Kwa Usanifu Mtakatifu
Mkono wa Bwana unakuongoza Kwa “usanifu mtakatifu” Yeye yuko katika sehemu ndogo ndogo za maisha yako na pia katika yaliyo makubwa.
Akina Kaka na akina dada, ninaposimama katika huu mkutano mkuu wa duniani kote wenye mwongozo nahisi nguvu yenu na roho yenu, ninashindwa kujizuia kufikiria maneno ya Mtume Petro: “[Bwana], ni vizuri kwetu kuwa hapa.”1
Hiki sio hasa kile Alma alichosema baada ya kuwahubiria watu wa Amoniha. Alma alitoka mji huu kwa sababu ya maovu ya watu. Punde malaika alimtokea Alma na kumwita “kurudi kwenye mji wa Amoniha, na kuwafundisha tena watu wa mji.”2
Alma kwa “haraka sana,” aliingia kwenye mji kwa njia nyingine.”3
“Na alipoingia mjini alikuwa na njaa, na akamwambia mtu fulani: Waweza kumpatia mtumishi mnyenyekevu wa Mungu kitu cha kula?”
“Na yule mtu akamwambia: Mimi ni Mnefi, na ninajua kwamba wewe ni nabii mtakatifu wa Mungu, kwani wewe ndiye yule mtu ambaye malaika alisema katika ono: Wewe utampokea.4
Mtu yule alikuwa ni Amuleki
Sasa, Je, Alma alimtokea tu kwa Amuleki? Hapana, haikuwa kwa bahati kuwa aliingia kwenye mji kupitia njia ambayo ingemuongoza kwa mtu huyu mwaminifu ambaye angekuwa mmsionari mwenzake.
Mzee Neal L. Maxwell alielezea: “Hakuna hata mmoja wetu atawahi kutumia fursa zote kwetu zitokanazo na watu ndani ya mzunguko wa urafiki wetu. Mimi na wewe tunaweza kuita kukutana hivi kama ‘bahati.’ Neno hili linaeleweka kwa wanadamu kutumia, lakini bahati sio neno sahihi kuelezea kazi za Mungu mwenye maarifa yote. Hafanyi vitu kwa ‘bahati’ lakini kwa ‘mpango mtakatifu.’”5
Maisha yetu ni kama ubao wa chesi na Bwana hutusogeza kutoka sehemu moja hadi nyingine—kama tutakuwa wa kuitikia misukumo ya kiroho. Tukiangalia nyuma, tunaweza kuona mkono Wake katika maisha yetu.
Tunaona usaidizi huu wa kimbingu pale Nefi aliporejea kuchukua bamba kutoka kwa Labani. “Aliongozwa na Roho, bila kujua mwanzoni vitu ambavyo [angefanya].”6 Punde Labani alikuwa mbele yake akiweweseka kwa ulevi na Nefi alimuua, akapata tena mabamba na kutorokea kwa kaka zake. Je, ilikuwa bahati kwake kuwa hiki kiilitokea kwa Labani? Au ililkuwa kwa “usanifu mtakatifu”?
Matukio muhimu hufunuliwa katika injili na katika kanisa ambayo huendeleza ufalme Mungu duniani. Hayatokei kwa bahati, lakini kwa mpango wa Mungu. Yeye ambaye alitengeneza dunia hii anaweza kutuliza bahari kwa neno Lake, na kuwaongoza wote Alma na Amuleki, na Nefi na Labani kuwa katika sehemu sahihi na katika muda mahususi na sahihi.
Vivyo hivyo, matukio na mahusiano hufunuliwa katika maisha ya kila mmoja wetu ambayo huendeleza kazi ya Mungu duniani.
Mzee Joseph B. Wirthlin wakati mmoja aliongea wakati Rais Monson alimwambia: “Kuna mkono elekezi juu ya vitu vyote. Mara kwa mara vitu vinapotokea, sio kwa bahati. Siku moja, tutakapoangalia nyuma kwa vile vilikuwa vinaonekana kama bahati katika maisha yetu, tutatambua kuwa labda hata hivyo havikuwa bahati.”7
Mara nyingi, kazi zetu nzuri zinajulikana kwa wachache tu. Hata hivyo, zinarekodiwa mbinguni. Siku moja, tutasimama kama mashahidi wa kujitoa kwa nafsi‑zetu zote katika kazi za utakatifu. Hakuna jaribio wala janga linaloweza kuangusha mpango wa furaha wa Mungu. Kwa hakika, kwa “mpango mtakatifu,” “shangwe huja asubuhi.”8 “Nilikuja kwenye ulimwengu kufanya mapenzi ya Baba,”9 Yesu alifundisha. Akina kaka na akina dada wapendwa, sisi pia.
Kupitia uzoefu wa safari ya maisha yangu, ninajua kwamba Bwana atatusogeza katika kile kinachoonekana kama ubao wa chesi kufanya kazi Yake. Kile kinaweza kuonekana kama bahati isiyo maalum, kikweli, kilisimamiwa na Baba wa Mbinguni mwenye upendo, ambaye anaweza kuhesabu nywele za kila kichwa.10 Hakuna hata shomoro anayeanguka bila Baba kutambua.11 Bwana yuko katika sehemu ndogo ndogo za maisha yetu, nyakati na fursa hizo ni kwa kutuandaa kuinua familia zetu na wengine tunapojenga ufalme wa Mungu duniani. Kumbuka, kama Bwana alivyomwambia Ibrahimu, “Jina langu ni Yehova, nami ninajua mwisho kutoka mwanzo; kwa hiyo mkono wangu utakuwa juu yako.”12
Bwana aliniweka nyumbani kwa wazazi wenye upendo. Katika vipimo vya kilimwengu, walikuwa watu wa kawaida; baba yangu mwenye bidii alikuwa dereva wa lori, malaika mama yangu, mama nyumbani. Bwana alinisaidia kupata mke mpendwa, Melanie; alisababisha msukumo kwa mfanyabiashara ambaye alikuja kuwa rafiki yangu mpendwa, kunipa nafasi ya ajira. Bwana aliniita kutumikia misheni, yote kama kijana na kama rais wa misheni; aliniita katika Akidi ya Sabini, na sasa ameniita kama Mtume. Nikitazama nyuma, ninatambua sikutengeneza hatua yoyote kati ya hizo; Bwana alifanya hivyo, kama anavyotengeneza hatua muhimu kwa ajili yako na wale unaowapenda.
Nini unatakiwa kukiangalia katika maisha yako? Miujiza gani ya Mungu inayokukumbusha kuwa yu karibu, akisema “Niko hapa”?Fikiria kuhusu nyakati hizo, zingine kila siku, ambapo Bwana alitenda katika maisha yako—halafu alitenda tena. Zithamini kama nyakati Bwana amekuonyesha kukuamini wewe na chaguzi zako. Lakini mruhusu Yeye afanye zaidi kwako kuliko unavyoweza mwenyewe. Thamini uhusika Wake. Wakati mwingine tunachukulia mabadiliko katika mipango yetu kama hatua zisizofaa safarini mwetu. Yafikirie zaidi kama hatua za awali kuwa “katika kazi ya Bwana.”13
Miezi kadhaa iliyopita mjukuu wetu wa kike alijiunga na kikundi cha vijana kutalii sehemu kadhaa za kihistoria za Kanisa. Utaratibu wa safari wa mwisho ulionyesha kuwa angepita katika eneo ambapo kaka yake mmisionari, mjukuu wetu wa kiume, alitumikia. Mjukuu wetu wa kike hakuwa na nia ya kumuona kaka yake katika misheni yake. Hata hivyo, wakati basi likiingia mjini ambapo kaka yake alitumikia, wamisionari wawili walionekana wakitembea mtaani. Mmoja wa wamisionari alikuwa ni kaka yake.
Msisimko ulijaa kwenye basi wakati kijana alipomwambia dereva wa basi asimamishe ili aweze kumsalimu kaka yake. Ndani ya dakika chache, baada ya machozi na maneno ya furaha, kaka yake alirudi katika njia yake kutimiza majukumu yake ya umisionari. Tuligundua baadaye kuwa kaka yake alikuwa katika mtaa huo kwa dakika zisizopungua tano, akitembea kutoka kwenye ahadi ya kuonana na mtu kwenda kwenye gari lake.
Baba yetu wa Mbinguni anaweza kuweka hali fulani kwa kusudi mahususi katika akili. Amefanya hivyo katika maisha yangu, na anafanya hivyo katika maisha yako, kama alivyofanya katika maisha ya wajukuuu wetu.
Kila mmoja wetu ni wa thamani na anapendwa na Bwana, ambaye hujali, hunong’oneza na ambaye hutuangalia kila mmoja wetu kwa njia za kipekee. Ni mwenye busara isiyo na mwisho na mwenye nguvu kuliko wanadamu. Anajua changamoto zetu, ushindi wetu na nia njema za mioyo yetu.
Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, nilipokuwa nikitembea kupitia Temple Square, mmoja wa dada wamisionari alinikaribia na kuniuliza, “Unanikumbuka? Natokea Florida.” Akaniambia jina lake, Dada Aida Chilan. Ndio, Nilikumbuka kwa udhahiri kukutana na yeye na familia yake. Rais wake wa kigingi alipendekeza tuitembelee familia ya Chilan. Ilikuwa wazi kuwa tulikuwa pale kwa ajili ya binti yao, Aida, ambaye alikuwa hajabatizwa. Baada ya matembezi yetu, na zaidi ya mwaka wa mafundisho na ushirika, Aida alibatizwa.
Baada ya kukutana Temple Square, Aida aliniandikia barua. Alisema “Najua kwa moyo wangu wote kwamba Baba yetu wa Mbinguni anamjua kila mmoja wetu na kwamba anaendelea kutuweka kila mmoja wetu katika njia ya kila mmoja kwa kusudi fulani. Asante kwa kuwa mmoja wa wamisionari wangu, kwa kunifikia na kunipata miaka mitano iliyopita.”14 Aida pia alinitumia hadithi ya maongezi akikumbuka “nyakati takatifu” ambazo zilimetokea maishani mwake ambazo zimepelekea ubatizo wake na kuthibitishwa, kutumikia misheni katika Temple Square na Ndoa yake hekaluni ya hivi karibuni.15
Je, ilikuwa bahati tu kuwa rais wa kigingi alituongoza nyumbani kwa Chilan au kwamba mimi na yeye tungekutana baadaye Temple Square? Ushuhuda wa Aida unathibitisha kuwa hii ilikuwa sehemu ya “Usanifu mtakatifu” wa Mungu.
Bwana anapenda kuwa nasi. Si kwa bahati kwamba unapohisi Roho Wake na kufuata ushawishi kwanza kwamba unamhisi Yeye kama alivyoahidi: “Nitakwenda mbele zenu. Nitakuwa mkono wenu wa kuume na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na malaika zangu watawazingira, ili kuwabeba juu.16
Wote tuna vitu vya kufanana vitokeavyo maishani mwetu. Tunaweza kukutana na mtu fulani ambaye anaonekana si mgeni, kufanya upya urafiki, au kutafuta usawa kwa wale ambao ni wageni kwetu. Hayo yanapotokea, labda Bwana anatukumbusha kwamba sisi wote ni kaka na dada. Kwa kweli tunajishugulisha katika lililo jema; kwa kile Joseph Smith alikiita “kusudi la Kristo.”17
Sasa uhuru wetu wa kujiamulia unafaa sehemu gani katika “usanifu mtakatifu”? Tuna uchaguzi wa kumfuata au kutomfuata Mwokozi na viongozi wake wateule. Mfumo uko wazi katika Kitabu cha Mormoni wakati wanefi waligeuka kutoka kwa Bwana. Mormoni aliomboleza:
“Na waliona … kwamba Roho ya Bwana haikuwahifadhi; ndio, ilikuwa imejiondoa kutoka kwao kwa sababu Roho ya Bwana haishi kwenye mahekalu yasiyo matakatifu—
“Kwa hivyo Bwana aliacha kuwahifadhi kwa miujiza yake na uwezo wake usiolinganishwa, kwani walikuwa wameanguka kwa hali ya kutoamini na uovu wa kutisha.”18
Sio kila kitu ambacho Bwana anatutaka tufanye ni matokeo ya jinsi gani tuna uwezo, tu waaminifu kiasi gani au kile tunachoweza kuwa tunajua. Fikiria kuhusu Sauli ambaye Bwana alimsimamisha akiwa njiani kwenda Dameski. Alikuwa akienda kwenye mwelekeo usio sahihi katika maisha yake, haishabihiani kwa vyovyote na kaskazini au wala kusini. Sauli aliongozwa tena kiungu. Akijulikana baadaye kama Paulo, huduma yake ya kitume ilitoa taswira ya kile Bwana alikuwa ameshakijua kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya na kuwa, si kile alichopanga kufanya kama Sauli. Katika namna hiyo hiyo, Bwana anajua kile kila mmoja wetu ana uwezo wa kufanya na kuwa. Mtume Paulo alifundisha nini? “Na tunajua kwamba vitu vyote hufanya kazi pamoja kwa manufaa kwa wale wanaompenda Mungu, kwa wale walioitwa kulingana na kusudi lake.”19
Tunapokuwa wema, wenye utayari na wenye uwezo, wakati tunajaribu kuwa wasafi kiroho na wa kustahili, tunaendelea katika sehemu ambayo hatujawahi fikiria na kuwa sehemu ya “usanifu mtakatifu” wa Baba wa Mbinguni. Kila mmoja wetu ana utakatifu ndani yake. Tunapoona Mungu akifanya kazi na sisi na kupitia sisi, na tuhamasike, na hata tuwe wenye shukrani kwa uongozi huo. Wakati Baba yetu wa Mbinguni alisema “Hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu,”20 alikuwa akiongea na watoto wake wote—Hususani wewe.
Mkono wa Bwana unakuongoza. Kwa “usanifu mtakatifu” Yeye yuko katika sehemu ndogo ndogo za maisha yako na pia katika yaliyo makubwa. Kama isemavyo katika Mithali “Amini katika Bwana kwa moyo wako wote; … naye ataongoza njia zako.”21 Ninashuhudia kwamba atakubariki, atakuwa mhimili wako na kukuletea amani. Katika jina la Yesu Kristo, amina.