Januari 23. Ni kwa Jinsi Gani Bwana Anaweza Kunisaidia Kutumikia kwa Uaminifu Zaidi? Mwanzo 5; Musa 6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)
Januari 23 Ni kwa Jinsi Gani Bwana Anaweza Kunisaidia Kutumikia kwa Uaminifu Zaidi? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022
Januari 23
Ni kwa Jinsi Gani Bwana Anaweza Kunisaidia Kutumikia kwa Uaminifu Zaidi?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org) Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Je, ni matukio gani ya hivi karibuni yameimarisha shuhuda zetu?
-
Utunzaji wa wale wenye shida. Je, ni akina nani wanahitaji msaada wetu na sala zetu? Je, ni nini tunahisi kuvutiwa kukifanya ili kuwasaidia?
-
Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa wanafamilia au marafiki ambao hawashiriki imani yetu?
-
Uunganisha familia milele. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha upendo zaidi na ufadhili kwa ajili ya familia zetu na kuleta tofauti chanya katika nyumba zetu?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 23–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Wakati Henoko alipopokea wito wake wa kumtumikia Bwana, alihisi kuwa na mapungufu kabisa (ona Musa 6:31). Lakini Bwana hamkutuma tu Henoko kwenda kufanya kazi Yake; Yeye alimuahidi Henoko kwamba angemlinda na kumsaidia (ona Musa 6:32–34).
Labda unaweza kuhusisha hisia za Henoko za mapungufu katika juhudi zenu mwenyewe za kutumika. Baadhi ya huduma yetu inatolewa kupitia miito ya Kanisa. Nyakati zingine, tunaona tu hitaji na kuhisi msukumo wa Roho kuonyesha upendo wetu na ufadhili. Hata hivyo fursa huja, tunaweza kujipa moyo, kama Henoko alivyofanya, tukijua kwamba Bwana atatusaidia tunapokubali mwaliko Wake “tembea nami” (Musa 6:34).
Unapojiandaa kufundisha kuhusu msaada tunaoweza kupokea kutoka kwa Bwana tunapowatumikia wengine, pitia Musa 6 na fikiria uzoefu uliopata ulipokuwa unawatumikia wengine. Ni kwa jinsi gani Bwana alikusaidia katika juhudi zako? Ni kitu gani unatumaini washiriki wa darasa lako au washiriki wa akidi watajifunza kutoka kwa mifano ya Henoko na wengine? Unaweza pia kusoma mojawapo wa jumbe hizi za Rais Henry B. Eyring: “Tembea Nami” (Liahona, Mei 2017, 82–85) au “Wanawake wa Agano katika Ubia na Mungu” (Liahona, Nov. 2019, 70–73).
Jifunzeni Pamoja
Kuwatumikia wengine hutoa fursa kwetu “kutembea na [Mungu],” na tutapokea msaada Wake tunapotumikia (Musa 6:34). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kuanza mjadala huu, unaweza kuwaomba wapekue Musa 6:32–39 kwa ajili ya njia Bwana alikuwa pamoja na Henoko katika huduma yake. Ni kwa jinsi gani Bwana anatusaidia wakati tunapomtumikia Yeye? Mawazo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuongoza mjadala kuhusu msaada wa kiungu tunaoweza kuupokea tunapowatumikia wengine.
-
Maandiko yamejaa mafundisho kuhusu huduma (ona, kwa mfano, Mathayo 25:31–40; Luka 10:25–37; Mosia 2:17). Fikiria kuwaalika wale unaowafundisha kushiriki vifungu vya maandiko ambavyo vimewapa mwongozo kuwatumikia wengine. Unaweza kuwaomba wao mapema waje wamejiandaa kushiriki vifungu vya maandiko kuhusu huduma au mifano ya huduma. Kama wanahitaji msaada, wahimize watafute kwenye “Huduma” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Tunahisi tumetiwa moyo kufanya nini kwa sababu ya kile tulichosoma?
-
Mwokozi aliwatumikia wengine kote katika huduma Yake. Nini tunajifunza kutokana na mfano Wake ambacho kinaweza kutusaidia tunapotumikia? Kujibu swali hili, kila mshiriki wa darasa au akidi angeweza kusoma mojawapo ya maandiko yafuatayo, akitafuta kitu yanachofundisha kuhusu mfano wa huduma ya Mwokozi: Mathayo 14:13–21; Yohana 9:1–11, 35–38; 13:4–5, 12–17; 3 Nefi 17:5–9. Alika kila mmoja kushiriki kitu alichokipata. Toa muda kwa ajili ya kila mmoja kufikiria juu ya mtu wanayeweza kumtumikia na jinsi watakavyofuata mfano wa Mwokozi katika huduma yao.
-
Wakati mwingine tunafikiria huduma humaanisha kufanya kitu kikubwa na cha kutumia muda mwingi. Hiyo inaweza kuwa sababu moja baadhi yetu hatuhudumii kama ambavyo tungeweza kutumikia. Unaweza kusema wazi kwamba Mwokozi kila mara alitumikia watu Yeye aliowaona kote katika shughuli Zake za kila siku (ona, kwa mfano, Mathayo 12:9–13; Marko 5:21–34; Luka 19:1–10; Yohana 4:3–26). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kufikiria njia rahisi wanazoweza kuwatumikia wengine katika maisha yao ya kila siku, unaweza kuonyesha mojawapo ya video zifuatazo: “When Ye Are in the Service—YM” au “When Ye Are in the Service—YW” (ChurchofJesusChrist.org). Waombe vijana washiriki mawazo yao. Ni vitendo gani vidogo vya huduma tulivyoviona wengine wakifanya? Je, tumetiwa moyo kufanya nini? Mwalike kila mtu aandike njia za kukamilisha kauli zifuatazo: “Mimi ninaweza kuwatumikia wengine kwa …” na “Mimi nitatafuta msaada wa Bwana katika juhudi zangu za kutumikia kwa …” “Kisha waombe baadhi washiriki kile walichoandika.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wao wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kunaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
“Opportunities to Do Good,” “Teachings of Thomas S. Monson: Rescuing Those in Need” (videos), ChurchofJesusChrist.org
-
Bonnie L. Oscarson, “Mahitaji Yaliyo Mbele Yetu” (Liahona, Nov. 2017, 25–27).