Uwe Hodari na Moyo wa Ushujaa
Acha sisi tuwe na ujasiri wa kukataa makubaliano, ujasiri wa kisimama kwa kanuni.
Ndugu zangu wapendwa, ni vyema sana kuwa nanyi tena. Naomba kwamba niweze kuwa na usaidizi wa kiungu ninapotumia fursa hii kuwahutubia.
Zaidi ya wale waliokusanyika katika Kituo cha Mkutano hiki, kuna maelfu wengine zaidi waliokusanyika katika makanisa na katika mazingira mngine kote duniani. Sote tuna kamba zinazofunga sote pamoja, kwa sababu tumethaminiwa na kuwa na ukuhani wa Mungu.
Tuko hapa duniani katika kipindi cha ajabu katika historia yake. Nafasi zetu karibu hazina kipimo, na bado tunakumbana pia na changamoto nyingi, baadhi yazo za kipekee kwa wakati wetu.
Tunaishi katika ulimwengu ambapo maadili yametupiliwa mbali kwa kiasi kikubwa, ambapo dhambi imeanikwa wazi, na ambapo majaribu kupotoka kutoka kwenye njia nyembamba na iliyosonga yanatuzunguka. Tunakabiliwa na mashinikizo yasiyokoma na ushawishi wa kudanganya unaoharibu kile ambacho ni cha heshima na kujaribu kukibadilisha na falsafa na utamaduni duni.
Kwa sababu hizi na changamoto zingine, maamuzi daima yako mbele yetu ambayo yanaweza kuamua hatima yetu. Ili kwetu sisi kufanya maamuzi sahihi, ujasiri unahitajika---ujasiri wa kusema hapana wakati tunapaswa, ujasiri wa kusema ndio wakati inafaa, ujasiri wa kufanya jambo la haki kwa sababu ni la haki.
Kwa sababu viwango vya jamii hivi sasa kwa haraka vinaachana kwa mbali na maadili na kanuni ambazo Bwana ametupa, sisi bila shaka tutaitwa kutetea kile ambacho tunaamini. Je, tutakuwa na ujasiri wa kufanya hivyo?
Rais J. Reuben Clark Jr., ambaye kwa miaka mingi alikuwa mshiriki wa Urais wa Kwanza, alisema: “Zinajulikana kesi ambapo [wale] wa imani ya kudhaniwa … wamehisi kwamba, kwa sababu ya kudhibitisha imani yao kamili huenda wakajiitia kejeli ya wenzao wasioamini, lazima aidha warekebishe au kuelezea vyema imani yao, ama kuizimua kiuangamizi, ama hata kujifanya kuitupilia mbali. Watu kama hao ni wanafiki.”1 Hakuna yeyote miongoni mwetu angependa kuitwa mnafiki, na bado tunasita kutangaza imani yetu katika hali fulani. ?
Tunaweza kujisaidia katika hamu yetu ya kufanya mema tukijiweka katika maeneo na kushiriki katika shughuli ambapo mawazo yetu yanashawishiwa kwa ajili ya mema na ambapo Roho wa Bwana atasikia vizuri kuwa.
Nakumbuka nikisoma hapo awali ushauri ambao baba alimpa mwanawe wakati akienda shule: “Ukiwahi kujipata mahali ambapo haupaswi kuwa, ondoka!” Nawapa kila mmoja wenu ushauri huo huo: “Ukijikuta wakati wowote mahali ambapo haupaswi kuwa, ondoka!”
Sote tunahitaji kila mara kuwa na ujasiri. Kila siku ya maisha yetu ujasiri unahitajika---si tu kwa ajili ya matukio makubwa, lakini mara nyingi zaidi tunapofanya maamuzi ama kutenda kwa ajili ya hali zilizo karibu nasi. Mshairi na mwandishi Mskoti Robert Louis Stevenson alisema: “Kila siku ujasiri una mashahidi wachache. Lakini ujasiri wako bado una heshima hata kama hakuna anayekutia moyo na hakuna umati unaokusifu.”2
Ujasiri huja kwa njia nyingi. Mwandishi Mkristo Charles Swindoll aliandika: “Ujasiri hauko tu kwenye uwanja wa vita … ama kwa kumshika kiushujaa mwizi katika nyumba yako. Vipimo halisi vya ujasiri ni kimya sana. Ni majaribio ya kindani, kama vile kubaki mwaminifu wakati hakuna mtu anayeangalia, … kama kusimama peke yako wakati watu hawaelewi imani yako.”3 Ningeongezea kwamba ujasiri huu wa ndani pia unajumuisha kufanya jambo la haki hata kama huenda kuwa unahofia, kutetea imani yetu katika hatari ya kudharauliwa, na kudumisha imani hizo hata baada ya kutishwa na kupoteza marafiki ama hadhi ya kijamii. Yule ambaye anasimama dhabiti kwa yale ambayo ni ya haki lazima ahatarishe kuwa wakati mwingine hakubaliwi na kukosa umaarufu.
Nilipokuwa nikihudumu katika Jeshi la Majini la Marekani nilikuja kujua kuhusu matendo ya ujasiri, matukio ya ushujaa, na mifano ya ujasiri. Mmoja ambao kamwe sitawahi sahau ilikuwa ujasiri usio wazi wa mwana maji wa umri wa miaka 18---sio wa imani yetu---ambaye hakuogopa kusali. Kwa watu 250 katika kitengo chetu, alikuwa ndiye peke yake ambaye kila usiku alipiga magoti kando ya kitanda chake, wakati mwingine akiwa anakejeliwa na kuchekwa na wasioamini. Akiwa ameinamisha kichwa, alimwomba Mungu. Kamwe hakuogopa kuomba. Kamwe hakuyumba. Alikuwa na ujasiri.
Muda mfupi uliopita, nilisikiliza mfano wa mtu ambaye hakika alionekana kukosa ujasiri huu wa ndani. Rafiki alisimulia kuhusu mkutano wa sakramenti wa kiroho na wa kukuza imani ambao yeye na mumewe walikuwa wamehudhuria katika kata yao. Mvulana aliyekuwa katika ofisi ya mkuhani katika Ukuhani wa Haruni aligusa mioyo ya mkusanyiko mzima alipozungumzia kweli za injili na furaha za kutii amri. Alishuhudia kwa dhati akisimama kwenye mimbari, akionekana kuwa msafi na nadhifu akiwa amevaa shati yake nyeupe na tai.
Baadaye siku hiyo hiyo, mwanamke huyu na mumewe walipokuwa wanaondoka kule, walimuona mvulana yule yule ambaye alikuwa amewavutia sana saa chache tu awali. Sasa, hata hivyo, alionekana kubadilika kabisa akitembea barabarani akiwa amevaa nguo chafu---na anavuta sigara. Rafiki yangu na mumewe hawakuwa wamesikitishwa sana na kuhuzunika tu, lakini pia walichanganyikiwa na jinsi angeweza kusadikisha kuonekana kuwa mtu mmoja katika mkutano wa sakramenti na kisha haraka hivyo kuonekana kuwa mtu mwingine kabisa.
Ndugu, je, wewe ni mtu yule yule popote ulipo na katika chochote unachofanya---mtu Baba yetu wa Mbinguni anataka uwe na mtu unajua unapaswa kuwa?
Katika mahojiano yaliyochapishwa katika gazeti ya kitaifa, mchezaji aliyejulikana wa mpira wa kikapu wa NCAA Mmarekani anayeitwa Jabari Parker, mshiriki wa Kanisa, aliombwa ashiriki ushauri bora kabisa aliokuwa amepokea kutoka kwa baba yake. Jabari alijibu, “[Baba Yangu] alisema, kuwa mtu yule yule unapokuwa peke yako na vivyo hivyo unapokuwa mbele ya watu.”4 Ushauri muhimu, ndugu zangu, kwetu sisi sote.
Maandiko yetu yamejaa mifano ya aina ya ujasiri unaohitajika na kila mmoja wetu leo. Nabii Danieli alionyesha ujasiri mkuu kutetea aliyoyajua kuwa ya haki na kwa kuonyesha ujasiri wa kuomba, ingawa alitishwa na kifo kama angefanya hivyo.5
Abinadi aliishi maisha ya ujasiri, ilivyoonyeshwa na kukubali kifo badala ya kukana ukweli.6
Si sote tunavutiwa na maisha ya vijana askari 2,000 wana wa Helamani, waliofundisha na kuonyesha umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kufuata mafundisho ya wazazi, kuwa waadilifu na wasafi?7
Pengine kila moja ya hadithi hizi za maandiko zimepambwa na mfano wa Moroni, ambaye alikuwa na ujasiri wa kustahimili katika haki hadi mwisho.8
Katika maisha yake yote, Nabii Joseph Smith alitoa mifano isiyohesabika ya ujasiri. Mojawapo wa mfano mkubwa zaidi ulitokea wakati yeye na ndugu wengine walifungwa minyororo pamoja---fikiria, kufungwa minyororo pamoja---na kufungiwa katika nyumba ambayo haijamalizika karibu na jumba la mahakama kule Richmond, Missouri. Parley P. Pratt, ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliofungwa, aliandika kuhusu usiku mmoja: “Tulikuwa tumelala ni kama tuko usingizini mpaka saa ya usiku wa manane kupita, na tulikuwa tumehuzunika sana, wakati tulikuwa tumesikiliza kwa masaa kejeli mbaya, maneno mabaya, kashfa kubwa na lugha chafu ya walinzi wetu.”
Mzee Pratt aliendelea:
“Nilikuwa nimesikiliza hadi nikachukizwa, nikasikitika, nikahudhika, na kujawa na roho ya haki ya kukasirika kwamba ilikuwa vingumu kwangu kujizuia kusimama na kuwakemea walinzi, lakini [mimi] sikuwa nimemwambia Joseph chochote, ama mtu yeyote mwingine, ingawa nilikuwa nimelala karibu naye na nilijua kwamba alikuwa macho. Ghafla, alisimama na kuzungumza kwa sauti ya nguvu kama mgurumo wa simba, akisema, vyema ninavyoweza kukumbuka, maneno yafuatayo:
“‘NYAMAZENI. ... Katika jina la Yesu Kristo nawakemea ninyi, na kuwaamurisha mtulie; sitaishi dakika ingine na kusikia lugha kama hiyo. Komeni kuongea hivyo, ama ninyi au mimi nife SAA HII!’”
Joseph “alisimama wima katika enzi ya kutisha,” kama ilivyoelezwa na Mzee Pratt. Alikuwa amefungwa kwa minyororo, bila silaha, na bado alikuwa mtulivu na mwenye heshima. Aliwaangalia walinzi waliohofia, ambao walikuwa wanarudi nyuma kwenye kona wakijikunyata miguu. Watu hawa walioonekana kutorekebishika waliomba msamaha kwake na wakabaki kimya.9
Si vitendo vyote vya ujasiri huleta matokeo ya kuvutia kama hayo ama ya mara moja, na bado yote huleta amani akilini na maarifa kwamba haki na ukweli umetetewa.
Ni vigumu kusimama vima wakati mtu anapanda mzizi yake kwenye changarawe inayonyong’onyea ya maoni na idhinisho linalobobea. Ujasiri kama ule wa Danieli, Abinadi, Moroni ama Joseph Smith unahitajika ili tubaki imara na dhabiti kwa yale tunayojua ni mema. Walikuwa na ujasiri wa kufanya kile ambacho akikuwa rahisi, bali kile kilichokuwa sahihi.
Sote tutakumbana na hofu, tutakejeliliwa, na kukutana na upinzani. Acheni sisi —sisi sote—tuwe na ujasiri kushinda yanayopendelewa na wengi, ujasiri wa kutetea kanuni zetu. Ujasiri, si kuridhisha, hutuletea tabasamu ya idhini ya Mungu. Ujasiri unakuwa sifa ya uwezo na ya kuvutia wakati unachukuliwa si tu kama nia ya kufa kidume lakini pia kama uamuzi wa kuishi kwa heshima. Tunavyosonga mbele, tukijitahidi kuishi kama tunavyopaswa, hakika tutapokea msaada kutoka kwa Bwana na tunaweza kupata faraja katika maneno Yake. Naipenda ahadi Yake katika kitabu cha Yoshua:
“Sitakupungukia wala sitakuacha. …
“...Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.”10
Ndugu zangu wapendwa, kwa ujasiri wa imani yetu, tutangazeni, pamoja na Mtume Paulo, “Siionei haya Injili ya Kristo.”11Kisha, kwa ujasiri huo huo, tufuateni ushauri wa Paulo : “Uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo, na katika roho na imani na usafi.”12
Migogoro ya janga huja na kwenda, lakini vita vinavyopigwa kwa nafsi za watu vinaendelea bila kukoma. Kama mwito linakuja neno la Bwana kwenu, kwangu mimi, na kwa wenye ukuhani kila mahali: “Kwa sababu hiyo, sasa acha kila mtu na ajifunze wajibu wake, na kutenda kazi katika ofisi ambayo ameteuliwa, kwa bidii yote.”13 Kisha tutakuwa, kama vile Mtume Petro alivyotangaza, hata “ukuhani wa kifalme,”14na umoja katika kusudi na kubarikiwa na nguvu kutoka mbinguni.15
Acha kila mmoja wetu aondoke usiku wa leo akiwa na dhamira na ujasiri wa kusema, pamoja na Ayubu wa kale, “Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,...sitajiondolea uelekevu wangu.”16 Naomba kwa unyenyekevu kwamba hii iweze kuwa hivyo katika jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Amina.