Na Uzima wa Milele Ndio Huu
Mungu anakujua wewe, na anakualika wewe kumjua Yeye.
Naongea nanyi, kizazi kinachoinukia—wavulana, wasicha na vijana wakubwa, waseja au waliooa—ninyi ambao ni viongozi wa baadaye wa Kanisa hili. Pamoja na maovu yote, machafuko, hofu, na mikanganyiko katika dunia ya leo, naongea nanyi kwa uwazi kuhusu ukuu na baraka zakuja kumjua Mungu.
Yesu Kristo alifundisha kweli nyingi ambazo zinaelezea kuhusu mpango mkuu wa Baba wa furaha, jukumu na nafasi yenu. Nitalenga kweli mbili ambazo zitakusaidia kuelewa utambulisho wako kama mtoto wa Mungu na kujua dhamira yako katika maisha.
Kwanza: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”1
Pili: “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”2
Tafadhali weka kweli hizi akilini—zinafundisha kwa nini—ninapojaribu kutafuta kuelezea jinsi wewe na sisi wote tunavyoweza kuja kumjua Mungu.
Mmjue kupitia Maombi
Marafiki zangu vijana, tunaweza kuanza kumjua Mungu kwa njia ya maombi.
Mnamo Aprili 7, 1829, Oliver Cowdery mwenye umri wa miaka 22 alianza kazi yake kama mwandishi wa Joseph Smith mwenye umri wa 23. Walikuwa vijana—kama ninyi. Oliver aliuliza uthibitisho kutoka kwa Mungu kuhusu Urejesho na kazi yake kwa hilo. Kwa majibu, alipokea ufunuo ufuatao:
“Tazama, na wewe wajua kwamba uliniuliza Mimi na Mimi nikaiangaza akili yako …
Ndiyo, ninakuambia, ili wewe upate kujua kwamba hapana yeyote ila Mungu ambaye hujua mawazo yako na dhamira ya moyo wako. …
“… Kama unataka ushahidi zaidi, rejesha mawazo yako juu ya usiku ule uliponililia katika moyo wako. …
“Sikusema amani akilini mwako … ? Ni ushahidi gani mkubwa zaidi unaoweza kupata kuliko kutoka kwa Mungu?3
Wewe unapoomba kwa faith, unatahisi upendo wa Mungu Roho Wake anapoongea na nafsi yako . Bila kujali jinsi ulivyo mpweke au jinsi unavyohisi kuwa na wasiwasi wakati mwingine, hauko peke yako katika ulimwengu huu. Mungu anakujua wewe , binafsi. Unapoomba, utaweza kumjua Yeye.
Mmjua kupitia Kujifunza Maandiko
Unapojifunza maandiko, hatujifundishi tu kuhusu Mwokozi, bali unaweza kuja .kumjua Yeye
Mnamo Aprili 1985, Mzee Bruce R. McConkie alinena katika mkutano mkuu—siku 13 kabla ya kufa. Alihitimisha kwa maneno haya:
“Mimi ni mmoja wa mashahidi wake, na katika siku ijayo nitahisi alama za misumari katika mikono yake na miguu yake na nitailowesha miguu yake kwa machozi yangu.
“Lakini sitajua vyema kuliko ninavyojua sasa kwamba yeye ni Mwana wa Mwenyezi wa Mungu, kwamba yeye ni Mwokozi na Mkombozi wetu, na kwamba wokovu huja katika na kwa njia ya damu yake ya kulipia dhambi na sio kwa njia nyingine.”4
Wale ambao tulimsikia Mzee McConkie akiongea siku hiyo hatujaweza kusahau jinsi tulivyojisikia. Alivyoanza hotuba yake, alibaini kwa nini shahidi wake alikuwa mwenye nguvu sana. Alisema:
“Katika kuzungumzia mambo haya ya kupendeza nitatumia maneno yangu mwenyewe, ingawa mnaweza kufikiri ni maneno ya maandiko. …
“Ni kweli yalitangazwa na wengine kwanza, lakini sasa ni yangu , kwani Roho Mtakatifu wa Mungu ametoa ushahidi kwangu kwamba ni ya kweli, na sasa ni kana kwamba Bwana ameyafunua wazi kwangu kwa mara ya kwanza. Hivyo nimesikia sauti yake na kujua neno Lake.”5
Unaposoma na kutafakari maandiko, wewe pia utasikia sauti ya Mungu, kujua maneno Yake, na kumjua Yeye. Mungu ataonyesha kweli zake za milele kwako, binafsi. Mafundisho na kanuni hizi zitakuwa sehemu ya uhalisi wako na zitatoka ndani ya nafsi yako.
Nyongeza ya masomo binafsi, kujifunza maandiko kama familia ni muhimu.
Katika nyumba yetu, tulitaka watoto wetu kujifunza kutambua sauti ya Roho. Tunaamini kwamba hicho kilitokea tulipokuwa tukisoma Kitabu cha Mormoni kila siku kama familia. Shuhuda zetu ziliimarika tulipoongelea kweli takatifu.
Kujifunza maandiko huwa njia ya Roho ya kumpatia kila mmoja wetu mafundisho yafaayo. Unaposoma maandiko kila siku, pekee yako na familia yako, wewe utajifunza kutambua sauti ya Roho na utakuja kumjua Mungu.
Mmjue kwa Kutenda Mapenzi Yake
Mbali na kuomba na kusoma maandiko, tunahitaji kufanya mapenzi Yake.
Mwokozi ni mfano wetu mkuu. Alisema, “Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.”6
Wakati Yesu mfufuka alipowatokea Wanefi, Alisema, “Na tazama mimi ni nuru na uzima wa ulimwengu; na nimekunywa kutoka katika kikombe kichungu ambacho Baba amenipatia, na nimemtukuza Bwana kwa kujivika dhambi za ulimwengu ambamo ndani yake nimevumilia mapenzi ya Baba katika mambo yote katika vitu vyote kutoka mwanzo.”7
Wewe na mimi tunafanya mapenzi ya Baba kwa kuheshimu maagano yetu, kushika amri, na kumtumikia Mungu na wanadamu wenzetu.
Mke wangu, Rhonda, na mimi tuna wazazi ambao ni watu wa kawaida tu-pengine zaidi kama wazazi wenu. Lakini jambo moja ninalopenda kuhusu wazazi wetu ni kwamba walijitolea maisha yao kwa kumtumikia Mungu, na walitufundisha kufanya hivyo.
Wakati wazazi wa Rhonda walipooana kwa miaka michache tu, babake mwenye umri wa miaka 23 aliitwa kutumikia misheni. Alimwacha nyuma mke wake mdogo na binti yao mwenye umri wa miaka 2. Kisha mkewe aliitwa kuhudumu pamoja naye kwa miezi saba ya mwisho ya misheni yake-akimwachaacha bintiye katika huduma ya jamaa zake.
Miaka michache baadaye, sasa wakiwa na watoto wanne , walihamia Missoula, Montana, ili baba yake aweze kuhudhuria chuo kikuu. Hata hivyo, walikuwa pale kwa miezi michache tu wakati Rais Spencer W. Kimball na Mzee Mark E. Petersen walipotoa wito kwa baba mkwe wangu ili kuwa rais wa kwanza wa kigingi kipya kilichoundwa cha Missoula. Alikuwa na miaka 34 tu. Mawazo ya chuo kikuu yaliachwa nyuma, alipotafuta kufanya mapenzi ya Bwana —si yake mwenyewe.
Wazaziwangu wamehudumu kama wafanyakazi wa ibada za hekaluni kwa zaidi ya miaka 30—Baba kama mfunganishaji, Mama kama mfanyakazi wa ibada. Pia wametumikia misheni tano—huko Riverside, California; Ulaanbaatar, Mongolia; Nairobi, Kenya; Hekalu la Nauvoo Illinois; na Hekalu la Monterrey. Huko Mexico, walijitahidi ili kujifunza lugha mpya, ambayo haikuwa rahisi kwa mwenye umri wa miaka 80. Lakini wao walitaka kufanya mapenzi ya Bwana badala ya kujiingiza katika tamaa zao wenyewe katika maisha.
Kwa Watakatifu wote wa siku za mwisho waliojitolea duniani kote, narudia maneno yalilosemwa na Bwana kwa nabii Nefi: “Umebarikiwa ewe, … kwa hivyo vitu ambavyo umefanya … bila kusita … … , hujatazamia maisha yako, lakini umetazamia kusudi langu, na kutii amri zangu.”8
Sisi tunapotafuta kufanya mapenzi ya Mungu kwa kumtumikia Yeye na wanadamu wenzetu kwa uaminifu, tunahisi idhini Yake na kwa kweli tunakuja kumjua Yeye.
Mjue kwa Kuwa kama Yeye
Mwokozi anatueleza kwamba njia bora sana ya kumjua Mungu ni kuwa kama Yeye. Alifundisha: “Kwa hivyo mnapaswa kuwa watu wa aina gani? Amin, nawaambia, hata kama vile nilivyo.”9
Ustahilivu ni muhimu ili kuwa kama Yeye. Aliamuru, “Jitakaseni; ndiyo, itakaseni mioyo yenu, na iosheni mikono yenu … niweze kuwafanya kuwa safi”10 Kuanzia katika barabara ya kuwa na kama Yeye, tunapotubu, kupokea msamaha Wake, na Yeye hutakasa nafsi zetu.
Ili kutusaidia tunapoendelea kumwelekea Baba, Bwana alitupatia ahadi hii: “Kila mtu atakayeziacha dhambi zake na kuja kwangu, na kulilingana jina langu, na kuitii sauti yangu, na kushika amri zangu, atauona uso wangu na kujua kwamba mimi ndiye.”11
Kupitia imani yetu katika dhabihu Yake ya upatanisho, Mwokozi hutusafisha, hutuponya, na Anatuwezesha kumjua kwa kuja kuwa kama Yeye. Mormoni alifundisha, “Ombeni kwa Baba kwa nguvu zote za moyo, … ili muwe wana [na mabinti] wa Mungu; kwamba wakati atakapoonekana tutakuwa kama Yeye.”12 Tunapojitahidi kuwa kama Mungu, Anaweza kutufanya zaidi kuliko tunavyoweza kujifanyia sisi wenyewe.
Mmjue kwa Kuwafuata Wanasihi
Ili kutusaidia katika juhudi zetu, Mungu ametupa mifano ya kuigwa na wanasihi. Nataka kushiriki nanyi hisia zangu kuhusu mmoja wa kwangu, Mzee Neal A. Maxwell. Yeye daima alitaka kusamilisha mapenzi yake kwa mapenzi ya Baba katika jitihada zake za kuwa kama Mungu.
Zaidi ya miaka 20 iliyopita, alishiriki nami hisia zake baada tu ya kupatikana na saratani Alkiniambia, “Nataka kuwa katika timu, upande huu [wa pazia] au upande ule mwingine. Sitaki kukaa kando. Nataka kucheza katika mchezo.”13
Katika wiki chache zilizofuata, alisita kumwomba Mungu amponye; alitaka tu kufanya mapenzi ya Mungu. Mkewe, Colleen, alisema kuwa kilio cha kwanza cha Yesu katika bustani ya Gethsemane kilikuwa “ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke. Hapo ndipo Mwokozi alisema, “walakini si kama nitakavyo bali kama utakavyo wewe..”14 Alimhimiza Mzee Maxwell kufuata mfano wa Mwokozi, ili kuomba msaada, na kisha kuwasilisha mapenzi yake kwa mapenzi ya Mungu, alifanya hivyo.15
Baada ya kupitia mateso ya kina, matibabu ya kudhoofisha kwa karibu mwaka moja, aliweza kurudi kabisa “katika mchezo.” Alihudumu kwa miaka saba zaidi.
Nilikuwa na kazi kadhaa pamoja naye katika miaka hiyo iliyofuata. Nilihisi ukarimu, huruma, na upendo wake. Nilishuhudia utakaso wake mwingi wa kiroho kupitia mateso yake yaliyoendelea na utumishi wake daima, kadiri alivyojitahidi kuwa kama Mwokozi.
Mfano na mnasihi wa msingi , anayepatikana kwetu sote, ni Bwana wetu na Mwokozi, Yesu Kristo, ambaye alisema: “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima: mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”16 “Njoo unifuate.”17
Kaka zangu wadogo na dada zangu, kumjua Mungu ni jitihada ya maisha yote. “Na uzima wa milele ndio huu, kwamba [sisi] tukujue wewe… Mungu pekee wa kweli, na Mwanao Yesu Kristo, ambaye [Baba] alimtuma.”18
“Je, si lazima sisi tuendelee katika kazi hii iliyo kuu? … Tuweni wajasiri, [marafiki zangu vijana]; na mbele, mbele kwenye ushindi!”19
Mungu anakujua wewe , na anakualika wewe kumjua Yeye. Omba kwa Baba, soma maandiko, tafuta kufanya mapenzi ya Mungu, jitahidi kuwa kama Mwokozi, na kuwafuata wanasihi wema. Unapofanya hivyo, wewe utaweza kumjua Mungu na Yesu Kristo, na utarithi uzima wa milele. Huu ni mwaliko wangu kwako, kama shahidi aliyeteuliwa na Wao. Wanaishi. Wanawapenda. Ninashuhudia hivyo katika jina la Yesu Kristo, Amina.