia hii.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kazi ya umisionari, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168). Jadilini kile wimbo unachofundisha kuhusu jinsi tunavyoweza kumsaidia Mungu kufanya kazi Yake.

Mafundisho na Maagano 5:10

Tumepokea neno la Mungu kupitia kwa Joseph Smith.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuimarisha shuhuda zao kwamba Joseph Smith na manabii wengine wanafundisha neno la Mungu?

Shughuli za Yakini

  • Ficha picha ya Joseph Smith mahala fulani ndani ya chumba (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 87). Soma Mafundisho na Maagano 5:10, na waalike watoto kutafuta picha ili kupata neno “kwako” linamaanisha nani. Toa ushuhuda wako kwamba tumepokea neno la Mungu kupitia Joseph Smith.

  • Waoneshe watoto nakala za Kitabu cha Mormoni na Mafundisho na Maagano. Elezea kwamba Mungu alitupatia sisi maandiko haya kupitia Joseph Smith. Shiriki baadhi ya mistari uipendayo kutoka kwenye vitabu hivi, na eleza kwa nini una shukrani kwa ajili ya vitabu hivyo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 3:5–10; 5:21–22

Napaswa kujali zaidi kuhusu kumpendeza Mungu kuliko kuwapendeza wengine.

Pale watoto wanapojifunza kuhusu uzoefu wa Joseph Smith na kurasa zilizopotea za tafsiri ya Kitabu cha Mormoni, wanaweza kupata msukumo kubaki waaminifu wakati wengine wanapowashawishi kutokuwa watiifu.

Shughuli za Yakini

  • Siku chache kabla, mwalike mmoja wa watoto kuja darasani akiwa amejitayarisha kushiriki hadithi ya Joseph Smith na Martin Harris wakipoteza kurasa za mwanzo za tafsiri ya Kitabu cha Mormoni (ona Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 18–21; au Watakatifu, 1:51–56). Someni pamoja Mafundisho na Maagano 3:5–8; 5:21–22, na tafuta baraka ambazo huja wakati tunapobaki waaminifu kwa Mungu.

  • Waalike watoto kufikiria kuhusu wakati ambapo walituhumiwa kwa kufanya jambo ambalo hawakulifanya. Waalike kutafuta kirai katika Mafundisho na Maagano 3:5–8; 5:21–22 ambacho kingeweza kuwasaidia katika kipindi cha hali hizo. Igizeni mifano michache.

Mafundisho na Maagano 4

Bwana ananihitaji mimi kufanya kazi Yake.

Mafundisho na Maagano 4 inaweza kuwashawishi watoto kuwa sehemu ya “kazi ya ajabu” ya Bwana (mstari wa 1).

Shughuli za Yakini

  • Andika ubaoni Mtumikie Mungu. Waalike watoto kupekua Mafundisho na Maagano 4 na kutengeneza orodha ya mambo wanayojifunza kuhusu kile inachomaanisha kumtumikia Mungu. Waombe waongeze kwenye orodha mambo wanayojifunza kutoka kwenye wimbo “I Will Be Valiant” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 162) au wimbo mwingine kuhusu kumtumikia Mungu.

  • Leta vifaa (au picha za vifaa) ambavyo mtu angeweza kutumia kufanya kazi shambani. Ni kwa jinsi gani vifaa hivi hutusaidia? Wasaidie watoto kutafuta vitu katika Mafundisho na Maagano 4:5–6 ambavyo vingeweza kuwa sawa na vifaa vya kufanya kazi ya Mungu.

  • Waalike wamisionari wa muda wote au wamisionari wa kata kushiriki jambo kutoka Mafundisho na Maagano 4 ambalo limewapa msukumo wa kufanya kazi ya Mungu. Ni nini tunaweza kufanya ili kusaidia katika kazi ya Mungu?

Mafundisho na Maagano 5:1–7, 11, 16, 23–24

Ninaweza kuwa shahidi kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.

Martin Harris aliahidiwa kwamba angekuwa mmoja wa mashahidi wa mabamba ya dhahabu ikiwa angekuwa mwaminifu. Hatutayaona mabamba kama Martin Harris, lakini tunaweza kupokea ushahidi wa kiroho wa Kitabu cha Mormoni. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujenga na kushiriki ushahidi wao wenyewe wa Kitabu cha Mormoni?

Shughuli za Yakini

  • Andika maswali sawa na yafuatayo ubaoni, na wasaidie watoto kupata majibu katika Mafundisho na Maagano 5:1–3, 7, 11: Ni nini Martin Harris alitamani kujua? Ni nani Joseph Smith angeweza kumwonesha mabamba ya dhahabu? Kwa nini kuona mabamba hakungetosha kumshawishi mtu kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli?

  • Waulize watoto shahidi ni nani na kwa nini shahidi ni muhimu. Ni nini Martin Harris alitakiwa kufanya ili kuwa shahidi wa mabamba ya dhahabu? (ona Mafundisho na Maagano 5:23–24). Japokuwa hatujayaona mabamba, ni nini tunaweza kufanya kuwa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni? (ona Mafundisho na Maagano 5:16; Moroni 10:3–5).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kuandika shuhuda zao za Kitabu cha Mormoni na kuzishiriki na mtu wanayemfahamu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Badilisha shughuli kukidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Mabadiliko madogo kwenye shughuli yanaweza kuhakikisha kwamba watoto wote wanaweza kujifunza kutokana na shughuli hizo. Kwa mfano, kama shughuli inapendekeza kuonesha picha, mnaweza kuimba wimbo kama mbadala ili kuwajumuisha watoto wenye mapungufu ya kuona.

Chapisha