2010–2019
Kwa Marafiki na Wachunguzi wa Kanisa
Aprili 2017


9:55

Kwa Marafiki na Wachunguzi wa Kanisa

Kama utalipia gharama ya ufunuo, ujinyenyekeze mwenyewe, usome, uombe, na utubu, mbingu zitafunguka na utajua, kwamba Yesu ndiye Kristo.

Siku ya Ijumaa mchana, Septemba 16, 1988, katika jengo la ibada la Kata ya Vicente López huko Buenos Aires, Argentina, nilibatizwa kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Rafiki yangu wa dhati Alin Spannaus, alinibatiza siku hiyo, na nilijisikia furaha, mwepesi, nikawa na shauku ya kujifunza zaidi.

Ubatizo wa Mzee Costa

Leo ningependa kushiriki baadhi ya masomo niliyojifunza katika safari yangu ya ubatizo—mafundisho ambayo ninategemea yatawasaidia ninyi mnaonisikiliza ambao sio waumini wa Kanisa bado. Ninaomba mioyo yenu iguswe na Roho wa Bwana kama ilivyokuwa kwangu.

Kwanza, Kutana na Wamisionari

Kwa nini mtu bila ya changamoto kali, mahitaji, au maswali magumuu awe na shauku ya kukutana na wamisionari na kusikiliza masomo yao? Sawa, kwa upande wangu ulikuwa ni mapenzi—mapenzi kwa msichana, msichana aliyeitwa Renee. Nilimpenda, na nilitaka kumuoa. Alikuwa tofauti na alikuwa na viwango tofauti na wanawake wengi niliowajua. Lakini nilimpenda na nikataka nimuoe—na alisema hapana!

Mzee na Dada Costa

Nilichanganyikiwa. Nilifikiri nilikuwa mwenye kuvutia mno! Nilikuwa mwenye umbile zuri, nilikuwa na miaka 24, na digrii yaa chuo kikuu mwenye kazi nzuri. Alizungumzia malengo yake—ya kuolewa na mtu ambaye angempeleka hekaluni, kuwa na familia ya milele—na alikataa ombi langu. Nilitaka kuendelea na uhusiano, hivyo nilikubali kuwasikiliza wamisionari. Je, hii ni sababu nzuri ya kukutana na wamisionari? Sawa, ilikuwa hivyo kwangu.

Wakati nilipokutana na wamisionari kwa mara ya kwanza, sikuelewa vizuri yale waliyosema, na kusema kweli, nilikuwa siwatilii maanani. Moyo wangu ulikuwa hauna nafsi kwa dini mpya. Nilitaka kuwahakikishia kuwa hawakuwa sahihi na kutaka muda wa kumshawishi Renee nimuoe hivyo hivyo.

Leo watoto wangu wamehudumu na wanahudumu misheni, na ninaelewa dhabihu ambayo hawa wavulana na wasichana wanaifanya kufundisha injili ya Yesu Kristo. Sasa natamani ningewasikiliza vizuri wale Mzee Richarson, Mzee Hyland, wamisionari wazuri walionifundisha mimi.

Hivyo, toka kwenye fundisho langu la kwanza, nina waambieni ninyi rafiki na mchunguzi wa Kanisa: mara unapokutana na wamisionari, tafadhali kuwa makini; wanatoa miaka muhimu katika maisha yao kwa ajili yako.

Pili, Nenda Kanisani

Mara ya kwanza nilipohudhuria mkutano wa Kanisa, nilisikia maneno mengi ambayo sikuyaelewa. Beehive walikuwa kina nani? Ukuhani wa Haruni ulikuwa ni nini? Je, Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama?

Kama hii ni mara ya kwanza umehudhuria mkutano wa Kanisa na unahisi kuchanganyikiwa na kitu usichokielewa, usiwe na wasiwasi! Nami sikujua chochote pia. Lakini bado ninakumbuka wazo, hisia mpya za amani na furaha niliyopata. Sikujua kwa wakati ule, lakini Roho Mtakatifu alikuwa ananinong’onezea kwenye masikio na moyo wangu, “Hii ni sahihi.”

Hivyo ngoja niweke somo hili katika sentensi moja: kama umechanganyikiwa, usiwe na shaka; kumbuka hisia ulizozipata; zinakuja toka kwa Mungu.

Tatu, Kusoma Kitabu cha Mormoni

Baada ya mikutano kadhaa na wamisionari, nilikuwa sina maendeleo yoyote. Nilihisi nilikuwa sijapokea uthibitisho wa ukweli wa injili.

Siku moja, Renee aliniuliza, “Je, unasoma Kitabu cha Mormoni?”

Nikajibu, “Hapana.” Nilikuwa nawasikiliza wamisionari—je hiyo haitoshi?

Akiwa na machozi katika macho yake, Renee alinihakikishia kwamba alijua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli na alielezea kwamba, kama nilitaka kujua ikiwa ni kweli, njia pekee—unajua nini—ni kukisoma! Na kisha uliza!

Soma, tafakarini katika mioyo yenu, na “muombe Mungu, Baba wa Milele, katika jina la Kristo, … kwa moyo wa dhati, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo” (Moroni 10:4) kama Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, kama hili ni Kanisa la kweli.

Kwa somo la tatu, kwa sentensi moja: unapopokea vitu hivi—Kitabu cha Mormoni—na unahimizwa kukisoma na kumwomba Mungu kama ni cha kweli, tafadhali fanya hivyo!

Mwisho, Kutubu

Uzoefu wa mwisho ninaopenda kushiriki ni kuhusu toba. Baada ya kumaliza masomo yote ya wamisionari, bado nilikuwa sijashawishika nilitakiwa kubadilika kila kitu katika maisha yangu. Ilikuwa Mzee Cutler, kijana, mmisionari mwenye kujiamini akiwa anaongea Kihispania kidogo, ambaye siku moja alisema, “Joaquin, naomba tusome pamoja Alma 42, na tutalijumuisha jina lako tukiwa tunasoma.”

Nilifikiri ni mzaha, lakini nilifanya kama Mzee Cutler alivyotaka na kusoma katika mstari wa 1: “Na sasa, mwana wangu [Joaquin], naona kuna kitu kidogo zaidi ambacho kinasumbua akili yako, ambacho huwezi kuelewa.” Oh! Kitabu kilikuwa kinaongea na mimi.

Na tukasoma katika mstari wa 2: “Sasa tazama, mwana wangu [Joaquin], nitakieleza hiki kitu.” na kisha Kuanguka kwa Adamu kukaelezewa.

Na kisha katika mstari wa  4: Na hivyo tunaona, kwamba kulikuwa na wakati ambao uliwekewa wewe [Joaquin] kutubu.”

Tuliendelea kusoma polepole, mstari kwa mstari, hadi kufikia kwenye mistari mitatu ya mwisho. Kisha nikashikwa na nguvu kubwa. Kitabu kiliongea moja kwa moja na mimi, na nikaanza kulia nikiwa ninasoma, “Na sasa, [Joaquin,] mwana wangu, nataka kwamba usiache vitu hivi vikusumbue mara nyingine, na ni dhambi zako tu zikusumbue, pamoja na taabu hiyo ambayo itakuleta … wewe kwenye toba (mstati wa 29).

Nikagundua sasa kwamba nilitarajia kupata ufunuo bila ya juhudi kubwa. Kabla ya hapo sikuwahi kuongea na Mungu, na wazo la kuongea na mtu asiyeonekana lilionekana la kijinga. Nilitakiwa kujinyenyekeza mwenyewe na kutenda yale niliyotakiwa kutenda hata kama, kwa fikra zangu, yalionekana ya upuuzi

Siku ile nikafungua moyo wangu kwa Roho wa Bwana, nikatamani kutubu, na nikataka kubatizwa! Kabla ya tukio hilo, niliwaza toba ni kama kitu hasi, kinachohusiana na dhambi na kutenda maovu, lakini ghafla nikaona kwa mwanga tofauti—kama kitu chanya ambacho kinasafisha njia ya ukuaji, na ya furaha.

Mzee Cutler yupo hapa leo, na nataka kumshukuru kwa kunifumbua macho yangu. Kila uamuzi nilioufanya katika maisha yangu toka wakati huo ulisababishwa na tukio hilo wakati nilipojinyenyekeza mwenyewe, kuomba kwa ajili ya msamaha, na Upatanisho wa Yesu Kristo kwa niaba yangu ukawa sehemu ya maisha yangu.

Hivyo, somo la mwisho, katika kauli moja: Fanya toba; hakuna kikuletacho karibu na Bwana Yesu Kristo zaidi ya kutaka kubadilika.

Mpendwa wangu mchunguzi, rafiki wa Kanisa, kama unasikiliza leo, upo karibu kufikia furaha iliyo kubwa. Upo karibu!

Naomba nikualike, kwa uwezo wa moyo wangu wote, na kina cha nafsi yangu, nenda na ukabatizwe! Ni kitu kizuri ambacho hutawahi kukifanya. Hakitabadilisha maisha yako tu bali pia maisha ya watoto na wajukuu zako.

Siku ya harusi ya Mzee na Dada Costa

Bwana amenibariki mimi na familia yangu. Nilimuoa Renee, na tuna watoto wazuri wanne. Na kwa sababu ya ubatizo wangu, ninaweza, kama nabii Lehi wa kale, kuwaalike kula tunda la mti wa uzima, ambalo ni upendo wa Mungu (ona 1 Nefi 8:15; 11:25). Ninaweza kuwasaidia kuja kwa Kristo.

Hivyo tafadhali fikiria uzoefu wangu, na (1) wachukulie wamisionari kwa umakini, (2) nenda kanisani na kumbuka hisia za kiroho, (3) soma Kitabu cha Mormoni na mwombe Bwana kama ni cha kweli, na (4) fanya toba na ubatizwe.

Ninashuhudia kwenu kwamba kama utalipia gharama ya ufunuo, ujinyenyekeze mwenyewe, usome, uombe, na utubu, mbingu zitafunguka na utajua, kama mimi nijuavyojua, kwamba Yesu ndiye Kristo, Yeye ni Mwokozi wangu na wako. Katika jina la Yesu Kristo, amina.