Mgeukie Bwana.
Hatuwezi kudhibiti yote yanayotutokea, lakini tuna udhibiti kamili juu ya jinsi gani tunajibu mabadiliko katika maisha yetu.
Katika msimu wa vuli mwaka 1998, Mimi na Carol tuliweza kuunganisha safari ya kibiashara pamoja na likizo ya familia na kuwaleta Hawaii kwa siku chache watoto wetu wanne, pamoja na mama mkwe wangu aliyekuwa amempoteza mumewe karibuni.
Usiku kabla ya ndege yetu kwenda Hawaii, mtoto wetu wa kiume mwenye umri wa miezi minne, Jonathon, aligunduliwa na maambukizi kwenye masikio yote mawili, na tuliambiwa kwamba asingeliweza safiri kwa angalau siku tatu hadi nne.Uamuzi ulifanywa kwa Carol kubaki nyumbani na Jonathon, wakati mimi ningelifanya safari pamoja na wanafamilia wengine.
Kiashirio cha kwanza kwamba hii haikuwa safari niliyotarajia, kilitokea mara tu baada ya kuwasili kwetu. Tukitembea chini ya mbalamwezi, njia ya mitende, pamoja na muonekano wa bahari mbele yetu, niligeuka kutoa maoni juu ya uzuri wa kisiwa hiki, na katika wakati ule mzuri, badala ya kumuona Carol, Nilijikuta nikiangalia katika macho ya mama mkwe wangu—ambaye, nawezaongeza, nampenda sana. Haikuwa kile nilichotarajia. Hata Carol hakutegemea kutumia likizo yake nyumbani akiwa pekee na mtoto wetu mgonjwa.
Kutakuwa na nyakati katika maisha yetu ambapo tutajikuta binafsi katika njia tusizotarajia, tukikabiliwa na mazingira mabaya zaidi kuliko likizo iliyovurugwa. Jinsi gani tunaitikia wakati matukio, mara nyingi yaliyo nje ya udhibiti wetu, yakibadilisha maisha tuliyokwisha panga au kutarajia?
Juni 6, 1994, Hyrum Shumway, kijana luteni daraja ya pili katika Jeshi la Marekani, alienda ufukoni katika Pwani ya Omaha kama sehemu ya siku ya uvamizi. Alifanikiwa kutua salama, lakini mnamo Julai 27, kama sehemu ya kundi la Washirika lililotangulia, alijeruiwa vibaya mno na mlipuko wa bomu la ardhini. Kwa papo hapo, maisha yake na kazi yake ya baadaye ya udaktari ilikuwa imeathiriwa pakubwa sana. Kufuatia upasuaji mwingi, ambao ulimsaidia kupona kutokana na majeraha yake makubwa, Ndugu Shumway hakuweza kuona tena. Je, angeliitikia vipi?
Kufuatia miaka mitatu katika hospitali marekebisho, alirudi nyumbani Lovell, Wyoming. Alijua kuwa ndoto yake ya kuwa daktari wa kimatibabu isingeliwezekana tena, lakini aliamua kuendelea, kuoa, na kukidhi familia.
Hatimaye akapata kazi Baltimore, Maryland, kama mshauri wa marekebisho na mtaalam wa ajira kwa vipofu. Katika mchakato wa marekebisho yake mwenyewe, alijifunza kwamba vipofu wana uwezo mkubwa zaidi kuliko alivyodhania, na kwa miaka minane katika wadhifa wake huu, aliwawezesha vipofu wengi kuajiriwa kuliko mshauri mwingine yeyote katika taifa.
Na sasa jasiri katika uwezo wake kusaidia familia, Hyrum alipendekeza kwa kipenzi chake kwa kumwambia, “Ikiwa utasoma barua, kupanga soksi, na kuendesha gari, nitafanya mengine.” Si muda mrefu walifunga ndoa katika Hekalu la Salt Lake na hatimaye kubarikiwa na watoto nane.
Mwaka wa 1954, akina Shumway walirudi Wyoming, ambapo Kaka Shumway alifanya kazi kwa miaka 32 kama Mkurugenzi wa Elimu ya Viziwi na Vipofu wa Jimbo. Katika wakati huo, alitumikia miaka saba kama askofu wa kata ya kwanza ya Cheyenne na, baadaye, miaka 17 kama Baba mkuu wa kigingi. Kufuatia kustaafu kwake, Kaka na Dada Shumway pia walihudumu kama wanandoa wakubwa waandamizi katika Misheni ya London England South.
Hyrum Shumway alifariki mnamo Machi 2011, akiacha nyuma urithi wa imani na tumaini kwa Bwana, hata katika mazingira magumu, kwa kizazi chake kikubwa cha watoto, wajukuu na vitukuu.1
Maisha ya Hyrum Shumway yangeliweza kubadilishwa na vita, lakini hakuwahi tia shaka asili yake ya kiungu na uwezo wa milele. Kama yeye, sisi ni wana na mabinti wa kiroho wa Mungu, na “tulikubali mpango Wake ambao [sisi] tungeweza kupokea mwili na kupata uzoefu wa dunia ili kukua kwa ukamilifu na hatimaye kupata maisha [yetu] matakatifu kama warithi wa maisha ya milele.”2 Hakuna kiasi cha mabadiliko, majaribu, au pingamizi kinaweza kubadilisha hiyo njia ya milele—ni chaguzi zetu tu, tunapotumia haki yetu ya kuchagua.
Mabadiliko, na changamoto zinazotokea, ambazo tunakabiliana nazo duniani huja kwa namna za maumbo na saizi na umwaathiri kila mmoja wetu katika njia pekee. Kama wewe, nimeshuhudia marafiki na familia wakikabiliana na changamoto zinazosababishwa na:
-
Kifo cha mpendwa wetu.
-
Talaka chungu.
-
Kutopata nafasi ya kuoa au kuolewa.
-
Ugonjwa au jeraha baya.
-
Na hata majanga asili, kama tulivyoshuhudia hivi karibuni ulimwenguni.
Na orodha inaendelea. Ingawa kila “badiliko” linaweza kuwa la kipekee katika hali binafsi, kuna kini cha kawaida katika jaribio au changamoto itakayotokea—matumaini na amani vinakuwepo daima kupitia dhabihu ya upatanisho ya Yesu Kristo. Upatanisho wa Yesu Kristo hutoa hatua za mwisho za kurekebisha na uponyaji kwa kila mwili uliojeruhiwa, roho iliyoharibiwa, na moyo uliovunjika.
Anajua, katika namna ambayo hakuna mwingine anaweza kuelewa, kile tunachohitaji, mmoja mmoja, ili kusonga mbele katikati ya mabadiliko. Si kama vile marafiki na wapendwa, Mwokozi sio tu anatuhurumia, bali Anaweza hisi kwa ukamilifu, kwa sababu Alishawahi kuwa pale tulipo. Zaidi ya kulipa gharama na mateso ya dhambi zetu, Yesu Kristo pia alitembea kila njia, alikabiliana na kila changamoto, alikutana na kila maumivu—kimwili, kimhemko au kiroho—ambayo tutakumbana nayo duniani.
Rais Boyd K. Packer alifundisha: “Rehema na neema za Yesu Kristo hazina kikomo kwa wale wanaotenda dhambi … , lakini zinajumuisha ahadi ya amani ya milele kwa wote ambao watamkubali na kumfuata Yeye. … Rehema Yake ni uponyaji mkuu, hata kwa yule majeruhi asiye na hatia.”3
Katika uzoefu wa hii dunia, hatuwezi kudhibiti vyote vinavyotutokea, lakini tuna udhibiti kamili juu ya jinsi gani tunajibu changamoto katika maisha yetu. Hii haimaanishi kwamba changamoto na majaribio tunayokumbana nayo hayana matokeo na ni rahisi kuyamudu au kukabiliana nayo. Haimaanishi kwamba tutakuwa huru kutokana na maumivu au huzuni mkubwa. Lakini kuna maana kwamba kuna sababu ya tumaini na kwamba kutokana na upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza songa mbele na kupata siku bora—hata siku zilizojaa shangwe, mwanga, na furaha.
Katika Mosia tunasoma simulizi ya Alma, aliyekuwa kuhani mkuu hapo awali wa Mfalme Nuhu, na watu wake, ambaye, “akiwa ameonywa na Bwana … [,] wakaondoka na kuelekea nyikani mbele ya majeshi ya mfalme Nuhu.” Baada ya siku nane, “wakaja katika … nchi ya kupendeza na nzuri” ambapo “wakapiga hema zao, na wakaanza kulima ardhi, na kuanza kujenga majengo.”4
Hali yao ilionekana yenye kutia moyo. Walikubali injili ya Yesu Kristo. Walibatizwa kama agano kwamba watamtumikia Bwana na kutii amri Zake. Na “waliongezeka na kuwa na kufanikiwa sana katika nchi.”5
Hata hivyo, hali zao zingelibadilika mara moja. “Jeshi la Walaamani lilikuwa katika mipaka ya nchi.”6 Alma na watu wake waliwekwa mara moja utumwani, na “ikawa kwamba mateso yao yalikuwa makuu hata kwamba wakaanza kumlilia Mungu.” Kwa nyongeza, waliamriwa hata na watekaji wao waache kusali, la sivyo, “yeyote atakayepatikana akimwita Mungu auawe.”7 Alma na watu wake hawakufanya chochote kustahili hali yao mpya. Je, wangejibu vipi?
Badala ya kumlaumu Mungu, walimgeukia Yeye na “walifungua mioyo yao Kwake.” Kama jibu kwa imani yao na sala za kimya, Bwana alijibu: “Mshereheke. … Nita … wapunguzia mizigo ambayo imewekwa mabegani mwenu, hata kwamba hamtaisikia kamwe migongoni mwenu.” Baada ya hapo, “Bwana aliwapatia nguvu kwamba wabebe mizigo yao kwa urahisi, na walinyenyekea kwa furaha na subira kwa mapenzi ya Bwana.”8 Ingawa bado hawakutolewa utumwani, kwa kugeuka kwa Bwana, na si kutoka kwa Bwana, walibarikiwa kulingana na mahitaji yao na kulingana na hekima ya Bwana.
Mzee Dallin H. Oaks amefundisha kwamba “Baraka za uponyaji huja kwa njia nyingi, kila moja inafaa kwa mahitaji ya mtu binafsi, kama ijulikanavyo Kwake atupendaye vyema. Wakati mwingine ‘uponyaji’ huponya magonjwa yetu au kuinua mizigo yetu. Lakini wakati mwingine ‘tunaponywa’ kwa kupatiwa nguvu au uelewa au uvumilivu kubeba mizigo iliyowekwa juu yetu.”9
Hatimaye, “imani yao na subira yao ilikuwa kuu sana,” kwamba Alma na watu wake waliokolewa na Bwana, jinsi itakavyokuwa kwetu “na walitoa shukrani” “ kwani walikuwa utumwani, na hakuna yeyote ambaye angewakomboa ila tu Bwana Mungu wao.”10
Kinyume chake cha kusikitisha ni kwamba, mara nyingi, wale walio na wahitaji sana hugeuka mbali na chanzo chao kikamilifu cha msaada—Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Simulizi ya maandiko inayojulikana ya nyoka wa shaba hutufundisha kwamba tuna uchaguzi tunapokabiliwa na changamoto. Baada ya watoto wengi wa Israeli kuumwa na “nyoka wakali warukao,”11 “mfano uliinuliwa … kwamba yeyote atakayeuangalia … aweze kuishi. [Lakini ilikuwa ni chaguo.] Na wengi waliangalia na wakaishi.
“… Lakini kulikuwa na wengi ambao walikuwa wamefanywa wagumu kwamba hawangeangalia, kwa hivyo waliangamia.”12
Kama Waisraeli wa kale, tunaalikwa na kuhimizwa pia kutazama kwa Mwokozi na kuishi—kwa kuwa nira Yake ni laini na mzigo Wake ni mwepesi, hata kama wetu ikiwa ni mzito.
Alma mdogo alifundisha kweli hii takatifu aliposema, “Najua kwamba wote watakaoweka imani yao katika Mungu watasaidiwa kwa majaribio yao, na taabu zao, na mateso yao, na watainuliwa juu katika siku ya mwisho.”13
Katika siku hizi za mwisho, Bwana ametupatia rasilimali nyingi, “nyoka wetu wa shaba,” ambao wote wamepangwa kutusaidia kumtazama Kristo na kuweka tumaini letu Kwake. Kukabiliana na changamoto za maisha sio juu ya kupuuza ukweli lakini zaidi ni wapi tunachagua kuzingatia na msingi ambao tunachagua kujenga.
Rasilimali hizi ni pamoja na, lakini sio pungufu:
-
Kusoma kila mara maandiko na mafundisho ya manabii wanaoishi.
-
Sala za dhati na kufunga kila mara.
-
Kupokea sakramenti kwa ustahili.
-
Kuhudhuria hekalu kila mara.
-
Baraka za Ukuhani.
-
Ushauri wa hekima kupitia wataalamu waliofunzwa.
-
Na hata dawa,wakati maagizo yameandikwa vizuri na kutumiwa kama ilivyoruhusiwa.
Badiliko lolote katika hali za maisha linaloweza kuja njiani kwetu, na njia yoyote isiyotarajiwa tutakayoweza pita, jinsi gani tunaitikia ni chaguo. Kumgeukia Mwokozi na kushikilia mkono Wake ulionyooshwa daima ni chaguo bora.
Mzee Richard G. Scott alifundisha ukweli huu wa milele: “Kweli, furaha ya kudumu na nguvu zinazoambatana, ujasiri, na uwezo wa kushinda matatizo magumu zaidi hutoka kutoka maisha ambayo kitovu chake ni Yesu Kristo. … Hakuna dhamana ya matokeo ya mara moja, lakini kuna uhakika kabisa kwamba, wakati wa Bwana, suluu zitakuja, amani itaendelea, na uhaba utajazwa.14
Kwa kweli hizi ninashirikisha ushahidi wangu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.