Agano la Kale 2022
Januari 9. Ni kwa Jinsi Gani Mungu Ananitaka Niwatunze Viumbe Wake, Ikijumuisha Mwili Wangu? Mwanzo 1–2; Musa 2–3; Ibrahimu 4–5


Januari 9. Ni kwa Jinsi Gani Mungu Ananitaka Niwatunze Viumbe Wake, Ikijumuisha Mwili Wangu? Mwanzo 1–2; Musa 2–3; Ibrahimu 4–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

Januari 9 Ni kwa Jinsi Gani Mungu Ananitaka Niwatunze Viumbe Wake, ikijumuisha Mwili Wangu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

mvulana akitembea kando ya ziwa

Januari 9.

Ni kwa Jinsi Gani Mungu Ananitaka Niwatunze Viumbe Wake, Ikijumuisha Mwili Wangu?

Mwanzo 1–2; Musa 2–3; Ibrahimu 4–5

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org) Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Tulijadili nini wakati uliopita, na ni mialiko gani au kazi gani zilitolewa? Tumefanya nini kuitikia mialiko hiyo au kazi hizo?

  • Utunzaji wa wale wenye shida. Tunaweza kusema nini au kufanya nini ili kuwafikia wale wanaoweza kuwa wanahisi kuwa wapweke au wako mbali na Baba wa Mbinguni?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Yesu Kristo?

  • Unganisha familia milele. Ni mawazo gani tunaweza kushiriki mmoja na mwingine ili kutusaidia kuimarisha familia zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

teach the doctrine icon

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; dakika 23–35

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia vijana fikiria kile wanachoweza kufanya kutunza vyema viumbe vya Mungu, andika vichwa vya habari vifuatavyo ubaoni: Muumba, Uumbaji na Majukumu Yetu. Waombe wao wapitie Mwanzo 1–2 na waandike kile wanachojifunza kuhusu Muumba na Uumbaji. Tunajifunza nini kuhusu majukumu yetu? (ona hasa Mwanzo 1:26–28; 2:15). Mawazo yafuatayo yanaweza kuwasaidia vijana kujadili majukumu yetu ya kutunza viumbe vya Mungu.

  • Unawezaje kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa kwamba miili yao ni uumbaji mtakatifu wa Mungu? Kwa mfano, unaweza kuwauliza wao kile wamejifunza kuhusu miili yetu kutoka katika 1 Wakorintho 6:19–20; Musa 2:26–27; Ibarhimu 4:26–27. Maneno “mfano” na “sura” yanamaanisha nini? Fanyeni kazi pamoja kutengeneza orodha ya baadhi ya vitu tunavyoweza kufanya ili kutunza miili yetu. (Ona “Afya ya Mwili na Akili,” Kwa Nguvu ya Vijana (kijitabu, 2011), 25–27.)

  • Vijana mara nyingi wanakabiliwa na jumbe ambazo zinawafanya wahisi kutojiamini kuhusu miili yao. Waalike vijana kutazama video “God’s Greatest Creation” (ChurchofJesusChrist.org). Waombe watafute jumbe ambazo zinawasaidia kusikia kuwa shukrani kwa ajili ya miili yao (ona pia Russell M. Nelson, “Mwili Wako: Zawadi Kuu ya Kutunzwa,” New Era, Aug. 2019, 2–7). Je, tunaweza kushiriki nini ili kumsaidia rafiki au mwanafamilia ambaye anahisi kutojiamini kuhusu mwili wake?

  • Waalike vijana kusoma kimya kimoja au zaidi kati ya vifungu vifuatavyo, wakitafuta umaizi kuhusu kwa nini Mungu aliiumba dunia na jinsi Yeye anatutaka tuitunze: Mwanzo 1:26–28; 2:15; 1 Nefi 17:36; Mafundisho na Maagano 49:19–21; 59:15–20; 104:13–18; Musa 2:26–31; 3:15. Waombe washiriki mawazo yao kuhusu kila kifungu cha maandiko. Kisha waalike wao wafanya kazi pamoja kutengeneza orodha ya vitu ambavyo wanaweza kufanya kibinafsi au kama kundi kutimiza majukumu yao ya kuitunza dunia (ona mawazo katika “Nyenzo Saidizi”). Ni mabadiliko gani tunahitaji kufanya katika mawazo yetu na matendo yetu ili kiutunza dunia vyema?

  • Fikiria kualika washiriki wa darasa au akidi kuja kwenye mkutano na kitu cha ambacho kinaonyesha uzuri wa dunia ambayo Mungu aliiumba, kama vile mchoro, picha, au shairi. Waalike wao kushiriki kile walicholeta na hisia walizonazo kwa ajili ya uumbaji wa Mungu. Onyesha video “Our Home” (ChurchofJesusChrist.org), na uwaombe wasikilize juu ya vitu ambayo vinaonyesha jinsi Mungu anahisi kuhusu dunia na vile vinavyowavutia wao kuitunza.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, waweza kushiriki mawazo yao. Waalike wao wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Njia tunazoweza kuitunza dunia.

  • Panda mbegu, miti, au bustani.

  • Okota takataka katika jumuiya yako.

  • Andaa mradi wa mtaani wa kusafisha au kuhidisha.

  • Nendeni matembezi ya masafa na mtafakari juu ya vitu mlivyo na shukrani navyo.

  • Tengenezeni sanaa kutoka kwa vitu ambavyo vingenevyo mngevitupa, na mvishiriki katika onyesho la sanaa la kundi.

  • Amua njia ambazo mnaweza kuhifadhi nishati na maji.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Wape washiriki wa darasa au akidi nafasi nyingi za kufundishana darasani, kwa vile mara nyingi wao hujifunza vyema kutoka kwa wenzao na kutoka katika uzoefu wa kufundisha.