2010–2019
Kupata Uaminifu kwa Bwana na Familia Yako
Oktoba 2017


2:3

Kupata Uaminifu kwa Bwana na Familia Yako

Watu wenye “uadilifu wa moyo” ni watu wenye kuaminika—kwa sababu uaminifu umejengwa kwenye uadilifu.

Ndugu, huenda hakuna sifa kubwa tunayoweza kuipata kutoka kwa Bwana zaidi ya kujua Anatuaminikuwa makuhani wema na waume na kina baba wazuri.

Jambo moja la uhakika: kupata kuaminika na Bwana ni baraka ambayo inakuja kwa juhudi kubwa kwa upande wetu. Uaminifu ni baraka itokanayo na utii wa sheria za Mungu. Kupata uaminifu kwa Bwana kuna kuja kwa matokeo ya kuwa mkweli katika maagano tuliyoweka kwenye maji ya ubatizo na kwenye hekalu takatifu. Tunapotii ahadi zetu kwa Bwana, uaminifu Wake kwetu unakua.

Ninayapenda maandiko yote ya kale na ya sasa ambayo yanatumia maneno “uadilifu wa moyo” wakati wa kuelezea tabia njema za mtu.1 Uadilifu au kukosa uadilifu ni sehemu muhimu ya tabia ya mtu. Watu wenye “uadilifu wa moyo” ni watu wenye kuaminika—kwa sababu uaminifu umejengwa kwenye uadilifu.

Kuwa mtu mwenye uadilifu ina maana kwamba makusudio yako, na pia matendo yako, ni masafi na yenye wema katika hali zote za maisha yako, kote katika hadhara na sirini. Katika kila chaguo tunalofanya, huwa tunastahili uaminifu wa Mungu au tunapunguza uaminifu Wake. Kanuni hii huenda inaonekana wazi katika majukumu yetu ya kiungu kama waume na baba.

Kama waume na kina baba, tumepokea jukumu takatifu kutoka kwa manabii, waonaji na wafunuzi wa sasa kwenye nyaraka ya “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Nyaraka hii hutufunza kwamba, akina baba wanapaswa kusimamia familia zao katika upendo na utakatifu,akina baba wana jukumu la kukimu mahitaji ya maisha na wana jukumu la kulinda familia zao.”2

Ili sisi tupate kuaminika na Mungu, tutahitaji kukamilisha majukumu haya matatu yaliyoteuliwa kwa familia zetu kwa njia ya Bwana. Kama ilivyoelezea zaidi kwenye tangazo la familia, Njia ya Bwana ni kutimiza majukumu haya pamoja na wake zetu “kama wenza sawa.”3 Kwangu mimi, hii ina maana hatusongi mbele kwa maamuzi yoyote mazuri kuhusiana na majukumu haya matatu bila ya kuungana na wake zetu.

Hatua ya kwanza katika jitihada zetu za kupata kuamikinika na Bwana ni kumwamini Yeye. Nabii Nefi alionyesha mfano huu wa kujitolea wakati alipoomba: “Ee Bwana, nimekutegemea wewe, na nitakutegemea wewe milele.” Sitaweka tumaini langu kwenye mkono wa mwanadamu.”4 Nefi alijitolea sana kutenda mapenzi ya Bwana. Katika nyongeza ya kusema angeweza “kuyafanya mambo ambayo Bwana amemwagiza,” Nefi alikuwa amesimama katika ahadi yake ya kukamilisha kazi zake, kama ilivyoonyeshwa katika aya hii: “kama Bwana aishivyo, na tuishivyo sisi, hatutarudi kwa baba yetu nyikani mpaka tukamilishe kile kitu ambacho Bwana ametuamuru sisi.”5

Kwa sababu Nefi kwanza alimwamini Mungu, Mungu akamwamini sana Nefi. Bwana alimbariki kwa mbubujiko wa Roho ambaye alibariki maisha yake, maisha ya familia yake, na maisha ya watu wake. Kwa sababu Nefi alisimamia kwa upendo na wema na alitoa ulinzi kwa familia yake na watu wake, aliandika, “Tuliishi kwa furaha.”6

Ili kuwakilisha taswira ya mwanamke juu ya suala hili, niliwaomba binti zangu wawili walioolewa kunisaidia. Niliwaomba kama wangeweza kunipa sentensi moja au mbili jinsi wanavyoona umuhimu wa uaminifu kama unvyoathiri maisha yao ya ndoa na familia. Haya ni mawazo ya Lara Harris na Christina Hansen.

Kwanza, Lara: “Mojawapo ya vitu muhimu kwangu mimi ni kujua kwamba mume wangu anapoendesha shughuli zake za siku, anafanya chaguzi ambazo zinaonyesha heshima na upendo kwangu. Pale tunapoaminiana kwa njia hii, huleta amani nyumbani mwetu, ambamo tunaweza kufurahi kuilea familia yetu pamoja.”

Sasa mawazo ya Christina: “Kumwamini mtu ni sawa na kuwa na imani na mtu. Bila ya kuamini na amani, inakuwa na woga na shaka. Kwangu mimi, mojawapo ya baraka kubwa ambayo inakuja kwa kumwamini zaidi mume wangu ni amani—amani ya mawazo nikijua kwamba hakika anafanya yale anayosema atayafanya. Kuamini huleta amani, upendo, na mazingira ambayo upendo unaweza kukua.”

Lara na Christina hawakuona kile kilichoandikwa na mwingine. Ilinifurahisha sana kwamba wote wawili binafsi walifikiria baraka za amani nyumbani kuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya kuwa na mume wanayeweza kumwamini. Kama ilivyoonyeshwa na mifano ya binti zangu, kanuni ya uaminifu ina nafasi muhimu sana katika maendeleo ya nyumba ambayo kitovu chake ni Kristo.

Pia niliweza kufurahi kwamba utamaduni uleule wa kumfanya Kristo awe sehemu ya maisha uendelee kukua nyumbani ambapo baba yangu aliuheshimu ukuhani wake na aliaminika na familia yake kwa “uadilifu wa moyo wake.”7 Napenda kushiriki nanyi uzoefu wa ujana wangu ambao unaonyesha matokeo mazuri ya kudumu ambayo baba ambaye anaelewa na kuishi kanuni ya imani iliyojengwa juu ya uadilifu inaweza kuwa na familia yake.

Nilipokuwa kijana mdogo, baba yangu alianzisha kampuni ambayo ni maalumu kwa mashine zinazojiendesha zenyewe. Biashara ya uhandisi, ulitengeneza, na kusimika mashine za kujiendesha zenyewe duniani kote.

Nilipokuwa katika shule ya upili, baba yangu alinitaka nijifunze jinsi ya kufanya kazi. Pia alitaka nijifunze biashara toka kwenye msingi kwenda juu. Kazi yangu ya kwanza ilikuwa pamoja na kutunza kiwanja na kupaka rangi maeneo ya kituo ambayo hayakuonekana kwa umma.

Nilipoingia sekondari, nilipandishwa cheo kufanyakazi kazi kiwandani. Nilianza kujifunza kusoma mipangilio na kutumia mashine nzito za kuunda vyuma. Baada ya mahafali ya sekondari, nilijiunga na chuo kikuu na kisha kwenda misheni. Niliporudi toka misheni, nikarudi kazini. Nilihitaji kupata pesa kwa ajili ya mwaka wa shule uliofuata.

Siku moja baada ya misheni, nilikuwa nafanya kazi kiwandani wakati baba yangu aliponiita ofisini kwake na kuniuliza kama ningependa kwenda naye katika safari ya kibiashara huko Los Angeles.Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa baba yangu kunialika kwenda naye katika safari ya kibiashara.Alikuwa ananiacha niende kwenye umma kuiwakilisha kampuni.

Kabla hatujaondoka kwenda safari, aliniandaa kidogo juu ya mteja huyu mpya ambaye ni muhimu. Kwanza, mteja alikuwa ni wa shirika la kimataifa. Pili, walikuwa wakiboresha mitambo yao ya uzalishaji duniani kote wakiweka mipya yenye tekinologia ya kujiendesha. Tatu, kampuni yetu haijawahi kuwasambazia huduma au tekinolojia ya kiuhandisi. Na hatimaye, afisa wao mhusika wa manunuzi wa ngazi ya juu aliitisha kikao hiki kupitia stakabadhi zetu zabuni za mradi mpya. Mkutano huu uliwakilisha fursa mpya na inayowezekana kwa kampuni yetu.

Baada ya kuwasili Los Angeles, baba yangu na mimi tulikwenda kwenye hoteli ya mtendaji kwa ajili ya mkutano. Mpangilio wa kwanza wa biashara ilikuwa kujadili na kuchambua ufafanuzi wa uhandisi wa mradi. Kipengele cha pili cha majadiliano kinachohusika na maelezo ya uendeshaji, ikiwa ni pamoja na usafiri na tarehe za kufikisha. Ajenda ya mwisho ililenga kwenye bei, masharti, na mapatano. Hapo ndipo mambo yakaanza kuvutia.

Afisa huyo wa shirika alituelezea kwamba pendekezo la bei yetu lilikuwa chini kabisa kulinganisha na wale ambao walikuwa wamewasilisha zabuni kwenye mradi huo. Kisha, kwa mshangao, alitueleza bei ya pili kwa udogo.Kisha akatuambia kama tulikuwa tayari kuliondoa pendekezo letu na kuliwakilisha tena. Alieleza kwamba bei yetu mpya ije kuwa chini kidogo ya ile bei ya juu zaidi. Kisha akaeleza kwamba tutagawana lile ongezeko la dola 1/2—1/2 na yeye. Alirazinisha kuwa kila mtu angeweza kushinda. Kampuni yetu ingeweza kushinda kwa sababu tungepata pesa zaidi kuliko zabuni yetu tuliyoitoa mwanzoni. Kampuni yake ingeshinda kwa sababu wangekuwa wanaendelea kufanya biashara na mzabuni wa chini. Na, hakika, angeshinda kwa kuchukua chake kwa sababu alishughulikia mambo haya.

Kisha akatupa namba ya sanduku la barua ambapo tungemtumia pesaalizoomba. Baada ya haya yote, alimtazama baba yangu na kumwuliza, “Kwa hiyo, tuna mpango?” Kwa mshangao wangu mkubwa, baba yangu aliinuka, akamshika mkono, na akamwambia tutawasiliana naye tena.

Baada ya kuondoka kwenye kikao, tulipanda kwenye gari la kukodi, na baba yangu akanigeukia, “Sawa, unafikiri tufanye nini?”

Nikamjibu kwa kusema sikudhani tunatakiwa kukubali ofa yake.

Kisha baba yangu akaniuliza,“Je, hufikiri tuna wajibu kwa wafanyakazi wetu wote ili kudumisha kazi nzuri.?”

Nikiwa natafakari swali lake na kabla sijajibu, alijibu swali lake mwenyewe. Alisema, “Sikiliza, Rick, mara uchukuapo rushwa au kuacha uadilifu wako, ni vigumu sana kuupata tena. Usijaribu kufanya, hata mara moja.”

Pamoja na kwamba ninashiriki uzoefu huu ina maana kwamba sijasahau kamwe kile ambacho baba yangu alinifundisha katika siku ile ya kwanza ya safari ya kibiashara pamoja naye.Ninashiriki uzoefu huu kuelezea ushawishi wa kudumu tulionao akina baba. Unaweza kuona uaminifu niliokuwanao kwa baba yangu kwa sababu ya uadilifu wa moyo wake. Aliishi na kanuni hizi hizi katika maisha yake binafsi na mama yangu, watoto wake, na wale wote aliokuwa karibu nao.

Ndugu, ni maombi yangu jioni hii kwamba sisi wote tuweze kumwamini Bwana, kama Nefi alivyoonyesha mfano, na kisha kwa njia ya uadilifu wa mioyo yetu tupate kuaminika na Bwana, pia uaminifu kwa wake na watoto wetu. Tunapoelewa na kuifanyia kazi kanuni hii takatifu ya uaminifu iliyojengwa kwenye uadilifu, tutakuwa wakweli kwenye maagano yetu matakatifu. Pia tutafanikiwa katika kusimamia kwenye familia zetu kwa upendo na wema, tukikidhi mahitaji ya maisha, na kuzilinda familia zetu dhidi ya maovu ya duniani. Juu ya kweli hizi mimi nashuhudia kwa unyenyekevu katika jina la Yesu Kristo, amina.