2010–2019
Mabinti katika Agano
Aprili 2014


17:7

Mabinti katika Agano

Ile njia … tunalazimika kuchukua katika safari yetu ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni … imepambwa na maangano matakatifu na Mungu.

Tumefunzwa na uwezo wa kiroho usiku wa leo. Natumaini kwamba maneno yaliyozungumzwa na hawa viongozi akina dada wakuu yataingia moyoni mwenu kama yalivyoingia wangu.

Huu ni mkutano muhimu wa kihistoria. Wanawake wote wa Kanisa wenye umri wa miaka nane na zaidi wamealikwa wajiunge nasi usiku wa leo. Wengi wetu tumeomba kwamba Roho Mtakatifu angekuwa nasi. Baraka hiyo iliridhiwa sisi tulipowasikia akina dada hawa wakizungumza na kusikiliza muziki wa kuinua. Natumaini kwamba Roho ataendelea kuwa nasi ninaposhiriki maneno machache ya himizo na ushuhuda kuongezea yale tayari yamesemwa---na hasa kushuhudia kwamba kile sisi tumeambiwa ni kile Bwana anngependa sisi tusukie.

Nitazungumza usiku wa leo kuhusu njia----ambayo kwayo njia maridadi zimeelezwa leo---kwamba lazima tuchukue kwenye safari yetu kurudi kwa Baba wetu wa Mbinguni. Njia hiyo imepambwa na maagano matakatifu na Mungu. Nitazungumza nanyi kuhusu furaha ya kufanya na kuweka maagano hayo na kuwasaidia wengine kuyaweka.

Wengi wenu mlibatizwa hivi karibuni na kupokea karama ya Roho Mtakatifu kwa kuwekelewa mikono. Kwenu ninyi, kumbukumbu hiyo ni wazi. Wengine walibatizwa kitambo, hivyo basi kumbukumbu ya hisia zenu za tukio hilo la agano huenda ikawa si wazi sana, lakini baadhi ya hisia hizo hurudi tunaposikiliza maombi ya sakramenti.

Hakuna atakaye kuwa na kumbukumbu sawa na mwingine ya siku tuliofanya agano hilo tukufu la ubatizo na kupokea karama ya Roho Mtakatifu. Lakini sote tulihisi idhini ya Mungu. Na tulihisi hamu ya kusamehe na kusamehewa na ongezeko la uamuzi kufanya mema.

Kiasi hisia hizo zilichoma mioyo yenu iliamuliwa kwa kiasi kikubwa na jinsi ulivyotayarishwa na watu wapendwa. Natumaini kwamba wale wenu ambao mlibatizwa Kanisani hivi karibuni mmebarikiwa kuketi karibu na mama yenu. Ikiwa mmebarikiwa hivyo, mnaweza kumpa tabasamu hivi sasa ili kumshukuru. Ninaweza kukumbuka hisia ya furaha na shukrani nikiketi nyuma ya mamangu kwenye safari nyumbani baada ya ubatizo wangu kule Philadelphia, Pennsylvania.

Mamangu alikuwa ndiye aliyenitayarisha kwa makini kwa ajili ya kufanya agano hilo na yote mengine ambayo yangefuata. Alikuwa mwaminifu kwa jukumu hili kutoka kwa Bwana:

“Na tena, ili mradi wazazi wanao watoto katika Sayuni, au katika kigingi chake chochote ambacho kimeundwa, ambao hawawafundishi wao kuelewa mafundisho ya toba, imani katika Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, na ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwekwa mikono, wafikapo miaka minane, dhambi zao zitakuwa juu ya vichwa vya wazazi.

“Kwani hii itakuwa sheria kwa wakazi wa Sayuni, au katika kila kigingi chake kilichoundwa.

“Na watoto wao watabatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao wafikishapo umri wa miaka minane na kupokea [Roho Mtakatifu].”1

Mamangu alikuwa ametekeleza jukumu lake. Alikuwa amewatayarisha watoto wake na maneno mengi sana kama yale ya Alma, kama yalivyoandikwa katika Kitabu cha Mormoni:

“Na ikawa kwamba aliwaambia: Tazameni, hapa kuna maji ya Mormoni (kwani hivyo ndivyo yaliitwa) na sasa, kwa vile mnatamani kujiunga na zizi la Mungu, na kuitwa watu wake, na mko radhi kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine, ili iwe mepesi;

“Ndio, na mko tayari kuomboleza na wale wanaoomboleza; ndio, na kufariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa, na kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote mlipo, hata hadi kifo, ili muweze kukombolewa na Mungu, na kuhesabiwa pamoja na wale wa ufufuko wa kwanza, ili mpokee uzima wa milele---

“Sasa ninawaambia, ikiwa hilo ndilo pendo la mioyo yenu, ni nini mnacho dhidi ya kubatizwa kwa jina la Bwana, kama shahidi mbele yake kwamba mmeingia kwenye agano na yeye, kwamba mtamtumikia na kushika amri zake, ili awateremshie Roho yake juu yenu zaidi?

“Na sasa wakati watu waliposikia haya maneno, walipiga makofi kwa shangwe, na wakasema kwa nguvu: Hili ndilo pendo la mioyo yetu.”2

Huenda haukupiga makofi yako uliposikia kwa mara ya kwanza mwaliko huo kuingia katika agano kupitia ubatizo, lakini hakika ulihisi upendo wa Mwokozi na kujitolea zaidi kuwatunza wengine kwa ajili Yake. Ninaweza kusema “hakika” kwa sababu hisia hizo zimo ndani kabisa katika mioyo ya mabinti wote wa Baba wa Mbinguni. Hiyo ni sehemu ya uridhi wenu wa kiungu kutoka Kwake.

Mlifundishwa Naye kabla hamjazaliwa katika maisha haya. Aliwasaidia kuelewa na kukubali kwamba mgekuwa na majaribio, vipimo na fursa yaliyochaguliwa kikamilifu kwa ajili yenu. Mlijifunza kwamba Baba yetu alikuwa na mpango wa furaha kuwasaidia kushinda majaribio hayo na kwamba mngesaidia wengine kushinda majaribio yao. Mpango huu umepambwa na maagano na Mungu.

Tuko huru kuchagua kama tutafanya na kuweka maagano hayo. Ni mabinti wake wachache tu ambao wana fursa katika maisha haya hata kujifunza maagano hayo. Ninyi ni miongoni mwa wachache waliobarikiwa. Ninyi, akina dada wapendwa, kila mmoja wenu---ni binti katika agano.

Baba wa Mbinguni aliwafundisha kabla mzaliwe kuhusu matukio mgekuwa nayo mlipomwacha na kuja duniani. Mlifundishwa kwamba njia ya kurudi Kwake haingekuwa rahisi. Alijua kwamba ingekuwa vigumu sana kwenu kusafiri bila usaidizi.

Mmebarikiwa si tu kupata njia ya kufanya maagano hayo katika maisha haya lakini kwa kuzingirwa na wengine ambao watawasaidia---ambao, kama ninyi, ni mabinti wa agano wa Baba wa Mbinguni.

Nyote mmehisi baraka ya kuwa pamoja usiku wa leo na mabinti wa Mungu ambao pia wako chini ya agano kuwasaidia na kuwaongoza kama walivyoahidi kufanya. Nimeona kile mlichoona kama akina dada wa agano wekeni ahadi hiyo ya kufariji na kusaidia---na mfanyeni hivyo na tabasamu.

Nakumbuka tabasamu ya Dada Ruby Haight. Alikuwa mke wa Mzee David B. Haight, aliyekuwa mshiriki wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. Kama mvulana alihudumu kama rais wa kigingi cha Palo Alto, California. Aliwaombea, na kujali kuhusu, wasichana katika darasa la Mia Maid katika kigingi chake mwenyewe.

Hivyo basi Rais Haight alivutiwa kumuuliza askofu amuite Ruby Haight kuwafunza wasichana hao. Alijua angekuwa shahidi wa Mungu ambaye angewainua, wafariji, na kuwapenda wasichana katika darasa hilo.

Dada Haight alikuwa angalau miaka 30 zaidi ya wasichana aliowafunza. Inhali miaka 40 baada ya kuwafunza, kila wakati angekutana na mke wangu, ambaye alikuwa mmoja wa wasichana katika darasa lake, angempa mkono wake, atabasamu, na kumwambia Kathy, “Ala! Mia Maid Wangu,” Niliona zaidi ya tabasamu yake. Nilihisi upendo wake wa kina ukionyeshwa kwa maneno kwa dada aliyemjali bado ni kama alikuwa bintiye mwenyewe. Tabasamu yake na maamkuzi ya furaha yalitokana na kuona kwamba dada na binti wa Mungu alikuwa bado kwenye njia ya agano kuelekea nyumbani.

Baba wa Mbinguni hufurahi nanyi pia kila anapowaona mkimsaidia binti Yake kutembea kwenye njia ya agano kuelekea uzima wa milele. Na anafurahia kila wakati mnapojaribu kuchagua haki. Yeye huona si tu mlivyo lakini pia uwezo wenu wa kuwa.

Huenda mlikuwa na mzazi wa kidunia aliyedhani kwamba mngekuwa bora zaidi kuliko mlivyodhania mnaweza kuwa. Nilikuwa na mama kama huyo.

Kile ambacho sikukijua nilipokuwa mdogo ni kwamba Baba yangu wa Mbinguni, Baba yenu wa Mbinguni, anaona uwezo zaidi katika watoto Wake kuliko vile sisi ama hata akina mama zetu wa kidunia wanaona kwetu. Na wakati wowote unaposonga juu kwenye njia kuelekea uwezo wenu, inamletea furaha. Na mnaweza kuhisi idhini Yake.

Yeye anaona uwezo huo mtukufu katika kila binti Yake popote walipo. Sasa, hiyo inaweka jukumu kuu kwenye kila mmoja wenu. Anawatarajia mwatendee kila mtu mnaokutana nao kama mtoto wa Mungu. Hiyo ndiyo sababu anatuamuru tuwapende majirani wetu kama tunavyojipenda na kuwasamehe. Hisia zenu za ukarimu na kusamehe wengine huja kama urithi wenu wa kiungu kutoka Kwake kama binti Yake. Kila mtu mnayekutana naye ni mtoto Wake mpendwa wa kiroho.

Mnapohisi udada huo mkuu, kile tulidhani kinatutenganisha, hupotea. Kwa mfano, akina dada wadogo na wazee hushiriki hisia zao na matarajio ya kuelewa na kukubaliwa. Ninyi mnafana zaidi kama mabinti wa Mungu kuliko vile mko tofauti.

Na mtazamio huu, wasichana wanapaswa watarajie kuingia kwao katika Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kama fursa ya kuongeza idadi ya akina dada wao jambo ambalo watakuja kuwajua, kuvutiwa, na kupenda.

Uwezo huo huo wa kuona kile tunaweza kuwa inaongezeka katika familia na katika Msingi. Inajitokeza katika mkutano wa jioni wa familia nyumbani na katika mipango ya Msingi. Watoto wadogo wanaongoza kusema mambo makubwa na ya ajabu, kama walivyofanya wakati Mwokozi aliwapatia uwezo wa kuongea alipowafundisha baada ya kufufuka.3

Wakati Shetani huenda anawashambulia akina dada wakiwa wadogo, Bwana anawainua akina dada kwa viwango vya juu zaidi vya kiroho. Kwa mfano, wasichana wanawafundisha akina mama zao jinsi ya kutumia FamilySearch kupata na kuwaokoa mababu. Baadhi ya akina dada wadogo ninaowajua wanachagua kwenda asubuhi na mapema kufanya ubatizo kwa niaba ya wengine katika mahekalu bila kushawishiwa na yoyote zaidi ya Roho ya Eliya.

Katika misheni duniani kote, akina dada wanaitwa wahudumu kama viongozi. Bwana aliumba haja ya huduma yao kwa kugusa mioyo ya akina dada kwa idadi kubwa zaidi kuhudumu. Zaidi ya marais wa misheni wachache wameona wamisionari kina dada wakiwa hata zaidi na uwezo kama wahubiri na hasa viongozi wa kutunza.

Uwe ama usiwe unahudumu kama mmisionari wa muda, unaweza kupata uwezo ule ule wakuimarisha ndoa yako na uwezo wa kulea watoto wa kuheshimika kwa kufuata mifano ya wanawake kubwa.

Fikiria kumhusu Hawa, mama yao wote walio hai. Mzee Russell M. Nelson alisema yafuatayo kumhusu Hawa: “Sisi na wanadamu wote tumebarikiwa milele kwa sababu ya ujasiri na hekima ya Hawa. Kwa kula tunda kwanza, alifanya kile kilichohitajika kifanywe. Adamu alikuwa na hekima ya kutosha kufanya vile vile.”4

Kila binti wa Hawa ana uwezo wa kuleta baraka ile ile kwa familia yake ambayo Hawa alileta kwa yake. Alikuwa muhimu sana katika kuanzisha familia kiasi kwamba tunakumbukumbu hii ya kuumbwa kwake: “Na Miungu wakasema: Na tuumbe msaidizi wa kumfaa mtu huyu, kwa maana siyo vyema mtu huyu kuwa peke yake, kwa hiyo tutamuumbia msaidizi wa kumfaa.”5

Hatujui usaidizi wote Hawa alimpa Adamu na familia yao. Lakini tunajua kuhusu karama moja kuu ambayo alitoa, ambayo kila mmoja wenu anaweza kutoa pia: aliisaidia familia yake kuona njia kwenda nyumbani, wakati njia iliyo mbele ilionekana kuwa ngumu. “Naye Hawa, mke wake, alisikia mambo haya yote na akafurahi, akisema: Kama isingelikuwa kwa uvunjaji wetu wa sheria kamwe tusingelikuwa na uzao, na kamwe tusingelijua mema na maovu, na shangwe ya ukombozi wetu, na uzima wa milele ambao Mungu huutoa kwa wote walio watiifu.”6

Mnao mfano wake kufuata.

Kwa ufunuo, Hawa alitambua njia ya kwenda nyumbani kwa Mungu. Alijua kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo ulifanya uzima wa milele uwezekane katika familia. Alikuwa na uhakika, kama mnavyoweza kuwa, kwamba alivyoweka maagano yake na Baba yake wa Mbinguni, kwamba Mkombozi na Roho Mtakatifu angemsaidia yeye na familia yake kupitia mateso yoyote na masikitiko ambayo yangekuja. Alijua angewatumainia.

“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote; wala usizitegemee akili zako mwenyewe.

“Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.”7

Najua kwamba Hawa alikabiliana na mateso na masikitiko, lakini ninajua pia kwamba alipata furaha katika ufahamu kwamba yeye na familia yake wangeweza kurudi kuishi na Mungu. Ninajua kwamba wengi wenu ambao mko hapa mnakabiliana na mateso na masikitiko. Ninawabariki kwamba, kama Hawa, muweze kuhisi furaha ile ile aliyohisi yeye, mnaposafiri kurudi nyumbani.

Nina ushuhuda wa hakika kwamba Mungu Baba anawajali ninyi kwa upendo. Anawapenda kila mmoja wenu. Ninyi ni mabinti zake katika agano. Kwa sababu anawapenda, atatoa usaidizi ambao mnahitji ili kujiinua wenyewe na wengine njiani kurudi kwa uwepo Wake.

Najua kwamba Mwokozi aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu zote na kwamba Roho Mtakatifu anashuhudia ukweli huu. Mmehisi faraja hiyo katika mkutano huu. Nina ushuhuda kwamba funguo zote ambazo hufunga maagano matakatifu zimerejeshwa. Zinashikiliwa na kutumiwa leo nabii wetu aliye hai. Ninawaachia maneno ya faraja na matumanini, mabinti Zake wapendwa wa agano, katika jina la Yesu Kristo, amina.