“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia
Nyenzo Hii Ni Kwa Ajili ya nani?
Nyenzo hii ni kwa ajili ya kila mtu binafsi na familia katika Kanisa. Imetengenezwa ili kukusaidia wewe kujifunza injili—iwe peke yako au na familia yako. Kama hujajifunza injili mara kwa mara huko nyuma, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuanza. Kama tayari una mazoea mazuri ya kujifunza injili, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuwa na uzoefu mwingi wa maana.
Je, Ni Kwa Namna Gani Ninapaswa Kuitumia Nyenzo Hii?
Tumia nyenzo hii katika njia ambayo ina manufaa kwako. Unaweza kuona ina manufaa kama mwongozo au msaada wa kujifunza maandiko kwako binafsi na kifamilia. Unaweza pia kuitumia kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani. Mihutasari huonesha kanuni muhimu zinazopatikana ndani ya Mafundisho na Maagano, hupendekeza mawazo ya kujifunza na shughuli kwa ajili ya watu binafsi na familia, na hutoa sehemu za kuandika misukumo yako.
Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia haikusudiwi kuwa mbadala au kushindana na mambo mazuri unayofanya. Fuata mwongozo wa Roho ili kuamua jinsi ya kuanza kujifunza kwako mwenyewe neno la Mungu.
Ni Kwa Jinsi Gani Nyenzo Hii Inahusiana na Kile Kinachotokea Kanisani?
Mihutasari katika nyenzo hii imepangwa kulingana na ratiba ya kusoma kila wiki. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili zinafuata ratiba sawa. Ili kusaidia juhudi zako za kujifunza na kuishi injili nyumbani, walimu wako kanisani watakupa fursa za kushiriki uzoefu wako, mawazo, na maswali kuhusu vifungu vya maandiko ambavyo umekuwa ukijifunza ukiwa nyumbani.
Kwa sababu Shule ya Jumapili inafundishwa mara mbili tu kwa mwezi, walimu wa Shule ya Jumapili wanaweza wakachagua kuunganisha au kuacha mihutasari ili kwenda sambamba na ratiba ya kila wiki. Hii yaweza pia kuwa ya muhimu katika wiki ambapo mikutano ya kawaida ya Kanisa haifanyiki kwa sababu ya mkutano wa kigingi au kwa sababu zinginezo. Katika muda wa wiki hizi unaalikwa kuendelea kujifunza Mafundisho na Maagano nyumbani.
Je, Ninahitaji Kufuata Ratiba?
Ratiba itakusaidia kumaliza kusoma Mafundisho na Maagano kufikia mwisho wa mwaka. Kwa kuongezea, kufuata ratiba sawa na wengine kunaweza kuongoza kwenye uzoefu wa maana nyumbani, kanisani, na kwingine kokote. Lakini usijisikie kufungwa na ratiba au kulazimishwa kusoma kila mstari; ratiba ni mwongozo wa kukusaidia kirahisi kujipima mwenyewe. Kitu cha muhimu ni kwamba unajifunza injili wewe binafsi na kama familia.