Mafundisho na Maagano 2021
Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2: “Tunaamini”


“Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2: “Tunaamini”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
blanketi likionesha mikono yenye ngozi za rangi nyingi

Kwa Waumini Wote wa Kiume Wenye Kustahili, na Emma Allebes

Desemba 6–12

Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2

“Tunaamini”

Unapojifunza Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2, fikiria matokeo ambayo yamekuwa nayo kwenye Kanisa. Ni nini kinachokuvutia kuhusu kweli yanayozifundisha?

Andika Misukumo Yako

Katika miaka 200 tangu Ono la Kwanza la Joseph Smith, Mungu ameendelea kutoa “ufunuo juu ya ufunuo, maarifa juu ya maarifa” kwa viongozi wa Kanisa Lake (Mafundisho na Maagano 42:61). Katika baadhi ya mambo, ufunuo ule uliwaongoza viongozi wa Kanisa kufanya mabadiliko kwenye sera na utekelezaji wa Kanisa, “kulingana na matakwa ya Bwana, akilinganisha rehema zake kulingana na hali za wanadamu” (Mafundisho na Maagano 46:15). Matamko Rasmi 1 na 2 yanawakilisha aina hii ya ufunuo—moja iliongoza kwenye mwisho wa zoezi la ndoa ya mitala, na lingine lilifanya baraka za ukuhani, ikijumuisha baraka za hekaluni, zipatikane kwa watu wa mbari zote. Mabadiliko kama haya ni sehemu ya kile inachomaanisha kuwa na “kanisa lililo hai na la kweli” (Mafundisho na Maagano 1:30), na nabii aliye hai na wa kweli.

Bali pia kuna vitu ambavyo havibadiliki—vya msingi, kweli za milele. Na wakati mwingine azma ya ufunuo ni kutupa mwanga wa ziada kwenye kweli hizi, kutusaidia kuziona kwa uwazi zaidi. Makala ya Imani—muhtasari wa kauli 13 za Joseph Smith za kile Watakatifu wa Siku za Mwisho wanachoamini—zinaonekana kuhudumia azma hii ya ufafanuzi. Aina zote za ufunuo zinaongoza na kubariki Kanisa, Kanisa ambalo kwa uimara limeanzishwa juu ya kweli za milele lingali bado linaweza kukua na kubadilika kadiri Bwana anavyoongeza uelewa wetu ili kutusaidia kukabiliana na changamoto za leo. Kwa maneno mengine, “Tunaamini yale yote ambayo Mungu ameyafunua, na ambayo sasa anayafunua, na tunaamini kwamba bado Yeye atayafunua mambo mengi makuu na muhimu yahusuyo Ufalme wa Mungu” (Makala ya Imani 1:9).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Makala ya Imani

Makala ya Imani zina kweli za msingi za injili ya urejesho.

Njia mojawapo unayoweza kujifunza Makala ya Imani ni kuorodhesha kweli ambazo zinapatikana katika kila moja na kisha tafuta maandiko yanayohusiana na kweli hizi. Ni jinsi gani maandiko haya yanasitawisha uelewa wako wa kweli katika Makala ya Imani?

Ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Makala ya Imani,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org; L. Tom Perry, “Mafundisho na Kanuni Zilizopo katika Makala ya Imani,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 46–48; “Chapter 38: The Wentworth Letter,” katika Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith, 435–47.

Makala ya Imani 1:9; na Matamko Rasmi 1 na 2

Kanisa la Yesu Kristo linaongozwa na ufunuo.

“Tunaamini kwamba [Mungu] bado atayafunua mambo mengi makuu na muhimu yahusuyo Ufalme wa Mungu” (Makala ya Imani 1:9), hata wakati vitu hivyo vinamaanisha kubadili sera za Kanisa na utekelezaji. Pamoja na kanuni hii akilini, rejea Matamko Rasmi 1 na 2, na tafuta maneno na mafungu ya maneno ambayo yanaimarisha imani yako katika ufunuo endelevu. Ni mifano gani mingine ya ufunuo endelevu kwa nabii wa Bwana unayoweza kuifikiria? Ni kwa jinsi gani funuo hizi zimeathiri maisha yako? Ni kwa jinsi gani zimeendeleza kazi ya ufalme wa Baba wa Mbinguni?

Ona pia Amosi 3:7; 2 Nefi 28:30.

Tamko Rasmi 1

Kazi ya Mungu lazima iendelee mbele.

Katika “dondoo kutoka Hotuba Tatu za Rais Wilford Woodruff kuhusu Manifesto” (mwisho wa Tamko Rasmi 1), ni sababu gani nabii alizitoa kwa Bwana kusitisha zoezi la ndoa ya mitala? Hii inakufundisha nini kuhusu kazi ya Mungu?

Kwa taarifa zaidi kuhusu chimbuko la kihistoria la Tamko Rasmi 1, ona “Mjumbe na Manifesto” (Ufunuo katika Muktadha, 323–31) na “Ndoa za Mitala na Familia katika Utah ya hapo Mwanzo” (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org).

Picha
picha ya kuchora ya Wilford Woodruff

Wilford Woodruff, na H. E. Peterson

Tamko Rasmi 2

Tunaweza kumwamini Bwana, hata wakati hatuna uelewa mkamilifu.

Maandiko yanatufundisha kumwamini Bwana (ona methali 3.5), na hicho ndicho waumini wengi wa Kanisa wa asili ya Afrika walifanya wakati Kanisa lilipozuia utawazo kwenye ukuhani na ibada za hekaluni kwao. Japokuwa hawakuelewa kwa nini sera hii ilikuwepo—na mara nyingi waliumizwa na maelezo yaliyofundishwa wakati ule, ambayo Kanisa limeyatupilia mbali leo—waumini wengi wacha Mungu wenye asili ya Kiafrika walimwamini Bwana na walibaki waaminifu maisha yao yote. Unaposoma Tamko Rasmi 2, tafakari jinsi ulivyojifunza kumwamini Bwana hata wakati huna uelewa mkamilifu.

Kujifunza kuhusu imani ya waumini weusi wa Kanisa kungeweza kukutia moyo. Haya ni baadhi ya maelezo yao, yanayopatikana kwenye history.ChurchofJesusChrist.org:

  • Jane Elizabeth Manning James” (Church History Topics)

  • In My Father’s House Are Many Mansions” (hadithi ya Green Flake)

  • You Have Come at Last” (hadithi ya Anthony Obinna)

  • “Break the Soil of Bitterness” (hadithi ya Julia Mavimbela)

  • I Will Take It in Faith” (hadithi ya George Rickford)

Ona pia “kushuhudia Uaminifu,” Ufunuo katika Muktadha, 332–41; Mada za Injili, “Mbari na Ukuhani,” topics.ChurchofJesusChrist.org; Ahmad Corbitt, “Insha Binafsi juu ya Mbari na Ukuhani,” sehemu ya 1–4, history.ChurchofJesusChrist.org; BeOne.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Makala ya Imani.Fikiria jinsi familia yako ingeweza kutengeneza “masomo mafupi” kwa ajili ya Makala ya Imani. Kwa mfano, katika wiki yote, kila mwanafamilia angeweza kuchagua makala moja na kutafuta andiko linalohusiana, picha, wimbo wa Kanisa, au wimbo wa watoto au kushiriki uzoefu binafsi.

Au wanafamilia wangeweza kufanya zamu kuulizana maswali kuhusu Kanisa na imani zetu na kisha kujibu maswali hayo kwa makala ya imani.

Tamko Rasmi 1 na 2.Tamko Rasmi 1 na 2 yanatusaidia kuelewa jukumu la ufunuo wa sasa katika Kanisa. Familia yako inapoyasoma pamoja, fikiria kujadiliana jinsi nabii anavyotuongoza “kwa misukumo ya Mwenyezi Mungu” (Tamko Rasmi 1). Ni kwa jinsi gani matangazo haya mawili yanaimarisha imani yetu katika Mungu anayeishi ambaye binafsi analiongoza Kanisa Lake? Ni kwa jinsi gani tunauona mkono Wake katika kazi ya Kanisa leo? Mnaweza kuamua kuchunguza pamoja baadhi ya nyenzo katika “Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko” hapo juu.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Keep the Commandments,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia mialiko ya kutenda. “Wakati unapofuatilia mwaliko wa kutenda, wewe unawaonyesha [wanafamilia wako] kwamba unawajali na jinsi gani injili inabariki maisha yao. Unawapa pia fursa kushiriki uzoefu wao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35).

Chapisha