Mafundisho na Maagano 2021
Desemba 20–26. Krismasi: Zawadi Isiyolinganishwa ya Mwana Mtukufu wa Mungu


“Desemba 20–26. Krismasi: Zawadi isiyolinganishwa ya Mwana Mtukufu wa Mungu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Desemba 20–26. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
sanaa ya Mariamu na mtoto Yesu

Kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika Shaba na Khaki nyekundu, na J. Kirk Richards

Desemba 20–26

Krismasi

Zawadi Isiyolinganishwa ya Mwana Mtukufu wa Mungu

Njia mojawapo ya kufokasi mawazo yako kwa Mwokozi katika Krismasi hii ni kujifunza “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume.” Muhtasari huu unapendekeza njia unazoweza kufanya ushuhuda huu wa kinabii kuwa sehemu yako binafsi na ya familia ya kujifunza injili.

Andika Misukumo Yako

Mnamo mwaka 1838, Nabii Joseph Smith alitangaza, “Kanuni za msingi za dini yetu ni ushuhuda wa Mitume na Manabii, kuhusu Yesu Kristo, kwamba Alikufa, Akazikwa, na Akafufuka tena siku ya tatu, na kupaa mbinguni; na mambo yote mengine ambayo yanahusiana na dini yetu ni viambatisho vyake” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith, 49). Miaka mingi baadaye, Rais Russell M. Nelson alisisitiza kwamba “ilikuwa kauli hii hasa ya Nabii ambayo ilitoa motisha kwa ajili ya manabii, waonaji, na wafunuzi 15, kutoa na kusaini ushuhuda wao ili kufanya ukumbusho wa maadhimisho ya miaka 2000 ya kuzaliwa kwa Bwana. Ushuhuda huo wa kihistoria unaitwa ‘Kristo Aliye Hai.’ Waumini wengi wamekariri kweli zake. Wengine kwa shida wanajua uwepo wake. Unapotafuta kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo, ninakusihi sana kujifunza ‘Kristo Aliye Hai’” (“Kupokea Nguvu ya Yesu Kristo kwenye Maisha Yetu,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 40).

Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunashangilia kwa baraka ya ufunuo endelevu kupitia manabii na mitume wa sasa. Tuna shukrani kwa maneno yao ya ushauri yenye msukumo, maonyo, na kutia moyo. Lakini zaidi ya yote, tumebarikiwa na shuhuda zao za nguvu za Yesu Kristo—wakati wa Krismasi na mwaka mzima. Haya ni zaidi ya maneno ya kusisimua tu ya waandishi stadi au wazungumzaji wa umma au umaizi kutoka kwa wataalamu wa maandiko. Haya ni maneno ya wateule wa Mungu, walioitwa, na kupewa mamlaka “mashahidi maalumu wa jina la Kristo ulimwenguni kote” (Mafundisho na Maagano 107:23).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

“Hakuna mwingine aliyekuwa na ushawishi mkubwa.”

Ni mawazo gani yanakujia unaposoma Luka 2:10–11 pamoja na aya ya kwanza ya “Kristo Aliye Hai”? Utasema nini kuunga mkono kauli kwamba “hakuna mwingine aliyekuwa na ushawishi mkubwa [kama Yesu Kristo] juu ya wote ambao wameishi na ambao bado wataishi juu ya dunia”? Tafuta kweli katika “Kristo Aliye Hai” ambazo zinaelezea ushawishi wa kina wa Mwokozi. Amekuvutia vipi na kukuletea “furaha kuu” ? (Luka 2:10).

“Alifufuka kutoka kaburini.”

Katika “Kristo Aliye Hai,” Mitume wanashuhudia juu ya Kufufuka kwa Mwokozi, wakitaja kutokea mara tatu kwa Bwana aliyefufuka (ona aya ya tano). Unaweza kusoma kuhusu ziara hizi katika Yohana 20–21; 3 Nefi 11–26; na Joseph Smith—Historia ya 1:14–20. Unajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye maneno Yake na vitendo wakati wa kujitokeza huku?

“Ukuhani Wake na Kanisa Lake vimerejeshwa.”

Wakati wa mafunzo yako ya Mafundisho na Maagano mwaka huu, umekuwa na fursa ya kujifunza zaidi kuhusu jinsi “ukuhani wa Mwokozi na Kanisa Lake vilivyorejeshwa.” Kweli gani au kanuni zilizorejeshwa zimekuwa hususani zenye maana kwako? Fikiria kurejea baadhi ya maandiko yafuatayo ambayo yanafundisha kuhusu Urejesho: Mafundisho na Maagano 1:17–23; 13; 20:1–12; 65; 110; 112:30–32; 124:39–42; 128:19–21. Tafakari jinsi kweli za injili ya urejesho zinavyokusaidia wewe kujua na kumwabudu Yesu Kristo (ona Mafundisho na Maagano 93:19).

“Siku moja atarudi duniani.”

Krismasi ni muda wa kutazama nyuma juu ya siku Yesu Kristo alipozaliwa na kungojea kwa hamu siku atakaporudi tena. Unajifunza nini kuhusu kurudi kwake kutoka aya ya pili mpaka ya mwisho ya “Kristo Aliye Hai”? Inaweza pia ikapendeza kusoma, kuimba, au kusikiliza nyimbo za Kanisa za Krismasi ambazo zinafundisha kuhusu Ujio wa Pili kama vile “Joy to the World” au “It Came upon the Midnight Clear” (Nyimbo za Kanisa, na. 201, 207).

“Yeye ni nuru, uzima, na tumaini la ulimwengu.”

Katika aya ya mwisho ya “Kristo Aliye Hai,” angalia sifa na vyeo vilivyotolewa kwa ajili ya Mwokozi. Maandiko yafuatayo yanaweza kukusaidia kutafakari jinsi ambavyo Yesu Kristo ni “nuru, uzima, na tumaini la ulimwengu”: Luka 2:25–32; 1 Wakorintho 15:19–23; Moroni 7:41; Mafundisho na Maagano 50:24; 84:44–46; 93:7–10. Ni kwa jinsi gani amekuwa nuru yako, uzima na tumaini? Ni sifa gani zingine au vyeo vya Mwokozi vina maana sana kwako?

Jinsi gani kujifunza “Kristo Aliye Hai” kuliathiri imani yako katika na upendo kwa ajili ya Mwokozi?

Picha
Yesu Kristo

Nuru ya Ulimwengu, na Howard Lyon

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

“Kristo Aliye Hai.”Ili kusaidia familia yako kuelewa kweli zilizofundishwa kuhusu Mwokozi katika “Kristo Aliye Hai,” ungeweza kuchagua baadhi ya virai muhimu na mfanye kazi pamoja kupata au kuchora picha ambazo zinaelezea virai hivyo. Kisha ungeweza kukusanya picha hizo na virai katika kitabu.

“Tunatoa ushuhuda wetu.”Tunajifunza nini kutoka “Kristo Aliye Hai” kuhusu kile inachomaanisha kutoa ushuhuda? Unaweza kutaka kuandika ushuhuda wako wa Kristo ili kuadhimisha kuzaliwa kwa Mwokozi.

“Alizunguka huko na huko, akitenda kazi njema.”Jinsi gani familia yako itafuata mfano wa Mwokozi wa huduma kwenye Krismasi hii? Utasambaza vipi “amani na upendo” katika familia yako na jumuiya? Jinsi gani unaweza kusaidia kuleta “uponyaji [kwa] wagonjwa”? Unaweza kupata mawazo katika baadhi ya Video za Krismasi kwenye Gospel Media app au Gospel Media library (medialibrary.ChurchofJesusChrist.org).

“Mungu ashukuriwe kwa ajili ya zawadi isiyolinganishwa ya Mwanaye mtukufu.” Ni zawadi gani tulizopokea kwa sababu ya Yesu Kristo? Pengine wanafamilia wangeweza kupata majibu katika “Kristo Aliye Hai” na kisha vifaa vya kufungia zawadi ambavyo vinawakilisha zawadi hizo kutoka kwa Mwokozi. Familia Yako ingeweza kufungua zawadi hizo siku ya Krismasi au katika wiki yote na kusoma maandiko yanayoendana na kila zawadi. Haya ni baadhi ya maandiko, ingawa familia yako inaweza kupata mengine mengi: Luka 2:10–14; 1 Petro 2:21; Mosia 3:8; Alma 11:42–43; Mafundisho na Maagano 18:10–12. Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu Mwokozi, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35), ili kupata zawadi zingine ambazo zinakuja kutoka Kwake.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Hark! The Herald Angels Sing,” Nyimbo za Kanisa, na. 209.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Fokasi kwa Mwokozi. “Kusoma kwa sala ‘Kristo Aliye Hai’ ni kama kusoma shuhuda za Mathayo, Marko, Luka, Yohana, na manabii wa Kitabu cha Mormoni. Itaongeza imani yako katika Mwokozi na kukusaidia kubaki umefokasi juu Yake” (M. Russell Ballard, “Return and Receive,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 65).

Chapisha