2010–2019
Nguvu ya Kitabu cha Mormoni
Aprili 2017


3:27

Nguvu ya Kitabu cha Mormoni

Mimi ninamsihi kila mmoja wetu kwa maombi kujifunza na kutafakari Kitabu cha Mormoni kila siku.

Wapendwa kaka na dada zangu, nawasalimu kwa moyo mkunjufu tunapokutana tena katika mkutano mkuu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kabla ya kuanza ujumbe wangu rasmi leo hii, ningependa kutangaza mahekalu matano mapya ambayo, yatajengwa katika maeneo yafuatayo: Brasília, Brazili; eneo la Manila, Philippines; Nairobi, Kenya; Pocatello, Idaho, Marekani; na Saratoga Springs, Utah, Marekani.

Asubuhi hii Ninazungumza kuhusu nguvu ya Kitabu cha Mormoni na hataji muhimu tulilonalo kama waumini wa Kanisa la kujifunza, kutafakari, na kuishi mafundisho yake katika maisha yetu. Umuhimu wa kuwa na ushuhuda thabiti na wa kweli juu ya Kitabu cha Mormoni hauwezi tiwa chumvi.

Tunaishi katika kipindi cha matatizo na uovu mkubwa. Ni kitu gani kitatulinda kutokana na dhambi na maovu yaliyomo duniani leo? Ninasisitiza kwamba ushuhuda imara wa Mwokozi, Yesu Kristo, na Injili Yake vitatusaidia kuwa salama. Kama hausomi Kitabu cha Mormoni kila siku, tafadhali fanya hivyo. Kama utakisoma kwa maombi na dhamira ya dhati kujua ukweli, Roho Mtakatifu atakushuhudia ukweli wake. Kama ni cha kweli—na nashuhudia hivyo—basi Joseph Smith alikuwa ni nabii aliyemuona Mungu Baba na Mwanae, Yesu Kristo.

Kwa sababu Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni Kanisa la Bwana duniani, na ukuhani mtakatifu wa Mungu umerejeshwa kwa manufaa na baraka za watoto Wake.

Kama hauna ushuhuda imara wa vitu hivi, fanya kile kinachohitajika kuupata. Ni muhimu kwako kuwa na ushuhuda binafsi katika nyakati hizi ngumu, kwani shuhuda za wengine zitakubeba kwa wakati tu. Hata hivyo, ukishapatikana, ushuhuda unapaswa kutunzwa vizuri na utakuwa hai kwa kuendelea kutii amri za Mungu na sala za kila siku na kujifunza maandiko.

Washirika wenzangu katika kazi ya Bwana, nawasihi kila mmoja wetu tujifunze kwa maombi na kutafakari Kitabu cha Mormoni kila siku. Na tukifanya hivyo, tutakuwa katika hali ya kusikia sauti ya Roho, kushinda majaribu, kukabili hofu na woga, na kupokea msaada wa mbinguni katika maisha yetu. Nashuhudia hivyo kwa moyo wangu wote, katika jina la Yesu Kristo, amina.