2010–2019
Jinsi Gani Roho Mtakatifu Anaweza Kukusaidia Wewe?
Aprili 2017


15:25

Jinsi Gani Roho Mtakatifu Anaweza Kukusaidia Wewe?

Roho Mtakatifu huonya, Roho Mtakatifu hufariji, na Roho Mtakatifu hushuhudia.

Jioni ya Jumatatu moja sio muda mrefu uliopita, mke wangu, Lesa, nami tulipitia nyumbani kwa familia changa katika mtaa wetu. Wakati tulipokuwa pale, familia ilitualika tukae kwa ajili ya jioni wa familia nyumbani, wakituambia kijana wao wa miaka tisa alikuwa ameandaa somo. Hakika, tulikaa!

Kufuatia wimbo wa kufungua, sala, na shughuli za kifamilia, kijana wa miaka tisa alianza kwa kusoma swali lenye  umaizi lililojumuishwa kwa somo lake aliloandika kwa mkono: “Jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia wewe?” Swali hili lilianzisha majadiliano ya maana ya kifamilia wakati kila mmoja alishirikisha mawazo na umaizi wake. Nilivutiwa na maandalizi ya somo ya mwalimu wetu na swali lake zuri sana, ambalo lilinichochoea tena na tena.

Somo la jioni ya familia nyumbani lililoandikwa kwa mknono

Tangu wakati huo, nimeendelea kujiuliza mwenyewe, “Jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia Wewe?”—swali hususani linawahusu watoto wa Msingi wanaoingia umri wa miaka nane na wanajitayarisha kwa ubatizo na kwa watoto wale ambao hivi karibuni wamebatizwa na wamepokea karama za Roho Mtakatifu Na pia linafaa kwa maelfu ya waongofu wa hivi karibuni.

Ninawaalika kila mmoja wetu, hususani watoto wa Msingi, kufikiria, “Jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia wewe?” Nilipotafakari swali hili, mara moja niliwaza juu ya uzoefu kutoka ujana wangu. Hii ni hadithi niliyomsimulia Mzee Robert D. Hales pindi baada ya wito wangu katika Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na ambayo alijumuisha katika makala ya gazeti la Kanisa aliyoiandika kuhusu maisha yangu.1 Baadhi yenu mmeweza kuwa mshasikia hadithi hii, lakini wengi hamjawahi.

Nilipokuwa na umri takribani miaka 11, baba yangu nami tulienda matembezi marefu siku ya majira ya joto katika milima karibu na nyumbani kwetu. Wakati baba alipopanda mwinuko mkali, niliruka kutoka kwa mwamba mmoja mkubwa kwenda mwingine, pembezoni mwa njia. Nikinuia kupanda moja ya miamba mikubwa, nilianza kupanda kwa shida mpaka juu yake. Wakati nafanya hivyo, nilishangazwa wakati baba yangu aliponinyakua kwa mkanda wangu na haraka kunivuta chini, akisema, “Usipande mwamba huo. Wacha tuu tubaki katika njia.”

Dakika chache baadaye, tulipoangalia chini kutoka juu zaidi ya njia, tulishangazwa tulipomwona nyoka hatari mkubwa akiota jua juu ya mwamba uleule niliounuia kupanda.

Baadaye, tulipokuwa ndani ya gari kurudi nyumbani, nilijua baba alikuwa ananingoja nimwulize, “Jinsi gani ulijua nyoka alikuwa pale?” Kwa hiyo niliuliza, na swali langu lilielekeza kwenye mjadala kuhusu Roho Mtakatifu na jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kutusaidia sisi. Kamwe sijasahau kile nilichojifunza siku ile.

Unaweza kuona jinsi Roho Mtakatifu alivyonisaidia? Mimi milele nashukuru kwamba baba yangu alisikiliza sauti ndogo, ya utulivu ya Roho Mtakatifu, kama ilivyoweza kuokoa maisha yangu.

Nini Tunachojua kuhusu Roho Mtakatifu

Kabla hatujafikiria zaidi swali “Jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia Wewe?” na turudie baadhi ya yale Bwana ametufunulia kuhusu Roho Mtakatifu. Kuna kweli nyingi za milele tungeweza kuziangalia, lakini leo nitasisitiza tatu tu.

Kwanza, Roho Mtakatifu ni mshirika wa tatu wa Uungu. Tunajifunza ukweli huu katika makala ya kwanza ya imani: “Tunaamini katika Mungu, Baba wa Milele, na katika Mwanawe, Yesu Kristo, na katika Roho Mtakatifu.”2

Pili, Roho Mtakatifu ni mtu wa Roho, kama ilivyoelezwa katika maandiko ya kisasa: “Baba ana mwili wa nyama na mifupa wenye kushikika kama wa mwanadamu; na Mwana vile vile; lakini Roho Mtakatifu hana mwili wa nyama na mifupa, bali ni mtu wa Kiroho. Kama isingekuwa hivyo, Roho Mtakatifu asingeweza kukaa ndani yetu.”3 Hii inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu ana mwili wa kiroho, tofauti na Mungu Baba na Yesu Kristo, wenye maumbile ya kimwili Ukweli huu unabainisha majina mwngine yaliyopewa kwa Roho Mtakatifu na yaliyozoeleka kwetu, pamoja na Roho Mtakatifu, Roho ya Mungu, Roho wa Bwana, Roho Mtakatifu wa Ahadi, na Mfariji.4

Tatu, Karama ya Roho Mtakatifu inakuja kwa kuwekewa mikono. Ibada hii, kufuatia ubatizo, inatuwezesha sisi daima kuwa na uenzi wa Roho Mtakatifu.5 Kufanya ibada hii, wenye Ukuhani wa Makizedeki wanaostahili wanaweka mikono yao juu ya kichwa cha mtu,6 anaitwa kwa jina lake, wanasema mamlaka ya Ukuhani wao, na katika jina la Yesu Kristo, kumdhibitisha kama muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, na kusema kishazi muhimu “Pokea Roho Mtakatifu.”

Jinsi Gani Roho Mtakatifu Anaweza Kukusaidia Wewe?

Pamoja na marejeo hayo rahisi ya kweli tatu muhimu kuhusu Roho Mtakatifu, tunarudi kwenye swali letu la kwanza: “Jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia wewe?”

Roho Mtakatifu Huonya

Kama nilivyoeleza uzoefu katika utoto wangu, Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia wewe kwa kukuonya mapema juu ya hatari za kimwili na kiroho. Nilijifunza tena wajibu muhimu wa kuonya wa Roho Mtakatifu wakati nilipohudumia katika Urais wa Eneo Japani.

Wakati huu, nilifanya kazi kwa karibu pamoja na Rais Reid Tateoka, wa misheni ya Sendai Japani. Kama sehemu ya utaratibu wake wa kawaida katika misheni, Rais Tateoka alipanga mkutano kwa viongozi wote wa sehemu ya kusini ya misheni yake. Siku chache kabla ya mkutano, Rais Tateoka alikuwa wazo, hisia katika moyo wake, kualika wote wamisionari wa ukanda ule wa kusini kwenye mkutano wa uongozi, badala ya idadi ndogo iliyoagizwa ya wazee na akina dada viongozi.

Alipotangaza nia yake, alikumbushwa kwamba mkutano huu haukukusudiwa kwa wamisionari wote bali tuu kwa viongozi wa misheni. Hata hivyo, kuweka mkutano wa namna ileile pembeni ili kufuata hisia alizopata, aliwaalika wamisionari wote wanaohudumia katika majiji kadha ya mwambao, pamoja na jiji la Fukushima, kwenye mkutano huo. Siku iliyochaguliwa, March 11,2011, wamisionari walikusanyika pamoja kwa mkutano wa misheni uliopanuliwa katika jiji la Koriyama la mikaoni.

Wakati wa mkutano huu, tetemeko la nchi lenye ukubwa wa 9.0 na tsunami vilipiga eneo la Japani ambako Misheni ya Sendai Japani ilipo. Kwa msiba, majiji mengi ya mwambao—pamoja na hayo ambayo wamisionari walikuwa wamekusanywa—yaliharibiwa na yalipatwa hasara kubwa ya vifo. Na jiji la Fukushima lilipata tukio la nyuklia kama matokeo.

Ingawa nyumba ya mkutano ambako wamisionari walikuwa wanakutana siku ile iliharibiwa na tetemeko la nchi, kupitia kufuata hisia za Roho Mtakatifu. Rais na Dada Tateoka na wamisionari wote walikusanika salama. Walikuwa mahali pa salama na maili nyingi kutoka na uharibifu wa tsunami na miale ya nyuklia.

Unapofuata hisia kutoka kwa Roho Mtakatifu—mawazo mara kwa mara kimya na tulivu—unaweza kutolewa, bila hata kujua, kutokana na hatari za kiroho na kimwili.

Akina kaka na akina dada, Roho Mtakatifu atawasaidia kwa kuwaonya, kama alivyomfanya baba yangu na Rais Tateoka.

Roho Mtakatifu Hufariji

Ili kuendelea kujibu swali “Jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia wewe?” wacha sasa tupeleleze wajibu Wake kama Mfariji. Matokeo yasiyotegemewa katika maisha yetu yote yanasababisha huzuni, maumivu, na masikitiko. Bado, miongoni mwa majaribu haya, Roho Mtakatifu anatuhudumia katika mojawapo wa kazi Zake muhimu—kama Mfariji, ambayo hasa ni mojawapo wa majina Yake. Maneno haya ya amani na kuhakikisha kutoka kwa Yesu Kristo yanaeleza jukumu hili takatifu. “Nitaomba kwa Baba , naye atawapa mfariji, ili akae nanyi daima hata milele.”7

Ili kuonesha hili zaidi, nashiriki taarifa ya kweli ya familia yenye wana watano waliohama kutoka Los Angeles, California Marekani, kwenda katika kijiji kidogo miaka kadha iliyopita. Vijana wawili wakubwa walianza kucheza michezo shule ya upili na kujiunga na marafiki, viongozi, na makocha—wengi kati yao walikuwa waumini waaminifu wa Kanisa. Mahusiano haya yalisaidia kuelekeza kwenye ubatizo wa Fernando, mkubwa wao na ndugu yake mdogo aliyefuata.

Fernando baadae alihamia mbali na nyumbani, ambako aliendelea na elimu yake na alicheza mpira wa miguu chuoni. Alifunga ndoa na kipenzi chake cha shule ya upili, Bayley, hekaluni. Kwa hamu walitarajia kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza—mtoto wa kike. Lakini wakati familia zao zilipokuwa zikimsaidia Fernando na Bayley kuhama kurudi nyumbani, Bayley na dada yake walikuwa wakiendesha gari na kuhusika katika ajali mbaya kwenye barabara huru na iliyohusisha magari mengi. Bayley na bintiye ambaye alikuwa hajazaliwa walifariki.

Fernando na Bayley

Bado pamoja na maumivu mazito yalivyokuwa kwa Fernando, pamoja na yale ya wazazi na ndugu, na ndivyo kilivyokuwa kina cha amani iliyotofautiana na faraja ambayo ilitiririka juu yao takribani wakati uleule. Roho Mtakatifu katika nafasi Yake kama Mfariji kwa kweli alimhimili Fernando kupitia mateso haya yasiyoeleweka. Roho anawasilisha amani ya kudumu ambayo ilimwongoza Fernando kwenye mtizamo wa kusamehe na upendo kwa kila mtu aliyehusika katika mgongano wa kifo.

Wazazi wa Bayley walimwita kaka yake aliyekuwa anahudumia kama mmisionari wakati wa ajali. Baadaye alielezea katika barua hisia zake baada ya kusikia taarifa ngumu ya mpendwa dada yake: “Ilikuwa kitu cha kushangaza kusikia sauti zenu zilizotulia katikati ya dhoruba. Sikujua nini cha kusema. …Yote niliyoweza kufikiria ni dada yangu hatakuwepo wakati nitakaporudi nyumbani  … Nilifarijiwa na ushuhuda wenu wenye uhakika wa Mwokozi na mpango Wake. Roho yuleyule wakupendeza ambaye hunileta kwenye ukingo wa machozi ninapojifunza na kufundisha amejazwa moyoni mwangu. Nikuwa nimefarijika na kukumbushwa vitu ambavyo navijua.8

Roho Mtakatifu atawasaidia kwa kuwafariji, kama alivyofanya kwa Fernando na familia ya Bayley.

Roho Mtakatifu Hushuhudia

Roho Mtakatifu pia hushuhudia na kutoa ushahidi wa Baba na Mwana na ukweli wote.9 Bwana, akizungumza na wafuasi Wake, alisema: “Lakini ajapo Mfariji, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba … yeye atanishuhudia.”10

Ili kueleza majukumu ya thamani ya Roho Mtakatifu kama shahidi, nitaendelea hadithi ya Fernando na Bayley. Kama unakumbuka, nilishiriki kwamba Fernando na ndugu yake walikuwa wamebatizwa, lakini wazazi wake na ndugu zake watatu walikuwa bado. Na, licha ya kupokea mialiko kadha kukutana na wamisionari zaidi ya miaka mingi, kila wakati familia ilikataa.

Baada ya maumivu ya kufariki kwa Bayley na mtoto wake, familia ya Fernando ilikuwa haifarijiki. Tofauti na Fernando na tofauti na familia ya Bayley, hawakupata faraja au amani. Hawakuweza kuelewa jinsi kijana wao wenyewe, pamoja na familia ya Bayley, waliweza kubeba mzigo wao mzito.

Hatimaye walihitimisha kwamba kile kijana wao alikuwa anamiliki na hawakuwa nacho ilikuwa injili ya urejesho ya Yesu Kristo, na hii sharti iwe chanzo chake cha amani na faraja. Kufuatia uelewa huu, waliwaalika wamisionari kufundisha familia yao injili. Matokeo yake, walipokea ushahidi wao wenyewe na ushuhuda wa mpango mkuu wa furaha, ambao uliwaletea amani nzuri na faraja tulivu waliyokuwa wanatafuta kwa kila njia.

Ubatizo wa familia ya Fernando

Miezi miwili baada ya kufariki kwa Bayley na mjukuu wao wa kike ambaye alikuwa hajazaliwa, wazazi wa Fernando pamoja na ndugu zake wawili walibatizwa, kuthibitishwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Ndugu ndogo wa Fernando, anangojea kwa hamu ubatizo wake wakati atakapofika miaka nane. Kila mmoja wao anashuhudia kwamba Roho, Roho Mtakatifu alitoa ushahidi wa ukweli wa injili, kuwaelekeza kutamani kubatizwa na kupokea karama ya Roho Mtakatifu.

Akina kaka na akina dada, Roho Mtakatifu atawasaidia kwa kushuhudia kwenu kama Yeye alivyosaidia familia ya Fernando.

Muhtasari

Wacha sasa tufanye muhtasari Tumetambua kweli tatu zilizofunuliwa ambazo zinatuleta kwenye uelewa wa Roho Mtakatifu. Nazo ni kwamba Roho Mtakatifu ni mshirika wa tatu wa Uungu, Roho Mtakatifu ni mtu wa kiroho, na kipawa cha Roho Mtakatifu huja kwa kuwekewa mikono. Pia tulitambua majibu matatu kwa swali “Jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia wewe?” Roho Mtakatifu huonya, Roho Mtakatifu hufariji, na Roho Mtakatifu hushuhudia.

Ustahili Kuwa na Karama

Kwa wale kati yenu wanaojitayarisha kubatizwa na kudhibitishwa, wale ambao hivi karibuni wamekuwa, au hata wale ambao kwa muda mwingi uliopita walikuwa, ni muhimu kwa usalama wetu kimwili na kiroho kwamba tuwe na karama ya Roho Mtakatifu. Tunaanza kufanya hivyo kwa kujitahidi kutii amri, kuwa na sala binafsi na ya kifamilia, kusoma maandiko na kutafuta mahusiano ya kupendana na kusameheana na familia na wapendwa wetu. Hatuna budi mawazo, matendo, na lugha yetu kuwa ya uadilifu. Hatuna budi kumwabudu Baba yetu wa Mbinguni katika nyumba zetu, kanisani, na inapowezekana, katika hekalu takatifu. Kaa karibu na Roho, naye Roho atakaa karibu nawe.

Ushuhuda

Sasa nafunga na mwaliko na ushahidi wangu wa hakika. Ninawaalika muishi kikamilifu maneno yanayoimbwa mara kwa mara watoto wetu wa Msingi, maneno ambayo nina hakika wanayatambua: “Sikiliza, Sikiliza. Roho Mtakatifu atanon’gona. Sikiliza, sikiliza kwa sauti ndogo tulivu.”11

Wapendwa kaka na dada zangu, wazee na vijana, natoa ushahidi wangu wa uwepo mtukufu wa viumbe vitakatifu ambao wanaunda Uungu. Mungu Baba, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu. Ninatoa ushuhuda kwamba mojawapo ya heshima tunayofaidi kama Watakatifu wa Siku za Mwisho tunaoishi katika utimilifu wa nyakati ni karama ya Roho Mtakatifu. Mimi najua kwamba Roho Mtakatifu ukusaidia na atakusaidia . Na pia naongeza ushahidi wangu maalumu wa Yesu Kristo na jukumu Lake kama Mwokozi na Mkombozi wetu na wa Mungu kama Baba yetu wa Mbinguni. Katika jina la Yesu Kristo, amina.