“Februari 27. Kwa Nini Ndoa ya Milele Ni Muhimu? Mwanzo 24–27,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)
“Februari 27. Kwa Nini Ndoa ya Milele Ni Muhimu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022
Februari 27
Kwa Nini Ndoa ya Milele Ni Muhimu?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org) Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Ni mada gani uaskofu umejadili katika mikutano ya baraza la vijana la kata yenu? Tunaweza kufanya nini kama darasa au akidi kulingana na umuhimu wa mijadala hiyo?
-
Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafikia watu katika njia za kama Kristo wakati tunaona hitaji na hatujui cha kusema?
-
Waalike wote kuipokea injili. Je, tumepata nini kutoka katika injili ya Yesu Kristo ambacho kinatuletea shangwe? Je, tunawezaje kushiriki shangwe hiyo na wengine?
-
Unganisha familia milele. Tunafanya nini ili kupata majina ya mababu zetu ambao wanahitaji ibada za hekaluni? Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kupata majina ya mababu zao?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Wakati ulipofika wa Isaka kuoa, Ibrahimu alimuomba mtumishi wake kutafuta mke kwa ajili ya Isaka. Ibrahimu na Isaka walitaka kumpata Isaka mke ambaye angefanya na kushika maagano na Bwana na kuyafundisha kwa watoto wake. Rebeka alikuwa mwanamke mwaminifu ambaye aliingia katika agano la ndoa na Isaka. Wakati maandiko hayaweki wazi kwamba ndoa ni ya umuhimu mkubwa kwa Mungu, mafundisho ya Mungu kuhusu ndoa yanatiwa changamoto katika wakati wetu. Lakini manabii wametangaza kwamba ndoa “ilitawazwa na Mungu” (“Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org). Ni muhimu kwa wale unaowafundisha kuelewa kweli za milele kuhusu ndoa. Kufanya hivyo kutawasaida kujiandaa kwa ajili ya na kushuhudia juu ya sehemu hii muhimu ya mpango wa Baba yetu wa Mbinguni.
Ni kwa jinsi gani vijana unaowafundisha wanahisi kuhusu ndoa ya milele? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kufikiria kwa nini ndoa ya milele ni kitovu cha mpango wa Baba wa Mbinguni? Unapojiandaa kufundisha, unaweza kupitia tena ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson, “Kwa Nini Ndoa, Kwa Nini Familia” (Liahona, Mei 2015, 50–53). Unaweza pia kupitia tena “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” (ChurchofJesusChrist.org).
Jifunzeni Pamoja
Vijana unaowafundisha wanaweza kutafakari umuhimu wa ndoa wanapokuwa wakisoma Mwanzo 24–27 wiki hii. Waalike wapitie tena Mwanzo 24. Waombe washiriki mistari inayoonyesha kwamba ndoa ilikuwa muhimu kwa watu walioelezwa katika sura hii. Waalike kufikiria kwa nini ndoa ya milele ni kitovu katika mpango wa Mungu. Shughuli hapa chini zinaweza kuwasaidia kuelewa vizuri zaidi umuhimu wa ndoa.
-
Washiriki wa darasa au akidi yako wanaweza kuwa na fursa za kuelezea kwa nini ndoa ni muhimu kwao. Waalike wao kufikiria wana rafiki anayeamini kwamba ndoa imepitwa na wakati na si lazima. Wanaweza kuwandikia rafiki taarifa ya kuelezea umuhimu wa ndoa katika mpango wa Baba wa Mbinguni. Wahimize kujumuisha kweli wanazozipata katika “Familia: Tangazo Kwa Ulimwengu.” Wanaweza kutumia maandiko wanayopata katika “Nyenzo Saidizi” au katika “Ndoa, Oa” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Waalike kushiriki pamoja na darasa kile walichokiandika.
-
Ili kuanzisha mjadala kuhusu umuhimu wa ndoa, andika ubaoni Kwa nini ndoa ya milele ni muhimu? Wape vijana dakika chache kuandika jibu la swali hili. Kisha waalike wao washiriki majibu yao. Wangeweza kutafuta majibu ya ziada katika ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson, “Kwa Nini Ndoa, Kwa Nini Familia” (Liahona, Mei 2015, 50–53). Wangeweza pia kutazama video “Why Is Marriage Sacred to Heavenly Father?” kutoka katika “Face to Face with Elder and Sister Renlund” (ChurchofJesusChrist.org). Waalike kushiriki ushuhuda zao kuhusu kwa nini ndoa ni muhimu.
-
Tunapokubali mafundisho ya Mungu kuhusu ndoa na kujitahidi kuyaishi, tutapokea baraka nyingi. Lakini baadhi ya watu—ikijumuisha wale wanaofanya vyema kuishi injili—wanakabiliwa na changamoto katika kuanzisha ndoa za milele, zenye furaha. Unaweza kuwaomba vijana kuzungumza kuhusu baadhi ya chamgamoto hizo. Tunaweza kufanya nini sasa kujiandaa kwa ajili ya changamoto hizo? Unaweza pia kuwaalika kusoma sehemu mbili za mwisho za ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Jicho la Imani” (Liahona, Mei 2019, 34–38). Washiriki wa darasa lako au akidi wanaweza kujadili mifano waliyoiona katika maisha yao au historia za familia za watu wanaoshughulikia kwa uaminifu changamoto kama zile zilizotajwa na Mzee Andersen. Ni kwa jinsi gani Mwokozi anaweza kuwasaidia wale wote ambao wanakabiliana na changamoto wanapotafuta baraka za ndoa ya milele?
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Mafundisho na Maagano 49:16–17 (Ndoa husaidia kutimiza kusudi la Uumbaji)
-
Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:15–21 (Ndoa ya milele inahitajika kwa ajili ya kuinuliwa)
-
“Renaissance of Marriage,” “How Did Elder and Sister Bednar Meet?” kutoka “Face to Face with Elder and Sister Bednar” (videos), ChurchofJesusChrist.org