Mafundisho na Maagano 2021
Februari 28. Kutubu Kunamaanisha Nini? Mafundisho na Maagano 18–19


“Februari 28. Kutubu Kunamaanisha Nini? Mafundisho na Maagano 18–19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Februari 28. Kutubu Kunamaanisha Nini?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
msichana akijifunza

Februari 28

Kutubu Kunamaanisha Nini?

Mafundisho na Maagano 18–19

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, ni nani mgeni katika kata yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia kuhisi wamekaribishwa? Ni kitu gani tunafanya ili kufanya muda wetu katika mikutano ya akidi au madarasa kuwa wa maana?

  • Wajibu wetu au majukumu. Ni yapi baadhi ya majukumu na wajibu tulionao kama wavulana au wasichana? Tunawezaje kuyatimiza vyema?

  • Maisha yetu. Ni nini tunafanya ili kuwa zaidi kama Yesu Kristo na kupokea nguvu Yake katika maisha yetu? Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja Kwake?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Ni vigumu kusoma Mafundisho na Maagano 19:16–19 bila kuhisi upendo wa Mwokozi kwetu. Katika mistari hii, Alielezea mateso aliyoyapata Alipokuwa akiteseka kwa ajili ya dhambi zetu na kufunua kwa nini Alikuwa yuko tayari kuteseka mateso makuu—“ili kwamba [sisi] tusiteseke kama [sisi] tutatubu.” Toba ni baraka iliyowezeshwa na Mwokozi. Ni juhudi endelevu, ya kila siku ya kugeuka kutoka katika dhambi na kumgeukia Mungu. Ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kutusaidia sisi kurudi Kwake. Kuelewa jinsi ya kutubu kunaweza kutusaidia kutakaswa dhambi zetu, kubadili mioyo yetu na akili, na kusogea karibu na Mungu.

Ni kwa jinsi gani toba imekusaidia kusogea karibu na Baba wa Mbinguni? Unawezaje kuwasaidia wale unaowafundisha kuwa na hamu ya kutubu? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wao kuona kwamba toba ni juhudi ya kila siku na siyo kwamba imewekwa kwa ajili ya dhambi kubwa? Unapojiandaa kufundisha, fikiria kusoma ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Tunaweza Kufanya Vizuri na Kuwa Wazuri” (Liahona, Mei 2019, 67–69).

Picha
Yesu Kristo akisali

Kristo akiwa Gethsemane, na Harry Anderson

Jifunzeni Pamoja

Manabii wote toka mwanzo wamewaita watu watubu. Hata hivyo, labda hakuna mwaliko wa kutubu ulio mkali kama wa Mwokozi unaopatikana katika Mafundisho na Maagano 19:15–19, ambao vijana wanaweza kuwa wameusoma wiki hii. Unaweza kuwauliza ni kipi wamejifunza kuhusu Mwokozi kutoka katika mistari hii. Mistari hii inasema nini kuhusu umuhimu wa kutubu mbele za macho ya Bwana? Mawazo yafuatayo yanaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuona toba kama baraka ya kila siku katika maisha yao.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuelewa jinsi toba inavyobariki maisha yao, unaweza kuanza kwa kuuliza maswali yafuatayo: Nitajuaje kama juhudi zangu za kutubu zinafanya kazi? Ni jinsi gani Mwokozi atanisaida kubadilika? Kwa kuongezea kwenye kusamehewa dhambi, ni baraka zipi zingine huja kutokana na toba? Waalike washiriki wa darasa kusoma moja au zaidi ya maandiko katika “Nyenzo Saidizi,” wakitafuta majibu ya maswali. Je, walipata nini? Kama sehemu ya mjadala huu, unaweza kuonyesha video ya “Repentance: A Joyful Choice” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Vijana wengi hawaelewi kutubu kuna maana gani. Wanaweza kuogopa toba au kufikiri inatumika kwa dhambi kubwa tu. Ili kusaidia kusahihisha kutokuelewa huku, unaweza kuwaalika washiriki wa akidi au darasa kusoma sehemu ya ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Tunaweza Kufanya Vizuri na Kuwa Wazuri” (Liahona, Mei 2019, 67–69), wakitafuta vifungu vya maneno ambavyo huwasaidia kuelewa kutubu kunamaanisha nini. Wamepata nini ambacho kimewasaidia kufikiria kuhusu toba katika njia mpya? Ni baraka zipi Rais Nelson aliahidi kwa wale wanaotubu?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa kwa nini na kwa jinsi gani tunatubu? Ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Kutakaswa kwa Toba” (Liahona, Mei 2019, 91–94) unaweza kusaidia. Unaweza kuigawa akidi au darasa katika makundi manne na kukipangia kila kikundi kusoma sehemu mojawapo ya sehemu nne za mahubiri ya Rais Oaks. Kila kikundi kisha kitawasilisha ufupisho wa kile walichosoma kwa makundi mengine, sambamba na maandiko yoyote kutoka kwenye ujumbe ambayo yanaunga mkono kile walichosoma. Unaweza kuhitimisha kwa kuwaomba washiriki wa akidi au darasa kushiriki shuhuda zao za umuhimu wa toba katika mpango wa Mungu.

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi aliwaalika watu kutenda kwa imani na kuishi kweli Alizofundisha. Unaweza kufanya nini ili kuwasaidia wale unaowafundisha kuona nguvu ya toba ya kila siku? (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 3135.)

Chapisha