Mafundisho na Maagano 2021
Januari 10. Kwa nini Ono la Kwanza Ni la Muhimu? Utangulizi wa Mafundisho na Maagano; Joseph Smith—Historia ya 1:1–26


“Januari 10. Kwa nini Ono la Kwanza Ni la Muhimu? Utangulizi wa Mafundisho na Maagano; Joseph Smith—Historia ya 1:1–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Januari 10. Kwa nini Ono la Kwanza Ni la Muhimu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
Joseph Smith akisali

Niliona Mwanga, na John McNaughton

Januari 10

Kwa nini Ono la Kwanza Ni la Muhimu?

Utangulizi wa Mafundisho na Maagano; Joseph Smith—Historia ya 1:1–26

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, nani anahitaji usaidizi wetu na sala zetu? Je, ni nini tunaweza kufanya ili kuwasaidia? Je, nani tumualike katika shughuli ijayo?

  • Wajibu wetu au majukumu. Je, ni majukumu gani tumeshayatimiza? Je, ni majukumu gani tunahitaji kuyatoa? Je, ni kwa jinsi gani tumewaalika wengine kuja kwa Kristo, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaalika wengine hivi sasa?

  • Maisha yetu. Je, ni uzoefu gani wa hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu? Je, ni nini kinatokea katika maisha yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Japo ni zaidi ya miaka 200 tangu Joseph Smith kwa mara ya kwanza alipopiga magoti na kusali katika Msitu Mtakatifu, jibu alilolipokea kwa kiasi kikubwa huathiri maisha yetu leo. Tafakari baraka ambazo zimekuja katika maisha yako kwa sababu Baba na Mwana walimtokea Joseph. Kwa nini ni muhimu kwa wale unaowafundisha kupata ushuhuda wao wenyewe wa Ono la Kwanza kutoka kwa Roho Mtakatifu? Je, utawasaidiaje kufanya hili? ungeweza kupata msaada kwa kurejea ujumbe kutoka mkutano mkuu wa Aprili 2020, ambao ulisherehekea kumbukizi ya miaka 200 ya ono hili tukufu.

Picha
wasichana darasani

Kila kijana anaweza kupokea ushuhuda binafsi wa Ono la Kwanza.

Jifunzeni Pamoja

Kwa sababu Joseph Smith alikuwa katika ujana wake wakati wa Ono la Kwanza, wale unaowafundisha wanaweza kujichukulia wao kwenye kutafuta kwake ukweli. Wapatie washiriki wa akidi au darasa dakika chache kushiriki mawazo yao na misukumo kuhusu Joseph Smith—Historia ya 1:1–26. Shughuli hapa chini zinaweza kuwasaidia wao kuimarisha shuhuda zao kwamba Mungu Baba na Yesu Kristo walimtokea Joseph Smith.

  • Ni kweli zipi za injili tunajifunza kutoka katika uzoefu wa Joseph Smith katika Msitu Mtakatifu? Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kusoma simulizi ya Joseph katika Joseph Smith—Historia ya 1:7–20 na kushiriki kweli wanazozipata. (Kwa mfano, Mungu husikia na kujibu maombi; Shetani na nguvu yake ni dhahiri, lakini nguvu ya Mungu ni kubwa; ufunuo bado haujakoma.) Ni kwa jinsi gani kweli hizi zimebariki maisha yetu?

  • Unaweza pia kuwaomba washiriki wa akidi au darasa kurejea jumbe kuhusu Ono la Kwanza kutoka katika Mkutano mkuu wa Aprili 2020 (ona Liahona, Mei 2020). Waalike kushiriki kile walichopata na hisia zao kuhusu Ono la Kwanza.

  • Kila Rais wa Kanisa ameshuhudia kuhusu kazi takatifu ya Nabii Joseph Smith. Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kunufaika kwa kusoma shuhuda zao katika mojawapo ya vitabu vya kiada vya Mafundisho ya Marais wa Kanisa. (Vingi vya vitabu hivi vya kiada vina sura kuhusu Nabii Joseph Smith. Kwa ajili ya orodha ya sura hizi, ona Mada za Injili, “Ono la Kwanza,” topics.ChurchofJesusChrist.org.) Siku chache kabla ya darasa, ungeweza kuwaalika washiriki wa akidi yako au darasa lako kuchagua mmoja wa Marais hawa na kushiriki kauli aliyoisema ambayo wangeweza kuitumia kumfundisha mtu kuhusu Ono la Kwanza.

  • Fikiria kuwaalika washiriki wa akidi au darasa kusoma “Urejesho wa Injili ya Yesu Kristo kupitia Joseph Smith” katika sura ya 3 ya Preach My Gospel ([2019], 36–38) na kufanya mazoezi ya kufundishana kuhusu Ono la Kwanza. Unaweza kuwapa changamoto ya kushiriki uzoefu wa Joseph Smith kwa kutumia baadhi ya maneno yake mwenyewe, yanayopatikana katika Joseph Smith—Historia ya 1:16–17

  • Je, wale unaowafundisha wanatambua kwamba kuna masimulizi kadhaa ya Ono la Kwanza? Kila moja ya masimulizi haya hutoa maelezo ya kipekee ambayo huleta uelewa mkamilifu wa kile kilichotokea katika Msitu Mtakatifu. Ungeweza kufupisha sehemu ya “Muhtasari” ya insha ya Mada za Injili “First Vision Accounts” (topics.ChurchofJesusChrist.org). Kisha ungeweza kuwaomba wale unaowafundisha kupitia ufupisho wa masimulizi manne yanayopatikana kwenye “Masimulizi ya Ono la Kwanza.” Wanaweza pia kusoma baadhi ya masimulizi halisi kwa kutumia viunganishi vilivyotolewa. Wamepata nini ambacho kimeimarisha ushuhuda wao wa Ono la Kwanza? Mnaweza kuangalia video “Ask of God: Joseph Smith’s First Vision” (ChurchofJesusChrist.org), ambayo huelezea Ono la Kwanza kwa kutumia taarifa kutoka katika masimulizi haya. Kwa nini ni vizuri kuwa na masimulizi kadhaa ya Ono la Kwanza? Ni kwa jinsi gani masimulizi haya hutusaidia kuwaelewa vyema Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda kulingana na misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama wangependa, washiriki wa akidi au darasa wangeweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

  • Mathayo 3:13–17; Matendo ya Mitume 7:54–60; 3 Nefi 11:3–10 (Mungu Baba na Yesu Kristo walijidhihirisha Wenyewe kwa watu duniani)

  • “Tunajifunza nini kuhusu asili ya Mungu kutoka katika Ono la Kwanza?” video kutoka Face to Face with President Eyring and Elder Holland (worldwide youth broadcast, Mar. 4, 2017), FacetoFace.ChurchofJesusChrist.org

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi aliwaalika wanafunzi wake kushuhudia ukweli wa mafundisho Yake. Na walipofanya hivyo, Roho aligusa mioyo yao. Unawezaje kuwahimiza wale unaowafundisha kutoa shuhuda zao? (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 11.)

Ona pia “Prepare to Teach” (video, ChurchofJesusChrist.org).

Chapisha