2010–2019
Lugha ya Injili
Aprili 2017


12:28

Lugha ya Injili

Mafundisho ya nguvu ni muhimu mno kuhifadhi injili katika nyumba zetu, na inahitaji bidii na jitihada.

Baada ya kuitwa kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka, Nilihama pamoja na familia yangu kutoka Costa Rica hadi Salt Lake City kwa kazi yangu ya kwanza. Hapa Marekani, Nimebarikiwa kutembelea watu wa ajabu wa mbari tofauti na tamaduni. Miongoni mwao ni wengi ambao, kama mimi, walizaliwa katika nchi za Amerika ya Kusini

Nimeona kwamba wengi wa uzao wa kwanza wa Wahispania hapa wanazungumza Kihispania kama lugha yao ya msingi na Kiingereza cha kutosha kuwasiliana na wengine. Uzao wa pili, ambao ama walizaliwa Merikani au walikuja wakiwa na umri mdogo na walihudhuria shule hapa, wanazungumza Kiingereza kizuri sana na labda baadhi Kihispania kibovu. Na mara kwa mara kwa uzao wa tatu, Kihispania, lugha ya asili ya mababu zao, imepotea.1

Katika mtajo wa isimu, hii kwa kawaida inaitwa “kupotea kwa lugha.” Kupotea kwa lugha kunaweza kutokea wakati familia zinapohamia nchi ya kigeni ambako lugha yao ya asili haina nguvu. Haitokei tu miongoni mwa Wahipania bali pia miongoni mwa watu duniani kote ambapo lugha ya wenyeji inabadilishwa kwa ajili ya kuenziwa kwa lugha mpya.2 Hata Nefi, nabii katika Kitabu cha Mormoni, alikuwa na hofu ya kupoteza lugha enyeji ya baba zake wakati alipokuwa anajiandaa kuondoka kwenda nchi ya ahadi. Nefi anaandika,“Na tazama, ni hekima katika Mungu tupate kuchukua haya maandishi, ili tuweze kuhifadhia watoto wetu lugha ya baba zetu.3

Lakini Nefi alikuwa pia na shaka kuhusu kupoteza aina ingine ya lugha. Katika mstari unaofuata,anaendelea, “Na pia kwamba tuwahifadhie maneno yaliyonenwa kwa vinywa vya manabii watakatifu, ambayo walipewa na Roho na nguvu za Mungu, tangu mwanzo wa ulimwengu, hadi nyakati za sasa.”4

Niliona kufanana kati ya kuhifadhi lugha ya mama na kuhifadhi injili ya Yesu Kristo katika maisha yetu.

Leo, katika analojia yangu, ningependa kusisitiza sio hasa lugha za kidunia bali kidogo lugha ya milele ambayo lazima ihifadhiwe katika familia zetu na kamwe isipotee. Nazungumzia juu ya lugha5 ya injili ya Yesu Kristo. Kwa “lugha ya injili,” Namaanisha mafundisho yote ya manabii wetu, utii wetu kwa mafundisho hayo, na kwa kufuata kwetu desturi za haki.

Nitajadili njia tatu ambazo lugha hii inaweza kuhifadhiwa.

Kwanza: Kuwa na bBidii Zaidi na Kujali Nyumbani

Katika Mafundisho na Maagano, Bwana aliwaalika waumini wengi mashuhuri wa Kanisa, pamoja na Newel K. Whitney, kuweka nyunba zao sawa. Bwana alisema, “Mtumishi wangu Newel K, Whitney … inafaa akemewe, na kuirekebisha nyumba yake, na kuona kuwa wanakuwa na bidii na wenye kujali nyumbani, na kuomba daima, au vinginevyo wataondoshwa kwenye nafasi yao.”6

Kitu kimoja ambacho kinashawishi upotevu wa lugha ni wakati wazazi hawatumii muda kufundisha watoto wao lugha ya asili. Haitoshi tuu kuzungumza lugha nyumbani. Kama wazazi wanatamani kuhifadhi lugha yao, lazima iwe inafundishwa. Utafiti umepata kwamba wazazi ambao wanafanya juhudi za kudhamiria za kuhifadhi lugha yao enyeji uenda wakafanikiwa katika kufanya hivyo.7 Kwa hiyo juhudi za kudhamiria za kuhifadhi lugha ya injili ni nini?

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitahadharisha kwamba “mafundisho na mtindo hafifu wa injili nyumbani” ni sababu yenye nguvu ambayo inaweza kuvunja mduara wa familia wenye wingi wa uzao katika Kanisa.8

Tunaweza kwa hiyo kuhitimisha kwamba mafundisho yenye nguvu ni muhimu mno katika kuhifadhi injili nyumbani kwetu, na inahitaji bidii na jitihada.

Tumealikwa mara nyingi kupata mazoezi ya kila siku ya mafunzo ya injili ya familia na binafsi.9 Familia nyingi ambazo zinafanya hivyo zinabarikiwa kila siku na umoja mkuu na uhusiano wa karibu na Bwana.

Baba na bintiye wakijifunza maadiko

Mafundisho ya kila siku ya maandiko yatafanyika lini? Yatafanyika wakati wazazi wakichukua maandiko mkononi na pamoja kwa upendo, kualika familia ikusanyike pamoja kujifunza. Ni vigumu kuona mafundisho haya yakitokea katika njia yoyote ingine.

Familia ikijifunza maandiko

Akina Baba na akina mama, msikose baraka hizi kuu. Usingoje mpaka uchelewe mno!

Pili: Mtindo wa Nguvu Nyumbani

Mtaalamu wa isimu aliandika kwamba kuhifadhi lugha enyeji, “unahitaji kuifanya lugha hiyo kuwa hai kwa watoto wenu.”10 “Tunaifanya lugha kuwa hai” tunapofundisha na kufanya mtindo wa kufanya pamoja.

Wakati nilipokuwa kijana, Nilifanya kazi katika kiwanda cha Baba yangu wakati wa likizo. Swali langu la baba yangu daima aliuliza baada ya mimi kupokea mshahara wangu lilikuwa “Utafanya nini ni hela zako?

Nilijua jibu na nilijibu, “Nitalipa zaka na niweke akiba ya misheni yangu.”

Baada ya kufanya pamoja naye kwa karibu miaka minane na kila mara kujibu swali hilo hilo, baba yangu aliona amenifundisha kuhusu kulipa zaka. Kile yeye hakutambua ni kwamba nilijifunza kanuni hii muhimu ndani ya wikiendi moja. Acheni niwaambie jinsi nilivyojifunza kanuni hiyo.

Baada ya baadhi ya matukio yaliyohusiana na vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Amerika ya Kati, biashara ya baba yangu ilifilisika. Alikwenda kutoka takribani wafanyakazi 200 wa kudumu mpaka wachache chini ya waendeshaji mashine 5 wa kushona waliofanya kazi kama walivyotakiwa katika karakana ya nyumbani kwetu. Siku moja, wakati wa muda huo mgumu, Niliwasikia wazazi wangu wakijadili kama wangelipa zaka au kununua chakula kwa watoto.

Siku ya Jumapili nilimfuata baba yangu kuona nini alikuwa anakwenda kufanya. Baada ya mikutano yetu ya Kanisa, Nilimwona akichukua bahasha na kuweka zaka yake ndani. Ile ilikuwa sehemu tuu ya somo. Swali ambalo lilibaki kwangu lilikuwa nini tutakula.

Mapema asubuhi ya Jumatatu watu fulani waligonga mlango wetu. Nilipoufungua, walitaka kumwona baba yangu. Nilimwita, na wakati alipofika, wageni walimwambia kuhusu agizo la haraka muhimu la ushonaji waliohitaji haraka iwezekanavyo. Walimwambia kwamba agizo lilikuwa la muhimu sana wangelilipia chambele. Siku ile nilijifunza kanuni za kulipia zaka na baraka ambazo hufuata.

Katika Agano Jipya, Bwana anazungumzia kufanya mtindo. Yeye anasema “Amini, amini, nawaambia, mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda, kwa maana yote ayatendayo yeye ndiyo ayatendayo Mwana vilevile.”11

Kuhudhuria hekalu

Haitoshi tu kusema kwa watoto wetu kuhusu umuhimu wa ndoa ya hekaluni, kufunga, na kuitakasa siku ya Sabato. Lazima watuone sisi tukiweka nafasi katika ratiba zetu kuhudhuria hekaluni mara kwa mara kadiri tunavyoweza. Wanahitaji kuona ahadi yetu ya kufunga mara kwa mara12 na kuitakasa siku yote ya Sabato takatifu. Kama vijana wetu hawawezi kufunga milo miwili, hawawezi kujifunza maandiko mara kwa mara, na hawawezi kuzima TV wakati wa mchezo mkubwa siku ya Jumapili, wataweza kuwa na nidhamu binafsi ya kiroho kuzuia majaribu yenye nguvu ya changamoto za leo za ulimwengu, ikijumuisha majaribu ya ponografia?

Tatu: Mila

Njia ingine lugha inaweza kubadilishwa au kupotea ni wakati lugha zingine na mila zimechanganywa na lugha ya mama.13

Katika miaka ya mwanzo ya Kanisa la urejesho, Bwana aliwaalika waumini maarufu wengi wa Kanisa kuweka nyumba zao sawa. Alianza mwaliko Wake kwa kuwaeleza njia mbili tunaweza kupotea nuru na ukweli kutoka kwenye nyumba zetu: “Na yule mwovu huja na kuziondoa nuru na kweli, kwa kutotii, kutoka kwa mwanadamu, na kwa sababu ya mapokeo ya baba zao.14

Kama familia, tunahitaji kuepuka mila yoyote ambayo itatuzuia sisi kutoifanya siku ya Sabato kuwa takatifu au kuwa na mafunzo ya maandiko kila siku na maombi nyumbani. Tunahitaji kufunga milango ya dijitali ya nyumbani mwetu kwa ponografia na vishawishi vingine vyote viovu. Kupambana na mila za kilimwengu za siku zetu, tunahitaji kutumia maandiko na sauti ya manabii wetu wa kisasa kufundisha watoto wetu kuhusu utabulisho wao mtakatifu, azima yao katika maisha, na ujumbe mtakatifu wa Yesu Kristo.

Hitimisho

Katika maandiko, tunakuta mifano kadha ya “upotevu wa lugha.”15 Kwa mfano:

“Sasa ikawa kwamba kulikuwa na wengi wa uzazi mchanga ambao hawakufahamu maneno ya mfalme Benyamini, kwani walikuwa watoto wadogo alipowazungumzia watu wake; na hawakuamini mila za babu zao.  …

“Na sasa kwa sababu ya kutoamini kwao hawakufahamu neno la Mungu; na mioyo yao ilikuwa imeshupazwa.”16

Kwa kizazi kinachochipua, injili ikawa lugha geni. Na wakati faida za kudumisha lugha ya asili mara nyingi zinajadiliwa, katika mazingira ya mpango wa wokovu, hakuna mjadala kuhusu matokeo ya milele ya kupoteza lugha ya injili katika nyumba zetu.

Mama akiomba pamoja na mwanawe mdogo

Kama watoto wa Mungu, sisi ni watu ambao si kamili tunajaribu kujifunza lugha iliyokamilika.17 Jinsi kama mama alivyo mwenye huruma na watoto wake wadogo, Baba yetu wa Mbinguni ni mvumilivu na kutokamilika kwetu na makosa yetu. Anathamini na kuelewa matamko yetu yaliyo dhaifu sana, yaliyomun’gunywa katika ukweli, kama vile yalikuwa mashairi laini; Anafurahia sauti yetu ya kwanza ya maneno ya injili. Yeye hutufundisha kwa upendo kamili.

Familia ikiomba pamoja

Hakuna mafanikio katika maisha haya, muhimu kama inavyoweza kuwa, kama tutapoteza lugha ya injili katika familia zetu.18 Ni ushuhuda wangu kwamba Baba wa Mbinguni atatubariki katika juhudi zetu wakati tunapojitahidi kukumbatia lugha Yake, hata mpaka tunakuwa fasaha katika ngazi hii ya juu ya mawasiliano, ambayo siku zote ilikuwa lugha mama yetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Miongoni mwa Wahispania, wa kizazi cha tatu “kiwango cha utumia wa lugha mpja ya Kiingereza ni … asilimia 72” (Richard Alba, “Bilingualism Persists, but English Still Dominates,” Migration Policy Institute, Feb. 1, 2005, migrationpolicy.org/article/bilingualism-persists-english-still-dominates).

  2. Kuzungumza Kiingereza peke yake ni mtindo wa kizazi cha tatu” (Alba, “Bilingualism Persists, but English Still Dominates”).

  3. 1 Nefi 3:19 ; mkazo umeongezewa.

  4. 1 Nefi 3:20; mkazo umeongezewa.

  5. Lugha inaweza kuelezewa kama “mfumo wa mawasiliano yanyotumika kwa nchi au jamii fulani” (Oxford Living Dictionaries, en.oxforddictionaries.com/definition/language).

  6. Mafundisho na Maagano 93:50; mkazo umeongezewa.

  7. “[Kuhifadhi kugha enyeji] inawezekana, lakini huitaji kujitolea na mpango” (“Heritage Languages: Fighting a Losing Battle?”onraisingbilingualchildren.com/2013/03/25/heritage-languages-fighting-a-losing-battle). “Kwa mfano wazungumzaji wa Kijerumani katika Marekani ya Kati walifanikiwa katika kudumumisha lugha ya mama kwa vizazi vingi” (Alba, “Bilingualism Persists, but English Still Dominates”).

  8. David A. Bednar, General Conference Leadership Meeting, Apr. 2015.

  9. Mfano mmoja wa kisasa ni maelekezo kutoka kwa Urais wa Kwanza: “Tunawasahuri wazazi na watoto kupatia kipaumbele maombi ya familia, jioni ya familia nyumbani, kujifunza injili na maelekezo, na shughuli za kufaa kwa familia” (First Presidency letter, Feb. 11, 1999).

  10. “Mnahitajika kuifanya lugha kuwa hai kwa watoto wenu, ili kwamba waweze kuelewa na kuwasilia na kuhisi kuwa sehemu ya watu wanaowakilisha na lugha hiyo” (Crisfield, “Heritage Languages: Fighting a Losing Battle?”); emphasis added.

  11. Yohana 5:19.

  12. “Kuishikia siku ya mfungo vyema hujumuisha kutokula chakula na kuja kwa milo miwili kwa kipindi cha saa 24, kuhudhuria mkutano wa mfungo na ushuhuda, na kutoa matoleo ya mfungo kwa ukatimu ili kuwasaidia wale walio na mahitaji” (Handbook 2: Administering the Church [2010], 21.1.17).

  13. Ona Omni 1:17.

  14. Mafundisho na Maagano 93:39; mkazo umeongezewa.

  15. Katika mkutadha katika hotuba hii, “kupoteza lugha” inarejea jinsi injili inaweza kupotea (ona Waamuzi 2:10; Omni 1:17; 3 Nefi 1:30).

  16. Mosia 26:1, 3; mkazo umeongezwa

  17. Ona Mathayo 5:48; 3 Nefi 12:48.

  18. Ona Mathayo 16:24–26.