“Februari 13. Je, Ni kwa Jinsi Gani Tunaweza Kubaki Wakweli kwa Mwokozi katika Ulimwengu wenye Uovu? Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)
“Februari 13. Je, Ni kwa Jinsi Gani Tunaweza Kubaki Wakweli kwa Mwokozi katika Ulimwengu wenye Uovu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022
Februari 13
Je, Ni kwa Jinsi Gani Tunaweza Kubaki Wakweli kwa Mwokozi katika Ulimwengu wenye Uovu?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org) Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Je, ni kwa jinsi gani tumekaribia Mwokozi? Je, ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?
-
Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni nani amekuwa katika akili zetu karibuni? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watu hawa?
-
Waalike wote kuipokea injili. Je, unaweza kujibu vipi maswali ya marafiki zako kuhusu Kanisa katika njia ambayo inaimarisha imani yao katika Mwokozi?
-
Unganisha familia milele. Ni njia zipi tunazoweza kuunganika vyema na wanafamilia wengine kama vile kina babu na ndugu zetu?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; dakika 23–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Kuishi kwa haki katika ulimwengu wenye uovu kamwe haijakuwa rahisi. Kwa Ibrahimu, shinikizo la kugeuka kutoka kwa Mungu halikutoka tu nje ya nyumba yake—hata baba yake Ibrahimu alikuwa amemuacha Bwana (ona Ibarhimu 1:5–12; 2:5). Ibrahimu na Sera walikumbana na magumu mengi, na bado walitumaini ahadi za Bwana “na wakashawishika nazo, na wakazikumbatia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na mahujaji juu ya nchi. ” (Waebrania 11:13).
Ni kwa jinsi gani utawasaidia washiriki wa darasa au akidi kubaki waaminifu wakati wanajihisi kama “wageni na mahujaji” katika ulimwengu kwa sababu wanaishi viwango vya Bwana? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwatia moyo kuwa jasiri wanapoishi wakweli kwa Bwana? Unapojiandaa kufundisha, fikiria kupitia tena Yohana 15:18–20 na ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Kuushinda Ulimwengu” (Liahona, Mei 2017, 58–62).
Jifunzeni Pamoja
Washiriki wa darasa lako au akidi wanaweza kuwa walivutiwa na mfano wa Ibrahimu wiki hii walipojifunza Mwanzo 12–17 na Ibrahimu 1–2. Unaweza kuwaalika wapitie tena Ibrahimu 1:1–19 na kushiriki kile kilichowavutia kuhusu mfano wa Ibrahimu. Ni mifanano gani tunayoiona kati ya changamoto zilizomkabili Ibrahimu na changamoto tunazokabiliana nazo leo? Chagua shughuli moja au zaidi hapo chini kuhamasisha mjadala kuhusu jinsi tunavyoweza kubaki waaminifu kwa Yesu Kristo katika hali zote.
-
Bwana na manabii wake mara nyingi wamewasihi wale waliowafundisha kuishi kwa uaminifu licha ya uovu unaowazunguka. Ni baadhi ya njia zipi ambazo Shetani huwajaribu vijana kuvunja amri za Mungu katika wakati wetu? Wale unaowafundisha wanaweza kusoma baadhi ya maandiko yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo Saidizi.” Waalike kujadili kile walichojifunza kuhusu kubaki wakweli kwa Kristo wakati ulimwengu unatujaribu tufanye kinyume au kutukejeli. Wanaweza kushiriki njia walizopata za kuishi kwa uaminifu wakati wengine hawafanyi hivyo. Lini sisi au wengine tunaowajua tumeweza kufanya hivyo? Ungeweza pia kuonesha moja au zaidi ya video katika “Nyenzo Saidizi.”
-
Ili kusaidia darasa lako au akidi kuelewa jinsi ya kushinda ulimwengu na kupokea baraka ambazo huja kutokana na kufanya hivyo, andika ubaoni Kuushinda ulimwengu ni … na Kuyashinda matokeo ya ulimwengu katika … Unaweza basi kuwaomba vijana wapitie tena ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Kuushinda Ulimwengu.” Waalike wao kushiriki njia za kukamilisha sentensi hizi, wakiandika kile walichojifunza ubaoni. Jadili kile walichokipata. Alika mtu mmoja mapema kuja amejiandaa kushiriki hadithi ya kuonyesha jinsi Yesu Kristo alibakia mkweli kwa Baba wa Mbinguni licha ya upinzani, (ona, kwa mfano Mathayo 4:1–11; Luka 22:39–44). Ni jinsi gani mifano ya Mwokozi inatusaidia kuelewa kuhusu kuushinda ulimwengu? (ona Yohana 16:33).
-
Wafuasi wa Yesu Kristo wawe “ulimwenguni bali sio wa ulimwenguni.” Kuwa “katika ulimwengu” kunaweza kumaanisha kwamba tunakabiliana na upinzani wakati tunaishi viwango vyetu. Lakini pia inamaanisha kwamba tunaweza kuwashawishi wengine kwa wema. Ili kufundisha kanuni hii, ungeweza kumwomba mtu fulani kuja darasani akiwa amejiandaa kushiriki moja au zaidi ya hadithi katika ujumbe wa Rais Bonnie H. Cordon “Kwamba Ili Waweze Kuona” (Liahona, Mei 2020, 78–80). Tunajifunza nini kutoka hadithi hizi kuhusu kutumia nuru yetu kuwasaidia wengine kuja karibu na Yesu Kristo? Alika darasa au akidi kutafuta ujumbe wa Rais Cordon kwa ajili ya sentensi ambazo zinawatia moyo kuwa nuru kwa wengine katika ulimwengu wenye uovu. Waalike wasome sentensi zao kwa sauti na kushiriki kile wanachohisi kuvutiwa kufanya.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Mathayo 5:14–16; 1 Nefi 15:23–25; Helamani 5:12; Mafundisho na Maagano 10:5; 27:15–18; 87:8 (Jinsi ya kubaki wakweli kwa Yesu Kristo katika ulimwengu wenye uovu)
-
“Stand Ye in Holy Places—Bloom Where You’re Planted,” “195 Dresses,” “Guided Safely Home” (videos), ChurchofJesusChrist.org