Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2016
Kwa Urais wa Kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho
Ndugu Wapendwa: Kama ilivyoagizwa kwenye sehemu ya 120 ya Mafundisho na Maagano, Baraza la Utumiaji wa Zaka—linajumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi—huidhinisha matumizi ya fedha za Kanisa. Mashirika ya Kanisa hugawa fedha kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa, sera, na taratibu.
Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, ambayo inajumuisha wataalamu wenye sifa na ni huru kutoka kwa idara nyingine zote za Kanisa, ina jukumu la kufanya ukaguzi kwa lengo la kutoa uhakika kuhusu michango inayopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na kulinda mali ya Kanisa.
Kulingana na kaguzi zilizofanywa, Idara ya Ukaguzi ya Kanisa ina maoni kwamba, katika mambo yote, michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanyika, na raslimali za Kanisa kwa mwaka 2016 vimerekodiwa na kusimamiwa kulingana na bajeti iliyopitishwa na Kanisa, sera, na taratibu za uhasibu. Kanisa linafuata taratibu zilizofundishwa kwa waumini wake za kuishi kulingana na bajeti, kuepuka deni, na kuweka akiba kwa ajili ya wakati wa shida.
Kwa heshima imewasilishwa,
Idara ya Ukaguzi ya Kanisa
Kevin R. Jergensen
Mkurugenzi Mkuu