“Machi 13. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kukabiliana na Dhiki kwa Imani? Mwanzo 37–41,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)
“Machi 13. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kukabiliana na Dhiki kwa Imani Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022
Machi 13
Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kukabiliana na Dhiki kwa Imani?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu?
-
Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana katika mambo tunayoyapitia?
-
Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia tekinolojia kama chombo cha kushiriki injili?
-
Unganisha familia milele. Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja kwa Kristo?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Kama mvulana, Yusufu wa Msiri alikabiliana na aina nyingi za dhiki. Alikabiliana na ubishi katika familia yake na aliteswa na kaka zake. Alikabiliwa na majabiru ya kuvunja sheria ya usafi wa kimwili. Lakini badala ya kuheshimiwa kwa ajili ya uadilifu wake, alitiwa gerezani. Washiriki wa darasa au akidi yako wanaweza kukabiliwa na majaribu kama hayo na mengi mengine. Unapojifunza uzoefu wa Yusufu katika Mwanzo 37–41, fikiria kuhusu wale unaowafundisha. Tafakari ni masomo gani yenye thamani maisha ya Yusufu yanaweza kuleta kwao (ona pia Etheri 12:27; Henry B. Eyring, “Jaribu, Jaribu, Jaribu,” Liahona, Nov. 2018, 90–93). Tukio la Yusufu linaweza kuwavutia washiriki wa darasa au akidi kuuliza, “Ninawezaje kukabiliana na dhiki zangu kwa Imani, na jinsi gani Mungu atanisaidia?
Jifunzeni Pamoja
Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa au akidi kuorodhesha ubaoni baadhi ya matukio kutoka katika maisha ya Yusufu wa Msiri, kama ilivyoelezwa katika Mwanzo 37 na 39–41. Kuonyesha baadhi ya picha, kama zile zilizo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kungeweza kuwasaida kukumbuka matukio haya. Je, ni kwa jinsi gani majaribu ya Yusufu yalifanana na changamoto ambazo vijana wanakabiliana nazo leo? Kama Yusufu angekuwa hai sasa, ni ushauri gani yeye angetupatia kuhusu kukabiliana na dhiki? Angesema nini kuhusu jinsi mahusiano yake na Bwana yalimsaidia? Tumia shughuli kama zifuatazo kuwasaidia vijana kufikiria kuhusu jinsi wanavyoweza kukabiliana na changamoto zao kwa imani katika Yesu Kristo.
-
Kujifunza jinsi Mwokozi alikabiliana na dhiki kunaweza kutusaidia kukabiliana na dhiki yetu kwa imani. Vijana wanaweza kupendekeza baadhi ya mifano ya dhiki Mwokozi alikabiliana nazo na mzipitie tena pamoja (ona “Nyenzo Saidizi” kwa baadhi ya mawazo). Ni kitu gani kinatuvutia sisi kuhusu jinsi Mwokozi alivyokabiliana kwa nyakati Zake za dhiki? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano Wake tunapokabiliana na dhiki yetu?
-
Wakati mwingine ni rahisi kukabiliana na dhiki wakati tunajaribu kuiona katika mtazamo wa Bwana. Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa hili, waombe watafute mifano ya tofauti ambazo mtazamo unaweza kuleta kwa kupitia tena ujumbe wa Mzee Rafael E. Pino “Mtazamo wa Milele wa Injili” (Liahona, May 2015, 117–19). Waalike washiriki kile walichokipata. Je, mifano hii inapendekeza nini kuhusu jinsi gani tunaweza kuona na kukabiliana na dhiki zetu? Kama Mwokozi angezungumza nasi kuhusu changamoto zetu, sisi tunafikiria Yeye angesema nini? Ili kujibu swali hili, vijana wanaweza kupitia tena maandiko katika “Nyenzo Saidizi.”
-
Fikiria kuwaomba vijana kushiriki mfano wa mtu fulani (labda babu) ambaye aliwavutia kwa njia yeye alikabiliana na jaribu gumu. Au unaweza ukashiriki mifano inayovutia ya watu unaowajua. Jumbe za mkutano mkuu mara kwa mara zinajumuisha hadithi za watu ambao walikabiliana na dhiki kwa imani (ona baadhi ya mifano katika “Nyenzo Saidizi”). Fikiria nini ungeweza kushiriki kutoka kwenye jumbe kama hizo ambacho kinaweza kuwa na maana sana kwa wale unaowafundisha. Mnapojadili mifano hii pamoja, pendekeza kwamba washiriki wa darasa au akidi walenge juu ya jinsi imani katika Yesu Kristo ilisaidia watu wakati wa dhiki zao. Ungeweza pia kushiriki orodha ya Askofu W. Christopher Waddell ya nyenzo ambazo Bwana ametupatia ili kutusaidia katika changamoto zetu, inayopatikana karibu na mwisho wa ujumbe wake “Mgeukie Bwana” (Liahona, Nov. 2017, 94–96).
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo waliyoipokea leo. Kama watapenda, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Mathayo 4:1–11 (Mwokozi alikuwa na imani wakati wa dhiki)
-
Mathayo 14:10–21; Luka 23:33–34; Yohana 19:25–27 (Mwokozi aliwatumikia wengine wakati wa dhiki Yake)
-
Mathayo 27:45–46; Luka 23:44–46 (Mwokozi alihisi mpweke wakati wa dhiki lakini alimtumaini Mungu)
-
Mathayo 5:38–45; Mosia 24:8–15; Mafundisho na Maagano 121:1–8; 122:5–9 (Mafundisho ya Mwokozi kuhusu kukabiliana na dhiki)
-
Neil L. Andersen, “Umizwa,” Liahona, Nov. 2018, 83–86
-
L. Todd Budge, “Uaminifu Endelevu na Thabiti,” Liahona, Nov. 2019, 47–49.
-
Jean B. Bingham, “Kwamba Shangwe Yenu Iwe Timilifu,” Liahona, Nov. 2017, 85–67.