Tafuteni Kutoka kwenye Vitabu Vizuri
Tunaposoma kutoka vitabu bora, tunajilinda dhidi ya mataya hatari ya wale wanaotafuta kutafuna mizizi yetu ya kiroho.
Mapema asubuhi moja, niliona kiwavi kilichokuwa na njaa na kilichojificha kijanja katika kichaka kizuri cha waridi. Kwa muonekano wa baadhi ya mimea isiyo na majani, ilikuwa dhahiri hata kwa mtazamaji asiye makini kuwa kilikuwa kikitafuna kuelekea kwenye matawi laini kwa kutumia mataya yake hatari.Kiistiari, sikuweza kujizuia kufikiria kwamba kuna baadhi ya watu ambao ni kama viwavi hawa; wanapatikana duniani kote, na wengine wamejificha kwa ujanja kiasi kwamba tunaweza tukawaruhusu katika maisha yetu, na kabla hatujatambua, wanakuwa wamekwisha kula mizizi yetu ya kiroho na ile ya wanafamilia na marafiki zetu.
Tunaishi katika kipindi ambacho upotovu kuhusu imani zetu umeenea. Katika nyakati kama hizi, kushindwa kulinda na kuimarisha mizizi yetu kiroho ni mwaliko kufanya itafunwe na wale wanaotafuta kuangamiza imani yetu katika Kristo na imani yetu katika Kanisa Lake la urejesho. Katika nyakati za Kitabu cha Mormoni, alikuwa ni Zeezromu aliyetaka kuangamiza imani ya waumini.
Maneno na matendo yake yalikuwa “ni mtego wa adui, ambao ameutega … ili awanase watu hawa, ili awatie [wao] katika utumwa wake, ili awazingire [wao] na minyororo yake” (Alma 12:6). Mitego kama hiyo ipo leo, na isipokuwa tujihadhari kiroho na kujenga msingi dhabiti juu ya Mkombozi wetu (ona Helamani 5:12), tunaweza kujikuta tumezingwa na minyororo ya Shetani na kupelekwa chini kwa makini kwenye njia zilizozuiliwa zilizosemwa katika Kitabu cha Mormoni (ona 1 Nefii 8:28).
Mtume Paulo alitoa onyo katika siku zake ambalo linafaa katika kipindi chetu: “Najua mimi ya kuwa, …katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao” (Matendo ya Mitume 20:29–30).
Onyo lake na yale ya manabii wetu na mitume hutukumbusha kuwa lazima tufanye yote tuwezayo kujihami kiroho dhidi ya maneno ya upinzani na udanganyifu. Ninapotembelea kata na vigingi vya kanisa, ninainuliwa na kile ninachoona, ninachosikia, na kuhisi pale watakatifu wanapopokea kwa uaminifu na wema kabisa mafundisho ya Mwokozi na watumishi Wake.
Ongezeko la kuzingatia siku ya Sabato ni mfano mmoja tu wa waumimi wanaojihami kiroho kwa kutilia maanani mwaliko wa kinabii. Kuimarika zaidi kunathibitishwa katika kuongezeka kwa kazi za hekalu na historia ya familia, wanafamillia wanapokusanya mababu zao kupitia ibada za hekaluni. Mizizi yetu kiroho huenda chini pale ambapo sala za dhati binafsi na za familia zinapokuwa misingi ya imani yetu, na tunapotubu kila siku, kutafuta ushirika wa Roho Mtakatifu, na kujifunza kuhusu Mwokozi wetu na sifa Zake na kujitahidi kuwa kama Yeye (Ona 3 Nefi 27:27).
Mwokozi wetu, Yesu Kristo, ni Nuru ya Dunia, na anatuita tumfuate Yeye. Yatupasa kumtazama Yeye wakati wote na hususani kama kuna usiku wa giza na dhoruba ambapo tufani la shaka na kutokuwa na uhakika, kama ukungu unaozangaa, uingiapo ndani. Lazima vidole vinavyonyooshwa kutoka “ng’ambo nyingine ya mto wa maji, [ambapo] jengo kubwa na pana [lipo]” (1 Nefi 8:26) vikionekana kuelekezwa kwako katika mtazamo wa kudhihaki, kudharau, na kuita, naomba kwamba ugeuke mara moja ili kwamba usishawishike na hila na namna ovu kujitenga na ukweli na baraka zake.
Hata hivyo, hili pekee halitatosha katika siku hii wakati vitu kaidi vinaongelewa, kuandikwa, na kusimuliwa. Mzee Robert D. Hales alitufundisha kwamba “Isipokuwa mmejihusisha kiufasaha katika kuishi injili—kuiishi kwa mioyo yenu yote, uwezo, akili na nguvu—humwezi kuzalisha nuru ya kiroho ya kutosha kushinikiza nyuma giza” (“Out of Darkness into His Marvelous Light,” Liahona, July 2002, 78). Hakika, tamaa yetu kumfuata Kristo, ambaye ni Nuru ya Dunia (ona Yohana 8:12), ina maana tunapaswa kufanyia kazi mafundisho Yake. Tunaimarishwa kiroho, na kulindwa tunapofanyia kazi neno la Mungu.
Kadiri mwanga unavyoongezeka katika maisha yetu, ndivyo kuna vivuli vichache. Hata hivyo, hata katika mwanga mwingi tunawekwa wazi kwa watu na maoni ambayo hayawakilishi imani yetu na kujaribu imani yetu. Mtume Yakobo aliandika kwamba “kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi” (Yakobo 1:3). Kwa ufahamu huu, Mzee Neal A. Maxwell alifundisha kwamba “Mfuasi mvumilivu … hatashangaa wala kupotoka wakati Kanisa linasemwa vibaya” (“Uvumilivu” [Ibada katika Chuo Kikuu cha Brigham Young, Nov. 27, 1979], speeches.byu.edu).
Maswali kuhusiana na historia ya Kanisa letu na imani hutokea. Pale tunapogeukia kutafuta majibu sahihi huhitaji umakinifu mkubwa. Hakuna tunachopata katika kupeleleza mitazamo na maoni ya wenye habari ndogo au wenye kupoteza imani.Ushauri bora uliotolewa na Mtume Yakobo: “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MunguYakobo 1:5).
Kumuuliza Mungu inapaswa kutanguliwe na kusoma kwa makini, kwani tupo chini ya jukumu la kimaandiko kutafuta “kutoka kwenye vitabu vizuri maneno ya hekima” na “kutafuta maarifa hata kwa kujifunza na pia kwa imani’ (M&M 88:118). Kuna utajiri mwingi wa vitabu hivi, vilivyoandikwa na viongozi wa kanisa waliongozwa na mbingu na wasomi wenye kutambuliwa, salama, na kuaminika wa historia ya kanisa na mafundisho. Na kwa kusema hilo, hakuna kinachopita utukufu wa neno la Mungu lililofunuliwa katika maandiko matakatifu.Kutoka katika hizo kurasa nyembamba zenye unene wa ufahamu wa kiroho, tunajifunza ukweli kupitia Roho Mtakatifu na hivyo ongezeko la mwanga.
Rais Thomas S. Monson ametusihi “sisi tujifunze kwa maombi na kutafakari Kitabu cha Mormoni kila siku” (“The Power of the Book of Mormon,” Liahona, Mei 2017, 87).
Miaka mingi iliyopita, wakati nilipokuwa nikihudumu kama Rais wa Misheni ya Fiji Suva, baadhi ya wamisionari walikuwa na uzoefu ambao uliwaimarisha kindani na nguvu ya kuongoa ya Kitabu cha Mormoni. Siku yenye joto na unyevunyevu, wazee wawili walifika katika nyumba katika sehemu ndogo ya makazi huko Labasa.
Mbisho katika mlango ulijibiwa na mtu dhaifu ambaye alisikiliza wakati wamisionari wakishuhudia ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Walimpatia nakala na kumualika kusoma na kusali ili kujua, kama wao, kama ni neno la Mungu. Jibu lake lilikuwa fupi: “Kesho nitarudi kuvua. Nitakisoma nikiwa baharini, na nikirudi, mnaweza kunitembelea tena.”
Alipokuwa mbali, mabadiliko yalifanyika, na juma chache baadae, wazee wenzi wapya walirudi kumtembelea mvuvi. Kwa wakati huu alikuwa amesoma Kitabu cha Mormoni chote alikuwa amepata uthibitisho wa ukweli wake na alikuwa na hamu ya kujifunza zaidi.
Huyu mtu aliongoka kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alishuhudia ukweli wa maneno ya thamani katika kila kurasa ya matukio na mafundisho yaliyofundishwa kitambo sana na kuhifadhiwa kwa siku yetu katika Kitabu cha Mormoni. Baraka hii ipo kwa kila mmoja wetu.
Nyumbani ni mahali sahihi kwa familia kujifunza na kushiriki ufahamu wa thamani kutoka katika maandiko, na maneno ya manabii na kupata vifaa vya kanisa katika LDS.org. Hapo utapata taarifa nyingi kuhusu mada za injili kama vile simulizi za Ono la Kwanza. Tunaposoma kutoka vitabu bora, tunajilinda dhidi ya mataya hatari ya wale wanaotafuta kutafuna mizizi yetu ya kiroho.
Kwa sala zetu zote, kujifunza, na kutafakari, pia kunaweza kubaki baadhi ya maswali yapaswayo kujibiwa, lakini hatupaswi kuacha hilo kuzima moto wa imani unaowakawaka ndani yetu. Maswali hayo ni mwaliko wa kujenga imani yetu na haipaswi kuchochea wakati wa kupita wenye shaka danganyifu. Ni kiini haswa cha dini, sio kuwa na jibu kamili kwa kila swali, kwani hili ndilo lengo moja la imani. Kwa hilo, Mzee Jeffrey R. Holland alitufundisha kwamba “kipindi nyakati hizo zinakuja na masuala yanatanda, maamuzi ambayo hayapatikani kwa mara moja, shikilia sana kile ambacho umekwisha fahamu na simama imara hadi ufahamu wa ziada utakapokuja”(“Lord, I Believe,”au Liahona, May 2013).
Tunaona tukizingirwa na furaha za wengi ambao wanasimama imara kwa kulisha daima mizizi yao kiroho. Imani yao na utii ni tosha kuwapatia tumaini kuu katika Mwokozi, na kutoka katika hayo huchipuka furaha kubwa. Hawasemi wanajua kila kitu, lakini wamelipa gharama kujua kiasi cha kuwawezesha kuwa na furaha na kuishi kwa uvumilivu wakiwa wanatafuta kujua zaidi.Mstari juu ya mstari, imani yao inaimarika katika Kristo, na wanasimama imara kama wenyeji pamoja na watakatifu.
Hebu kila mmoja wetu aishi ili kwamba mataya hatari ya viwavi waliojificha kijanja wasipate nafasi, si sasa au baadae, katika maisha yetu ili kwamba tubaki “imara katika imani ya Kristo, hata mpaka mwisho” (Alma 27:27). Katika jina la Yesu Kristo, amina