Mafundisho na Maagano 2021
Nyenzo za Ziada


“Nyenzo za Zaida,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Nyenzo za ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
familia ikijifunza nyenzo za Kanisa

Nyenzo za Ziada

Nyingi ya nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika Gospel Library app na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Kwa kuongezea kwenye matoleo yaliyochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za kusikiliza na video za nyimbo nyingi za Kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika Sacred Music app.

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo hutoa chimbuko la kihistoria na maoni ya kimafundisho kwa kanuni na matukio yanayopatikana katika maandiko.

Majarida ya Kanisa

Majarida ya The Friend, New Era, Ensign, na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuongezea kwenye kanuni unazofundisha kutoka kwenye Mafundisho na Maagano.

Mada za Injili

Katika Mada za Injili unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za masomo ya injili, pamoja na viunganisho vya nyenzo saidizi, kama zile zinazohusiana na jumbe za mkutano mkuu, makala, maandiko, na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa majibu ya kina ya maswali ya kimafundisho na ya kihistoria.

Hadithi za Mafundisho na Maagano

Hadithi za Mafundisho na Maagano hutumia picha na lugha iliyorahisishwa kuwasaidia watoto kujifunza kutoka kwenye Mafundisho na Maagano. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika Gospel Library app na kwenye Gospel Media Library kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Kitabu Cha Kupaka Rangi Cha Historia za Maandiko: Mafundisho na Maagano

Nyenzo hii ina kurasa za shughuli zilizobuniwa kuongeza ujifunzaji wa watoto kutoka kwenye Mafundisho na Maagano.

Video na sanaa

Kazi ya sanaa, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuisaidia familia yako kupata taswira ya mafundisho na hadithi zenye uhusiano na maandiko. Tembelea Gospel media Library kwenye ChurchofJesusChrist.org kuperuzi mkusanyiko wa Kanisa wa nyenzo za vyombo vya habari. Nyenzo hizi pia zinapatikana katika Gospel Media app, na picha nyingi pia zinapatikana katika Kitabu Cha Sanaa za Injili

Ufunuo katika Muktadha

Ufunuo katika Muktadha: Hadithi zilizopelekea kutokea kwa Sehemu za Mafundisho na Maagano ni mkusanyiko wa insha kuhusu historia inayozungumzia funuo zilizopo katika Mafundisho na Maagano. Muktadha uliotolewa katika nyenzo hii unaweza kukusaidia kuelewa vyema kile ambacho maneno ya Bwana katika Mafundisho na Maagano yalimaanisha kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho wa hapo mwanzo.

Watakatifu

Watakatifu ni masimulizi ya juzuu nyingi za historia ya Kanisa. Juzuu ya 1, Kiwango cha Ukweli, na juzuu ya 2, Hakuna Mkono Usio Mtakatifu, zinaelezea kipindi kile kile cha historia ya Kanisa kama Mafundisho na Maagano. Historia hizi zinaweza kukupa ufahamu wa muktadha unaopelekea funuo unazojifunza katika Mafundisho na Maagano.

Mada za Historia ya Kanisa

Makala nyingi kuhusu watu, vitu vilivyobuniwa, jiografia, na matukio ya Kanisa vinaweza kupatikana kwenye ChurchofJesusChrist.org/study/history/topics.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Nyenzo hii inaweza kukusaidia kujifunza na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo.

Chapisha