2010–2019
Wabeba Nuru ya Mbinguni
Oktoba 2017


2:3

Wabeba Nuru ya Mbinguni

Kama mbeba ukuhani wa Mungu na kama mfuasi wa Yesu Kristo, wewe ni mbeba nuru

Mtu mzee alikuwa amesimama kwenye mstari katika ofisi ya posta kununua stempu kwenye meza ya huduma. Msichana mdogo aligundua kwamba alitembea kwa taabu na akajitolea kumwonyesha jinsi ya kununua stempu katika mashine ili kuokoa muda. Muungwana mzee akasema, “Asante, lakini napendelea kusubiri. Mashine haitaniuliza kuhusu yabisi yangu.”

Wakati mwingine inasaidia kuongea na mtu ambaye anajali matatizo yetu.

Maumivu, huzuni, na ugonjwa ni uzoefu tunaoshiriki wote—nyakati za ajali, huzuni, na taabu zaweza kuongeza ukubwa wa kumbukumbu ndani ya nafsi zetu.

Linapokuja suala la afya yetu kimwili, tunakubali kuzeeka na ugonjwa kama sehemu ya safariyamaisha yetu ya muda. Tunatafuta ushauri wa wataalamu wanaoelewa mwili wetu. Tunapoteseka na hisia za kuhuzunisha au ugonjwa wa akili, tunatafuta msaada wa wataalamu wanaotibu aina hizi za maradhi.

Kama vile tunavyopitia majaribu ya kimwili na kihisia katika maisha haya ya kufa, tunapitia pia changamoto za kiroho. Wengi wetu tumepitia nyakati katika maisha yetu ambapo ushuhuda wetu uliwaka kwa uangavu. Pia tunaweza kuwa tumepitia nyakati ambapo Baba yetu wa Mbinguni alionekana kuwa mbali. Kuna nyakati ambapo tunathamini vitu vya Kiroho kwa mioyo yetu yote. Pia kunaweza kuwa na nyakati ambapo vinaonekana vyenye thamani ndogo au visivyo na umuhimu.

Leo ningetamani kuzungumzia juu ya uzima kiroho—jinsi tunavyoweza kupata uponyaji kutoka kwenye kukwama na kutembea njia ya kusisimua, afya ya kiroho.

Kuugua kiroho.

Wakati mwingine ugonjwa wa kiroho huja kama matokeo ya dhambi au majeraha ya hisia. Wakati mwingine kuvunjika kiroho huja taratibu kwamba hatuwezi kuona kinachotokea. Kama tabaka za mwamba mashapo, maumivu ya kiroho na huzuni yanaweza kujilimbikiza, yakitia uzito nafsi zetu mpaka inakua ni nzito sana kustahimili. Kwa mfano, hii inaweza kutendeka wakati majukumu yetu kazini, nyumbani na Kanisani yanakuwa mengi mno hadi tunakosakukumbuka shangwe ya injili. Tunaweza kujihisi kwamba hatuna chochote cha kuchangia walakutii amri za Mungu ni jambo gumu

Lakini kwa sababu tu majaribu ya kiroho ni halisi haimaanishi kwamba hayana tiba.

Tunaweza kupona kiroho.

Hata majeraha ya ndani ya kiroho—ndiyo, hata yale yanayoonekana kutotibika—yanaweza kuponywa.

Marafiki zangu wapendwa, nguvu ya uponyaji ya Yesu Kristo haikosekani katika siku yetu.

Mguso wa Mwokozi wa uponyaji unaweza kubadilisha maisha katika siku yetu kama ilivyokuwa katika siku Zake. Kama tu tutakuwa na imani, anaweza kutushika mikono, kuzijaza nafsi zetu na nuru ya mbinguni na uponyaji, na kuzungumza nasi maneno ya baraka, “Simama, jitwike godoro lako, uende.”1

Giza na Nuru

Chochote kinachosababisha maradhi yetu ya kiroho, vyote vina mfanano wa kitu kimoja: ukosefu wa nuru takatifu.

Giza hupunguza uwezo wetu wa kuona vizuri. Hufifisha uoni wetu kwa kile kilichokuwa mwanzo cha kueleweka na wazi. Tunapokuwa gizani, ni rahisi kufanya chaguzi mbaya, kwa sababu hatuwezi kuona hatari katika njia zetu. Tunapokuwa gizani, ni rahisi kupoteza tumaini, kwa sababu hatuwezi kuona amani na furaha inayotusubiri kama tutaendelea kusonga mbele.

Nuru kwa upande mwingine, huturuhusu kuona vitu jinsi vilivyo kiuhalisia. Huturuhusu kutambua kati ya ukweli na uongo, kati ya muhimu na upuuzi. Tunapokua nuruni, tunaweza kufanya chaguzi za haki zilizo katika kanuni za kweli. Tunapokuwa nuruni, tunakuwa na “mng’aro mkamilifu wa tumaini,”2 kwa sababu tunaona majaribu yetu ya maisha ya muda kwa mtazamo wa milele.

Sisi tutapata uponyaji wa kiroho tunapopiga hatua kutoka kivuli cha ulimwengu kwenda kwenye Nuru ya Kristo ya milele.

Tunapojua zaidi na kutumia dhana ya kimafundisho ya nuru, ndivyo zaidi tunajilinda dhidi ya ugonjwa wa kiroho unaotutesa au kutusumbua kila upande na mkono, na vyema tunavyoweza kutumikia kama wenye nguvu, ujasiri, kujali, na wabeba ukuhani mtakatifu wanyenyekevu—watumishi wa kweli na wafuasi wa mpendwa wetu na Mfalme wa milele.

Nuru ya Ulimwengu

Yesu Kristo alisema, “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu: yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”3

Hii inamaanisha nini?

Rahisi hivi: Yule amfuataye Yesu Kristo kwa unyenyekevu ataona na kushiriki katika nuru Yake. Na nuru ile itakua mpaka hatimaye kufukuza hata giza totoro.

Inamaanisha kwamba kuna nguvu, ushawishi wa nguvu, ambao huanzia kwa Mwokozi. Huendelea “mbele kutoka uwepo wa Mungu kujaza nafasi kubwa sana.”4 Kwa sababu nguvu hii huelimisha, huinua, na kuangaza maisha yetu, maandiko mara nyingi huiita nuru, lakini pia hutajwa kama roho na kweli.

Katika Mafundisho na Maagano tunasoma, “Kwa kuwa neno la Bwana ni ukweli, na lolote lililo kweli ni nuru, na lolote lililo nuru ni Roho, hata Roho wa Yesu Kristo.”5

Umaizi huu wa kina—kwamba nuru ni roho ambayo ni kweli na kwamba nuru hii huangaza juu ya kila nafsi inayokuja ulimwenguni—ni muhimu kama inavyotumainiwa. Nuru ya Kristo huelimisha na kujaza nafsi za wote wanaosikiliza sauti ya Roho.6

Nuru ya Kristo huujaza ulimwengu.

Huijaza dunia.

Na inaweza kujaza kila moyo.

“Mungu hana upendeleo.”7 Nuru Yake ipo kwa wote—wakuu na wadogo, matajiri na masikini, waliobahatika na wenye upungufu.

Kama ukifungua akili na moyo wako kupokea Nuru ya Kristo na kwa unyenyekevu kumfuata Mwokozi, utapokea nuru zaidi. Mstari juu ya mstari, hapa kidogo na pale kidogo, mtakusanya nuru zaidi na kweli katika nafsi zenu, mpaka giza litakapokuwa limeondolewa katika maisha yenu.8

Mungu atafungua macho yenu.

Mungu atawapa moyo mpya.

Upendo wa Mungu, nuru, na kweli vitafanya vitu vilivyodumaa kupata uhai, na utazaliwa upya katika upya wa maisha ndani ya Yesu Kristo.9

Bwana ameahidi, “Na kama macho yenu yatakuwa katika utukufu wangu pekee, miili yenu yote itajazwa na nuru, na hakutakuwa na giza ndani yenu; na mwili ule uliojazwa na nuru hufahamu mambo yote.”10

Hii ni tiba ya mwisho ya ugonjwa wa kiroho. Giza hutoweka kwenye uwepo wa nuru.

Sitiari ya Giza la Kiroho.

Hata hivyo, Mungu hatatulazimisha kukumbatia nuru Yake.

Kama tukiridhika na giza, hamna uwezakano wa mioyo yetu kubadilika.

Kwa mabadiliko kutokea, tunahitaji kuiruhusu nuru iingie.

Wakati wa safari zangu kama rubani wa ndege kote katika sayari yetu dunia, nilikuwa daima navutiwa na uzuri na ukamilifu wa uumbaji wa Mungu. Niluona kuwa unapendeza mno hasa uhusiano kati ya dunia na jua Nalifikiria kama somo kuu la vitu la jinsi giza na nuru huwepo.

Kama sote tunavyojua, kila masaa 24 usiku hugeuka mchana na mchana hugeuka usiku.

Kwa hivyo, basi, usiku ni nini?

Usiku sio kitu zaidi ya kivuli.

Hata katika usiku wa giza, jua haliachi kunururisha nuru yake. Linaendelea kuwakakwa uangavu kama kawaida. Lakini nusu ya dunia ipo gizani.

Kutokuwepo kwa nuru husababisha giza.

Wakati giza la usiku linapoingia, hatuna hofu na wasiwasi kwamba jualimekoma. Hatudai kwamba jua halipo au limekufa. Tunaelewa kwamba tupo kivulini, kwamba dunia itaendelea kuzunguka, na kwamba hatimaye miale ya jua itatufikia tena.

Giza siyo ashirio kwamba hakuna nuru. Mara nyingi, humaanisha tu kwamba hatuko sehemu sahihi kupokea nuru. Wakati wa kupatwa jua kwa hivi majuz, wengi walifanya juhudi za kupata ukanda mwembamba uliosababishwa na mwezi katikati ya siku ya jua angavu.

Katika njia inayofanana, nuru ya kiroho daima huangaza kwa viumbe vyote wa Mungu. Shetani atafanya kila juhudi kutuweka kwenye kivuli tulichotengeneza wenyewe. Atatulazimisha kutengeneza kupatwa jua kwetu, atatusukumakwenye pango lake la giza.

Giza la kiroho huweza kuleta pazia la kusahau hata kwa wale ambao wamewahi kutembea nuruni na kufurahi katika Bwana. Hata hivyo, katika nyakati za giza totoro, Mungu husikia maombi yetu ya unyenyekevu, tunapoomba, “Bwana, naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.”11

Katika siku za Alma kulikuwa na wengi waliohangaika kukubali mambo ya kiroho, na “sasa kwa sababu ya kutokuamini kwao,” nuru na kweli ya Mungu haikuingia nafsini mwao, “na mioyo yao ilikuwa imeshupazwa.”12

Sisi ni wabeba nuru

Akina kaka, ni juu yetu kuwa katika mahali sahihi kuona nuru takatifu na ukweli wa injili ya Yesu Kristo. Hata wakati usiku unapoingia na dunia imejaa giza, tunaweza kuchagua kutembea katika nuru ya Kristo, kutii amri zake, na kwa ujasiri kushuhudia juu ya uhalisia na ukuu Wake.

Kama mbeba ukuhani wa Mungu na kama mfuasi wa Yesu Kristo, wewe ni mbeba nuru. Endelea kufanya vitu ambavyo vitakuza nuru Yake takatifu. “Angaza nuru yako”13 na “na iangaze mbele ya watu”—sio kwamba ili wawaone na kuwatamani, lakini “wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”14

Wapendwa kaka zangu, ninyi ni vyombo mikononi mwa Bwana kwa lengo la kuleta nuru na uponyaji kwenye nafsi za watoto wa Baba wa Mbinguni. Labda unahisi kutostahili kuponya wale ambao ni wagonjwa kiroho—hakika si zaidi ya mwajiriwa wa posta ambaye amehitimu kusaidia mwenye yabisi. Labda unakumbana na changamoto zako za kiroho. Hata hivyo, Bwanaamekuita. Amekupa mamlaka na wajibu kuwafikia wale wenye mahitaji. Amekutunuku na nguvu ya ukuhani Wake mtakatifu kuleta nuru gizani na kuinua na kubariki watoto wa Mungu. Mungu amerejesha Kanisa Lake na injili Yake ya thamani, “inayoponya nafsi iliyojeruhiwa.”15 Ameandaa njia ya uzima kiroho, kupata uponyaji wa kudumaa na kwenda kwenye afya ya kusisimua ya kiroho.

Kila mara unapoelekeza moyo wako kwa Mungu katika sala ya unyenyekevu, unapata uzoefu wa nuru Yake. Kila mara unapotafuta neno Lake na mapenzi Yake katika maandiko, nuru huzidi kung’ara. Kila mara unapomwona mwenye hitaji na kutoa msaada wako kumfikia kwa upendo, nuru huongezeka na kuvimba. Kila mara unapokataa jaribu na kuchagua kuwa safi, kila mara unapotafuta au kutoa msamaha, kila mara unaposhuhudia juu ya kweli kwa ujasiri, nuru hufukuza giza na kuwavuta wengine ambao pia wanatafuta nuru na ukweli.

Fikiria uzoefu wako binafsi, nyakati za huduma kwa Mungu na binadamu wenzako ambapo nuru takatifu imeangaza katika maisha yako ndani ya hekalu takatifu, katika meza ya sakramenti, katika wakati mtulivu wa kutafakari, katika mikutano ya familia, au wakati wa tendo la huduma ya ukuhani. Shiriki nyakati hizo na familia, marafiki, na hasa na vijana wetu, ambao wanaitafuta nuru. Wanahitaji kusikia kutoka kwako kwamba pamoja na nuru hii huja tumaini na uponyaji, hata katika ulimwengu uliojaa giza.

Nuru ya Kristo huleta tumaini, furaha, na uponyaji wa jeraha lolote la kiroho au maradhi.16 Wale wanaopitia uzoefu huu wa utakaso wanakuwa vyombo katika mikono ya Nuru ya Dunia kutoa nuru kwa wengine.17 Watahisi vile Mfalme Lamoni alivyohisi: “Nuru hii ilikuwa imejaza nafsi yake na shangwe, wingu la giza likiwa limeondolewa, na… nuru ya uzima usio na mwisho ilikuwa imewashwa katika nafsi yake.”18

Wapendwa ndugu zangu, marafiki zangu wapendwa, ni jukumu letu kumtafuta Bwana mpaka nuru Yake ya uzima wa milele iwake ndani yetu na ushuhuda wetu uwe imara na jasiri hata katikati ya giza.

Ni maombi na baraka yangu kwamba mtaendelea katika kutimiza kudra yenu kama wenye ukuhani wa Mwenyezi Mungu na daima kuwa wabeba nuru Yake ya mbinguni wenye furaha. Katika jina Yesu Kristo, Amina.