“Februari 14. Ukuhani ni nini? Mafundisho na Maagano 12–13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)
“Februari 14. Ukuhani ni nini?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021
Februari 14
Ukuhani ni nini?
Mafundisho na Maagano 12–13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75.
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):
-
Akidi au darasa letu. Je, ni shughuli gani tumeshafanya hivi karibuni? Je, zilifanikiwa? Ni nini kilifanyika vizuri, na ni jinsi gani tunaweza kuziboresha?
-
Wajibu wetu au majukumu. Ni nani anahitaji huduma yetu? Tunawezaje kuwasaidia?
-
Maisha yetu. Ni malengo gani tunayashughulikia kibinafsi? Ni uzoefu gani tunaweza kuushiriki? Ni baraka zipi tumezipokea?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Unaposoma kuhusu urejesho wa Ukuhani wa Haruni katika Mafundisho na Maagano 13, jaribu kusoma kupitia macho ya wale unaowafundisha. Je, wanaelewa nguvu ya ukuhani katika maisha yao? Ni kwa jinsi gani ibada za ukuhani kama vile ubatizo na sakramenti zimekusaidia kupokea nguvu ya Mwokozi? Fikiria kuhusu uzoefu unaoweza kuushiriki. Ili kujiandaa binafsi kwa ajili ya kufundisha kuhusu ukuhani, fikiria kusoma maandiko yaliyopendekezwa katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na “Ukuhani” katika Mwongozo kwenye Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).
Jifunzeni Pamoja
Kwa kuanza mjadala kuhusu ukuhani, unaweza kuwaalika washiriki wa akidi au darasa kushiriki kile wanachojua kuhusu urejesho wa Ukuhani wa Haruni, ikihusisha kile walichosoma wiki hii katika Mafundisho na Maagano 13 na Joseph Smith—Historia ya 1:66–75. Unaweza pia kuonyesha picha ikielezea urejesho wa Ukuhani wa Haruni (kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, [2009], na. 93) na waalike washiriki wa akidi au darasa kushiriki kile wanachojua kuhusu tukio hili. Kwa nini tunashukuru kwamba ukuhani ulirejeshwa? Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema ukuhani ni nini na jinsi gani tunabarikiwa nao.
-
Ni kwa jinsi gani washiriki wa akidi au darasa wataelezea ukuhani ni nini kwa mtu ambaye hajawahi kuusikia kabla? Ili kuwasaidia, unaweza kuorodhesha ubaoni baadhi ya maswali ambayo watu wanaweza kuwa nayo kuhusu ukuhani, kama vile Ukuhani ni nini? Ni kwa jinsi gani mtu hupokea ukuhani? Ni kwa jinsi gani mwenye ukuhani anapaswa kutenda? Je, wenye ukuhani hufanya nini? Waalike wale unaowafundisha kutafuta majibu wakitumia maandiko na nyenzo nyinginezo zinazopatikana katika “Nyenzo Saidizi” na waandike majibu yao ubaoni. Unaweza kuwaomba kushiriki baraka zilizokuja maishani mwao kwa sababu ya ukuhani. Unaweza pia kuonyesha na kujadili video ya “How the Priesthood Works” (ChurchofJesusChrist.org; ona pia Dale G. Renlund, “Ukuhani na Nguvu ya upatanisho ya Mwokozi,” Liahona, Nov. 2017, 64–67).
-
Kama unafundisha wenye Ukuhani wa Haruni, wanaweza kunufaika kwa kurejea ujumbe wa Kaka Douglas D. Holmes “Kile Ambacho Kila Mwenye Ukuhani wa Haruni Anahitaji Kuelewa” (Liahona, Mei 2018, 50–53). Unaweza kumpangia kila mshiriki wa akidi kurejea baadhi ya aya za ujumbe au mojawapo ya sehemu zingine nne. Mwalike kila mtu kutafuta kitu ambacho anahisi kila mwenye Ukuhani wa Haruni anatakiwa kuelewa. Mpe fursa ya kushiriki kile alichojifunza na kuelezea kwa nini amechagua funzo hilo.
-
Kama unafundisha wasichana, unaweza kushiriki ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Hazina za Kiroho,” ambao ulitolewa kwao (Liahona, Nov. 2019, 76–79). Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kuchunguza ujumbe wake wakitafuta kitu wanachoweza kufanya ili “kuleta nguvu ya Mwokozi” kikamilifu zaidi katika maisha yao (ukurasa wa 77). Ni kitu gani Rais Nelson alifundisha kuhusu jinsi tunavyoweza kufikia nguvu ya ukuhani? Ni kwa jinsi gani nguvu ya ukuhani inatubariki? Wahimize wasichana kufikiria jinsi watakavyotenda kwa mwaliko huu wa Rais Nelson: “Ninawasihi kujifunza kwa maombi kweli zote mnaoweza kupata kuhusu nguvu ya ukuhani” (ukurasa wa 79).
Tenda kwa Imani
Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.
Nyenzo Saidizi
-
Mafundisho na Maagano 84:17–22; 107:1–5 (Ukuhani ni nguvu na mamlaka ya Mungu)
-
Waebrania 5:4; Makala ya Imani 1:5 (Wenye ukuhani huitwa na Mungu na kutawazwa na yule mwenye mamlaka)
-
Mafundisho na Maagano 121:34–46 (Nguvu na mamlaka ya ukuhani hufanya kazi kupitia kanuni za haki tu)
-
Mathayo 3:1–6; 28:16–19; Yohana 15:16; Mafundisho na Maagano 12:3–4 (Wanaume na wanawake wanaostahili huhubiri injili)
-
Matendo ya Mitume 3:1–8; Yakobo 5:14–15 (Wenye ukuhani hutoa baraka ili kuponya wagonjwa na wanaoteseka)
-
3 Nefi 11:21–22; 18:1–5; Mafundisho na Maagano 107:20 (Wenye ukuhani huhudumu katika ibada)
-
Mafundisho na Maagano 65:2; 107:18–21 (Wenye ukuhani husaidia katika kuongoza kanisa)
-
True to the Faith, “Aaronic Priesthood,” “Melchizedek Priesthood,” “Priesthood,” 3–4, 101–2, 124–28