2010–2019
Sauti ya Onyo
Aprili 2017


15:15

Sauti ya Onyo

Wakati wajibu wa kuonya unahisiwa zaidi na manabii, ni wajibu unaoshirikiwa na wengine vile vile.

Nabii Ezekieli alizaliwa takribani miongo miwili kabla ya Lehi na familia yake kuondoka Yerusalemu. Mnamo mwaka 597 K.K, akiwa na umri wa miaka  25, Ezekieli alikuwa mmoja wa wengi waliochukuliwa mateka kwenda Babeli na Nebukadreza, na kwa kadiri tunavyojua tunaweza kusema, aliishi maisha yake yote huko.1 Alikuwa wa ukoo wa kikuhani wa Haruni, na alipokuwa na umri wa miaka 30, alikuwa nabii.2

Katika kumtawaza Ezekieli, Yehova alitumia sitiari ya mlinzi.

“Ikiwa, [mlinzi] aonapo upanga unakuja juu ya nchi hiyo, apiga tarumbeta na kuwaonya watu;

“Basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.”3

Kwa upande mwingine, “bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa, na upanga ukaja ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao, … damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo.”4

Kisha akizungumza moja kwa moja kwa Ezekieli, Yehova alitangaza, “Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu.”5 Onyo lilikuwa ni kuacha dhambi zao.

“Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

“Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako …

“Tena, ninaposema kwa mtu mbaya, hakika utakufa; kama hatendi dhambi , na kufanya kile kilicho halali na cha haki; …

“Katika dhambi zake zote alizozitenda, hata mojawapo haitakumbukwa juu yake; ametenda yaliyo halali na haki; hakika ataishi.”6

Cha kupendeza, onyo hili pia linawahusu wenye haki. “Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika [matendo yake ya haki], hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo.”7

Akiwasihi watoto Wake, Mungu anamwambia Ezekieli, “Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?”8

Badala ya kuwa na hamu ya kulaani, Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu wanataka sisi tuwe na furaha na kutusihi tutubu, kwa sababu wanajua vizuri sana kwamba “kamwe uovu haujapata [na kamwe hutakuwa] furaha.”9 Kwa hiyo Ezekieli na kila nabii kabla na sasa, wakizungumza neno la Mungu kwa hisia ya ndani, wameonywa wote ambao watamghairia Shetani, adui wa roho zao, na “kuchagua uhuru na uzima wa milele, kupitia Mpatanishi mkuu wa watu wote.”10

Wakati wajibu wa kuonya unahisiwa zaidi na manabii, ni wajibu unaoshirikiwa na wengine vile vile. Kwa kweli, “ni wajibu wa kila mtu ambaye ameonywa amwonye jirani yake.”11 Sisi tuliopokea elimu ya mpango mkuu wa furaha—na utekelezaji wake wa amri—tungehisi tamaa ya kushiriki elimu ile kwa vile ina athari kubwa sana, hapa na milele. Na kama tukiuliza, “Nani ni jirani yangu ili nimwonye?” kwa hakika jibu litapatikana katika fumbo linaloanza na, “Mtu mmoja alishuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyan’ganyi, [ na kadhalika].”12

Kufikiria fumbo la Msamaria mwema katika muktadha huu inatukumbusha kwamba swali “nani ni jirani yangu?” limeunganishwa na amri kuu mbili: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.”13 Motisha kwa kuinua sauti ya onyo ni upendo—upendo wa Mungu na upendo wa binadamu mwenzio. Kuonya ni kujali. Bwana anaelekeza kwamba inatakiwa ifanywe “kwa upole na unyenyekevu”14 na kwa ushawishi, kwa ustahimilifu, kwa uraufu … , na kwa upendo wa kweli.”15 Inaweza kuwa jambo la dharura, kama wakati tunapomwonya mtoto asiweke mkono wake katika moto. Lazima iwe wazi na wakati mwingine thabiti. Wakati mwingine, onyo linaweza kuwa kama aina ya karipio “kwa wakati wake, utakapokuwa umeongozwa na Roho Mtakatifu,”16 lakini siku zote iwe ni kwa msingi wa upendo. Ushahidi, kwa mfano upendo huhamasisha huduma na dhabihu za wamisionari wetu.

Kwa hakika upendo utalazimisha wazazi kuwaonya “majirani” zao wa karibu, watoto wao wenyewe. Hii inamaanisha kufundisha na kushuhudia kweli za injili. Inamaanisha kuwafundisha watoto mafundisho ya Kristo: imani, toba, ubatizo, na kipawa cha Roho Mtakatifu.17 Bwana huwakumbusha wazazi, “Lakini nimewaamuru ninyi kuwalea watoto wenu katika nuru na kweli.”18

Kigezo muhimu cha wajibu wa uzazi kuonya sio tuu kuelezea matokeo ya kuhuzunisha ya dhambi lakini pia furaha ya kutembea katika utii kwa amri hizi. Kumbuka maneno ya Enoshi kuhusu kile kilichompelekea yeye kumtafuta Mungu, kupokea ondoleo la dhambi, na kuongolewa.

Tazama, nilienda kuwinda wanyama porini; na maneno ambayo nilikuwa nimezoea kumsikia baba yangu akizungumza kuhusu uzima wa milele, na shangwe ya watakatifu, yakapenya ndani ya moyo wangu.

“Na nafsi yangu ikapata njaa; na nikapiga magoti mbele ya Muumba wangu, na nikamlilia kwa sala kuu na nikamsihi.”19

Kwa sababu ya upendo usio kifani na kuwajali wengine na furaha yao,Yesu hakuwa anasita kuonya. Mwanzoni mwa huduma Yake, “Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”20 Kwa sababu anajua kwamba sio kila njia yoyote inaelekea mbinguni, Yeye aliamuru:

“Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo:

“Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”21

Alitumia muda mwingi na wenye dhambi, akisema, “Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”22

Kuhusu waandishi, Mafarisayo, na Masadukayo, Yesu alikuwa thabiti katika kulaani unafiki wao. Maonyo yake na amri zake zilikuwa moja kwa moja: “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.”23 Kwa hakika hakuna ambaye angemshitaka Mwokozi kwa kuto wapenda hawa waandishi na Mafarisayo—hata hivyo aliteseka na kufa ku waokoa pia. Lakini kwa kuwapenda Yeye asingeweza kuwaacha waendelee kuishi katika dhambi zao, bila kuwasahihisha. Mfuata kanuni mmoja aliandika, “Yesu alifundisha wafuasi wake kufanya kama alivyo fanya: kumkaribisha kila mtu lakini pia kufundisha kuhusu dhambi, kwa kuwa upendo unahitaji, kuwaonya watu kuhusu nini kinaweza kuwaumiza.”24

Wakati mwingine wale ambao wanapaza sauti ya onyo hupuuzwa kama wahukumu. Kimafumbo, hata hivyo, hao wanaodai kwamba ukweli ni kuwiana na kwamba viwango vya uadilifu ni jambo la maamuzi binafsi, mara kwa mara ni walewale ambao mara nyingi hukosoa kwa ukali watu ambao hawakubali kaida ya sasa ya “mawazo sahihi.” Mwandishi mmoja alirejea hili kama uamuzi wa “tamaduni ya aibu.”

Katika tamaduni ya hatia unajua wewe ni mzuri au mbaya kwa vile dhamiri yako inavyosikia. Katika utamaduni wa aibu unajua wewe ni mzuri au mbaya kwa kile jamii yako husema kukuhusu wewe, kwa vile inavyokuheshimu au kukutenga. … [Katika utamaduni wa aibu] maisha ya uadilifu haya jengwi juu ya mwenendo wa chanya na hasi,unajengwa juu ya mwenendo wa pamoja na wa zuio. …

“… Kila mtu daima sio salama katika mfumo wa uadilifu unaozingatia kukumbatia na kutenga. Hakuna kiwango cha kudumu, ila tuu kubadilika kwa uamuzi wa kundi. Ni utamaduni wa kuzidi kwa kiwango cha hisia, kufanya zaidi, na wasiwasi wa uadilifu mara kwa mara, wakati ambao kila mtu anahisi kushurutishwa. … 

“Utamaduni wa hatia unaweza kuwa mkali, lakini angalau ungeweza kuchukia dhambi na bado ukampenda mwenye dhambi. Utamaduni wa aibu wa kisasa kama unavyodhaniwa unadhamini kukumbatia na kuruhusu, lakini unaweza kuwa kwa kiajabu usio na huruma kwa wale wasiokubali na kwa wale wasiofaa katika mwingiliano.”25

Ikitofautishwa na hii ni “mwamba wa Mkombozi wetu,”26 msingi thabiti na wa kudumu wa haki na maadili. Ni vizuri zaidi kuwa na sheria isiyobadilika ya Mungu, ambayo kwayo tunaweza kuchagua majaliwa yetu badala ya kuwa mateka wa sheria zisizotabirika na hasira za wahuni wa vyombo vya habari. Ni vizuri zaidi kujua ukweli kuliko “kupeperushwa huku na huko, na kubebwa na kila upepo wa mafundisho.”27 Ni afadhali zaidi kutubu na kujitahidi kuishi kufuatana na kiwango cha injili kuliko kujifanya hakuna chanya na hasi na kunyong’onyea katika dhambi na masikitiko.

Bwana ameshatangaza, “Na sauti ya onyo itakuwa kwa watu wote, kwa vinywa vya wanafunzi wangu, ambao nimewachagua katika siku hizi za mwisho.”28 Kama walinzi na wanafunzi, hatuwezi kuwa tusiopendelea upande wowote kuhusu hili “njia bora zaidi.”29 Kama Ezekieli, hatuwezi kuona upanga ukija juu ya nchi na “bila kupuliza tarumbeta.”30 Hii siyo kusema kwamba tunapaswa kugonga mlango wa jirani au kusimama kwenye uwanja wa umma tukipaza sauti “Tubu!” Kwa kweli ukifiria kuhusu jambo hili, tunacho katika injili ya urejesho kile watu, wanakitaka hasa. Kwa hiyo sauti ya onyo kwa kawaida siyo tu ya ustarabu, bali katika kishazi cha Mtunga Zaburi, ni “kelele za shangwe.”31

Mhariri wa maoni Hal BoydDeseret News alitoa mfano wa tendo linalodhuru la asili kwa kukaa kimya. Aliona kwamba ingawa wazo la ndoa bado ni jambo la “mdahalo wa wasomi” miongoni mwa matabaka Marekani, ndoa yenyewe sio jambo la mdahalo kwao kidesturi. “Matabaka yanapata na yanakaa katika ndoa na wanahakikisha watoto wao wanafaidi matunda ya ndoa imara. … Tatizo, hata hivyo, ni kwamba [hawa], hawahubiri kile wanachofanya.” Hawataki “kuwalazimisha” wale ambao wangetumia uongozi wao wa uadilifu, bali “labda ni wakati wa wale wenye elimu na familia imara kusitisha kujifanya hawaegemei upande wowote na kuanza kuhubiri kile wanachokifanya kuhusu ndoa na uzazi … [na] kuwasaidia Wamarekani wenzao kukikumbatia.”32

Tunaamini kwamba hususani nyinyi wa kizazi chipukizi, vijana na vijana wakubwa ambao Bwana lazima awategemee kwa ufanisi wa kazi Yake katika miaka ijayo, mtaidhinisha mafundisho ya injili na viwango vya Kanisa katika umma vilevile katika sirini. Msiwatelekeze wale ambao wakekubali ukweli na kisha kujikwaa na kushindwa kwa sababu ya ujinga. Msishindwe na fikra za uongo za ruhusa au woga—woga wa usumbufu, kutokubalika, au hata kuteseka. Kumbukeni ahadi ya Mwokozi:

“Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.

“Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.”33

Mwishowe, sisi wote tunawajibika kwa Mungu kwa ajili ya chaguzi zetu na maisha tunayoishi. Mwokozi alitangaza,“Na Baba yangu alinituma ili nipate kuinuliwa juu kwenye msalaba; na baada ya kuinuliwa juu kwenye msalaba, kwamba ningeleta watu wote kwangu, kwamba kama nilivyoinuliwa juu na watu, hata hivyo watu wainuliwe juu na Baba, kusimama mbele yangu, na kuhukumiwa kwa vitendo vyao, ikiwa vitakuwa vizuri au ikiwa vitakuwa viovu.”34

Tukitambua hili, ukuu wa Bwana, nasihi kwa maneno ya Alma:

“Na sasa, ndugu zangu na [kina dada], natamani kutoka sehemu ya ndani kabisa ya moyo wangu, ndio, kwa wasiwasi mwingi na hata kwa uchungu, kwamba … mtupe dhambi zenu, na kwamba msiahirishe siku ya toba yenu;

“Lakini kwamba mtajinyenyekeza mbele ya Bwana, na mliite jina lake takatifu, na kukesha na kusali daima, kwamba msijaribiwe zaidi ya yale ambayo mnaweza kuvumilia, na hivyo mwongozwe na Roho Mtakatifu, … ;

“Mkimwamini Bwana; mkitumaini kwamba mtapokea uzima wa milele; mkiwa na upendo wa Mungu daima katika mioyo yenu, kwamba muinuliwe katika siku ya mwisho na muingie katika pumziko lake.”35

Na kila mmoja wetu aweze kusema kwa Bwana pamoja na Daudi: “Sikusitiri haki yako moyoni mwangu; Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako: Sikuficha fadhili zako wala kweli yako katika kusanyiko kubwa. Nawe, Bwana, usinizuilie rehema zako.36 Katika jina la Yesu Kristo, amina.