Kizazi Kinzani kwa Dhambi
Mnapofundisha, kuongoza, na kuwapenda watoto, mnaweza kupokea ufunuo binafsi ambao utawasaidia kutengeneza na kujenga watoto hodari kinzani kwa dhambi.
Mwaka mmoja na nusu uliopita, Rais Russell M. Nelson aliongea juu ya haja ya kufundisha na kusaidia kuinua kizazi kinzani kwa dhambi.”1 Kishazi — “kizazi kinzani kwa dhambi” yaligonga noti za kiroho ndani yangu.
Tunawaheshimu watoto ambao wanajitahidi kuishi maisha masafi na ya utiifu. Nimeshuhudia nguvu ya watoto wengi duniani kote. Wanasimama imara, “thabiti na wasiotingishika”2 katika hali ya changamoto na mazingira tofauti. Watoto hawa wanaelewa asili yao takatifu, huhisi upendo wa Baba wa Mbinguni, na hutafuta kutii mapenzi Yake.
Hata hivyo, kuna watoto wanaong’ang’ana kusimama “thabiti na wasiotingishwa” na ambao akili zao changa zinajeruhiwa.3 Wanashambuliwa kila upande kwa “mishale ya moto ya adui”4 na wako katika hitaji la kutiwa moyo na kusaidiwa Wao ni msukumo mkubwa kwetu kuingilia kati na kupigana vita dhidi ya dhambi katika juhudi zetu za kuleta watoto wetu kwa Kristo.
Sikiliza maneno ya Mzee Bruce R. McConkie karibu miaka 43 iliyopita:
“Kama waumini wa kanisa, tunajihusisha na mapambano makuu. Tuko vitani. Tumejiunga na Kristo kupigana dhidi ya Lusiferi. …
“Vita kuu vinavuma kila upande na ambayo kwa bahati mbaya husababisha majeruhi wengi, wengine kufa, sio kitu kipya. …
Sasa hakuna na hakuwezi kuwepo kutopendelea upande wowote katika vita hivi.”5
Hivi leo vita vinaendelea kwa kiwango cha juu. Vita vinatugusa sote, na watoto wetu wapo mstari wa mbele wakitazama majeshi yanayokinzana. Hivyo, kuna haja kwetu kuzidisha na kutia nguvu zaidi mikakati yetu ya kiroho.
Kuimarisha watoto kuwa kinzani kwa dhambi ni jukumu na baraka kwa wazazi, bibi na babu, wanafamilia, walimu, na viongozi. Sote tunabeba jukumu la kusaidia. Hata hivyo, Bwana kwa mahususi amewaelekeza wazazi kuwafunza watoto wao “kuelewa injili ya toba, imani katika Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, na ya ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu” na “kuomba, na kutembea wima mbele za Mungu.”6
Jinsi ya “kuwalea watoto [wetu] katika nuru na kweli”7 yaweza kuwa swali la changamoto kwani ni swala binafsi kwa kila familia na kila mtoto, lakini Baba wa Mbinguni ametupa miongozo ya jumla ambayo itatusaidia. Roho atatuvuvia katika njia sahihi tunazoweza kuwakinga watoto wetu kiroho.
Kwanza, kuwa na ono la umuhimu wa jukumu hili ni muhimu. Lazima tuelewe asili yetu—na yao—takatifu na lengo kabla ya kuweza kuwasasidia watoto wetu kuona wao ni nani na kwa nini wako hapa. Lazima tuwasaidie kujua bila shaka kwamba wao ni wana na mabinti wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo na kwamba ana matarajio matakatifu toka kwao.
Pili, kuelewa injili ya toba ni muhimu ili kuwa kinzani kwa dhambi. Kuwa kinzani kwa dhambi haimaanishi kutokuwa na dhambi, lakini humaanisha ni kuendelea kutubu siku zote, kuwa mwangalifu, na hodari. Pengine kuwa kinzani kwa dhambi huja kama baraka kwa kuepuka dhambi mara kwa mara. Kama Yakobo alivyosema, “Mpingeni shetani, naye atawakimbia.”8
Vijana jasiri “walikuwa hodari sana kwa ujasiri … ; lakini tazama hii haikuwa yote—walikuwa … watu wa ukweli wakati wote kwa kitu chochote ambacho walikabidhiwa. Ndio, … walikuwa wamefundishwa kutii amri za Mungu na kutembea wima mbele yake.”9 Hawa vijana wadogo walikwenda vitani wakiwa wamebeba wema wa Kristo kama silaha dhidi ya maadui zao. Rais Thomas S. Monson alitukumbusha ya kwamba “mwito wa kuwa na ujasiri huja mara kwa mara kwa kila mmoja wetu. Kila siku ya maisha yetu ujasiri unahitajika—sio tu kwa matukio yale makuu lakini mara nyingi wakati tunapofanya maamuzi au tunapojibu hali karibu nasi.”10
Watoto wetu wanajivika dereya ya kiroho wanapodumisha mpangilio wa uanafunzi wa kila siku. Pengine hatutilii maanani uwezo wa watoto kuelewa kanuni ya ufuasi wa kila siku . Rais Henry B. Eyring alitushauri “kuanza mapema na kuwa imara.”11 Kwa hiyo kanuni ya tatu kuwasaidia watoto kuwa kinzani kwa dhambi ni kuanza katika umri mdogo kwa upendo kufundisha kanuni muhimu za injili- kutoka kwenye maandiko matakatifu, Makala ya Imani, kijitabu cha Kwa Nguvu za Vijana , nyimbo za Msingi, nyimbo za kanisa, na shuhuda zetu binafsi—ambazo zitawaongoza watoto kwa Mwokozi.
Kukuza tabia endelevu ya sala, kusoma maandiko, jioni ya familia nyumbani, na kuabudu siku ya sabato huongoza kwenye ukamilifu, msimamo wa ndani, na utashi imara wa thamani—kwa maneno mengine, nguvu ya kiroho. Katika dunia ya leo, ambapo uadilifu umepotea kabisa, watoto wetu wanastahili kuelewa upi ni uadilifu wa kweli na kwa nini ni muhimu—hasa tunapowaandaa kuweka na kutunza maagano matakatifu wakati wa ubatizo na hekaluni. Kama Hubiri Injili Yangu inavyofundisha, “Kutunza ahadi huwaandaa watu[ikijumuisha vijana wadogo kabisa] kufanya na kutunza maagano matakatifu.”12
Mzee Jeffrey R. Holland amefundisha, “Tunapoongelea kuhusu kutunza maagano, tunaongelea kuhusu moyo na nafsi ya lengo letu katika maisha ya duniani.”13 Kuna nguvu isiyo ya kawaida katika kufanya na kutunza maagano na Baba yetu wa Mbinguni. Mjaribu analijua hili, hivyo amevuruga kanuni ya kufanya maagano.14 Kuwasaidia watoto kuelewa, kufanya, na kutunza maagano matakatifu ni umuhimu mwingine katika kutengeneza kizazi kinzani kwa dhambi.
Tunawaandaaje watoto wetu kufanya na kutunza maagano matakatifu wanapoingia na kuendelea katika njia ya agano? Kuwafundisha watoto kutunza ahadi ndogo ndogo wakiwa wadogo kutawawezesha wao kutunza maagano matakatifu baadae maishani.
Wacha nishiriki mfano rahisi: Katika jioni ya familia nyumbani, baba aliuliza, “Tuna mahusiano gani kama familia?” Lizzie mwenye umri wa miaka mitano alilalamika kwamba kaka yake mkubwa, Kevin, alikuwa akimtania sana na kuumiza hisia zake. Kevin kwa kusita alikiri kwamba Lizzie alikuwa sahihi. Mama yake Kevin alimuuliza angefanya nini kuelewana vizuri zaidi na dada yake. Kevin alifikiria na kuamua angemuahidi Lizzie kwamba angemaliza siku nzima bila kumtania.
Mwisho wa siku iliyofuata wakati kila mmoja alipokusanyika kwa maombi ya familia, baba ya Kevin alimuuliza Kevin jinsi alivyofanya. Jibu la Kevin lilikua “Baba, Nimetunza ahadi yangu!” Lizzie alikubali kwa furaha na familia ilimpongeza Kevin.
Mama yake Kevin kisha akapendekeza kwamba kama aliweza kutunza ahadi yake kwa siku moja, kwa nini asiweze kufanya kwa siku mbili? Kevin alikubali, kujaribu tena. Siku mbili zilipita, Kevin alikuwa amefanikiwa kutunza ahadi yake, na lizzie alikuwa na shukrani zaidi! Baba yake alipouliza kwa nini alitunza ahadi zake vizuri, Kevin alisema, “Nilitunza ahadi yangu kwa sababu nilisema ningetunza.”
Mfululizo wa ahadi ndogo zinazotunzwa vizuri huongoza kwenye uadilifu. Tabia endelevu ya kutunza ahadi ni maandalizi ya kiroho kwa watoto kupokea agano lao la kwanza la ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu, ambapo wanaagana kumtumikia Mungu na kutii amri Zake.15 Ahadi na maagano hayatenganishwi.
Katika kitabu cha Danieli tunajifunza juu ya Shadraki, Meshaki na Abed-nego wakikataa kuabudu sanamu ya Mfalme Nebukadreza.16 Mfalme aliwaonya kwamba wangetupwa kwenye tanuru iwakayo moto kama wasingetii. Walikataa na wakasema:
“Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto …
“Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako.”17
“Bali kama si hivyo.” Fikiria maana ya maneno haya matatu na jinsi yanavyohusiana na kutunza maagano. Hawa vijana watatu hawakuweka utiifu wao katika kukombolewa. Hata kama wasingekombolewa, wangetunza ahadi yao kwa Bwana kwa sababu walisema wangetunza. Kutunza maagano yetu daima hakubadiliki kutegemea hali zetu. Hawa vijana watatu, kama vile vijana jasiri, ni mifano ya kupendeza kwa watoto wetu wanaokinzana na dhambi.
Jinsi gani mifano hii hutumika nyumbani kwetu na kwa familia zetu? “Mstari juu ya mstari, kanuni juu ya kanuni,”18 tunawasaidia watoto kuonja mafanikio katika ming’ato midogo. Wanapotunza ahadi zao, wanahisi Roho katika maisha yao. Mzee Joseph B. Wirthlin alifundisha kwamba “Zawadi timilifu ya uadilifu ni kuwa na Roho Mtakatifu daima.”19 Ndipo “kujiamini kwa watoto wetu kutakuwa imara katika uwepo wa Mungu.”20 Kutoka kisima cha uadilifu huja kizazi kinzani kwa dhambi chenye nguvu.
Akina kaka na dada, wawekeni wachanga wenu karibu—karibu sana kwamba waone tabia yenu ya dini kila siku na wawaone mkitunza ahadi na maagano yenu. “Watoto ni waigaji wakubwa, hivyo wapeni kitu kikuu cha kuiga.”21 Kwa kweli tunasaidia kufundisha na kukuza kizazi kinzani kwa dhambi kwa Bwana ahadi kwa ahadi na agano kwa agano.
Ninashuhudia kwamba Yesu Kristo huongoza Kanisa hili. Mnapofundisha, kuongoza, na kupenda watoto katika njia ya Mwokozi, mnaweza kupokea ufunuo binafsi ambao utawasaidia kutengeneza na kujenga watoto hodari kinzani kwa dhambi. Ombi langu ni kwamba watoto wetu watarudia maneno ya Nefi: “Je, utanifanya kwamba nitetemeke nikiona dhambi?22 Ninashuhudia kwamba Mwokozi wetu alifanya upatanisho kwa dhambi za ulimwengu23—kwa sababu alisema angefanya, na kwamba anatupenda kuliko sisi wenye kufa tunavyoweza kufikiria24—kwa sababu alisema angetupenda. Katika jina la Yesu Kristo, amina.