2010–2019
Mahitaji yaliyo mbele yetu
Oktoba 2017


12:6

Mahitaji yaliyo mbele Yetu

Baadhi ya mahitaji muhimu zaidi tunayoweza kukumbana nayo yapo ndani ya familia zetu, miongoni mwa marafiki zetu, katika kata zetu, na katika jamii zetu.

Katika siku za hivi karibuni tumeona idadi kubwa ya majanga ya asili huko Mexico, Marekani, Asia, Caribbean, na Afrika. Yamefunua kilicho bora zaidi kwa watu kwani maelfu wamejiunga kuwasaidia wale walio katika hatari au wenye uhitaji na ambao wamepata hasara. Nimefurahi sana kuona wasichana huko Texas na Florida, ambao, pamoja na wengine wengi, wamevaa T-shirts za rangi ya njano za Mormon Helping Hands na wanasaidia kusafisha nyumba zilizojaa uchafu kufuatia vimbunga vya hivi karibuni. Maelfu zaidi wangefurahi kwenda katika vituo vya msaada isingekuwa ni umbali. Badala yake, mmetoa michango ya ukarimu ili kupunguza mateso. Ukarimu na huruma yenu inatia moyo na ni kama ya Kristo.

Wasichana pamoja na Rais Eyring

Leo hii ninataka kutaja kipengele cha huduma ambacho ninahisi ni muhimu kwa wote—bila kujali pale tulipo. Kwa wale kati yetu ambao tumetazama habari za matukio ya hivi karibuni na kuhisi tusiojiweza kujua cha kufanya, jibu linaweza kuwa hasa hapa mbele yetu.

Mwokozi alifundisha, “Kwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.”1 Rais Thomas S. Monson alisema juu ya andiko hili: “Ninaamini Mwokozi anatuambia kwamba tusipojipoteza wenyewe katika huduma, kuna maana ndogo katika maisha yetu wenyewe. Wale wanaoishi tu kwa ajili ya wao wenyewe hatimaye hunyauka na kistiari hupoteza maisha yao, wakati wale wanaojitoa katika utumishi kwa wengine hukua na kustawi—na hakika huokoa maisha yao.”2

Tunaishi katika utamaduni ambapo zaidi na zaidi tunazingatia skrini ndogo ndogo mikononi mwetu kuliko watu walio karibu nasi. Tumebadilisha kutuma jumbe na mtwito kwa hasa kuangalia mtu fulani machoni na kutabasamu au, hata mara chache, kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana. Mara nyingi tunahusika zaidi na followers na likes tulizonazo ni ngapi kuliko kumkumbati rafiki kwa mkono na kuonyesha upendo, kujali, na maslahi halisi. Kwa ajabu teknolojia ya kisasa inavyoweza kuwa kwa kueneza ujumbe wa Injili ya Yesu Kristo na kutusaidia kuunganisha na familia na marafiki, ikiwa hatutakuwa makini jinsi tunavyotumia vifaa vyetu vya kibinafsi, sisi pia tunaweza kuanza kugeukia ndani na kusahau kwamba kiini cha kuishi injili ni huduma.

Nina upendo mkubwa na imani katika wale ambao wako katika umri wenu wa ujana na utu uzima. Nimeona na kuhisi hamu zenu za kuhudumu na kuleta tofauti ulimwenguni. Ninaamini kwamba waumini wengi wanaona huduma kuwa kitovu cha maagano yao na ufuasi wao. Lakini nadhani pia kwamba wakati mwingine ni rahisi kupoteza fursa kubwa zaidi za kuwatumikia wengine kwa sababu tunasumbuliwa au kwa sababu tunatafuta njia za hadhi za kubadilisha ulimwengu na hatuoni kwamba baadhi ya mahitaji muhimu zaidi tunayoweza kutatua yapo ndani ya familia zetu, kati ya marafiki zetu, katika kata zetu, na katika jamii zetu. Tunaguswa tunapoona mateso na mahitaji makubwa ya wale walio mbali duniani kote, lakini tunaweza kushindwa kuona kuna mtu anayehitaji urafiki wetu ameketi hasa karibu nasi katika darasa.

Dada Linda K. Burton alielezea hadithi ya Rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wa kigingi ambaye, akifanya kazi na wengine, alikusanya mafarishi kwa watu wenye mahitaji wakati wa miaka ya 1990. “Yeye na binti yake waliendesha gari ya mizigo lililojaa hayo mafarishi kutoka London hadi Kosovo. Njiani akirudi nyumbani, alipokea mnong’ono wa kiroho ambao ulizama kwa kina katika moyo wake. Mnong’ono ulikuwa hivi: “Kile ulichofanya ni kitu kizuri sana. Sasa nenda nyumbani, tembea mtaani, na ukamhudumie jirani yako!”3

Inasaidia nini kuokoa ulimwengu kama tutapuuza mahitaji ya wale walio karibu kabisa nasi na wale tuwapendao zaidi?Kuna thamani gani katika kurekebisha dunia kama watu walio tuzunguka wanaanguka na hatutambui? Baba wa Mbinguni anaweza kuwaweka wale wanaotuhitaji karibu nasi zaidi, kwa kujua kwamba sisi tunafaa zaidi kukidhi mahitaji yao.

Dada na dadake wakitembea

Kila mmoja anaweza kutafuta njia kutoa huduma kama ya Kristo. Mshauri wangu, Dada Carol F. McConkie, hivi karibuni aliniambia kuhusu mjukuu wake wa miaka 10 Sarah ambaye, alipofahamu kwamba mama yake ni mgonjwa, aliamua mwenyewe kuwa wa msaada. Alimwamsha mdogo wake wa kike, akamsaidia kuvaa, kumsafisha meno, kumchana nywele, na kula kifungua kinywa ili mama yake apumzike. Kwa ukimya alifanya kitendo hiki rahisi cha huduma pasipo kuombwa kwa sababu aliona haja hiyo na alitamani kusaidia. Sio tu kwamba Sarah alimbariki mama yake, lakini nina uhakika alijisikia mwenye shangwe pia kujua alimpunguzia mzigo mtu aliyempenda na, katika njia hiyo, kuimarisha uhusiano wake na dada yake. Rais James E. Faust alisema: “Kuhudumia wengine kunaweza kuanza katika umri wowote. … Hakuhitaji kuwa katika kiwango kikubwa, na ni vyema ikiwa ndani ya familia.”4

Sarah na dadake wakisoma kitabu

Je, ninyi watoto mnatambua ni kiasi gani inavyofariji wazazi wenu na wanafamilia mnapotafuta njia za kutumikia nyumbani? Kwa wale mlio katika miaka ya ujana, kuimarisha na kutumikia wana familia wenu inapaswa kuwa kati ya vipaumbele vyenu vya juu mnapotafuta njia za kubadilisha ulimwengu. Kuonesha ukarimu na kuwajali ndugu zako na wazazi wako husaidia kuunda hali ya umoja na hualika Roho nyumbani. Kubadilisha dunia huanza kwa kuimarisha familia yako mwenyewe.

Eneo lingine la kuzingatia huduma yetu inaweza kuwa katika familia za kata zetu. Mara kwa mara watoto wetu hutuuliza sisi swali, “Ni kwa nini napaswa kuenda katika shughuli za Mutual? Huwa sinufaiki kutokana nazo.”

Kama ningelikuwa na wakati mzuri wa kufunza, ningejibu, “Ni kitu gani kinachokufanya ufikiri unaenda katika shughuli za Mutual kwa sababu ya kile unachokipata kutoka huko?”

Marafiki zangu wadogo, ninaweza kuwahakikishia kwamba daima kutakuwa na mtu katika kila mikutano ya kanisa unaohudhuria ambaye ni mpweke, anayepitia changamoto na anahitaji rafiki, au anayehisi kutostahili kuwapo. Mna kitu fulani muhimu cha kuchangia katika kila mkutano au shughuli, na Bwana anatamani muangalie kati yenu na kisha kuhudumia jinsi Yeye angehudumia.

Mzee D. Todd Christofferson alifundisha, “Sababu kubwa ya Bwana kuwa na kanisa ni ili kujenga jumuia ya Watakatifu ambayo itasaidiana katika ‘njia hii nyembamba iliyosonga ambayo inaelekea uzima wa milele.” Anaendelea kusema, “Dini hii haihusiki tu na binafsi; bali wote tumeitwa kuhudumia. Sisi ni macho, mikono, kichwa, miguu, na sehemu zingine za mwili wa Kristo.”5

Ni kweli kwamba tunahudhuria mikutano ya kila wiki ya kanisa kushiriki katika ibada, kujifunza mafundisho, na kutiwa moyo, lakini sababu nyingine ya muhimu sana ya kuhudhuria ni kwamba, kama familia ya kata na kama wafuasi wa Mwokozi Yesu Kristo, tulindane, tuhamasishane, na kutafuta njia kuhudumiana na kuimarishana. Sisi sio wapokeaji na wachukuaji tu wa kile kinachotolewa kanisani; tunapaswa kuwa watoaji na wasambazaji. Wavulana na wasichana, wakati mwingine mkiwa katika shughuli za Mutual, badala ya kuchukua simu yako kuona kile rafiki zako wanafanya, simama, tazama, na jiulize, “Nani ananihitaji leo?” Unaweza kuwa ufunguo katika kuwafikia na kugusa maisha ya mwenzako au kutoa hamasa kwa rafiki ambaye anasumbuka kimya kimya.

Muulize Baba yako wa Mbinguni akuonyeshe wale walio kuzunguka wanaohitaji msaada wako na kukutia msukumo katika jinsi bora ya kuwatumikia. Kumbuka kwamba Mwokozi mara nyingi alisaidia mtu mmoja kwa wakati.

Ethan na familia yake

Mjukuu wetu Ethan ana miaka 17. Niliguswa msimu huu wa kiangazi aliponiambia kwamba, akitiwa moyo na mfano wa mama yake, alisali kila siku kupata nafasi ya kumtumikia mtu mmoja. Tulipotumia muda na familia yake, niligundua jinsiEthan anawachukulia kaka na dada zake kwa uvumilivu, upendo, na ukarimu na yeye ni msaada kwa wazazi wake; na hutafuta njia za kuwafikia wengine. Nimevutiwa na jinsi alivyo na uelewa wa watu wanaomzunguka na hamu yake ya kuwatumikia. Yeye ni mfano kwangu. Kufanya kama Ethan afanyavyo—kumualika Bwana atusaidie kutafuta njia za kutumikia—itaruhusu Roho kufungua macho yetu kuona mahitaji yanayotuzunguka, kumuona “mtu” ambaye anatuhitaji siku hiyo, na kujua ni jinsi gani ya kumhudumia mtu huyo.

Picha ya Ethan

Kwa nyongeza kutumikia familia yako na waumini wa kata yako, tafuta nafasi za kutumikia katika ujirani na jamii yako. Hali wakati mwingine tunaitwa kusaidia baada ya janga kubwa, katika siku hadi siku tunahamasishwa kuangalia nafasi katika mazingira yetu binafsi kuinua na kusaidia wenye uhitaji. Nilifunzwa hivi karibuni na Rais wa eneo, anayetumikia katika nchi yenye changamoto nyingi sana za kimwili, kwamba njia bora ya kusaidia wenye uhitaji katika sehemu nyingine duniani ni kutoa matoleo ya dhati ya mfungo, kuchangia katika misaada ya Kibinadamu ya Kanisa, na kutafuta njia za kuwatumikia wale katika jamii yako popote unapoishi. Hebu fikiria jinsi gani dunia ingebarikiwa kama kila mmoja angefuata ushauri huu!

Kaka na Dada zangu, na hususani vijana, mnapojitahidi kuwa zaidi kama Mwokozi Yesu Kristo na kuishi maagano yenu, mtaendelea kubarikwa na hamu ya kupunguza mateso na kusaidia maskini. Kumbuka kwamba baadhi ya mahitaji makubwa yanaweza kuwa yale yalio mbele yako. Anzeni huduma katika nyumba zenu wenyewe na katika familia zenu wenyewe. Haya ni mahusiano ambayo yanaweza kuwa ya milele. Hata kama—na labda hususani—hali ya familia yako haijakamilika, unaweza tafuta njia kutumikia, kuinua, na kuimarisha. Anza pale ulipo, wapende kama walivyo, na andaa familia unayotaka kuwa nayo baadaye.

Sali kwa msaada katika kugundua wale katika familia ya kata yako wanaohitaji upendo na hamasa. Badala ya kuhudhuria kanisa na swali la “kipi nitapata kutoka kwenye mkutano?” uliza, “ni nani ananihitaji mimi leo. Ni kitu gani nitachangia?”

Unapobariki famila yako na washiriki wa kata yako, tafuta njia za kutumikia katika ujirani na jamii yako. Kama una muda wa huduma pana au unatoa masaa machache kwa mwezi, jitihada zako zitabariki maisha na pia zitakubariki katika njia usizoweza hata kufikiria.

Rais Spencer W. Kimball alifundisha: “Mungu anatuona, na anatuchunga. Lakini mara nyingi ni kwa kupitia mtu mwingine Yeye hukidhi mahitaji yetu.”6 Ninaomba tutambue upendeleo na baraka zilizopo katika kushiriki kutimiza kazi ya Baba wa Mbinguni tunapokidhi mahitaji ya watoto Wake ni sala yangu katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Luka 9:24.

  2. Thomas S. Monson, “Ni kipi nimefanya kwa mtu fulani leo?” au Liahona, Nov. 2009, 85.

  3. Linda K. Burton, “Nilikuwa Mgeni,” Liahona, May 2016, 15.

  4. James E.James E. Faust, “Uwanawake: Sehemu ya juu sana ya H,” Liahona, July 2000, 117.

  5. D. Todd Christofferson, “Kwanini Kanisa,” Liahona, Nov. 2015, 108, 109.

  6. Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball (2006), 82.