Mafundisho na Maagano 2021
Januari 24. Ninawezaje Kujiandaa Kushiriki katika “Kazi ya Maajabu” ya Mungu? Mafundisho na Maagano 3–5


“Januari 24. Ninawezaje Kujiandaa Kushiriki katika ‘Kazi ya Maajabu’ ya Mungu? Mafundisho na Maagano 3–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Januari 24. Ninawezaje Kujiandaa Kushiriki katika ‘Kazi ya Maajabu’ ya Mungu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

wasichana na mvulana wakiwa mbele ya hekalu

Januari 24

Ninawezaje Kujiandaa Kushiriki katika “Kazi ya Maajabu” ya Mungu?

Mafundisho na Maagano 3–5

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Tunaweza kufanya nini ili kujenga umoja miongoni mwa washiriki wa akidi au darasa? Je, ni malengo gani tunahitaji kuyashughulikia pamoja?

  • Wajibu wetu au majukumu. Tunafanya nini ili kushiriki injili? Ni uzoefu gani tumeupata wakati tunafanya kazi ya hekalu na historia ya familia?

  • Maisha yetu. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu? Ni nini kimetutia moyo katika kujifunza kwetu maandiko wiki hii?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Wakati Watakatifu wa mwanzo walipoanza kusikia ujumbe wa injili ya urejesho, wengi walitaka kujua wangeweza kufanya nini ili kusaidia katika kazi. Baba wa Nabii Joseph Smith, Joseph Smith Mkubwa, ni miongoni mwa wale walioomba kujua mapenzi ya Bwana kwa ajili yake. Jibu la Bwana, lipatikanalo katika Mafundisho na Maagano 4, tangu hapo limewatia moyo vizazi vya watu kutumikia kwa “moyo, uwezo, akili na nguvu” zao zote (mstari wa 2). Kama unatumikia misheni au unatumikia katika wito wowote au jukumu katika Kanisa, vigezo vya huduma ni sawa: tamaa ya kumtumikia Mungu ikiambatana na imani, tumaini, hisani, na upendo (ona Mafundisho na Maagano 4:2–6). Unawezaje kuwasaidia washiriki wa akidi yako au darasa lako kukuza hamu yao ya kumtumikia Bwana na kujiandaa kwa ajili ya fursa za baadaye za kutumikia?

Ili kujiandaa kwa ajili ya kuongoza washiriki wa akidi au darasa katika somo hili, unaweza kusoma na kutafakari moja au zaidi ya jumbe zinazopatikana katika “Nyenzo Saidizi.”

wavulana wakimtembelea mzee

Kuwajali wale wenye mahitaji ni sehemu ya kazi ya wokovu.

Jifunzeni Pamoja

Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kuwa wamehamasishwa kumtumikia Bwana kwa bidii zaidi kwa kusoma Mafundisho na Maagano 3–5 wiki hii. Ili kuwahimiza kushiriki mawazo yao, unaweza kuwaalika wafikirie kwamba wanaomba kazi. Ni vigezo gani wataviweka kwenye wasifu binafsi au kuviongelea kwenye usaili? Wanaweza kurejea Mafundisho na Maagano 4 na kutafuta vigezo ambavyo Bwana anavihitaji kwa wale wanaotaka kushiriki katika kazi Yake. Chagua shughuli moja au zaidi hapa chini ili kuwasaidia wale unaowafundisha kufikiria ni nini wanahitajika kufanya ili kushiriki kikamilifu katika “kazi ya maajabu” ya Mungu (Mafundisho na Maagano 4:1).

  • Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kujifunza jinsi ya kushiriki katika kuharakisha kazi ya wokovu, andika ubaoni maana ifuatayo ya kazi ya wokovu: Mungu huwaalika wote kuja kwa Kristo na kusaidia katika kazi Yake kwa kuishi injili ya Yesu Kristo, kuwajali wale wenye mahitaji, kuwaalika wote kupokea injili, na kuunganisha familia milele zote. Waalike washiriki wa akidi au darasa kujadili jinsi sifa zilizotajwa katika Mafundisho na Maagano 4 zitakavyowasaidia kufanya kila kipengele cha kazi ya wokovu. Wagawe vijana katika makundi, na liruhusu kila kundi lijadili jinsi wanavyoweza kukuza sifa hizi. Je, tunaweza kufanya nini ili kufanya kazi ya wokovu kuwa sehemu muhimu sana ya maisha yetu?

  • Waalike washiriki wa akidi au darasa kurejea mojawapo ya jumbe zinazopatikana katika “Nyenzo Saidizi,” wakitafuta nukuu wanayoweza kuishiriki kuhusu jinsi ya kumtumikia Bwana kwa uaminifu katika miito ya Kanisa, kazi, au majukumu mengineyo. Waombe kushiriki nukuu waliyoichagua na kwa nini wanaiona ni ya kufaa. Ni kwa jinsi gani watatumia yale waliyojifunza sasa na baadaye?

  • Baadhi ya washiriki wa akidi au darasa wanaweza kuwa wanajiandaa kutumikia kama wamisionari. Unaweza kuwaomba kushiriki jinsi wanavyojiandaa kutumikia. Ili kuwahimiza katika jitihada zao, unaweza kushiriki swali ambalo Mzee David A. Bednar alisema mara kwa mara hulipokea: “Nifanye nini ili nijiandae ipasavyo kutumikia kama mmisionari wa muda wote?” (“Becoming a Missionary,” Liahona, Nov. 2005, 45). Ni kwa jinsi gani washiriki wa akidi au darasa watajibu swali hili? Ni mawazo gani Mzee Bednar aliyatoa? Unaweza kualika mmsionari mmoja aliyerudi au wengi zaidi ili kushiriki kile walichofanya kujiandaa kwa ajili ya misheni na kile walichotamani wangefanya.

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi aliwaalika wanafunzi Wake kushuhudia, na walipofanya hivyo, Roho aligusa mioyo yao. Wakati unapofundisha kuhusu utiifu, kwa mfano, waalike washiriki wa akidi au darasa kushiriki shuhuda zao za umuhimu wa kutii amri. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 1132.)