Moyo wa Mjane
Hebu tufanye kile ambacho ni muhimu ili kuwa na moyo wa mjane, kufurahia kweli katika baraka ambazo zitajaza “mahitaji” yatakayotokea.
Nimekuwa na baraka kubwa ya kutumikia miongoni mwa Watakatifu wa Pasifiki kwa muda mrefu wa maisha yangu ya utu uzima. Imani, upendo, na dhabihu za ajabu za Watakatifu hawa waliojitolea unijaza kwa msukumo, shukrani, na furaha. Hadithi zao ni kama yako mwenyewe.
Naona kuwa Watakatifu hawa wana mengi yanayofanana sana na mjane ambaye Mwokozi alimwona alipokuwa “Ameketi … na akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.
“Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili. …
“Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amini, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina:
“Maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia”1
Ingawa senti zake mbili zilikuwa ni mchango mdogo, kwa Mwokozi zawadi yake ilikuwa ya thamani kubwa, kwa sababu yeye alitoa kila kitu. Kwa wakati huo, Mwokozi alimjua mjane kikamilifu, kwa kuwa zawadi yake ilimwonyesha moyo wake. Ubora na kina cha upendo wake na imani yake ulikuwa vile alitoa akijua kwamba “mahitaji” yake yatakidhiwa.
Nimeona moyo huo huo kwa Watakatifu wa Pasifiki.Katika kijiji kidogo katika mojawapo ya visiwa hivi, mtu mzee na mke wake walikubali mwaliko wa wamisionari kwa kumwomba Bwana kwa dhati kama masomo waliyofundishwa yalikuwa ya kweli.Katika mchakato huu, pia walitazama matokeo ya sharti ambazo wangehitaji kufanya ikiwa jibu ambalo walipata lingewapelekea kukubali injili iliyorejeshwa.Walifunga na kuomba ili kujua ukweli wa Kanisa na ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Jibu la sala zao lilikuja kwa namna ya uthibitisho wa kupendeza: “Ndiyo! Ni kweli!”
Baada ya kupokea ushahidi huu, walichagua kubatizwa.Hii haikuwa chaguo bila gharama za kibinafsi. Uamuzi wao na ubatizo ulikuwa wa gharama ghali.Walipoteza ajira, walipoteza hadhi yao katika jamii, urafiki muhimu uliharibika, na msaada, upendo, na heshima ya familia ziliondolewa.Wao sasa wanatembea kwenda kanisani kila Jumapili, wakitupiana macho ya kufedhehesha na marafiki na majirani waliokuwa wakitembea kuelekeana.
Katika mazingira haya magumu, ndugu huyu mzuri aliulizwa jinsi alivyohisi kuhusu uamuzi wao wa kujiunga na Kanisa.Jibu lake rahisi na lisilotingika lilikuwa “Ni kweli, sivyo?Uchaguzi wetu ulikuwa wazi.”
Watakatifu hawa wawili wapya walioongoka kweli walikuwa na moyo wa mjane. Wao, kama mjane, “walitia vyote” ambavyo wangeweza kutoa, wakijua wanatoa kwa ajili ya “mahitaji” yao.Kama matokeo ya mioyo yao yenye kuamini na imani ya kudumu wakati wa nyakati hizo ngumu, mizigo yao ilipungua.Walisaidiwa na kuzungukwa na waumini wenye msaada na huduma, na waliimarishwa binafsi na huduma yao katika wito wa Kanisa.
Baada ya kutia “yote” yao, siku kubwa zaidi ya furaha kwao ilikuja wakati walipofunganishwa katika hekalu kama familia ya milele. Kama Yeye alivyofanyia waongofu chini ya uongozi wa Alma, “Bwana aliwapatia nguvu kwamba wabebe mizigo yao kwa urahisi, na walinyenyekea kwa furaha na subira kwa mapenzi ya Bwana.”2 Hivyo ndivyo moyo wa mjane ulivyoonyeshwa katika wanandoa hawa wa ajabu.
Acha nizungumze juu ya uzoefu mwingine ambapo moyo wa mjane ulikuwa na mtazamo kamili. Kule Samoa, tunafanya kazi na baraza za vijiji ili kupata fursa za wamisionari kuhubiri injili.Miaka michache iliyopita, nilikuwa na mazungumzo na chifu kutoka kijiji ambako wamisionari wetu walikuwa wamekatazwa kwa miaka mingi zaidi. Mazungumzo yangu hayakuwa muda mrefu baada ya chifu mkuu kufungua kijiji kwa Kanisa, kuruhusu wamisionari wetu wafundishe wale wanaopenda kujifunza kuhusu Injili na mafundisho yake.
Baada ya miaka mingi, kuwa na mabadiliko haya ya ajabu ya matukio, nilikuwa na hamu ya kujifunza juu ya kile kilichotokea ili kumfanya chifu mkuu kuchukua hatua hii.Niliuliza juu ya jambo hili, na chifu ambaye nilikuwa nikizungumza naye akajibu, “Mtu anaweza kuishi katika giza kwa kipindi fulani, lakini wakati utafika atataka kuingia katika nuru.”
Chifu mkuu, katika kufungua kijiji, alionyesha moyo wa mjane-moyo ambao hulainika wakati joto na mwanga wa ukweli umefunuliwa. Kiongozi huyu alikuwa tayari kuacha miaka ya desturi, kupambana na upinzani mwingi, na kusimama imara ili wengine waweze kubarikiwa.Huyu alikuwa kiongozi ambaye moyo wake ulizingatia ustawi na furaha ya watu wake, badala ya kuzingatia mila, utamaduni, na nguvu za kibinafsi. Aliwaacha wasiwasi huo kwa ajili ya kile Rais Thomas S. Monson ametufundisha: “Tunapofuata mfano wa Mwokozi, yetu itakuwa ni nafasi ya kuwa nuru katika maisha ya wengine.”3
Hatimaye, acha nishiriki nanyi uzoefu mmoja zaidi kati ya Watakatifu wa Pasifiki ambao unabakia ndani na kukita mizizi kiroho katika nafsi yangu.Miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa mshauri chipukizi kwa askofu katika kata mpya huko Samoa ya Amerika.Tulikuwa na waumini 99 wakiwemo wakulima wadogo, wafanyakazi wa viwanda vya kutia chakula makoponi, wafanyakazi wa serikali, na familia zao. Wakati Urais wa Kwanza walipotangaza mnamo 1977 kwamba hekalu lingejengwa huko Samoa, kulikuwa na furaha na shukrani iliyodhihirishwa na sisi wote. Kwenda hekaluni kutoka Samoa ya Amerika wakati huo ilihitaji kusafiri kwenda Hawaii au New Zealand.Hii ilikuwa safari ya gharama kubwa ambayo ilikuwa juu ya uwezo wa wauminii wengi wa Kanisa.
Katika kipindi hiki, washiriki walihimizwa kuchangia hazina ya kujenga ili kusaidia katika ujenzi wa mahekalu. Katika moyo huu, uaskofu wetu uliwauliza waumini wa kata kuzingatia kwa maombi yale wangeweza kutoa. Tarehe iliwekwa kwa familia kukusanyika ili kutoa mchango wao.Baadaye, wakati michango hiyo ilipofunguliwa faraghani, uaskofu wetu alinyenyekezwa na kuguswa na imani na ukarimu wa waumini wetu wa kata wa ajabu.
Kujua kila familia na hali zao, nilihisi hisia kali na ya heshima ya kudumu, heshima, na unyenyekevu.Hizi zilikuwa, kwa kila namna, senti za kisasa za mjane zilizotolewa kwa hiari kutoka kwa“mahitaji”yao kwa furaha katika baraka ya ujenzi ulioahidiwa wa hekalu takatifu la Bwana huko Samoa. Familia hizi ziliweka wakfu kila kitu ambacho wangeweza kwa Bwana, kwa imani kwamba hawataachwa na mahitaji. Toleo lao lilionyesha mioyo yao ya mjane.Wote waliotoa walifanya hivyo kwa hiari na kwa furaha kwa sababu moyo wa mjane ndani yao ungeona kwa macho ya imani baraka kuu zilizohifadhiwa kwa familia zao, na watu wote wa Samoa na Samoa ya Amerika, kwa vizazi vijavyo. Najua kwamba matoleo yao matakatifu, senti zao za mjane, zilijulikana na kukubaliwa na Bwana.
Moyo wa mjane aliyetoa senti zake mbili ni moyo ambao utatoa kila kitu kwa dhabihu; kwa kuvumilia shida, mateso, na kukataliwa; na kwa kubeba mizigo ya aina nyingi Moyo wa mjane ni moyo unaohisi, unaosikia, na kujua nuru ya kweli na utatoa chochote ili kukubali ukweli huo.Pia husaidia wengine kuona nuru hio hio na kuja kwenye kipimo sawa chafuraha ya milele na shangwe. Hatimaye, moyo wa mjane huelezewa na nia ya kutoa yote kwa ajili ya kujenga ufalme wa Mungu duniani.
Hebu tuungane kama Watakatifu wa duniani kote katika kufanya kile ambacho ni muhimu ili kuwa na moyo wa mjane, kufurahia kweli katika baraka ambazo zitakidhi “mahitaji” yatakayotokea. Sala yangu kwa kila mmoja wetu ni ombi la kuwa na moyo wa kubeba mizigo yetu, kufanya dhabihu muhimu, na kuwa na mapenzi ya kutenda na kutoa. Ninaahidi kwamba Bwana hatakuacha ukiwa na mahitaji. Moyo wa mjane umejazwa na shukrani kwamba Mwokozi alikuwa “mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko”4 ili tusingehitaji kuonja “kikombe kichungu.”5 Licha ya udhaifu wetu na mapungufu, na kwa sababu yayo, Yeye anaendelea kunyoosha mikono Yake, ambayo ilichomwa kwa ajili yetu. Atatuinua juu ikiwa tunataka kuja katika nuru ya Injili Yake, kumkumbatia, na kumruhusu kujaza “mahitaji” yetu.
Ninatoa ushuhuda wangu wa upendo mkubwa ambao tunaweza kushiriki kama wanafunzi na wafuasi wa Bwana Yesu Kristo. Ninampenda na kumkubali Rais Thomas S. Monson kama nabii wa Mungu duniani. Kitabu cha Mormon ni ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo ulimwenguni, na ninawakaribisheni wote kukisoma na kugundua ujumbe wake kwa ajili yenu. Wote wanaokubali mwaliko wa Bwana wa kuja Kwake watapata amani, upendo, na nuru. Yesu Kristo ndiye Mfano wetu mkuu na Mkombozi. Ni kupitia tu kwa Yesu Kristo, na muujiza wa Upatanisho Wake usio na kipimo, ndipo tunaweza kupokea uzima wa milele. Ninashuhudia hayo katika jina Lake tukufu, hata Yesu Kristo, amina.