Mpendane, kama Alivyotupenda Sisi.
Kwa kuwatumikia na kuwasamehe wengine kwa upendo wa halisi tunaweza kuponywa and kupokea nguvu za kushinda changamoto zetu.
Wakati wa Karamu ya Mwisho, Mwokozi alitoa amri mpya kwa wafuasi Wake, akisema:
“Amri mpya nawapa, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
“Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. 1
Wafuasi wa Mwokozi walipewa amri mpya kufanya kitu fulani zaidi, kitu kikubwa sana, na kitu fulani kitukufu zaidi. Amri hii mpya na mwaliko imefupishwa katika kishazi muhimu “kama nilivyo wapenda nyinyi”
Upendo ni Kitendo; Upendo ni Huduma
“Upendo ni hisia za upendo wa dhati, shughuli, na huba Mfano mkubwa wa upendo wa Mungu kwa watoto wake unapatikana katika Upatanisho wa Yesu Kristo usio na kikomo.”2 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,” Yohana alirekodi, “hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”3 “Upendo kwa Mungu na wanadamu wenzetu ni tabia ya wafuasi wa Yesu Kristo.”4
Miaka kadha iliyopita, wakati mjukuu wetu mkubwa, Jose, alikuwa miaka 4 alikuwa anacheza na mke wangu. Wakati walikuwa wanacheka na wakifurahi pamoja, mjukuu wetu aliuliza, ”Bibi, unanipenda?”
Alimjibu , “Ndiyo, Jose, ninakupenda.”
Kisha alimwuliza bibi yake swali lingine: “Unajuajekwamba unanipenda?”
Alimwelezea hisia zake na pia alimwambia yote aliyofanya na alikuwa tayari kumfanyia kwa ajili yake.
Baadaye mke wangu alimwuliza Jose maswali kama yale, pamoja na maulizo yanayopenya:”Unajuaje kwamba unanipenda?”
Kwa jibu maasumu lakini la dhati, alisema, “ Nakupenda kwa sababunahisi hivyo ndani ya moyo wangu,” Tabia ya upendo ya Jose kwa bibi yake siku ile na daima inaonesha kwamba upendo ni mchanganyiko wa vitendo vilevile hisia za kina.
Mfalme Benjamin alifundisha, “Na tazama, nawaambia vitu hivi ili mpate hekima; ili mjifunze kwamba mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu.”5
Katika ulimwengu wa leo wa mateso mengi kwa hali tofauti ya mambo, kutuma ujumbe wa maneno na emoji ya kuchekesha au kutuma picha mzuri na maneno “Nakupenda” ni mzuri na yenye thamani. Lakini kile wengi wetu tunahitaji kufanya ni kuacha nyuma vyombo tamba vyetu na, kwa mikono na miguu yetu, kuwasaidia wengine walio katika mahitaji makubwa. Upendo bila huduma ni kama imani bila kazi; imekufa kabisa.
Upendo ni Msamaha
Upendo safi wa Kristo, ambao ni hisani,6sio tuu inatuvutia kufanya na kutoa huduma bali pia kuwa na nguvu ya kusamehe, bila kujali hali ilivyo. Naomba kushiriki pamoja nanyi uzoefu ambao umeathiri na kubadili maisha yangu. Ted na Sharon, wazazi wa Cooper, ambao wako hapa leo, wamenipa ruhusa kushiriki kile kilichotokea kwa familia yao zaidi ya miaka tisa iliyopita. Nitaeleza uzoefu kutoka taswira ya Ted, baba yake Cooper:
August 21, 2008, ilikuwa siku ya kwanza ya shule, na kaka wakubwa watatu wa Cooper, Ivan, Garrett, na Logan, wote walikuwa kituo cha basi wakingojea kuabiri mabasi. Cooper, aliyekuwa na umri wa miaka 4, alikuwa amepanda baisikeli yake, mke wangu, Sharon, alikuwa katembea.
Mke wangu alikuwa upande wa pili wa barabara na alimwashiria Cooper kuvuka.Wakati huohuo, gari polepole likapinda kushoto na likamkanyaga Cooper.
Nilipokea simu kutoka kwa jirani akiniambia Cooper amegongwa na gari. Haraka niliendesha gari kwenda kituo cha bus kumwangalia. Cooper alikuwa amelala kwenye nyasi, akijitahidi kupumua, bali hakuwa na majeraha yanayoonekana.
Nilipiiga magoti karibu na Cooper na kusema vitu vya kumtia moyo kama “mambo yatakuwa sawa. Shikilia” Wakati ule kiongozi wa kundi la makuhani wakuu Nathan, alitokea na mkewe. Mkewe alipendekeza tumpe Cooper baraka ya ukuhani. Tuliweka mikono yetu juu ya kichwa cha Cooper. Siwezi kukumbuka nini nilisema katika baraka, bali nakumbuka kwa udhahiri uwepo wa wengine waliotuzunguka, na ilikuwa wakati ule nilijua Cooper angefariki.
Cooper alirushwa kwa helikopta hospitalini lakini, kwa kweli, alifariki. Nilihisi Baba wa Mbinguni alikuwa ananiambia kwamba usimamizi wangu wa kidunia umekwisha na kwamba Cooper sasa alikuwa katika uangalizi Wake.
Tuliweza kutumia muda mchache na Cooper hospitalini. Wafanyakazi pale walimtayarisha ili tuweze kumshika na kusema buriani zetu na kuturuhusu kutumia muda mwingi pamoja naye, tukimshika kama tulivyotamani.
Njiani tukirudu nyumbani, mke wangu mwenye huzuni kubwa na mimi tulitazamana na kuanza kuzungumza kuhusu mvulana aliyekuwa anaendesha gari. Hatukumjua, japokuwa aliishi mtaa mmoja tu upande mwingine na ndani ya mipaka yetu ya kata.
Siku iliyofuata ilikuwa ngumu sana kwetu kwa vile tulikuwa wote tumezidiwa na huzuni. Nilipiga magoti na kusali sala ya dhati ambayo sijawahi kusali. Nilimwomba Baba wa Mbinguni katika jina la Mwokozi wangu kuondoa huzuni yangu iliyonizidi. Alifanya hivyo.
Baadaye siku ile mmoja wa washauri katika urais wa kigingi chetu alipanga kwamba sisi tukutane na yule kijana—dereva wa lile gari—na wazazi wake nyumbani kwake. Sharon na mimi tulimsubiri kijana na wazazi wake kuwasili. Wakati mlango ulipofunguliwa, tulikutana nao kwa mara ya kwanza. Askofu wangu alininong’oneza sikioni mwangu, ”Nenda kwake.” Sharon na Mimi tulimkumbatia katika mkumbatio wa kundi kubwa. Tuliomboleza pamoja kwa kile kilichoonekana kuwa ni muda mrefu. Tulimwambia tulijua kwamba kile kilichotokea kilikuwa dhahiri ni ajali.
Ilikuwa kimiujiza kwa Sharon na mimi, kwamba sote tulihisi vile tulivyofanya na vile bado tunafanya.Kwa neema za Mungu, tuliweza kuchukuwa njia kuu, njia halisi, njia pekee, na kumpenda huyu kijana mzuri.
Tumekuwa karibu sana naye na familia yake kwa miaka mingi. Ameshiriki nasi matukio yake muhimu ya kihistoria yenye thamani. Tulikwenda hata hekaluni pamoja naye alipokuwa anajiandaa kwa misheni yake.7
Ted anajua bila wasiwasi wowote kwamba Baba yetu wa Mbinguni anatupenda. Anajua kwamba kuweza kusamehe, na kujitua mzigo yeye mwenyewe kwa njia ile, ni kutamu kama kusamehewa. Utamu huu unakuja kutoka kufuata mfano wa Mfano wetu Mkubwa. Katika Kitabu cha Mormoni, Alma alitangaza juu ya Mwokozi: “Na atakwenda, na kuteseka maumivu na masumbuko na majaribio ya kila aina; na hii kwamba neno litimizwe ambalo linasema atabeba maumivu na magonjwa ya watu wake.”8
Akina Kaka na Akina dada, ni hadithi ya ajabu ya upendo wa kweli na msamaha jinsi gani. Sisi, vilevile, tunaweza kuwa na shangwe na furaha tunapowahudumia na kuwasamehe wengine. Georgy, mjukuu wetu mwingine, mara nyingi anasema, “Sisi ni familia ya aina gani?” Na ana jibu, “Sisi ni familia yenye furaha!”
Rais Thomas S. Monson ametushauri, akisema: “Na chunguze maisha yetu na kuamua kufuata mfano wa Mwokozi kwa kuwa wenye huruma, kupenda, na wenye fadhila.”9
Najua kwamba Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo, wanatupenda na wapo tayari kutusaidia kufanya kama tunapopendana kama walivyotupenda. Na ninajua ya kwamba kwa kuwatumikia na kuwasamehe wengine kwa upendo wa kweli tunaweza kuponywa and kupokea nguvu za kushinda changamoto zetu. Na mimi nashuhudia hayo katika jina la Yesu Kristo, amina.