Nabii Joseph Smith
Mafunuo ambayo yalitiririka juu ya Joseph Smith yanathibitisha kwamba yeye alikuwa nabii wa Mungu.
Ono la Kwanza
Mvulana mdogo anasoma Biblia, na macho yake yanatua kwenye kishazi kimoja cha maandiko. Huu ni wakati ambao utabadilisha ulimwengu.
Ana dukuduku la kujua ni kanisa gani linaloweza kumwongoza kwenye ukweli na wokovu. Amejaribu karibu kila kitu kingine, na sasa anageukia Biblia na kusoma maneno haya: “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.”1
Anatafakari juu yake zaidi na zaidi sana. Mwangaza hafifu wa kwanza unapenya katika giza. Hili ni jibu, njia ya kutoka kwenye mkanganyiko na giza? Inaweza kuwa rahisi hivi? Muulize Mungu na Yeye atajibu? Baada ya muda yeye anaamua yeye sharti amuulize Mungu au daima atabakia katika giza na mkanganyiko.
Na hali akiwa na dukuduku kama alivyokuwa, hakimbii pembeni kimya na kwa mchachariko anatoa sala kwa haraka. Yeye ana miaka 14 tu, lakini katika hima ya kujua, yeye hana haraka. Haya si maombi yoyote tu. Anachagua pale pa kwenda na kisha akafanya jaribio. Anajitayarisha kuongea na Mungu.
Na kisha siku ikaja. Ni “asubuhi ya siku maridadi angavu, msimu wa kuchipua mapema ya mwaka wa [1820].”2 Alitembea peke yake katika utulivu wa kichaka kilicho karibu chini ya miti aliyokuwa mirefu juu yake. Anafika mahali ambapo yeye alikuwa anadhamiria kwenda. Anapiga magoti na kutoa shauku za moyo wake.
Akieleza kile kinachotendeka baadaye, anasema:
“Niliona nguzo ya mwanga juu ya kichwa changu, ambao ulikuwa ni mng’aro uliozidi mwangaza wa jua, ambao ulishuka taratibu hadi ukashuka juu yangu.
“… Mwanga ulipotua juu yangu nikawaona Viumbe wawili, ambao mng’aro na utukufu wao wapita maelezo yote, wakiwa wamesimama juu yangu angani. Mmoja wao akaniambia, akiniita mimi kwa jina na kusema, huku akimwonyesha yule mwingine—[Joseph,] Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!”3
Miaka 24 tu baadaye, Joseph Smith na kaka yake Hyrum watakufa kwa sababu ya kile kilichoanzia hapa.
Upinzani
(Joseph) alisema kwamba alipokuwa na umri wa miaka 17, malaika alimwambia kwamba “jina lake litafikiriwa kwa mema na maovu miongoni mwa mataifa yote, … miongoni mwa watu wote.” 4 Unabii huu wa ajabu unaendelea kutimia leo wakati Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linaposambaa kote ulimwenguni.
Upinzani, ukosoaji, na uhasama ni wenzi wa ukweli. Wakati wowote ukweli kuhusu madhumuni na kudra ya binadamu unapofunuliwa, kutakuwa daima na juhudi za kuupinga. Kuanzia na Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni, mpaka kwenye huduma ya Kristo, na kuendelea hadi siku yetu, daima kumekuwa na kutakuwa na juhudi za kudanganya, kupotosha, kupinga, na kuvuruga mpano wa uzima.
Tafuta wingu kubwa la vumbi linalotanda juu ya taka kuu ambazo zinatupiwa Mtu ambaye alipingwa sana, kubishwa, na kukataliwa, kutengwa, na kusulubiwa, Mtu ambaye aliteremka chini ya vitu vyote, na hapo utapata ukweli, Mwana wa Mungu, Mwokozi wa wanadamu wote. Kwa nini hawangemwacha peke Yake ?
Kwa nini? Kwa sababu Yeye ni ukweli, na ukweli kila mara utapingwa.
Na kisha utafute mtu ambaye alileta ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo na maandiko mengine, tafuta mtu ambaye alikuwa chombo ambacho kwacho ujalivu wa injili na Kanisa la Yesu Kristo lilirejeshwa ulimwenguni, mtafute yeye na utarajie kuona taka zikiruka. Kwa nini asiachwe?
Kwa nini? Kwa sababu yeye alifundisha ukweli, na ukweli kila mara utapingwa
Gharika ya Ufunuo
Mafunuo ambayo yalitiririka juu ya Joseph Smith yanathibitisha kwamba yeye ni nabii wa Mungu. Acha tuangalia baadhi yao, hebu angalia baadhi ya nuru na ukweli uliofunuliwa kupitia kwake ambao unaangaza kinyume wazi na imani za kawaida za siku yake na siku yetu.
-
Mungu ni kiumbe binafsi, kilichoinuliwa, Baba wa Milele. Yeye ni Baba yetu.
-
Mungu Baba, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu ni viumbe tofauti.5
-
Wewe ni zaidi kuliko binadamu. Wewe ni mtoto wa Mungu Baba wa Milele, na unaweza kuwa kama Yeye6 kama utakuwa na imani katika Mwanawe, kutubu, kupokea maagizo, kupokea Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho.7
-
Kanisa la Yesu Kristo leo kimsingi ni Kanisa lile lile Aliloanzisha hapo kale wakati wa huduma Yake ya duniani, akiwa na manabii na mitume, Ukuhani wa Melkizedeki na Walawi, wazee, makuhani wakuu, mashemasi, walimu, maaskofu, na sabini, wote jinsi walivyoelezwa katika Biblia..
-
Mamlaka ya Ukuhani yaliondolewa duniani kufuatia vifo vya Mwokozi na Mitume Wake na yalirejeshwa tena katika siku zetu.
-
Ufunuo haujakoma, na mbingu hazijafungwa. Mungu huongoea na manabii leo, na Yeye ataongea na wewe na mimi pia.8
-
Kuna mengi baada ya maisha haya kuliko tu mbinguni na jehanamu. Kuna vyeo vya utukufu, na inajalisha sana kile tunachokifanya katika maisha haya.9
-
Zaidi kuliko kuwa na tu imani baridi katika Kristo tunapaswa “kumtegemea [Yeye] katika kila wazo,”10nawe utafanya yale yote uyafanyayo katika jina la Mwana,”11 na “daima kumkumbuka, na kushika amri … ili daima Roho wake apate kuwa pamoja [nasi].” 12
-
Mabilioni ya wale wanaoishi na kufa bila injili na maagizo yanayohitajika kwa ajili ya wokovu hawajapotea. Kupitia Upatanisho wa Kristo, wanadamu wote “wanaweza kuokolewa, kwa utiifu wa sheria na maagizo ya Injili,”13 yanayofanywa kwa wote walio hai na wafu.14
-
Kila kitu hakikuanzia na kuzaliwa. Wewe uliishi mapema katika uwepo wa Mungu kama mwana au binti Yake na kujitayarisha kwa ajili ya maisha haya ya duniani. 15
-
Ndoa na familia si mapatano ya wanadamu mpaka kifo kitakapotutenganisha. Inatakiwa kuwa ya milele kwa maagano tunayofanya na Mungu. Familia ni mpangilio wa mbinguni.16
Na hii ni sehemu tu ya gharika ya ufunuo uliotiririka juu ya Joseph Smith. Ni wapi haya yote yalitokea mafunuo haya yanayotoa nuru kwa giza, uwazi kwa shaka, na ambayo yameongoza na kujenga mamilioni ya watu? Ambayo inawezekana, kwamba aliyaota haya yote mwenyewe au alikuwa na msaada kutoka Mbinguni? Je! Maandiko aliyotoa yanaonekana kama maneno ya mtu au maneno ya Mungu?
Hatimisho
Hamna ubishi kuhusu kile Joseph Smith alitimiza, ni tu kile yeye alifanya na kwa nini. Na hamna mbadala. Yeye alikuwa aidha ni mtu wa kujisingizia au nabii. Aidha alifanya kile alifanya peke yake au alipata msaada kutoka mbinguni. Angalia ushahidi, lakini angalia ushahidi wote, picha mipangilio yote ya maisha yake, wala si sehemu moja pekee. Cha muhimu sana, fanya kama kijana Joseph alivyofanya na “uliza … Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye [atakupa wewe].” 17 Hii siyo tu jinsi unaweza kujua ukweli kuhusu Kitabu cha Mormoni na Joseph Smith, pia ndiyo mpangilio wa kujua ukweli wa vitu vyote. 18
Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu, kama alivyo Thomas S. Monson leo. Kupitia Joseph Smith, funguo za ufalme wa Mungu “zakabidhiwa [tena] kwa mwanadamu duniani, na … injili itaenea … kama vile jiwe lililochongwa mlimani bila kazi ya mikono… ,hadi litaijaza dunia yote.”19
Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, na Yesu ndiye Kristo. Tunawaabudu Wao. Hakuna chochote kinachoweza kulinganishwa na uumbaji Wao, mpango wa wokovu, na dhabihu ya upatanisho ya Mwanakondoo wa Mungu. Katika kipindi hiki, tunatimiza mpango wa Baba na kupokea matunda ya Upatanisho tu kwa utiifu wa sheria na maagizo ya injili iliyorejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith. Mimi natoa ushuhuda Wao—Mungu Baba wa Milele na Yesu Kristo Mwokozi wa ulimwengu. Na ninafanya hivyo katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.