2010–2019
Bwana, Nifumbue Macho Yangu Nipate Kuona.
Oktoba 2017


2:3

Bwana, Nifumbue Macho Yangu Nipate Kuona.

Sharti tuwaangalie wengine kupitia macho ya Mwokozi wetu.

The Lion King ni filamu ya fasihi iliyohuishwa kuhusu uwanda wa Afrika. Simba mfalme anapofariki wakati akimwokoa mwanawe, mwana wa simba mfalme analazimishwa kwenda uhamishoni huku mtawala mdhalimu akiharibu usawa katika uwanda. Mwana wa simba mfalme anauchukua tena ufalme kupitia usaidizi wa mnasihi. Macho yake yanafunguliwa kwa umuhimu wa usawa katika duara kubwa ya maisha katika uwanda. Akidai urithi wake wa haki kama mfalme, simba mdogo alifuata ushauri wa “kuangalia zaidi ya kile unachokiona.”1

Tunapojifunza kuwa warithi wa kila kitu alichonacho Baba yetu, injili inatushauri tuangalie zaidi ya kile tunachoona. Kuangalia zaidi ya kile tunachoona, lazima tuwaangalie wengine kupitia macho ya Mwokozi. Wavu wa injili umejaa watu kwa aina zao zote. Hatuwezi kuelewa kwa ukamilifu chaguzi na historia ya saikolojia ya watu ulimwenguni wetu, kwenye mikutano ya Kanisa, na hata katika familia zetu, kwa sababu tuna ufahamu mdogo kuhusu wao ni kina nani. Lazima tuangalie kupita makadirio rahisi na ubaguzi na kupanua lenzi ndogo ya uzoefu wetu wenyewe.

Nilipata kufumbuliwa macho “kuangalia zaidi ya nilichoweza kuona” wakati nikihudumu kama rais wa misheni. Mzee kijana alifika akiwa na hofu katika macho yake. Tulipokutana katika usahili, alisema kwa huzuni, “Nataka kurudi nyumbani.” Nikafikiri nafsini mwangu, “Vema, tunaweza kurekebisha hili.” Nilimshauri afanye kazi kwa bidii na kusali kuhusu hilo kwa wiki moja na kisha anipigie simu. Wiki moja baadaye, mara moja, alipiga. Bado alitaka kurudi nyumbani. Nilimshauri tena kusali, kufanya kazi kwa bidii, na kunipigia ndani ya wiki. Katika usahili wetu uliofuata, mambo hayakubadilika. Bado alisisitizakurudi nyumbani.

Sikuwa tayari kuruhusu hili lifanyike. Nilianza kumfundisha kuhusu asili takatifu ya wito wake. Nilimtia moyo “ajisahau [yeye mwenyewe] na afanye kazi.”2 Lakini bila kujali kanuni yoyote niliyotoa, mawazo yake hayakubadilika. Hatimaye ilinijia kwamba naweza kuwa sina picha kamili. Ndipo hapo nilihisi msukumo kumuuliza swali: “Mzee, nini kigumu kwako?” Kile alichosema kiligusa moyo wangu: “Rais, Siwezi kusoma.”

Ushauri wa busara niliodhani ni wa muhimu sana kwake kusikia haukua sawasawa na mahitaji yake. Alichohitaji zaidi ilikuwa ni mimi kuangalia zaidi ya makadirio yangu ya haraka na kuruhusu Roho anisaidie kuelewa kile hasa kilichokuwa katika mawazo ya mzee huyu. Alinihitaji nimuone kwa usahihi na kutoa sababu ya tumaini. Badala yake, nilifanya kama mpira mkubwa wenye kubomoa. Mzee huyu hodari alijifunza kusoma na akawa mfuasi safi sana wa Yesu Kristo. Alifungua macho yangu kwenye maneno ya Bwana: “Maana mwanadamu hutazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo” (1 Samweli 16:7).

Ni baraka iliyoje wakati Roho wa Bwana anapopanua mtazamo wetu. Kumbuka nabii Elisha alipoamka na kukuta jeshi la Asheri limezunguka jiji lake na farasi na magari yao. Mtumishi wake wa kiume alipata hofu na akamuuliza Elisha wangefanya nini dhidi ya tukio lile. Elisha alimwambia aondoe hofu kwa maneno ya kukumbukwa: “Usiogope:maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao” (2 Wafalme 6:16).Mtumishi wa kiume hakujua kile nabii alikuwa akiongelelea. Hakuweza kutazama zaidi ya kile alichoweza kuona. Hata hivyo, Elisha aliona jeshi la malaika waliojiandaa kupigana kwa ajili ya watu wa nabii. Hivyo Elisha aliomba kwa Bwana kufungua macho ya kijana mdogo, “naye akaona: na, tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote” (2 Wafalme 6:17).

Elisha na jeshi la mbinguni

Mara nyingi sisi hujitenga na wengine kwa tofauti kwenye kile tunachoona. Tunajisikia vizuri kati ya wale wanaofikiri, kuongea, kuvaa, na kutenda kama sisi na vibaya kwa wale wanaotoka katika mazingira au historia tofauti. Kiuhalisia, je, sisi sote hatutoki katika nchi tofauti na kuongea lugha tofauti? Je, hatuoni ulimwengu kupitia vikomo vikubwa vya uzoefu wetu wenyewe wa maisha? Kwani baadhi huona na kuongea kwa macho ya kiroho, kama nabii Elisha, na baadhi huona na kuwasiliana kwa kutazama kama nilivyokuwa na mmisionari asiyejua kusoma.

Tunaishi katika ulimwengu ambao hushiba kwenye kujilinganisha, kubandika nembo, na kukosoa. Badala ya kuona kupitia lenzi ya mitandao ya kijamii, tunahitaji kuangalia ndani kwa sifa za uungu ambazo kila mmojahuzistahili. Sifa hizi za uungu na shauku haziwezi kusambazwa kwenye Pinterest au Instagram.

Kuwakubali na kuwapenda wengine haimaanishi kukumbatia mawazo yao. Ni dhahiri, ukweli huhitaji utiifu wetu mkuu, japo haitakiwi kamwe kuwa kikwazo kwa ukarimu. Kupenda wengine kikweli huhitaji mazoezi endelevu ya kukubali juhudi nzuri ya watu ambao uzoefu wa maisha na mipakayao hatuwezi kujuakwa undani. Kutazama zaidi yatunachoweza kuona huitaji kufahamu kwa kulenga kwa Mwokozi.

Gari la mazingira yote

Mnamo Mei 28, 2016, Beau Richie wa miaka 16 na Austin rafiki yake walikuwa katika shamba la mifugo la familia yao kule Colorado. Beau na Austin walipanda ndani ya gari lao kwa matarajio makubwa ya siku ya tukio la ajabu. Hawakuwa wamekwenda mbali walipokabiliwa na hali za hatari, ambapo janga lilipiga. Gari alilokuwa akiendesha Beau lilibingirika kwa ghafla, likimbana Beau chini ya paundi 400 (180 kg) za chuma. Wakati Austin rafiki ya Beau alipomfikia, alimwona Beau akihangaika kujiokoa. Kwa kila nukta ya nguvu zake, alijaribu kuvuta gari kulitoakwa rafiki yake. Halikusonga. Aliomba kwa ajili ya Beau kisha kwa majonzi akaenda kutafuta msaada. Watu wa huduma za dharura hatimaye walifika, lakini masaa machache baadaye Beau alifariki. Alipumzishwa kutoka maisha haya ya dunia.

Wazazi wake waliovunjika mioyo walifika. Walipokuwa wamesimama ndani ya hospitali ndogo na rafiki mpendwa wa Beau na familia, afisa wa polisi aliingia chumbani na alimpa mama yake Beau simu ya mwanae. Alipochukua simu, kengele ya kusikika iliita. Alifungua simu na kuona kengele ya kila siku ya Beau. Alisoma kwa sauti ujumbe wa kijana wake mpenda burudani, na matukio ya ajabu aliouweka kusoma kila siku. Ulisema, “Kumbuka kumweka Yesu Kristo kama kitovu cha maisha yako leo.”

Kulenga kwa Beau kwa Mkombozi wake hakupunguzi huzuni ya wapendwa wake katika kutokuwepo kwake. Hata hivyo, kulitoa tumaini kubwa na maana kwa maisha ya Beau na chaguzi zake maishani. Kuliruhusu familia yake na marafiki kutazama zaidi ya huzuni ya kifo chake cha mapema kwa uhalisia wa furaha ya maisha yajayo. Ni huruma ororo iliyoje kwa wazazi wa Beau kuona kupitia macho ya kijana wao jambo alilolipa thamani kubwa.

Kama waumini wa Kanisa, tumezawadiwa kengele zetu binafsi za kiroho ambazo hutuonyapale tunapoangalia tu kwa macho ya kimwili mbali na wokovu. Sakramenti ni ukumbusho wetu kila wiki wa daima kulenga kwa Yesu Kristo kwamba daima tumkumbuke Yeye na kwamba daima Roho Wake apate kuwa nasi (ona M&M 20:77). Bado wakati mwingine tunapuuza hisia hizi za ukumbusho na kengele. Tunapokuwa na Yesu Kristo kwenye kitovu cha maisha yetu, atafanya kwamba macho yetu yafumbuliwe kwa uwezekano mkubwa kuliko sisi peke yetu tunavyoweza kufahamu.

Nilipokea barua hii ya kupendeza sana kuhusu kengele ya ulinzi iliyotokea kwa dada mwaminifu. Aliniambia kwamba katika juhudi zake kumsaidia mume wake kuelewa alivyohisi, alianza kuweka orodha ya kielektroniki katika simu yake ya vitu alivyofanya au kusema vilivyomuudhi. Alisema kwamba kwa wakati muafaka, angekuwa ameweka ushahidi wa maandishi ambao angeshiriki naye ambao kwamba ungemfanya atake kubadili njia zake. Hata hivyo, Jumapili moja wakati wa kupokea sakramenti na kulenga kwenye Upatanisho wa Mwokozi, aligundua kwamba kuweka hisia zake mbaya kuhusu mume wake ilikuwa kweli kumfukuza Roho kutoka kwake na haingembadilisha mumewe.

Kengele ya kiroho ilipiga ndani ya moyo wake ambayo ilisema: “Achana nayo, achana nayo yote. Futa maelezo hayo. Hayana msaada.” Kisha aliandika, na nanukuu: “Ilinichukua muda kubonyeza ‘chagua zote’ na hata muda zaidi kubonyeza ‘futa.’ Lakini, nilipofanya hivyo, hisia zote zilizokuwa mbaya zilitoweka kabisa. Moyo wangu ulijaa upendo—upendo kwa mume wangu na upendo kwa Bwana. Kama Sauli katika njia ya Dameski, yeye alipata ono lake kubadilika. Vipimo vya upotoshaji viliondoka machoni pake.

Mwokozi kila mara alifumbua macho ya vipofu kimwili na kiroho. Kufumbua macho yetu kwenye kweli takatifu, kiuhalisia na kwa kistiari, hutuandaa kuponywa kutokana na kutoona mbali. Tunapotilia maanani “kengele” za kiroho ambazo huashiria hitaji la marekebisho ya njia au mtazamo mkubwa wa milele, tunapokea ahadi ya sakramenti kuwa na Roho Wake pamoja nasi. Hii ilitokea kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland ambapo kweli za kushawishi zilifundishwa na Yesu Kristo aliyeahidi kwamba “pazia” la na vikwazo vingeondolewa kutoka akilini [mwao], na macho [yao] ya ufahamu yangefunguliwa” (M&M 110:1).

Ninatoa ushahidi kwamba kupitia nguvu ya Yesu Kristo, tunakuwa na uwezo wa kutazama kiroho zaidi ya tunavyoona kiuhalisia. “Tunapomkumbuka Yeye na kuwa na Roho Wake pamoja nasi, macho yetu ya ufahamu yatafumbuliwa Kisha uhalisia mkuu wa uungu ulio ndani ya kila mmoja wetu utavutiwa kwa nguvu zaidi juu ya mioyo yetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Kutoka kwa The Lion King 1½ (2004); nje ya Amerika Kazikazin, inajulikana kama The Lion King 3: Hakuna Matata.

  2. Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinckley (2016), 201.