2010–2019
Kwamba Shangwe Yenu Iwe Kamili
Oktoba 2017


2:3

Kwamba Shangwe Yenu Iwe Kamili

Yesu Kristo ndiye kiini cha uponyaji wote, amani na maendeleo ya milele.

Akina kaka na kina dada zangu, ni shangwe kuwa nanyi. Na hicho ndicho ningependa kuongea nanyi kukihusu asubuhi hii—kuwa na ujalivu wa injili.

Kichwa cha habari za hivi karibuni kilisomeka “Majanga yatikisa taifa [na] dunia.”1 Kutoka vimbunga na mafuriko mpaka joto kali na ukame, kutoka mioto ya porini mpaka na matetemeko mpaka vita na magonjwa yenye kubananga, inaonekana “dunia yote [iko] katika ghasia.”2

Mamilioni ya watu wamehamishwa, na maisha yasiyohesabika yamevurugwa na changamoto hizi. Mabishano katika familia na jamii vilevile mahangaiko ndani kwa ndani kwa uwoga, mashaka, na matarajio yasiotimilizwa pia yametuacha katika zahama. Inaweza kuwa vigumu kuhisi shangwe ambayo Lehi alifundisha kuwa ndio azma ya maisha.3 Sisi sote kwa wakati fulani tumewahi kuuliza, “Ninaweza kugeukia wapi nipate amani? Faraja yangu iko wapi … ?”4 Tunajiuliza, nawezaje kupata shangwe licha ya magumu ya maisha ya dunia?

Jibu linaweza kuonekana rahisi sana, lakini imethibitika kuwa kweli tangu siku za Adamu. Shangwe ya kudumu inapatikana katika kufokasi kwa Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na kuiishi injili kama ilivyoonyeshwa na kufundishwa Naye. Zaidi tunapojifunza, kuhusu, na kuwa na imani kwake, na kufuata mfanowa Yesu Kristo, tunakuja kupata uelewa zaidi kuwa yeye ni kiini cha uponyaji wote, amani na maendeleo ya milele. Anatualika kila mmoja wetu kuja Kwake,5 mwaliko ambao Rais Henry B. Eyring ameupa sifa kama “mwaliko muhimu sana yeyote angeweza kuukubali.”6

Jifunze juu ya Yesu Kristo.

Tunawezaje kuja Kwake? Aprili iliyopita Rais Russell M. Nelson na Mzee M. Russell Ballard walituhimiza kusoma “Kristo aliye Hai”7 kama sehemu ya kujifunza kuhusu Mwokozi. Wengi wamekubali mwito na wamebarikiwa. Si muda mrefu uliopita, rafiki mpendwa alimpa kila moja wa watoto wake ambao ni watu wazima nakala za hati hio zikiwa na picha za injili kuelezea kila kirai. Aliwahimiza watoto wake kuwasaidia wajukuu wake kuielewa na kuikariri. Muda fulani baadaye, rafiki yangu alishiriki video ya mjukuu wake wa kike wa miaka sita, Laynie akikariri kwa shauku na makini. Niligundua kuwa kama mtoto wa miaka sita angeweza kufanya hivyo, basi nami pia naweza!

Laynie, ambaye alikariri “Kristo Aliye Hai”

Nilipojifundisha maisha na mafundisho ya Yesu Kristo kwa fokasi zaidi na kukariri“Kristo Aliye Hai” katika kumbukumbu, shukrani zangu na upendo kwa Mwokozi umeongezeka. Kila sentensi ya hati hii ya kuvuvia imebeba mahubiri na imeongeza uwezo wangu wa kuelewa kazi Yake tukufu na misheni Yake duniani. Kile ambacho nimejifunza na kuhisi katika muda huu wa kujifundisha na kutafakari kimethibitisha kuwa Yesu kweli “ni mwanga, maisha na tumaini la dunia.”8 Maandiko ya kale na maneno ya manabii wa siku za mwisho yaliyoandikwa au kusemwa katika kumsifu Yeye hushuhudia kuwa “Njia Yake ni njia ambayo inaelekeza kwenye furaha katika maisha haya na maisha ya milele katika ulimwengu ujao.”9

Kuwa na imani katika Yesu Kristo

Wakati unapojifundisha maisha na mafundisho ya Kristo katika njia nyingi, imani yako Kwake itaongezeka. Utakuja kumjua kuwa Anakupenda kibinafsi na anakuelewa kikamilifu. Katika miaka 33 ya maisha Yake duniani, alipata kusumbuliwa na kukataliwa; kushutumiwa, njaa ya mwili, kiu, na uchovu;10 upweke; uonevu kimaneno na kimwili na mwishowe kifo cha kuteseka katika mikono ya watu wenye dhambi.11 Katika bustani ya Gethsemane na kwenye msalaba wa Kalvari alihisi maumivu yetu, masumbuko, majaribu, magonjwa na mapungufu.12

Haijalishi ni kiasi gani tumesumbuka, yeye ni kiini cha uponyaji. Wale ambao wamepitia aina yoyote ya uonevu, hasara ya kuhuzunisha, magonjwa ya muda mrefu au masumbuko ya kutoweza, shutuma zisizo kweli, mateso makali au uharibifu kiroho kutokana na dhambi au kutoelewana wanaweza kufanywa wazima kupitia Mkombozi wa Ulimwengu. Hata hivyo, hataingia bila mwaliko. Lazima tuje Kwake na kumwacha afanye miujiza Yake.

Siku moja nzuri ya majira ya kuchipua, niliacha mlango wazi kufurahia hewa safi. Ndege mdogo alipaa kupitia mlango wazi na baadaye kugundua kuwa alikuwa pale ambapo hakutaka kuwa. Alipaa kwa hofu chumbani, akipaa mara nyingi kwenye dirisha la kioo kwa kujaribu kutoroka. Nilijaribu taratibu kumwongoza kuelekea mlango wazi, lakini aliogopa na kuendelea kurukaruka. Mwishowe alitua juu ya pazia la dirisha akichanganywa na uchovu. Nilichukua ufagio na taratibu nikafikia mwisho wa pazia ambapo kwa woga ndege alitua. Wakati nikinyanyua sehemu ya kichwa ya ufagio karibu na miguu yake, ndege kwa woga alitua kwenye nywele za ufagio. Taratibu, taratibu sana, nilitembea hadi kwenye mlango uliokuwa wazi, nikibeba ufagio kwa uthabiti kadiri niwezavyo. Punde tu tulipofikia kwenye mlango uliokuwa wazi, ndege kwa urahisi alipaa kuwa huru.

Kama ndege huyo, wakati mwingine tunaogopa kuamini kwa sababu hatuelewi upendo halisi na nia ya Mungu kutusaidia. Lakini wakati tunapojifunza mpango wa Baba wa Mbinguni na kazi ya Yesu Kristo, tunaelewa kuwa lengo Lao pekee ni furaha yetu na maendeleo yetu ya milele.13 Wanafurahia kutusaidia wakati tunaomba, kutafuta na kubisha.14 Wakati tunatumia imani na kwa unyenyekevu kufungua nafsi zetu kwa majibu Yao, tunakuwa huru kutokana na sitafahamu na dhana, na tunaweza kuonyeshwa njia kwenda mbele.

Yesu Kristo pia ni kiini cha amani. Anatualika “kuegemea mkono [Wake] wenye nafasi”15 na kuahidi “amani … Inapitayo uelewa wote,”16 hisi a ambayo huja Roho Wake “akiongea amani katika nafsi zetu”17 licha ya changamoto zinazotuzunguka. Iwe ni mapambano ya kibinafsi, shida za kifamilia, au migogoro ya jamii, amani itakuja tunapoamini kwamba Mwana wa Mungu wa Pekee ana uwezo wa kutuliza nafsi zetu zenye maumivu.

Snježana Podvinski, ni muumini katika Koreshia

Snježana Podvinski, mmoja kati ya idadi ndogo ya Watakatifu huko Karlovac, Koreshia, alimuegemea Mwokozi wakati mume wake na wazazi wake wote walifariki chini ya kipindi cha miezi sita mwaka jana. Akiwa na huzuni, lakini akiwa na ushuhuda kuwa familia ni za milele, alitumia akiba yake yote kusafiri kwenda hekaluni, ambapo aliunganishwa kwa mume wake na wazazi wake. Alishiriki kuwa siku hizo katika hekalu zilikuwa za kuvutia sana maishani mwake. Kwa sababu ya ushuhuda wake imara wa Yesu Kristo na Upatanisho Wake, amehisi amani na uzoefu wa uponyaji ambao pia umekuwa nguvu kwa wale walio karibu naye.

Imani katika Yesu Kristo huleta zawadi zaidi kuliko uponyaji na amani. Kama Rais Henry B. Eyring alivyoshiriki: “Nimekuwa na shukrani kwa njia nyingi ambazo Bwana amenitembelea pamoja na Mfariji wakati nilihitaji amani. Hata hivyo Baba yetu wa Mbinguni hajali tu juu ya faraja yetu lakini hata zaidi juu ya maendeleo yetu kwenda juu.”18

Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, ambao hujumuisha zawadi ya ukombozi na ufufuko, tunaweza kutubu, kubadilika na kuendelea milele. Kwa sababu ya nguvu anayotupatia tunapokuwa watiifu, tunao uwezo wa kuwa zaidi, kuliko tunavyoweza kufanya peke yetu. Tunaweza tusielewe kikamilifu ni kwa nanma gani, lakini kila mmoja wetu ambaye amehisi imani katika Kristo ikiongezeka pia amepokea uelewa mkubwa kuhusu lengo letu na utambulisho wetu mtakatifu, na kutupelekea kufanya chaguzi ambazo ni thabiti kutokana na uelewa huo.

Licha ya dunia ambayo itajaribu kutuangusha kwenye kiwango ambacho ni “kama wanyama tu,”19 kujua kuwa Mungu ni Baba yetu hutuhakikishia kuwa tuna uwezo mtakatifu na ahadi ya kifalme. Licha ya dunia ambayo hutuambia kuwa maisha haya ni ya mwisho, kujua kuwa Mwana wa Pekee wa Mungu amewezesha ukombozi na ufufuko kwa ajili yetu hutupatia tumaini kwa maendeleo ya milele.

Muige Yesu Kristo

Tunapojifunza zaidi juu ya Yesu Kristo, tunatengeneza imani kubwa Kwake na kiuhalisia tunataka kufuata mfano Wake. Kushika amri Zake huwa hamu yetu kubwa. Mioyo yetu hutamani kuwasaidia wengine katika mahangaiko yao, kama alivyofanya, na tunataka na wao wapitie uzoefu wa amani na furaha kama tulivyopata.

Ni kwa nini kujaribu kufanya kama alivyofanya kwa nguvu sana? Kwa sababu tunapoweka imani yetu katika matendo, Roho Mtakatifu hushuhudia ukweli wa milele.20 Yesu huwaelekeza wanafunzi Wake kushika amri Zake kwa sababu Anajua kuwa tunapofuata mfano Wake, tutaanza kupata uzoefu wa shangwe, na tunapoendelea katika njia Yake, tutakuja kufikia utimilifu wa shangwe. Alifafanua, “Vitu hivi nimewaambieni, ili kwamba shangwe yangu ibaki kwenu, na kwamba shangwe yenu iwe timilifu.”21

Je, shuhuda zetu zimejengwa kwenye msingi wa mwamba wa Yesu Kristo na injili Yake? Wakati ambapo tufani za maisha zitatusukuma, je, kwa wasiwasi tunatafuta kitabu cha jinsi ya kufanya au ujumbe kwenye intaneti kwa ajili ya msaada? Kuchukua muda kujenga na kuimarisha ujuzi wetu na ushuhuda wa Yesu Kristo utazaa faida kubwa katika nyakati za majaribu na dhiki. Usomaji wa maandiko matakatifu kila siku na kutafakari maneno ya manabii wanaoishi; kujumuika katika sala zenye maana za binafsi; kupokea sakramenti kwa uzingatifu kila wiki; kutoa huduma kama vile Mwokozi angetoa—kila mojawapo ya shughuli hizi rahisi huwa ni tofali la kujenga maisha ya shangwe.

Nini hukupatia shangwe? Kuwaona wapendwa wako mwishoni mwa siku? Kuridhika na kazi nzuri iliyofanywa? Nuru katika macho ya mtu fulani wakati ukiwasaidia shida zao? Maneno ya nyimbo takatifu ambayo hufika ndani kwa kina kwenye moyo wako? Kushikwa mkono na rafiki yako wa karibu? Chukua muda wewe binafsi utafakari juu ya baraka zako, halafu tafuta njia ya kuzishiriki. Unavyoendelea kuwafikia na kuwatumikia wengine na kuinua kaka zako na dada zako walio katika ujirani wako au katika dunia nzima iliyo na ghasia nyingi, utahisi amani kubwa na uponyaji na hata maendeleo.

Njooni Kwake. Ninashuhudia kuwa unapofanya kiini cha maisha yako kuwa Yesu Kristo, utapata shangwe katika hali zako, zozote zile. Kweli, “Yeye Pekee,”22 ndiye jibu. Tafuta muda na uchukue muda kuja kumjua Yesu Kristo kupitia kujifunza kwa bidii, kukuza imani kubwa Kwake, na kujitahidi kuwa milele kama Yeye. Tunapofanya hivyo, sisi pia tutahisi kusema, pamoja na Laynie kadogoo, “Mungu ashukuriwe kwa zawadi yake kuu ya mwanawe mtakatifu.”23 Katika jina lililobarikiwa na takaktifu la Yesu Kristo, amina.