2010–2019
Uungu na Mpango wa Wokovu
Aprili 2017


15:17

Uungu na Mpango wa Wokovu

Kwa sababu tuna ukweli kuhusu Uungu na uhusiano wetu na Wao, tuna ramani ya msingi na hakika wa safari yetu kupita maisha ya dunia.

I.

Makala ya kwanza ya imani yetu inasema “Tunaamini katika Mungu, Baba wa Milele, na katika Mwanawe, Yesu Kristo, na katika Roho Mtakatifu. Tunaungana na Wakristo karibu wote katika imani hii katika Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Hatuamini katika kile ulimwengu wa Kikristo huita mafundisho ya Utatu Mtakatifu. Katika Ono lake la Kwanza, Joseph Smith aliwaona watu wawili tofauti, watu wawili, hivyo ikieleza waziwazi kuwa, imani zilizokuwa zimetawala kuhusu Mungu na Uungu zilikuwa si kweli.

Tofauti na imani kuwa Mungu haelezeki na ni fumbo lisilojulikana, Sisi tunaamini kuwa ukweli kuhusu asili ya Mungu na uhusiano Wake na sisi unajulikana na ni ufunguo wa kila kitu katika mafundisho yetu. Mwokozi alifundisha: “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3).

Biblia Takatifu

Juhudi za kumjua Mungu na kazi Yake zilianza kabla ya maisha ya hapa duniani na hazitaishia hapo. Nabii Joseph Smith alifundisha “Itachukuwa muda mrefu baada ya kupita pazia kabla ya kujifundisha … kanuni zote za kuinuliwa.”1 Tunajenga juu ya elimu tuliyoipata katika ulimwengu wa kiroho kabla ya kuzaliwa. Hivyo, katika kujaribu kuwafundisha Waisraeli asili ya Mungu na uhusiano Wake kwa watoto Wake, nabii Isaya alisema, kama ilivyoandikwa katika Biblia:

“Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani?

“Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia? (Isaya 40:18, 21).

Tunajua kuwa washirika watatu wa Uungu ni viumbe mbali mbali na tofauti. Tunajua hili kutokana na maelezo yaliyotolewa na Nabii Joseph Smith: “Baba ana mwili wa nyama na mifupa wenye kushikika kama wa mwanadamu; na Mwana vile vile; lakini Roho Mtakatifu hana mwili wa nyama na mifupa, bali ni mtu wa Kiroho. Kama isingekuwa hivyo, Roho Mtakatifu asingeweza kukaa ndani yetu.” (M&M 130:22)

Kama sehemu iliyo kuu kabisa ya Mungu Baba katika Uungu, na vile vile ya majukumu ya kuheshimika ambayo kila mmoja hufanya, Nabii Joseph alifafanua:

Nabii Joseph Smith

“Mtu yeyoye ambae aliwahi kuona mbingu zikifunguka hujua kuwa kuna watu watatu mbinguni ambao wanashikilia funguo za nguvu, na mmoja anayesimamia yote. …

“… Watu hawa … wanaitwa, Mungu wa kwanza, Muumbaji; Mungu wa pili, Mwokozi; na Mungu wa tatu, Shahidi au Muusia.

“[Ni] jimbo la Baba kuongoza kama Chifu au Rais, Yesu kama Mpatanishi na Roho Mtakatifu kama Muusia au Shahidi.”2

II. Mpango

Tunaelewa uhusiano wetu kwa washirika wa Uungu kutokana na kile ambacho kimefunuliwa kuhusu mpango wa wokovu.

Maswali kama “Tulitoka wapi? “Kwa nini tuko hapa? na Tunaelekea wapi? yanajibiwa katika kile ambacho maandiko huita “mpango wa wokovu” “mpango mkuu wa furaha” au “mpango wa ukombozi” (Alma 42:5, 8, 11). Injili ya Yesu Kristo ni kitovu cha mpango huu.

Kama watoto wa kiroho wa Mungu, katika kuishi kabla ya maisha ya dunia, tulitamani hatima yetu ya uzima wa milele lakini tuliendelea kadiri tulivyoweza bila kuwa na miili ya kushikika. Ili kutoa nafasi hiyo, Baba yetu wa Mbinguni alisismamia uumbaji wa ulimwengu huu, ambapo kuzuiwa kwa kumbukumbu zetu kulitangulia kuzaliwa kwetu duniani, tungeweza kuthibitisha utayari wetu wa kuziishi amri Zake na kupata uzoefu na kukua kupitia changamoto zingine za maisha ya kimwili. Lakini katika kipindi hicho cha uzoefu wa maisha ya kimwili, na kama matokeo ya anguko la wazazi wetu wa kwanza, tungeteseka na kifo cha kiroho kwa kutolewa katika uwepo wa Mungu, tukichafuliwa na dhambi, na kuwa chini ya kifo cha kimwili. Mpango wa Baba ulitazamia na kutoa njia za kushinda vikwazo hivyo vyote viwili.

III. Uungu

Kwa kujua lengo kuu la mpango wa Mungu, sasa tunaangalia majukumu ya kuheshimika ya washirika watatu wa Uungu katika mpango huo.

Tunaanza na mafundisho kutoka katika Biblia. Kwa kukamilisha barua yake ya pili kwa Wakorintho, Mtume Paulo anaweka hili kukaribia marejeo ya haraka juu ya Uungu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika [au uenzi3] wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote” (2 Wakorintho 13:14).

Andiko hili la kibiblia huwakilisha Uungu na marejeo ya upendo wote wa Mungu Baba wenye kutia moyo, huduma ya rehema na kuokoa ya Yesu Kristo, na uenzi wa Roho Mtakatifu.

Mungu Baba

Yote huanza na Mungu Baba. Wakati tukijua kwa kiasi kidogo kumhusu Yeye, kile tujuacho ni cha mwisho katika uelewa wa sehemu Yake kuu kabisa, uhusiano wetu Naye, na kazi Yake ya uangalizi katika mpango wa wokovu, Uumbaji na vingine vyote ambavyo hufuata.

Kama Mzee Bruce R. McConkie alivyoandika kabla tu ya kifo chake: “Katika hali kuu na ya mwisho ya neno, kuna Mungu mmoja wa kweli anayeishi. Yeye ni Baba, Mwenyezi Elohimu, Kiumbe Kikuu, Muumbaji na Mtawala wa ulimwengu.”4 Yeye ni Mungu na Baba ya Yesu Kristo pia na sisi wote. Rais David O. McKay alifundisha kuwa “ukweli muhimu wa kwanza uliotetewa na Yesu Kristo ulikuwa ni huu, kwamba nyuma ya, juu zaidi ya vyote kuna Mungu Baba, Bwana wa mbingu na dunia.”5

Tunachojua kuhusu asili ya Mungu Baba ni kile ambacho tunaweza kujifunza kutoka kwenye huduma na mafunzo ya Mwanawe wa Pekee, Yesu Kristo. Kama Mzee Jeffrey R. Holland alivyofundisha, mojawapo ya lengo kuu la huduma ya Yesu ilikuwa kufunua kwa wanadamu “vile Mungu Baba yetu wa Milele alivyo, … kufunua na kulifanya kuwa maalumu kwetu ukweli wa asili ya Baba Yake, Baba yetu wa Mbinguni.”6 Biblia inabeba ushuhuda wa kitume kwamba Yesu alikuwa “chapa ya nafsi” ya Baba Yake (Waebrania 1:3), ambapo inaelezea tu mafunzo ya Yesu mwenyewe kwamba “Yeye aliyeniona mimi amemwona Baba”(Yohana 14:9).

Mungu Baba ni Baba ya roho zetu. Sisi ni watoto Wake. Anatupenda, na vyote ambavyo hufanya ni kwa manufaa yetu ya milele. Yeye ni mtunzi wa mpango wa wokovu, na ni kwa nguvu Zake kwamba mpango Wake hufikia madhumuni ya utukufu wa mwisho wa watoto Wake.

Mwana

Kwa wanadamu, mshirika wa Uungu anayeonekana sana ni Yesu Kristo. Kauli ya fundisho kuu la Urais wa Kwanza mwaka 1909 linamtangaza Yeye kuwa ndiye “mzaliwa wa kwanza katika wana wote wa Mungu—mzaliwa wa kwanza kiroho na mzawa pekee katika mwili.”7 Mwana, mkuu kuliko wote, alichaguliwa na Baba kutekeleza mpango wa Baba—kutumia nguvu za Baba kuumba dunia zisizo na hesabu (Ona Musa 1:33) na kuwaokoa watoto wa Mungu kutokana na mauti kwa ufufuko Wake na kutoka dhambini kwa Upatanisho Wake. Hii dhabihu kuu kweli inaitwa “tendo kuu katika historia yote ya binadamu.”8

Bwana Yesu Kristo

Katika fursa hizo za kipekee na takatifu ambapo Mungu Baba mwenyewe alimtambulisha Mwana, Alisema, “Huyu ni Mwana wangu mpendwa: msikilize” (Marko 9:7; Luka 9:35; ona pia 3  Nefi 11:7; Historia ya—Joseph Smith 1:17). Basi, ni Yesu Kristo, Yehova, Bwana Mungu wa Israeli, anayeongea na, na kupitia manabii.9 Basi ndiyvo ilivyokuwa Yesu alipowatokea Wanefi baada ya ufufuko wake, alijitambulisha kama “Mungu wa ulimwengu wote” (3 Nefi 11:14). Basi ni huyo Yesu ambaye kila mara huongea na manabii wa Kitabu cha Mormoni na Watakatifu wa Siku za Mwisho kama “Baba na Mwana” jina ambalo lilielezewa kwenye fundisho fasiri la mwogozo wa kiungu la Urais wa Kwanza miaka 100 iliyopita.10

Roho Mtakatifu

Mshirika wa tatu wa Uungu ni Roho Mtakatifu, pia anaitwa kama Roho Mtakatifu, Roho wa Bwana na Mfariji. Ni mshirika wa Uungu ambaye ni wakala wa ufunuo binafsi. Kama mtu wa kiroho (ona M&M 130:22), Yeye anaweza kukaa ndani yetu na kufanya shughuli muhimu ya kimawasiliano kati ya Baba na Mwana na watoto wa Mungu duniani. Maandiko mengi yanafundisha kuwa kazi Yake ni kumshuhudia Baba na Mwana (ona Yohana 15:26; 3 Nefi 28:11; M&M 42:17). Mwokozi aliahidi kwamba Mfariji atawafundisha vitu vyote, na kuwakumbusha vitu vyote, na kuwaongoza katika ukweli wote (ona Yohana 14:26; 16:13). Basi, Roho Mtakatifu hutusaidia kutambua kati ya ukweli na uongo, hutuongoza katika maamuzi yetu makuu, na hutusaidia kupita changamoto za kimwili.11 Yeye pia ni njia ambayo kwayo tunatakaswa, kusafishwa na kuwekwa wasafi kutokana na dhambi (ona 2 Nefi 31:17; 3 Nefi 27:20; Moroni 6:4).

IV.

Kwa hiyo ni kwa namna gani uelewa wa fundisho hili la kimbinguni lililofunuliwa kuhusu Uungu na mpango wa wokovu hutusaidia katika changamoto zetu leo?

Kwa sababu tuna ukweli kuhusu Uungu na uhusiano wetu na Wao, dhumuni la maisha, na asili ya mwisho wetu wa milele, tunayo ramani ya muhimu na hakika wa safari yetu kupita maisha ya duniani. Tunajua ni nani tunayemwabudu na kwa nini tunamwabudu. Tunajua sisi ni nani na nani tunayeweza kuwa (ona M&M 93:19). Tunajua nani anawezesha yote, na tunajua nini tunatakiwa kufanya ili kufurahia baraka za mwisho ambazo huja kupitia mpango wa wokovu wa Mungu. Tunajuaje yote haya? Tunajua kupitia funuo za Mungu kwa manabii Wake na kwa kila mmoja wetu binafsi.

Kufikia kile Mtume Paulo alichoelezea kama “kipimo cha cheo cha utimilifu wa Kristo” (Waefeso 4:13) huitaji zaidi ya kupata elimu. Hata haitoshi kwetu kushawishiwa na injili; tunatakiwa kufanya na kufikiria ili kwamba tuongolewa nayo. Kinyume na asasi za kidunia, ambazo hutufundisha kujua kitu fulani, mpango wa wokovu na injili ya Yesu Kristo hutupa chanagamoto sisi ya kuwa kitu fulani.

Rais ThomasS. Monson

Kama Rais Thomas S.Monson alivyotufundisha katika mkutano wetu mkuu uliopita:

“Muhimu katika mpango [wa wokovu] ni Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Bila dhabihu Yake ya upatanisho, yote yangepotea. Haitoshi, hata hivyo, kuamini tu katika Yeye na utumishi Wake. Tunahitaji kufanya kazi na kujifunza, kupekua na kusali, kutubu na kujiboresha zaidi. Tunahitaji kujua sheria za Mungu na kuziishi. Tunahitaji kupokea ibada Zake zenye kuokoa. Kwa kufanya hivyo tu, tutapata furaha ya kweli ya milele. …

“Kutoka kwenye kina cha moyo wangu, na kwa unyenyekevu wote, ninashuhudia zawadi kubwa ambayo ni mpango wa Baba yetu kwa ajili yetu. Ni njia moja kamilifu ya amani na furaha kote hapa na katika ulimwengu ujao.”12

Ninaongeza ushuhuda wangu kwa ule wa nabii wetu mpendwa. Ninashuhudia kwamba tuna Baba yetu wa Mbinguni, ambaye anatupenda. Nashuhudia kwamba tuna Roho Mtakatifu, ambaye hutuongoza. Na nashuhudia juu ya Yesu Kristo, Mwokozi wetu; ambaye huwezesha yote, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 268.

  2. Teachings: Joseph Smith, 42.

  3. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kawaida ya ushirika wakati neno hilo lilipochaguliwa na wafasiri wa King James (see The Oxford Universal Dictionary, 3rd ed., rev. [1955], 352).

  4. Bruce R. McConkie, A New Witness for the Articles of Faith (1985), 51.

  5. David O. McKay, in Conference Report, Oct. 1935, 100.

  6. Jeffrey R. Holland, “The Grandeur of God,” Liahona, Nov. 2003, 70.

  7. First Presidency, “The Origin of Man,” Ensign, Feb. 2002, 26, 29.

  8. Ona, kwa mfano, Russell M. Nelson, “Drawing the Power of Jesus Christ into Our Lives,” Liahona, May 2017, 40; “The Living Christ: The Testimony of the Apostles,” Liahona, Apr. 2000, 2.

  9. Ona Joseph Fielding Smith, Doctrines of Salvation, comp. Bruce R. McConkie (1954), 1:27.

  10. Ona First Presidency and Quorum of the Twelve Apostles, “The Father and the Son,” Ensign, Apr. 2002, 13–18.

  11. Ona Robert D. Hales, “The Holy Ghost,” Liahona, May 2016, 105–7.

  12. Thomas S. Monson, “The Perfect Path to Happiness,” Liahona, Nov. 2016, 80–81.