Utumishi Ona pia Upendo; Ustawi Msaada uliotolewa au kazi iliyofanywa kwa manufaa ya Mungu na wengine. Tunapowatumikia wengine, tunamtumikia pia Mungu. Chagueni hivi leo mtakayemtumikia, Yos. 24:15. Kadiri mlivyomtendea mmoja wa wadogo hawa, mmenitendea mimi, Mt. 25:35–45. Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, ambayo ndiyo utumishi wenu ulio na maana, Rum. 12:1. Tumikianeni kwa upendo, Gal. 5:13. Siku zako zitatumika katika utumishi wa Mungu wako, 2 Ne. 2:3. Wakati mkiwa katika utumishi wa viumbe wenzenu mnakuwa tu katika utumishi wa Mungu wenu, Mos. 2:17. Watu wanaoimiliki nchi ya ahadi lazima wamtumikie Mungu au watafagiliwa mbali, Eth. 2:8–12. Wale wajiingizao katika utumishi wa Mungu yawapasa kutumikia kwa moyo wao wote, M&M 4:2. Bwana alitoa amri kwamba wanadamu yawapasa kumpenda na kumtumikia yeye, M&M 20:18–19. Katika jina la Yesu Kristo nawe utamtumikia Mungu, M&M 59:5. Mimi, Bwana, napenda kuwaheshimu wale wanaonitumikia, M&M 76:5. Mwabudu Mungu, kwani ni yeye pekee utamtumikia, Musa 1:15.